Kisa Changu

Kisa Changu

By The Standard Group PLCSociety & CulturePersonal Journals
Download on the App Store

Kisa Changu episodes

  • Kisa Changu Podcast: Maisha Uarabuni; Ukoloni Mamboleo - Faith Murunga, Sehemu 2
    Katika sehemu ya kwanza Faith Murunga alisimulia namna alivyojiandaa na kusafiri hadi saudia kwa kazi za nyumbani. Anasema alipowasili huko, maisha yalikuwa tofauti na alivyodhania. Faith anasema alidhulumiwa na kuteswa na mwajiri wake ambaye alimhitaji kufanya kazi nyingi tofauti na walivyokubaliana, hakupata chakula cha kutosha na alichapwa hata bila kukosea.
    Maji yalizidi unga hadi akaamua kuanza safari ya kurejea Kenya baada ya mwaka mmoja unusu wakati mwajiri wake alipomchoma mkono kwa kummwagia maji ya moto. Je, alitumia mbinu gani hadi akarejea nyumbani? Sikiliza sehemu ya pili ya podcat hii na Carren Omae.
    20 min
  • Kisa Changu Podcast: Mateso Uarabuni; Ukoloni Mamboleo-Faith Murunga, Sehemu 1
    Baada ya kukosa njia ya kujiinua kimaisha nchini Kenya, Faith Murunga aliamua kwenda Saudi Arabia kujitafutia riziki. Faith anasema aliposikia kuhusu fursa zilizoko huko, hakufikiria mara mbili akidhani kwamba ingekuwa suluhu ya matatizo ya kifedha yaliyomkumba.
    Anasema mipango ya kuelekea Saudi Arabia ni rahisi tu, na wapo mawakala na maajenti walio tayari kutoa usaidizi huo, jinsi ambavyo anasimulia katika sehemu ya kwanza ya podcast hii, katika mahojiano na Carren Omae.
    13 min
  • Kisa Changu Podcast: Hata adui usimwombee korona - Etale, sehemu 2
    Katika sehemu ya kwanza, Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Chama cha ODM, Philip Etale alieleza jinsi alivyougua Covid-19 na safari yake ya matibabu. Katika sehemu hii ya pili, anaeleza jinsi alivyochungulia kaburi kwani wagonjwa wote waliolazwa naye ICU walifariki dunia.
    Rosa Agutu anaendeleza mazungumzo hayo katika sehemu ya pili ya podcast hii inayohumu masimulizi ya Etale, mmoja wa walioathiriwa vibaya na korona.
    20 min
  • Kisa Changu Podcast: Hata adui usimwombee korona - Etale, sehemu 1
    Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Chama cha ODM, Philip Etale aliugua korona mara mbili chini ya mwaka mmoja.
    Wakati huo wote, alilazwa ICU. Etale ambaye sasa anaendelea kupata nafuu anasema wakati mmoja, aliondoa mashine ya oksijeni, na kukaa kwa dakika 15 bila hewa hiyo inayoshikilia uhai.
    Amezungumza na Rosa Agutu, katika sehemu ya kwanza ya podcast hii inayohumu masimulizi ya mmoja wa walioathiriwa vibaya na makali ya korona.
    18 min
  • Kisa Changu Podcast: Everlyne, nilimpokonya jambazi bunduki na kuokoa familia yangu
    Everlyne Barasa mwenye umri wa miaka 51 alimkabili, akampiga miereka na kumwangusha sakafuni jambazi kisha akampokonya bunduki aina ya AK 47.
    Everlyne ambaye ni mama wa watoto 3 mkazi wa Kijiji cha Kaptegaa, Trans Nzoia amemsimulia mwanahabari wetu, Martin Ndiema jinsi jambazi huyo alivyoingia ghafla chumbani na kumwamuru kusalia kimya la sivyo amwangamize yeye, wanawe na mume wake aliyekuwa akisinzia kwenye kochi.
