Kisa Changu

Kisa Changu

By The Standard Group PLCSociety & CulturePersonal Journals
Download on the App Store

Kisa Changu episodes

  • Kisa changu Podcast; Ugonjwa wa Fistula ulivyoathiri maisha yangu -Sharon Korir Sehemu ya 1
    Wakili Sharon Korir mwathiriwa wa Fistula, anasema alipitia nyingi baada ya kugundua anaugua Fistula ukiwamo unyanyapaa kutoka kwa familia na jamaa zake. Anasema alianza kuugua baada ya kujifungua mwanawe wa pili.
    Baada ya kudhalilishwa na hata kutengwa na mumewe alipokuwa na Fistula, Wakili Korir hakukataa tamaa aliamua kumwelezea shemejiye kuhusu tatizo hilo kisha akapata matibabu.
    Amezungumza na Carren Papai kuhusu jinsi mambo yalivyoanza, akiwa hospitalini na kipindi cha kupona katika sehemu hii ya kwanza ya Kisa Changu Podcast
    10 min
  • Kisa Changu Podcast: Sina mikono; mahangaiko na kusaidiwa -Jackline Mwende, Sehemu ya 2
    Katika sehemu ya kwanza ulifahamu kuhusu kilichofanya Jackline Mwende kupoteza mikono yote miwili. Katika sehemu hii ya pili, Mwende anaeleza namna ambavyo sasa inamlazimu kuwategemea watu wengine hasa wazazi wake kumfanyia majukumu hata ya kimsingi kama kumwosha.
    Aidha, anasema hali yake ya maisha imewasababishia mahangaiko makubwa wazazi wake na hata kuwasababishia matatizo ya kiafya.
    Maisha ya Mwende - mama wa mtoto mmoja yamebadilika vipi tangu tukio hilo la miaka 5 iliyopita? Sikiliza podcast hii.
    13 min
  • Kisa Changu Podcast: Sina mikono; ilikatwa na mume aliyenishuku - Jackline Mwende, Sehemu ya 1
    "Nikamuuliza, Ngila utaniua na unimalize? Akaniambia umeongea kwa mara ya kwanza na ya mwisho, akaendelea na kunikatakata.'' Jackline Mwende mwenye umri wa miaka 32 anaanza kusimulia mahangaiko yanayomkumba baada ya mumewe kumkata mikono yote miwili.
    Ilikuwa Jumamosi Julai 23, mwaka 2016 Mwende aliporejea nyumbani usiku alikokuwa akiishi peke yake kwa sababu mumewe alikuwa ametoweka kwa miezi mitatu.
    Kwa miaka mingi, Mwende na mumewe Stephen Ngila waliishi bila kujaaliwa mtoto hali iliyosababisha matatizo katika ndoa yao. Ilisemekana Ngila alimshambulia Mwende kwa kumkatakata kwa upanga alipobaini kwamba alikuwa na mpenzi mwingine.
    Fahamu zaidi katika podcast hii kuhusu kilichotokea usiku huo, alivyookolewa na aliko Stephen Ngila.
    11 min
  • Kisa Changu Podcast: HIV yanisababishia upweke - Ali Mwinyi
    Ali Mwinyi, mkazi wa Kaunti ya Kilifi amekuwa akiugua ukimwi kwa miaka 15.
    Anasema licha ya kampeni za kuuhamasisha umma kuhusu ukimwi, safari yake imekuwa na pandashuka nyingi. Mbali na kutopata huduma zinazofaa kwa haraka inavyostahili, anasema amekabiliwa na unyanyapaa na ubaguzi kutoka kwa wanajamii.
    Mwanahabari wetu, Marion Kithi amemtembelea nyumbani na hapa anatupa taswira kamili ya mahangaiko wanayopitia waathiriwa wa ukimwi, miaka 40 tangu virusi vya HIV kugunduliwa duniani.
    11 min
  • Kisa Changu Podcast: Ukatili wa kubomolewa nyumba Mukuru, Nairobi
    Bridgit Achieng' ni miongoni mwa maelfu ya wakazi wa mtaa wa mabanda wa Mukuru ambao hawana makao baada ya serikali kubomoa nyumba zao, kupisha ujenzi wa barabara ya Nairobi Expressway.
    Bridgit mwenye umri wa miaka 25 na mama wa mtoto mmoja anasema ameishi mtaani Mukuru maisha yake yote na hatua hiyo imemwathiri pakubwa kwani alilazimika kuanza upya tena maisha yake.
    Lakini kinachovutia zaidi kutoka kwa Bridgit si changamoto za kuishi katika mtaa wa mabanda au kukosa makazi bali ni kuamua kutumia mahangaiko yanayomkumba kuwatia motisha vijana kupitia mtandao wake wa Facebook.
