Sign up to save your podcastsEmail addressPasswordRegisterOrContinue with GoogleAlready have an account? Log in here.
Podcast mahususi kujifunza mambo ya maendeleo binafsi (Personal development/Self-improvement), maisha, mahusiano, saikolojia na elimu ya fedha.Ni podcast ya kipekee ambayo utajifunza mambo mengi amb... more
FAQs about Maisha Ni Kuthubutu Podcast:How many episodes does Maisha Ni Kuthubutu Podcast have?The podcast currently has 119 episodes available.
March 10, 2022Sababu Saba (07) Za Kwanini Unapaswa Kujua Nguvu Ya Mabadiliko Kwenye Maisha Yako.Je Unataka kubadili mfumo mzima wa maisha yako, mtazamo wako, aina ya marafiki, namna unavyofanya, mahusiano yako, biashara yako, Huduma yako n.k? Basi episode hii itakupa ufahamu wa nguvu wa mabadiliko kwenye maisha yako na kuweza kuchukua hatua Ili upate mabadiliko . Sikiliza mpaka mwisho upata kujua kwanini unaweza kupata mabadiliko kwenye eneo lolote ambalo upo...more17minPlay
February 22, 2022Mambo Matatu (03) Ambayo Hupaswi Kumshirikisha Kila Mtu Kwenye Maisha YakoMuda mwengine unashindwa kupiga hatua kwenye maisha yako Kwa sababu ya kushirikiana watu baadhi ya mambo ambayo hayapaswi kabisa kuwashirikisha lakini kwa kuchukulia poa imekuwa inagharimu sana watu wengi, hivyo unapaswa kuwa makini kujua mambo gani unapaswa kutoshirikisha kabisa watu na mambo gani ambayo unaweza kushirikisha watu kwa maana hiyo maisha ni kuwa na kiasi kujua nini ufanye na nini usifanye kwahiyo Podcast hii itakusaidia kujua jinsi ya kuweza kuwa na kiasi/mipaka kwenye kushirikisha watu mambo yako, enjoy to listen podcast don’t forget to subscribe on Castbox and Apple podcast...more9minPlay
February 15, 2022Maswali Matano (05) Ambayo Yatakusaidia Kugundua Kusudi La Kuzaliwa Kwako.Je unataka kujua kwanini umezaliwa? Kabla ya kujua umezaliwa kufanya nini basi tambua kuwa wewe hujazaliwa kwa bahati mbaya, hujazaliwa kwa bahati nasibu, hujazaliwa kwa miujiza, hujazaliwa kwa kuwa wazazi wako walitaka mtoto. Lakini tambua kwamba wewe umezaliwa kwa kusudi hivyo haupo duniani kwa bahati mbaya. Ili maisha yako yawe yenye maana ni kujua kusudi la kuzaliwa kwako. Sikiliza Episode hii itakupa majibu ya KWANINI umezaliwa na hatimaye kuongeza thamani ya maisha yako kwa kuliishi kusudi lako...more18minPlay
February 06, 2022Onyo! Hata Usifikirie Kushinda Tabia Ya Kughairisha Malengo Yako Mpaka usikilize Hii...Sababu kuu tano (05) za kwanini unapaswa kushinda tabia ya kughairisha malengo yako kwenye maisha yako...! Sikiliza mpaka mwisho utajifunza mengi...more14minPlay
January 30, 2022Mambo Matano (05) Ya Kufanya Ili Uboreshe Mahusiano YakoJe unajua jinsi ya kuboresha mahusiano yako yadumu kwa muda mrefu? Mahusiano ni zaidi ya kupendana kwa maana upendo hautoshi kufanya mahusiano yadumu, ni mahusiano mangapi yamevunjika japokuwa watu bado wanapendana? Ni kwa sababu ya kutojua namna gani wanaweza kuboresha mahusiano yako Basi Podcast hii Itakusaidia kujua namna gani unaweza kuboresha mahusiano yako na kuweza kudumu kwa muda mrefu. Subscribe kisha niandikie maoni yako umejifunza nini kwenye Podcast hii...more12minPlay
January 22, 2022Hatua Saba (07) Za Kuzingatia Wakati Unapanga Malengo Yako.Je unataka kutimiza malengo yako kwa asilimia ngapi? Unajua kwamba kutimiza malengo yako inategemea sana namna ya kupanga malengo yako kwa bahati mbaya changamoto kubwa watu wengi hawajui namna gani wanapanga malengo vizuri na kwa ufanisi. Sikiliza Podcast hii mpaka mwisho utaweza kujua hatua saba za kuzingatia wakati unapanga maalengo yako, Kutimiza malengo ipo ndani ya uwezo wako ni wewe kujua hatua saba za kuzingatia wakati unapanga malengo yako. Usisahau ku- Subscribe kwenye Apple Podcast na kuweka Nyota 🌟 5....more12minPlay
January 15, 2022Jinsi Ya Kubadili Mtazamo Hasi Na Kuwa Na Mtazamo Chanya.Mtazamo Chanya ndio kila kitu maishani, bahati mbaya mtazamo hasi ndio hutawala akili zaidi kutokana na sababu mbalimbali kama vile jinsi unavyojitazama, sehemu ambazo unashinda, aina ya marafiki ambao unao, maneno ambayo unajiambia, tabi zako n.k. lakini Podcast hii itakusaidia mbinu sita rahisi za kuwa na mtazamo chanya kwenye maisha yako. Sikiliza Podcast hii kisha Subscribe kwenye platform ambayo unasikiliza....more14minPlay
January 09, 2022Gundua Maajabu Ya Kutumia Kioo Kubadili Maisha Yako.Je unajua kioo kinaweza kubadili maisha yako? Kioo ni zaidi ya kujitazama kwa maana kwamba Kioo kina faida na matumizi mengi zaidi unavyojitazama. Sikiliza episode hii mpaka mwisho ujue maajabu ya kutumia kioo....more14minPlay
January 02, 2022Jinsi Ya Kupanga Bajeti Ya Fedha Zako Kupitia Kanuni Ya 40/30/10/10/10.Hii ni kwa watu wanaotaka kujua Kupanga bajeti ya fedha zao kwa usahihi lakini hawajaanza bado, Sikiliza mpaka mwisho utaweza kupanga bajeti ya fedha zako na Kanuni ya 40/30/10/10/10 ambayo ni rahisi sana. Kazi kwako kusikiliza madini haya kisha fanyia kazi ili mwaka 2022 uwe mwaka wa kufanikiwa wewe kwenye eneo la fedha...more11minPlay
December 26, 2021Jinsi Ya Kutimiza Malengo Yako Ya Mwaka 2022 Kwa Kishindo...Je unataka kutimiza malengo yako? Je unajua namna gani unaweza kutimiza malengo yako...? Usijali Sikiliza Podcast hii mpaka mwisho utaweza kujua ufanye nini Ili utimize malengo yako kwa kishindo mwaka 2022...more16minPlay
FAQs about Maisha Ni Kuthubutu Podcast:How many episodes does Maisha Ni Kuthubutu Podcast have?The podcast currently has 119 episodes available.