Watu wengi wamekuwa wakitafuta kuombewa badala ya kutafuta hekima ya Mungu ama mkakati wa Mungu wa kuwatoa hapo walipo, tunaona mfano mzuri ni maisha ya Musa, Musa kila wakati alikuwa na tabia ya kwenda katika hema ya kukutania kumuuliza Mungu kuhusiana na jambo lililokuwa likimkabiri, Daudi pia alikuwa na tabia inayofanana na ya Musa, na walipoenda mbele za Bwana, Bwana aliwapa maelekezo na walipochukua hatua sawasawa na maelekezo ya Bwana walipata matokeo, leo hii Mwalimu Huruma Gadi anafundisha kama wewe una madeni ama umefika mahali umekwama kiuchumi hatua ya kwanza ni tafuta kujua Mungu anasema nini kuhusu madeni yako ama hali yako. Kisha utakaposikia hicho alichokisema chukua hatua ya kushirikiana na hicho ambacho amekuelekeza. Tusikilize somo.