Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

By RFI Kiswahili
Download on the App Store

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii episodes

  • Kinara wa upinzani nchini DRC afariki dunia, Francois fillon kuwakilisha rasmi chama chake kwenye uchaguzi mkuu
    Makala ya juma hili imeangazia kifo cha mpinzani mkongwe nchini Jamhuri ya Kongo Etienne Tshisekedi wa Mulumba, akiwa na umri wa miaka 84. Umauti ambao ulimfika akiwa kwenye matibabu jijini Brussels Ubelgiji, watu 124 raia wa Burundi kurejeshwa nyumbani kwao kutoka Uvira upande wa DRC,wakati kimataifa, tumegusia uchaguzi wa Ufaransa na mazungumzo ya amani kuhusu Syria.
    Karibu kujiunga na mwandishi Reuben Lukumbuka kupata marefu.....
    21 min
  • Rais Donald Trump aapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani
    Makala hii imeangazia kuapishwa kwa rais Donald Trump kuwa rais wa 45 wa Marekani punde baada ya kuibuka mshindi kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi novemba mwaka wa jana, lakini pia kupatikana kwa mwafaka wa mwanzo kuhusu utekelezwaji wa makubalia no ya desemba 31 mwaka jana huko DRC, na hatua ya rais Yahya Jammey wa Gambia kukubali kuondoka nchini na kupewa hifadhi nchini equatorial Guine.
    22 min
  • Viongozi zaidi ya 40 wakutana katika mkutano wa 27 wa Africa na Ufaransa Bamako nchini Mali
    Makala hii inaangazia mkutano wa 27 wa viongozi zaidi ya 40 ambao wanakutana jumamosi hii kujadili maswala ya usalama na ya kijamii, mkutano ambao unaongozwa na rais wa Ufaransa Francois Hollande katika mji mkuu wa Mali, Bamako. Mkutano huu unafanyika wakati ambapo kuna hali ya wasiwasi nchini humo kufuatia kuwepo kwa makundi kadhaa ya wapiganaji wenye kushirikiana na magaidi katika eneo hilo. Pia tumeangazia hali iliyojiri wiki hii huko Burundi, DRC, Gambia, Rwanda, Uganda na maadhimisho ya miaka 53 ya mapinduzi visiwani Zanzibar, wakati kimataifa kauli ya katibu mkuu mpya wa umoja wa mataifa, Antonio Guterres.
    22 min
  • Wapinzani nchini DRC waendelea kusaini makubaliano ya desemba31
    Makala hii ya mwanzo wa mwaka wa 2017 imeangazia juhudi za kanisa katoliki nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, kuwahamasisha wanasiasa wa upinzani kukubali kusaini makubaliano ya hivi karibuni, na wapinzani wa Kenya kukutana wiki ijayo, lakini pia kuapishwa kwa rais mteule wa Ghana Nana Akuffo Ado jumamosi hii; Wakati, kimataifa hatua ya Urusikuondoa wanajeshi wake Syria, na mvutano kati ya Urusi na Marekani kuhusu uchaguzi uliompa ushindi Donald Trump.
    21 min
  • Mazungumzo ya kisiasa nchini DRC kutamatika leo, Jamhuri day nchini Kenya
    Makala ya mtazamo wako juma hili imeangazia mazungumzo ya kisiasa chini ya usuluhishi wa baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kutamatika baadaye leo huku kukiwa na hali ya wasiwasi, katika miji mikubwa ya nchi hiyo, maadhimisho ya miaka 53 ya uhuru wa Kenya, juhudi za jumuia ya nchini za Afrika magharibi kuutanzua mgogoro wa Gambia mara baada ya uchaguzi, lakini pia kimataifa tumegusia mapigano kule Alepo, nchini Syria.
    21 min
  • Mgomo wa madaktari nchini Kenya, Bernard Caseneuve ateuliwa kuwa waziri mkuu mpya Ufaransa
    Mgomo wa madaktari nchini Kenya, kesi inayomkabili mmoja kati ya viongozi wa kundi la waasi wa uganda wa LRA nchini Uganda, na awamu ya pili ya mazungumzo ya kisiasa nchini DRC, ni miongoni mwa habari zilizopewa uzito katika matangazo yetu juma hili, wakati kimataifa bunge la Korea Kusini kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais Park, lakini pia nchini Ufaransa, waziri wa mambo ya ndani Bernard Caseneuve kuteuliwa kuwa waziri mkuu akimrithi Manuel Valls, aliyetangaza nia ya kuwania kiti cha urais.
    21 min
  • Mauaji ya mjini Kasese Uganda, Shambulio katika Kambi ya Luhanga DRC
    Makala ya wiki hii imeangazia mauaji yaliyofanyika huko Kasese nchini Uganda, na kule DRC katika kambi ya Luhanga, mashariki mwa nchi hiyo, na wanasiasa wa upinzani kusisitiza kuendelea na maandamano ya kumshinikiza rais Joseph Kabila kuondoka madarakani, ushindi wa kiongozi wa upinzani nchini Gambia, wakati kimataifa, tumeangazia habari za kimataifa ikiwemo hatua ya rais wa Ufaransa Francois Hollande kutangaza kutowania urais kwa muhula wa pili mwaka ujao.
    .
    22 min
  • Mjadala wa wagombea wa urais Ufaransa, na kampeni bye bye Kabila kuanza DRC
    Makala hii imeangazia mdahalo wa wagombea wa kiti cha urais Ufaransa na barani Afrika kumefunguliwa mkutano wa nchi zinazozungumza lugha ya kifaransa: francophonie, na nchini DRC umoja wa ulaya kuiomba serikali ya Kinshasa kuandaa mazingira mazuri kufanikisha kufanyika kwa uchaguzi, lakini pia kampeini Bye bye Kabila, na huko Marekani maswali mengi kuanza kujitokeza kuhusu ushindi wa rais mteule wa Marekani Donald Trump
    22 min
  • Hotuba ya rais Kabila wa DRC na kuahirishwa kufungwa kambi ya Dadaab Kenya
    Katika makala hii, tumeangazia DRC hotuba ya rais Joseph Kabila Kabange, uteuzi wa Samy Badibanga kama waziri mkuu wa nchi hiyo, wafadhili wa kimataifa kuahidi $2.2 za kimarekani kwa jamhuri ya Afrika ya kati, kutamatika kwa mkutano wa kimataifa kuhusu mabadikiliko ya tabia nchi, mjini Marakech nchini Morocco, kuahirishwa kufungwa kwa kambi ya Dadaab nchini Kenya, lakini pia katika uga wa kimataifa uchaguzi wa mwakani nchini Ufaransa, na ziara ya rais Barack Obama barani ulaya.
    22 min

About Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

From the publisher's feed

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea…

More shows like Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

2 Listeners

Gurudumu la Uchumi by RFI Kiswahili

Gurudumu la Uchumi

0 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

1 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Wimbi la Siasa by RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Changu Chako, Chako Changu by RFI Kiswahili

Changu Chako, Chako Changu

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Jukwaa la Michezo by RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

0 Listeners