    Sikiliza masimulizi kamili katika makala haya na Carren Omae.
    14 min
  • Kisa Changu Podcast: Familia Yalilia Haki -Jamaa Wao Aliuliwa na Mwanajeshi wa Uingereza
    Miaka 9 baada ya Agnes Wanjiru kuuliwa kinyama na mwanajeshi wa Uingereza wa Kitengo cha BATUK kinachofanyia mazoezi yake eneo la Nanyuki kwenye Kaunti ya Laikipia, Familia yake sasa inaomba haki kutendeka na kufidiwa baada ya mwanajeshi huyo kukiri kutekeleza mauaji hayo.
    Kama anavyoeleza, Rosemary Wanjiku ambaye ni Dadake Agnes changamoto alizopitia kumlea mwanawe Agnes kwani alimwacha akiwa na umri wa miezi mitano pekee. Rosemary anaelezea alivyopokea habari za kifo cha dadake huku akiwalaumu maafisa wa polisi wa Kenya kwa kuzembea kazini wakati wa uchunguzi.
    13 min
  • Kisa Changu Podcast: Si kurogwa, bali ''ovarian cancer''
    Faustine Andeso alikuwa mwenye wasiwasi wakati ambapo mwanawe wa kike alianza kutokwa na chunusi (pimples) usoni akiwa na miezi minne.
    Mwanawe Bibian, alipofika umri wa miezi mitano alianza kutokwa na damu katika sehemu ya uke halafu akaanza kuonesha dalili za msichana anayebaleghe.
    Awali alidhani kuwa mwanawe alikuwa amerogwa na akatafuta matibabu ya kiasili lakini hakupona.
    Alipofika hospitalini ilibainika kuwa Bibian alikuwa na uvimbe kwenye kifuko cha yai la kizazi uliotolewa kupitia upasuaji na kupimwa ambapo mwishowe ilibainika kwamba alikuwa na Ovarian Cancer.
    Faith Kutere amezungumza na Faustine kuhusu hali ya mwanawe ambaye kwa sasa anaendelea kupata nafuu baada ya kutibiwa saratani.
    16 min
  • Kisa Changu Podcast: Ulemavu si hoja; ndoa ni ya dhati
    Linet Kagasa mwenye umri wa miaka 30 asiye na miguu yote miwili vilevile aliyelemaa mkono wa kushoto alikuwa na ndoto ya kupata mtu wa kumpenda na kumfanya mkewe. Alipatana na Peter Odiwuor kwenye mtandao wa Facebook na wakaanza uhusiano ambao uliwafikisha katika ndoa na sasa wanaishi pamoja. Katika Kisa Changu wiki hii wawili hawa wanazungumza na Faith Kutere kuhusu safari yao ya mapenzi na jinsi jamii ilivyochukulia uhusiano wao.
    20 min
  • Kisa Changu Podcast: Ulemavu si hoja; ndoa ni ya dhati
    Linet Kagasa mwenye umri wa miaka 30 asiye na miguu yote miwili vilevile aliyelemaa mkono wa kushoto alikuwa na ndoto ya kupata mtu wa kumpenda na kumfanya mkewe.
    Alipatana na Peter Odiwuor kwenye mtandao wa Facebook na wakaanza uhusiano ambao uliwafikisha katika ndoa na sasa wanaishi pamoja.
    Katika Kisa Changu wiki hii wawili hawa wanazungumza na Faith Kutere kuhusu safari yao ya mapenzi na jinsi jamii ilivyochukulia uhusiano wao.
    20 min
  • Kisa Changu Podcast: "Said yu wapi?" Familia yalilia haki
    Tunu Said mwenye umri wa miaka 51 anadaiwa kuchukuliwa kwa nguvu na watu wanaoaminika kuwa maafisa wa Kitengo cha Kukabili Ugaidi, ATPU. Kundi la takriban watu 20 lililokuwa limejihami kwa bunduki na kufunika nyuso lilivamia boma la Said kwenye Mtaa wa Kona Mpya, Likoni katika Kaunti ya Mombasa kisha kutoweka naye.
    Mwanahabari Robert Menza amezungumza na familia ya Said, inayoeleza jinsi maafisa hao walivyolivamia boma lao usiku wa manane na kuwahangaisha kabla ya kutoweka naye.
    20 min

About Kisa Changu

From the publisher's feed

Watu mbalimbali wanasimulia wanayopitia ama kushuhudia kwa namna ya kugusa moyo, kushtua na kuliza machozi, vilevile kauli za matumaini.