Salama Na

Salama Na

Download on the App Store

Salama Na episodes

  • Ep. 3 - Salama Na Jokate | KAMISHNA

    Maana halisi ya ’nyota njema huonekana alfajiri’, najua sikuwepo hiyo ‘alfajiri’ wakati Mh Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe anazaliwa lakini hakika nilikuwepo wakati anamaliza wa pili kwenye mashindano ya Miss Tanzania mwaka 2006. Nilikuwepo pia kushuhudia jinsi alivyokua anapangua mikuki na mishale iliyokua inarushwa upande wake kwa zaidi ya miaka kumi na mitatu kabla hajapata cheo alichonacho sasa.


    Jokate amekua muerevu toka siku ya kwanza na kwa mazungumzo haya nilifanya naye bila ya shaka yatakupa mwangaza zaidi juu ya haya niyasemayo. Focus alokua naweka kwenye kila afanyalo ni funzo tosha kwetu sote na maana halisi hasa ya adui wa ndoto zako ni kupotea njia na kusahau nia na madhumuni ya mambo yako ulojiwekea kuyakamilisha.

    Ni msomi, mrembo, mwenye huruma, mwenye kumjua Mungu, mwenye connection zake, mwenye kutafuta na asichoke na mwenye akili zake timamu haswa. Kama rafiki, nikaona nisiwe mchoyo na kwa ruhusa yake ambayo tuliifuata Kisarawe tumeweza kukaa nae mezani na kuzungumza juu ya siku ya kwanza alipopata tarifa ya kwamba ameteuliwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, usomi ndani ya familia yao, kwenda chuoni baada ya kugombea taji la urembo wa Miss Tanzania, jinsi anavyopambana kuijenga Kisarawe na kumbukumbu zake za utotoni.

    Please Enjoy.

    Love,
    Salama.

    1 hr 9 min
  • Ep. 2 - Salama Na Marco Chali | DOKTA

    DOKTA

    Marco na mimi tumekua marafiki wa miaka mingi na moja kati ya vitu vimetufanya tuwe marafiki ni kufanana kwetu kwa kupenda vitu vya aina moja. Kuanzia teknolojia mpaka muziki, nakumbuka siku ya kwanza kukutana naye, ilikua ni uzinduzi wa kipindi cha Bongo Star Search ambao ulifanyika Much More pale juu, alinifuata akaniambia juu ya mapenzi yake ya kipindi changu cha Planet Bongo enzi hizo na baada ya hapo ikawa ni urafiki ulodumu mpaka leo. Kipindi changu cha Mkasi kilizaliwa kwenye kibaraza cha studio kwa Marco Chali pale MJ RECORDS ambako ilikua ni maskani yetu kubwa mimi na AY.

    Marco anajua KILA KITU, kuanzia kuendesha baskeli, kutengeneza mabiti, kuandika, kuimba, kuogelea,kucheza basketball kupambana na maisha na ni mwingi wa Imani pia. Amekua akijinyima karibu kila siku ilimradi watu anaowapenda wapate chochote, zaidi kwa familia yake. Katika watu ambao naweza kuwapigia simu nikawaambia sina kitu Marco ni mmoja wapo na anaweza akawa nae ni vivo hiyo ila akanipa mimi na yeye akaenda kutafuta nyengine.

    Mwaka jana rafiki yangu Mwenyezi Mungu alimbariki mtoto wake wa kwanza, binti, anaitwa Yoy, tabasamu ambalo rafiki yangu analo sikuwahi kuliona likiwa endelevu kama ambavyo toka Yoy amekuja duniani… Mwenyezi Mungu amlindie na amkuzie kwenye misingi iliyo bora na afya njema.

    Kwenye kikao chetu hiki ingekua inawezekana tungeweza kuongea hata masaa 24, yeah, story zetu zinaweza kufika huko, na siku nyengine tunaweza hata tusiongee kabisa, ikawa mikausho mikali tu ila humu tulipata wasaa wa kumuongelea Yoy, muziki, career yake, Mwenyezi Mungu, Godzilla, mawazo na discipline. Yangu matumaini utapata kadhaa ya kujifunza na kukusogeza.

    Love,
    Salama.

    1 hr 4 min
  • Ep. 1 - Salama Na Lil Ommy | AIR TABORA

    2016 ndo mwaka nilikutana na Lil Ommy mara ya kwanza, pengine nilishawahi kukutana naye huko nyumba ila sikumbuki. Aliniomba niende kwenye kipindi chake cha The Playlist enzi hizo kikiwa Jumamosi asubuhi ya tarehe 20 mwezi wa nane. Sikuwahi kupenda kufanyiwa interview ila siku hiyo nilimpa Ommy nafasi, sikuwahi kujutia na pengine hiyo ndo sababu ya kumfanya yeye awe mgeni nambari moja kwenye Podcast hii. Anayejitambua, anayejituma, anayesoma, mwenye nia na mipango endelevu… Nilimuomba aje na hapa tulizungumza karibia yote. Ya kwao Tabora, familia yao, marehemu Mzee wake, marehemu Dada yake, ndugu zake wa kambo, utundu wa udogoni, kutafuta kazi, maisha ya mjini na marafiki, muziki wa kizazi kipya na ushindani wa kazi. Times FM na siku ya harusi yake. Na hakua mchoyo wa kunikhadithia. Hii ni kwa ajili yako, na nyengine nyingi zijazo zinakuhusu pia. Chukua baadhi ya kurasa kwenye kitabu cha AIR TABORA na tumia baadhi ya aliyoyoyasema kuboresha kitabu chako maana nami nafanya hivyo. Enjoy. Love, Salama.

    1 hr 8 min

About Salama Na

From the publisher's feed

‘Salama na’ – meaning ‘Salama and’ is a one hour Podcast chat show hosted by a re known Radio &; TV personality Salama Jabir and available on Both Video and Audio of Various Platforms. In Salama…