Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

By RFI Kiswahili
Download on the App Store

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii episodes

  • Matukio makubwa yalitokea duniani wiki hii
    Tumekuandalia mkusanyiko wa matukio makubwa yaliyojiri duniani wiki hii, kuanzia barani Afrika na maeneo mengine duniani.Ikiwa ni pamoja na hali ya kisiasa na usalama nchini DRC na Tanzania lakini pia Mkutano wa Maendeleo kati ya Japan na Mataifa ya Afrika bila kusahau tetemeko la ardhi nchini Italia.
    22 min
  • Serikali ya DRC yajiapiza kutokomeza ADF wilayani Beni
    Makala ya mtazamo wako kwa yaliyojiri wiki hii imeangazia mauaji ya watu zaidi ya hamsini katika kata ya rwangoma mjini Beni DRC na mikakati ya serikali katika kuwatokomeza waasi wa Uganda wa ADF wanaodaiwa kuhusika na mauaji hayo, na tume ya umoja wa mataifa, Monusco imemsafirisha kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini Riek Machar hadi DRCongo kabla ya kuelekea Ethiopia, pia tumeangazia siasa za Burundi, Kenya, na Tanzania.Kimataifa tumetupia jicho ziara ya rais wa Urusi Vladmir Putin huko Crimea jimbo lililojitenga na Ukraine.
    Kusikiliza zaidi, ungana na mwandishi wetu Reuben Lukumbuka Ben Saleim.
    23 min
  • Matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Zambia kuanza kutolewa
    Makala ya mtazamo wako kwa yaliyojiri wiki hii, yameangazia uchaguzi mkuu uliofanyika hivi majuzi nchini Zambia, ambapo matokeo yake ya awali yameonyesha upinzani kuongoza, wakati nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC mvutano wa kisisa kuelekea uchaguzi ambao hadi sasa hatima yake iko mashakani, siasa za kenya, Tanzania na Sudan Kusini, pia zimeangaziwa na kampeini za wagombea wa kiti cha urais nchini Marekani.
    Ungana na mwandishi wetu Reuben Lukumbuka kusikiliza zaidi.
    22 min
  • Ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa nchini Tanzania na Kenya na manufaa yake
    Makala haya yameangazia ziara ya Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault nchini Kenya na Tanzania, ziara inayolenga kuimarisha uhusiano kidiplomasia kati ya Ufaransa na nchi hizi mbili za Afrika Mashariki.Juma hili mataifa ya DRC na Uganda yamekubaliana kuhusu kuimarisha usalama wa eneo la mashariki mwa DRCongo ambako waasi wa Uganda wa ADF wamekuwa wakishutumiwa kuzorotesha usalama wilayani Beni, lakini pia tumeangazia Burundi kutupilia mbali mpango wa kupelekwa kikosi cha walinda wa UN wakati katika uga wa kimataifa tumegusia hali ya siasa za Marekani, inavyoendelea kabla ya uchaguzi mkuu nchini humo.
    21 min
  • Mazungumzo ya kitaifa kuhusu DRC kuahirishwa
    Makala ya mtazamo wako kwa yaliyojiri juma hili, imeangazia siasa inayoendelea nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, wakati huu nchi hiyo ikijiandaa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, ambapo wananchi nchini humo wameshuhudia kurejea nyumbani kwa mpinzani mkongwe nchini humo Etienne Tshisekedi, na mikutano ya kisiasa.lakini pia kuteketezwa moto kwa mashule kadhaa nchini Kenya, na azimio mpya la baraza la umoja wa mataifa kuhusu Burundi, wakati kimataifa tumegusia siasa za Marekani.
    Ungana na mwandishi wetu Reuben Lukumbuka kusikiliza zaidi.
    22 min
  • Mgororo wa Sudan Kusini kuwa na sura mpya
    Makala ya mtazamo wako kwa yaliyojiri wiki hii imejikita kuangazia mgogoro wa kisiasa unaolikumba taifa changa la Sudan Kusini, wakati huko DRC, vyama vya kisiasa vinavyomuunga mkono rais Joseph Kabila kuwa na mkutano maalum mwishoni mwa mwezi huu, na nchini Burundi mfumuko wa bei za bidhaa mbali mbali kuwaathiri wakaazi wa nchi jirani na wananchi wenyewe wa Burundi.Katika uga wa kimataifa tunaangazia bilionea wa Marekani Donald Trump kuteuliwa kuwa mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Republican.
    22 min
  • Viongozi wa AU kujadili Sudan Kusini leo
    Mtazamo wako kwa yaliyojiri juma hili imeangazia mashambulizi ya kigaidi yaliyotekelezwa mjini Nice ambapo gaidi aliendesha lori lake kuelekea umati wa watu  wakati wakisherehekea siku ya kitaifa ya mapinduzi, huku kukirushwa fataki Alhamisi usiku.Tumeangazia pia mkutano wa viongozi wa mataifa ya Umoja wa Afrika AU, leo mjini Kigali nchini Rwanda, kujadili juu ya mgogoro wa Sudan Kusini, na huko DRC Mkuu wa tume ya Umoja wa mataifa Monusco kuelezea kuridhika kwake na maandalizi ya mjadili wa kitaifa unaotazamiwa kufanyika Kinshasa mwishoni mwa mwezi huu wa Julai 2016.
    22 min
  • Mawakili nchini Kenya wagoma kulaani mauaji ya mwenzao
    Makala ya Mtazamo wako kwa yaliyojiri wiki hii imeangazia mgomo wa Mawakili nchini Kenya kulaani mauaji ya mwenzao Willie Kimano na wengine, huku wakiomba serikali kuhakikisha wahusika wa mauaji hayo wanapatikana, lakini pia maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka mitano ya uhuru wa Sudan Kusini huku kukiwa na mapigano makali kati ya wanajeshi wa serikali na wale waliokuwa waasi, wakati kimataifa tunaangazia mauaji ya watu weusi nchini Marekani.
    22 min
  • Raia wa DRC Kuomboleza kifo cha Malu Malu
    Ziara ya siku mbili ya rais Paul Kagame wa Rwanda nchini Tanzania, maadhimisho ya  kumbukumbu ya miaka 56 ya uhuru wa DRC pamoja na kanisa katoliki nchini humo kutangaza kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi CENI Padre Apolinaire Malumalu alhamisi juni 30 na pia mashambulizi ya kigaidi Mjini Istanbul nchini Uturuki ni miongoni mwa mengi utakayoyasikia katika makala: Mtazamo wako kwa yaliyojiri Wiki hii.
    22 min
  • Uingereza kuuvua uanachama kwenye Umoja wa ulaya
    Katika makala hii tumeangazia kura ya maoni iliyopigwa na raia wa Uingereza ambapo asilimia 52 ya waingereza wamepiga kura ya kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya, lakini pia barani afrika tumeangazia yaliyojiri nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kuhusu Marekani kuzuia mali za afisa wa polisi nchini humo, jenerali celestin Kanyama wakati nchini Tanzania rais John Pombe Magufuli wiki hii, alitoa wito kwa wanasiasa wa upinzani kushirikiana naye kuwatumikia wananchi na kuacha kupiga siasa badala ya kuwatumiakia wananchi.
    .
    22 min

About Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

From the publisher's feed

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea…

More shows like Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

2 Listeners

Gurudumu la Uchumi by RFI Kiswahili

Gurudumu la Uchumi

0 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

1 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Wimbi la Siasa by RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Changu Chako, Chako Changu by RFI Kiswahili

Changu Chako, Chako Changu

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Jukwaa la Michezo by RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

0 Listeners