Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

By RFI Kiswahili
Download on the App Store

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii episodes

  • Mlipuko wa ugonjwa wa ebola DRC, Emmanuel Macron kutawazwa rasmi rais mpya wa Ufaransa
    Katika makala hii tumeangazia kuapishwa kwa rais mpya wa Ufaransa Emmanuel Macron ambapo katika hotuba yake ameahidi kuwaunganisha wafaransa, lakini pia huko DRCongo kuripotiwa kwa mlipuko wa ugionjwa wa ebola kwenye maeneo ya kaskazini mashariki, nchini Tanzania, Kenya na Somalia. Kimataifa pia imeangaziwa hatua ya rais wa Marekani Donald Trump ya kumfuta kazi mkuu wa shirika la upelelezi la FBI.
    Jiunge na mwandishi wetu Reuben Lukumbuka kusikiliza zaidi.
    22 min
  • Uchaguzi wa duru ya pili nchini Ufaransa, maaskofu DRC wataka Katumbi arejee nchini
    Makala hii imeangazia uchaguzi wa duru ya pili nchini Ufaransa Jumapili ya mei 07 mwaka huu kati ya mgombea mwenye msimamo wa kati Emmanuel Macron na mgombea mwenye msimamo mkali Marine Le Pen, lakini pia wito wa maaskofu wa kanisa katoliki kwa serikali ya DRC mjini Kinshasa wa kumruhusu mwanasiasa wa upinzani Moise Katumbi arejee nyumbani, Wabunge wa chama cha republican nchini Marekani wamepitisha mswada unaoondoa na kubadilisha mpango wa bima ya afya ya obamacare iliyoanzishwa na rais wa zamani Barrack Obama.
    22 min
  • Upinzani nchini Kenya NASA wamtangaza Raila Odinga kuwa mgombea wake,
    Katika makala hii tunaangazia uteuzi wa aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga kama mgombea wa urais katika uchaguzi unaopangwa kufanyika nchini Kenya mwezi agosti mwaka huu, kusainiwa kwa makubaliano maalum kule DRC, kuendelea kwa kampeni ya uchaguzi nchini Ufaransa, lakini pia hukumu ya miaka kumi kutolewa dhidi ya mwanahabari wa Rfi Haussa Ahmed Abba.
    22 min
  • Polisi nchini Ufaransa waimarisha ulinzi kuelekea uchaguzi mkuu aprili 23
    Makala ya mtazamo wako kwa juma hili imeangazia tukio la shambulizi la kigaidi kwenye eneo la champs elysee jijini Paris nchini Ufaransa ambapo mtu mmoja aliwafyeturia risasi polisi na kumuua mmoja kabla ya kuuawa kwake katika majibizano makali ya risasi, tukio ambalo limekuja wakati wananchi wanajiandaa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu siku ya jumapili ya aprili 23 mwaka huu wa 2017, tumegusia pia matukio kutoka mataifa mengine kama DRC, Uganda na kwingineko duniani.
    22 min
  • Polisi wanane wauawa Tanzania, waziri mkuu DRC kuandaa serikali ya mpito, Korea kaskazini tayari kwa Vita na Marekani
    Makala hii imeangazia kutokea kwa mauaji ya polisi 8 pwani ya Tanzania, rais John Magufuli alaani, na waziri mkuu wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Bruno Tshibala akamilisha mikutano na wanasiasa wa pande zote kuelekea uundwaji wa serikali ya mpito, mataifa kumi ya Afrika yamekutana kujadili mpango wa kuundwa jeshi la pamoja. Kimataifa mapigano ya nchini Syria, kampeni za uchaguzi nchini Ufaransa, Korea Kaskazini yasema iko tayari kujibu mashambulizi ya Marekani.
    Ungana na mwandishi wetu Reuben Lukumbuka kusikiliza zaidi.
    22 min
  • Bruno Chibala ateuliwa kuwa waziri mkuu mpya wa DRC, Video ya vijana imbonerakure nchini Burundi yazua masikitiko
    Ni juma ambalo limekuwa na mambo mengi ikiwemo uteuzi wa waziri mkuu mpya wa DRC Bruno Chibala, Rwanda kufikia tamati ya juma la kumbukumbu ya mauaji ya kimbari, na kumalizika kwa mkutano wa kimataifa kuhusu maendeleo ya kibiashara kati ya ufaransa na mataifa ya afrika mashariki, kama Tanzania, lakini pia Marekani kushutumua Syria kuhusu matumizi ya silaha za kemikali.
    Kusikiliza zaidi ungana na mwandishi wetu Reuben Lukumbuka
    22 min
  • Mitazamo tofauti kuhusu sikukuu ya mwanamke duniani, mvutano wa kisiasa katika upinzani wa DRC
    Makala hii imeangazia sikukuu ya mwanamke duniani, changamoto na mafanikio ya mwanamke katika suala la maendeleo ya jamii barani afrika, lakini pia tumegusia mvutano wa kisiasa katika muungano wa vyama vya upinzani wa rassemblement nchini DRCongo, tangu kuteuliwa kwa Felix Tshisekedi kuwa mwenyekiti wa muungano huo, kule Nigeria kurejea nyumbani kwa rais Muhammadu Buhari, wakati kimataifa tumeangazia hatua ya rais Donald Trump wa Marekani kusaini upya sheria kuhusu wahamiaji toka mataifa kadhaa ya kiisilamu.
    20 min
  • Felix Tshisekedi ateuliwa kuwa kiongozi wa Upinzani DRC, muwindaji wa Tanzania ahukumiwa miaka 12 jela
    Makala hii imeangazia hatua ya muungano wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ya kumteua Felix Tshisekedi kuwa kiongozi mpya wa muungano huo, baada ya kifo cha aliyekuwa kiongozi wa muungano huo, Etienne Tshisekedi jijini Brussels, Ubelgiji, pia muwindaji haramu wa pembe za ndovu nchini Tanzania ambaye pia alifahamika kama shetani wa wanyama amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela.lakini pia mgomo wa madaktari nchini Kenya, wakati katika uga wa kimataifa tumegusia siasa za Marekani, Ufaransa na kwingineko duniani.
    22 min
  • Mazungumzo ya amani Burundi mjini Arusha, DRC yajitetea kuhusu uchaguzi, Trump awalaumu wanahabari
    Makala hii imeangazia mazungumzo ya amani ya Burundi kujaribu kuleta pande pinzani katika meza ya mazungumzo ya moja kwa moja, mjini Arusha nchini Tanzania, chini ya mwezeshaji wa usuluhishi, rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa, lakini pia kauli ya serikali ya DRC kusema kwamba haina pesa kuandaa uchaguzi mkuu kuzua hisia tofauti katika ulingo wa kimataifa, na siasa za ukanda huu wa Afrika mashariki,pia Marekani. Ungana na mwandishi wetu Reuben Lukumbuka kupata mengi zaidi.
    22 min

About Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

From the publisher's feed

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea…

More shows like Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

2 Listeners

Gurudumu la Uchumi by RFI Kiswahili

Gurudumu la Uchumi

0 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

1 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Wimbi la Siasa by RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Changu Chako, Chako Changu by RFI Kiswahili

Changu Chako, Chako Changu

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Jukwaa la Michezo by RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

0 Listeners