Kisa Changu

Kisa Changu

By The Standard Group PLCSociety & CulturePersonal Journals
Download on the App Store

Kisa Changu episodes

  • Kisa Changu Podcast: Nabaguliwa kwa kuwa nina ulemavu wa ngozi 'albinism'
    Denis Kazungu ni mwenye ulemavu wa ngozi yaani albinism. Kazungu mwenye umri wa miaka 29 na ambaye ni mkazi wa Malindi-Airport, Kilifi anasema hali yake imemsababishia changamoto nyingi tangu alipozaliwa hadi sasa.
    Kazungu amepitia unyanyapaa; amebaguliwa si tu na jamii bali pia kwenye maeneo ya kazi akisema ulemavu wake umesababisha kampuni nyingi kutilia shaka uwezo wake wa kutekeleza majukumu.
    Je, amefanikiwa vipi na hata kupiga hatua maishani licha ya changamoto hizo? Sikiliza masimulizi yake katika makala yafuatayo ya ''Kisa Changu Podcast'' na Robert Menza.
    16 min
  • Kisa Changu Podcast: Mpenzi alinitoroka nilipougua saratani
    Jane Chepchumba mwenye umri wa miaka 32, ni mama wa mtoto mmoja. Chepchumba alianza kuugua saratani ya tumbo mwaka 2012 akiwa katika chuo kikuu.
    Anasema alipoanza kutibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Moi Mjini Eldoret madaktari walimweleza kwamba huenda asiweze kupata watoto siku za usoni kutokana na athari za saratani. Anasema mpenziwe aliyekuwa naye alivunjwa moyo na hilo na kumwacha.
    Anasema baada ya zaidi ya miaka mitano ya matibabu ya Chemotherapy, mwaka 2016 madaktari walimfahamisha kuwa hana saratani tena. Baadaye alifanikiwa kupata mpenzi mwingine ambaye alijaliwa naye mtoto mwaka 2019, ila naye akatoweka. Jepchumba anasema furaha yaka sasa ni mwanawe. Sikiliza masmulizi ya safari ya Jepchumba katika makala haya ya Kisa Changu Podcast.
    20 min
  • Kisa Changu Podcast: Kilio cha Mama
    Ruth Keino mkazi wa Nandi ni mama mwenye machungu. Keino amekuwa akitafuta haki tangu mwanawe alipoaga dunia zaidi ya mwaka mmoja uliopita akiwa shuleni.
    Beryl Cherop aliyekuwa na miaka 16 alifariki dunia miezi michache tu baada ya kujiunga na kidato cha kwanza katika Shule ya Upili ya St Teresa of Avila Girls. Kinachomuumiza Keino roho hata zaidi ni kwamba hakuna mtu ahta mmoja aliyehudhuria hafla ya mazishi ya mwanawe kuifariji familia.
    Anasema hatachoka hadi pale haki itakapopatikana kufuatia kifo cha mwanawe. Sikiliza masimulizi ya kina katika makala yafuatayo
    20 min
  • Kisa Changu Podcast: Kwa nini niliamua kutumia Facebook kumtafuta mtu anipe figo: Eunice Rop -Sehemu ya Kwanza
    Eunice Rop mkazi wa Nandi Hills alikuwa na matatizo ya kiafya tangu mwaka 2011 ambapo alikuwa akitibiwa katika hospitali moja bila mafanikio.
    Mwaka 2013 alitafuta huduma za matibabu katika hospitali moja mjini Eldoret ambapo ilibainika kuwa alikuwa na matatizo ya figo na kuanza matibabu
    Mwaka 2015 ndugu zake 2 waljitoleakupata figo nyingine lakini walipofanyika uchunguzi ikagunduliwa wao pia walikuwa na matatizo ya figo.
    Baada ya miaka 7 ya matibabu ya figo, mwaka 2019 Mei, Eunice aliamua kutumia mtandao wa Facebook kumtafuta mtu yeyote ambaye angemsaidia kupata figo nyingine.
    Je, alifanikiwa? Sikiliza masimulizi ya Eunice na Faith Kutere katika sehemu ya kwanza ya makala yafuatayo.
    14 min
  • Kisa Changu Podcast: Waliomuua mume wetu wanatuandamana -Wake wa Isaac Juma
    Zaidi ya miezi miwili tangu aliyekuwa shabiki sugu wa kandanda nchini Isaac Juma kuuliwa, familia yake ya wake wawili na watoto kumi na saba ingali inahangaika. Wakati wa hafla ya mazishi wanawe Juma waliitaka serikali kuwaondoa katika eneo hilo wakidai maisha yao yalikuwa hatarini.
