Kisa Changu

Kisa Changu

By The Standard Group PLCSociety & CulturePersonal Journals
Download on the App Store

Kisa Changu episodes

  • KISA CHANGU PODCAST: Niliponea kifo Saudi Arabia
    Rebecca Chesang, mzawa wa Kaunti ya Nandi alielekea Saudi Arabia mwaka 2019 mwezi Februari kufanya kazi za nyumbani.
    Chesang alilenga kuisaidia familia yake kwa kufanya kazi jijini Riyadh, Mji Mkuu wa Saudi Arabia, lakini alijipata katika mji wa Arar, kilomita 60 kutoka mpaka wa Saudi Arabia na Iraq.
    Anasema maisha Uarabuni yalikuwa magumu na mara kadhaa alidhulumiwa na mwajiri wake na akalazimika kupiga ripoti katika idara mbalimbali kuhusu masaibu yaliyomkumba.
    Alipata usadizi na kurejea nchini baada ya Shirika la Habari la Standard kuangazia yaliyomkumba Saudia, jinsi alivyomsimulia mwanahabari wetu, Faith Kutere.
    29 min
  • KISA CHANGU PODCAST: TB ya mifupa ilinilemaza mguu
    Je, unajua nini kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu yaani TB? Umewahi kusikia kwamba TB pia huathiri mifupa? Doris Sambu, mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Multimedia ana ulemavu wa mguu kutokana na TB ya mifupa. Doris, anasema alianza kuugua akiwa na umri wa miaka 7.
    Anasema mamaye alipompeleka katika Hospitali ya Londiani, Kericho, ugonjwa huo haukutambuliwa hali iliyomlazimu kukaa hospitalini kwa muda hadi pale alipopelekwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta KNH, jijini Nairobi. Alipokuwa KNH ndipo ilipobainika kwamba alikuwa akiugua TB ya mifupa kisha akafanyiwa upasuaji katika paja. Licha ya juhudi za madaktari, mguu wake ulilemaa.
    Anasema mbali na ulemavu huo kumsababishia changamoto nyingi kama vile msongo wa mawazo, uhusiano wake wa kimapenzi umesambaratika kutokana na hali hiyo. Hata hivyo, amepiga moyo konde na kuendelea na maisha kama kawaida.‚Äč Amezungumza na Esther Kirong katika makala haya.
    22 min
  • KISA CHANGU PODCAST: Nilikaa Kamiti miaka 5 kwa kosa ambalo sikulifanya
    John Mutua maarufu Kaploti alikaa katika Gereza la Kamiti kwa miaka 5 akikabiliwa na tuhuma za mauaji.
    Kaptoli anasema alikamatwa alipopatikana kwenye eneo la tukio ambapo mtu mmoja aliuliwa kwa kudungwa kisu na vijana waliokuwa wakimwibia.
    Anadai kwamba hakuwa na pesa za kuwahonga polisi waliomsingizia kuwa ndiye aliyekuwa mshukiwa mkuu bila uchunguzi kufanywa. Kesi dhidi yake iliendelea kwa miaka mitano lakini hatimaye akaachiliwa huru kufuatia ukosefu wa ushahidi wa kutosha.
    Kaploti amezungumza na Carren Omae na kusimulia jinsi hali ilivyokuwa tangu kukamatwa, maisha gerezani na maisha yake baada ya kuachiliwa huru.
    19 min
  • KISA CHANGU PODCAST: Mwanamke ahangaika baada ya kufutwa na mume kumtoroka
    Wilkister Maluki, mama wa watoto wawili vilevile mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha South Eastern Kenya University, SEKU amelazimika kusitisha masomo kwa kukosa karo baada ya kufutwa kazi katika kampuni moja jijini Nairobi. Wilkister ambaye anaishi katika Mtaa wa Mabanda wa Mukuru Kayaba jijini Nairobi sasa anawafulia watu nguo ili kukimu mahitaji ya familia yake changa.