    Everlyne anasema alimkabili vilivyo jambazi huyo kutumia mbinu za karate alizofunzwa na mwalimu wake miaka 30 iliyopita alipokuwa katika Shule ya Msingi ya Sendera kwenye taarafa ya Kapsokwony kwenye Eneo Bunge la Mlima Elgon, Kaunti ya Bungoma.
    11 min
  • KISA CHANGU PODCAST: Chifu, miaka 20 jela kwa kusingiziwa ubakaji
    Aliyekuwa chifu wa Kata ya Kanamkemer katika Kaunti ya Turkana, Suleiman Loriu aliyehukumiwa kifungo cha miaka 20 kwa kwa madai ya kumbaka mtoto wa miaka 15 ametoka garezani.
    Suleiman anasema aliyedaiwa kumbaka hakuwa mtoto ila mtu mzima tena mke wake.
    Baada ya kukaa gerezani kwa miaka 11, alishinda rufaa aliyowasilisha baada ya kuthibitisha kuwa hakumbaka mtoto. Ameiomba jamii msamaha na kuitaka imkubali kwani hakuwa na hatia. Loriu ameshiriki mazungumzo na Mike Ekutan.
    12 min
  • Kisa Changu Podcast: Ugonjwa wa kinga mwilini kushambulia seli umenivurugia maisha!
    Dickson Kibiwott alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Masinde Muliro takriban miaka 5 iliyopita alipougua ghafla.
    Alipatakina na tatizo la kiafya ambapo kinga ya mwili hushambulia seli mwilini, ugonjwa ambao unajulikana kama multiple sclerosis, ambao ulimlemaza baada ya siku tatu tu.
    Ugonjwa huu hauna tiba na wakati mwingine humsababisha mtu kupooza, kukosa kuona vizuri, kuhisi uchovu mwingi, kushindwa kutafuna chakula na kumeza, kushindwa kuzungumza miongoni mwa matatizo mengine mengi.
    Kibiwott alilazimika kusitisha masomo yake na mamaye akilazimika kusitisha biashara ili kumshughulikia akiwa nyumbani.
    Faith Kutere amezungumza na Kibiwott pamoja na mamaye, Loice Tum anayeeleza changamoto za kumshughulikia mwanawe ambaye ni mtu mzima kama mtoto mdogo baada ya ugonjwa huo kumlemaza.
    14 min
  • KISA CHANGU PODCAST: Anazuru kote nchini kwa baiskeli kuhamasisha kuhusu korona
    Fredrick Ochieng mwenye umri wa miaka 27, amejipa jukumu la kuufikisha ujumbe kuhusu janga la korona kote nchini. Ochieng' anasema amechukua hatua hiyo baada ya kuwaona Wakenya wengi wakipuuza masharti ya kukabili janga hilo.
    Anasema haja yake ni kumwona kila Mkenya akitii masharti hayo hatua itakayowasaidia kurejelea maisha ya kawaida.
    Mwanahabari Mike Ekutan amekutana na Ochieng' baada ya kuwasili mjini Lowdor, katika Kaunti ya Turkana ambapo amemsimulia kuhusu hali yake safarini.
    8 min
  • KISA CHANGU PODCAST: Kukosa uwezo wa kuona si kizingiti
    Eunice Waithera, mzawa wa Molo alipoteza uwezo wa kuona akiwa na umri wa miaka sita pekee, likini hilo halikumvunja moyo. Alijikakamua masomoni na sasa ni mwalimu wa shule ya upili.
    Eunice ni mwalimu wa kipekee, kwani wanafunzi wake hawana matatizo ya kuona jinsi ingetarajiwa. Mwalimu huyu wa somo la Kiswahili anasema hajawahi kukata tamaa.
    Katika masimulizi na mwanahabari wetu William Omasire, Eunice anasema alichopoteza ni uwezo wa kuona tu wala si mwelekeo maishani.
    14 min

About Kisa Changu

From the publisher's feed

Watu mbalimbali wanasimulia wanayopitia ama kushuhudia kwa namna ya kugusa moyo, kushtua na kuliza machozi, vilevile kauli za matumaini.