    Katika simulizi ifuatayo Wake wa Juma Christine na Farida Juma wamethibitisha madai hayo wakisema watu wasiowajua wamewavamia mara si moja tangu mume wao alipozikwa huku idara za usalama zikisalia kimya.
    Mwanahabari Benard Lusigi amewahoji Christine na Farida Juma.
    9 min
  • Kisa Changu Podcast: Watoto wa Marehemu Isaac Juma Walilia Haki
    Isaac Juma alikuwa shabiki sugu wa kandanda nchini. Alijijengea jina kwa kuhudhuria na kushabikia Timu ya Kitaifa ya Harambee Stars na ile ya Gor Mahia akiwa amejichora mwili wote kutumia rangi za bendera ya Kenya.
    Katika Spoti, Juma alikuwa na wafuasi waliompenda sana wakiwamo mashabiki wenzake. Ila maisha nyumbani kwake yalikuwa tofauti; mbali na kusalia maskini hohehahe licha ya umaarufu huo, ulikuwapo mzozo wa umiliki wa ardhi baina yake na dada zake. Alisema wazi kwamba maisha yake yalikuwa hatarini, huku akiomba ulinzi, lakini alipuuzwa na mwishowe akaangamizwa. Na sasa wanawe wanahofia huenda yaliyompata baba yao yakawapata pia wakitaka kuhamishwa na kupewa eneo mbadala la kuishi.
    Aliwaacha watoto 17.14 miongoni mwao wanazungumzia hofu waliyo nayo na mahangaiko marehemu baba yao alipitia kabla ya kifo katika masimulizi haya.
    9 min
  • Kisa Changu Podcast: Wanaume wanaochapwa na wake zao wafungua roho
    Visa vya dhuluma za kijinsia vimekuwa zikiripotiwa humu nchini kila kukicha. Hata hivyo mara nyingi utapata kwamba wanawake ndio huwa wepesi wa kuzungumzia dhuluma hizo huku wanaume wakijificha kwa hofu ya unyanyapaa, kuchekwa, kusimangwa na kukejeliwa na wanajamii.
    Martin Ndiema amewahoji baadhi ya wanaume wanaopita dhuluma hizo ila wanaogopa kutafuta usaidizi. Sikiliza mahangaiko wanayopitia katika masimulizi yafuatayo.
    8 min
  • Kisa Changu Podcast: John Kiriamiti - maisha ya uhalifu; alianzia uandishi jela
    Anafahamika kufuatia visa vyake vya wizi sugu wa pesa katika benki wakati wa miaka ya 70. John Kiriamiti aliacha masomo akiwa katika kidato cha kwanza akiwa mwanafunzi katika shule ya upili ya Prince of Wales ambayo sasa ni Nairobi School, na hapo ndipo alipoanza uhalifu. Hata hivyo, wasemao husema kwamba siku za mwizi ni arubaini.
    Kiriamiti pamoja na wenzake walikamatwa na kuhukumiwa jela kutokana na uhalifu huo. Akiwa jela, John Kiriamiti alianza uandishi wa vitabu, ambavyo baadaye vilikuwa maarufu nchini na kupendwa sana hasa na wanafunzi. Vitabu vilivyoandikwa na Kiriamiti ni kama My Life in Crime, My Life With a Criminal, My Life in Prison. Fahamu zaidi kuhusu maisha yake katika masimulizi yafuatayo.
    49 min
  • Kisa Changu Podcast; Kwa nini niliamua kuwasaidia wanaougua fistula - Sharon Korir. Sehemu ya 2
    Katika sehemu ya pili Wakili Korir anaeleza namna mahangaiko yake yalivyompa msukumo wa kuanzisha Shirika la Save a Woman, Fistula Foundation ili kuwapa matumaini wanawake na wasichana ambao wameathiriwa na Fistula.
    Akiwa wakili kwa ushirikiano na washikadau mbalimbali, anahisi serikali haijafanya vyema sana katika kuihamasisha jamii kuhusu Fistula hali ambayo imechangia kuwapo kwa unyanyapaa dhidi ya wanawake wanaougua Fistula.
    Sikiliza masimulizi haya katika sehemu hii ya pili na Carren Papai.
    14 min

About Kisa Changu

From the publisher's feed

Watu mbalimbali wanasimulia wanayopitia ama kushuhudia kwa namna ya kugusa moyo, kushtua na kuliza machozi, vilevile kauli za matumaini.