Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

By RFI Kiswahili
Download on the App Store

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii episodes

  • Ushindi wa D.Trump nchini Marekani, Ujumbe wa UN kutembelea DRC
    Sehemu kubwa ya makala hii imeangazia uchaguzi wa rais wa Marekani ambapo Donald J.Trump ameibuka mshindi na kuwa rais wa 45 wa nchi hiyo, pia tumeangazia hatua ya shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) kutoa wito kwa wajumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa ambao wameanza ziara yao ya siku tatu nchini DRCongo kukemea "ukandamizaji wa kisiasa".
    Karibu kujiunga na mwandishi Reuben Lukumbuka.
    21 min
  • Mjumbe wa umoja wa mataifa kuhusu maziwa makuu atembelea DRC
    Makala hii imeangazia maadhimisho ya miaka mitatu tangu kuuawa kwa waandishi wa habari wawili wa RFI Ghislain Dupont na Claude Verlon mjini Kidal kaskazini mwa Mali, hali ya kisiasa inayojiri kwa sasa nchini DRCongo kuelekea uchaguzi mkuu, mashirika ya kiraia nchini Kenya kuitisha maandamano, rais wa Tanzania kusimamia mkutano wa wahariri katika muktadha wa kutimiza mwaka mmoja ya utawala wake na mengineyo.
    22 min
  • Viongozi wa kanda ya maziwa makuu wataka vikosi zaidi DRC
    Makala ya yaliyojiri juma hili imeangazia hatua ya marais wa nchi za maziwa makuu na SADC kuomba wanajeshi zaidi wa umoja wa mataifa wapelekwe nchini DRC, ziara ya waziri mkuu wa Ufaransa katika mataifa ya Afrika magharibi lakini pia, Gambia kujiondoa wanachama wake kwenye mahakama ya ICC, nchini Tanzania na kwingineko duniani, haswa kampeini ya uchaguzi mkuu nchini Marekani inavyoendelea.
    21 min
  • Makubaliano kuhusu uchaguzi DRC, ziara ya mfalme wa Morocco nchini Rwanda
    Makala ya mtazamo wako kwa yaliyojiri juma hili imeangazia makubaliano ya kisiasa yaliyofikiwa kati ya wajumbe wa serikali ya DRC na wapinzani walioshiriki mwazungumzo chini ya mpatanishi wa umoja wa Afrika Edem Kojo, huku kukiwa mitazamo tofauti kutoka kwa wadau wa kitaifa na wa kimataifa, lakini pia makala imeangazia ziara ya mfalme mohammed wa VI wa Morocco katika mataifa ya Afrika mashariki kuanzia nchini Rwanda.Siasa za Marekani kuelekea uchaguzi novemba 8, na mapigano huko Iraq.
    22 min
  • Mjumbe wa umoja wa mataifa kutumwa Burundi wiki ijayo
    Makala hii ya yaliyojiri juma hili imeangazia hatua ya wabunge nchini Burundi kuridhia mpango wa serikali wa kujiondoa kama mwanachama wa mahakama ya kimataifa ya  ICC, na siasa zinazoendelea nchini Jamhuri ya kidemokrasia umoja wa mataifa ukielezea wasiwasi wake kuhusu mustakabali wa taifa hilo, na katika uga wa kimataifa, mbali na maandalizi ya uchaguzi nchini Marekani, makala hii pia imeangazia mdahalo wa kwanza wa wagombea wa kiti cha rais nchini Ufaransa.
    22 min
  • Tanzania na DRCongo kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na usalama
    Makala hii imeangazia ziara ya rais joseph Kabila nchini Tanzania ambapo kiongozi hguyo pamoja na mwenyeji wake wa Tanzania John pombe Magufuli wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kibiashara lakini pia wa kiusalama kati ya mataifa hayo mawili, , ziara ya maafisa wa umoja wa mataifa wanaoshughulikia haki za binadamu, wakati katika uga wa kimataifa uhusiano kati ya Urusi na Marekani kuendelea kuwa mashakani.
    22 min
  • Sintofahamu ya kiuongozi ndani ya chama cha upinzani cha CUF Tanzania
    Hali ya sintofahamu ya kiuongozi ndani ya chama cha upinzani cha CUF cha nchini Tanzania na Zanzibar, Marekani kuwawekea vikwazo magenerali wawili huko jamhuri ya kidemokrasia ya Congo: John Numbi, na Tango Four, kuapishwa kwa rais Ali Bongo Ondimba pamoja na mdahalo wa wagombea wawili katika uchaguzi unaotazamiwa kufanyika mwezi ujao nchini Marekani, ni miongoni mwa mengi yaliyoangaziwa juma hili hapa Rfi Kiswahili. Ungana na mwandishi wetu Martha Saranga kusikiliza zaidi.
    21 min
  • Mazungumzo ya kisiasa kutamatika jumamosi hii DRC
    Makala hii imeangazia kuhusu mazungumzo ya kitaifa ya nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kutamatika jumamosi hii mjini Kinshasa huku matarajio ya wananchi kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwaka huu kwa mujibu wa katiba kuingia mashakani, baada ya pande zote kushindwa kuafikiana, kuachiliwa huru kwa madereva wa kutoka Tanzania na Kenya mashariki mwa DRC, pia mapigano mapya ya Sudan Kusini, siasa za Marekani na Syria zimetamatisha makala hii.
    22 min
  • Kilichotokea duniani wiki hii
    Wiki hii, mengi yametokea kutoka barani Afrika hasa nchini Gabon ambako kunashuhudiwa mvutano wa kisiasa baada ya Ali Bongo kutangazwa mshindi, matokeo ambayo yamepingwa vikali na mpinzani wake Jean Ping.
    Nchini DRC Mazungumzo ya kisiasa yameanza.Tunachambua haya kwa kina na kukumbusha mambo yalivyojiri kutoka kona mbalimbali za dunia.
    22 min

About Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

From the publisher's feed

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea…

More shows like Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

2 Listeners

Gurudumu la Uchumi by RFI Kiswahili

Gurudumu la Uchumi

0 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

1 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Wimbi la Siasa by RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Changu Chako, Chako Changu by RFI Kiswahili

Changu Chako, Chako Changu

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Jukwaa la Michezo by RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

0 Listeners