"Alitoa wengine kuwa Mitume, na wengine kuwa manabii, na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke..." - Waefeso 4: 11-12 Ulipopelekwa mahali kwenye mwili wa Kristo unatarajiwa ushiriki katika kujenga mwili wa Kristo, haitoshi tu kukaa na kujifunza, Je wewe unashiriki vipi katika kusababisha maono yaliyoko katika hilo kanisa ama huduma yanatimia? Ungana na Mwalimu Huruma Gadi katika somo hili.