    Anasema alianza kuwafulia watu nguo wiki tatu tu baada ya kujifungua mwanawe wa pili na kumwathiri pakubwa kiafya.
    Isitoshe, mumewe alitoweka punde tu baada ya yeye kuachishwa kazi kutokana na janga la korona.
    Kwa sasa, maisha yanazidi kuwa magumu, familia nayo inamtegemea na hana ajira. Kifungua-mimba wake pia ameacha masomo kutokana na ukosefu wa karo. Esther Kirong amezungumza naye katika Podcast hii.
    16 min
  • KISA CHANGU PODCAST: Machungu ya baba aliyepokonywa wanawe
    Sammy Natoo, mkazi wa Kaunti ya Turkana ana machungu moyoni baada ya kunyang'anywa watoto miaka kadhaa iliyopita kwa kutomlipia mahari mkewe.
    Kila Jumapili ya tatu ya mwezi Juni wazazi wengine wa kiume wanaposherehekea Siku ya Akina Baba Duniani Natoo anasema inamkumbusha tu masaibu ambayo amekuwa amekuwa akipitia tangu mwaka 1993.
    Amezungumza na Mike Ekutan na kumweleza kwa kina masaibu yake.
    15 min
  • KISA CHANGU PODCAST: Polisi aliyeshushwa ngazi kwa kutofautiana na bosi
    John Kipitanui Koech, afisa wa polisi wa kitengo cha upelelezi anayehudumu katika Kaunti ya Kirinyaga anasema alishushwa daraja kwa njia tatanishi.
    Koech anasema ataelekelea mahakamani kuharamisha uamuzi huo.
    Amemweleza mwanahabari wetu John Mbuthia kuwa licha ya juhudi za kuwaeleza wakubwa wake kilio hicho amepuuzwa, hivyo kulazimika kuwasilisha kilio chake katika vyombo vya habari.
    13 min
  • KISA CHANGU PODCAST: Kilio cha miaka13; risasi katika uti wa mgongo
    Stephen Nyoka mwenye umri wa miaka 56 mkazi wa Kijiji cha Embakasi, Saboti katika Kaunti ya Trans Nzoia, alishambuliwa na waliokuwa wanachama wa kundi la Saboat Land Defence Force, SLDF lililosambaratishwa mwaka wa 2008 na kikosi cha jeshi katika operesheni ya Okoa Maisha.
    Katika kisa hicho cha Machi 3, 2008, watoto wake watatu waliuliwa na mke wake kujeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi pia kwa kukatwa kwa upanga.
    Nyoka anaishi akiwa na risasi hiyo kwani madaktari walimwonya kwamba ikiwa upasuaji utafanyika kujaribu kuiondoa basi atafariki dunia.
    Afya ya Nyoka inaendelea kudhoofika kutokana na athari za risasi hiyo na msongo wa mawazo jinsi utakavyosikia katika mahojiano kati yake na Martin Ndiema.
    18 min
  • KISA CHANGU PODCAST: Tuliacha wizi baada ya wenzetu kuangamizwa
    Fredrick Okinda na Robert Muchiri ni vijana waliokuwa wahalifu sugu waliowahangaisha watu mtaani Korogocho.
    Lakini sasa wamebadilika kabisa mbali na kujihusisha na miradi ya utunzaji wa mazingira. Aidha, wanawahamasisha vijana wenzao kwamba uhalifu haulipi. Juhudi zao zimefanikiwa? Wanapitia changamoto zipi? Matumaini yao ya baadaye ni yapi? Yapate majibu yote haya katika kipindi hiki cha Kisa Changu Podcast na Carren Omae.
    20 min

About Kisa Changu

From the publisher's feed

Watu mbalimbali wanasimulia wanayopitia ama kushuhudia kwa namna ya kugusa moyo, kushtua na kuliza machozi, vilevile kauli za matumaini.