Salama Na

Salama Na

Download on the App Store

Salama Na episodes

  • Ep. 23 - Salama Na Nizar | RAHA LEO KUCHELE
    Wakati Vancouver White Caps wanamtaka Nizar Khalfan baada ya kumuona akiwa anakipiga hapa nyumbani wakati yuko na timu ya Taifa ya Tanzania haikua habari au jambo la kushangaza miungoni mwa wachezaji na walokua wakimuona na kumfahamu mchezaji huyo vizuri. Kila mtu kati ya hao alikua akiomba ki vyake kijana huyu kutoka Kusini mwa Tanzania apate nafasi ya kwenda kuwakilisha Taifa na kuendeleza kipaji chake maridhawa kabisa.
    Nizar ametokea Mtwara na kwenye familia yake kwa mujibu wa maongezi yetu Mzee wake alikua akiupiga ingawa si mwingi kama wa Master Chef Khalfan maana yeye alianza akiwa mduchu haswa, watu wazima wa mtaani walikua wakimuamini na kumpa namba kwenye karibia kila mchezo. Habari hii haikupokelewa vyema na Mzee wake ambaye alipiga STOP nyendo hizo za mwanaye kitu kilocho sababisha wazee wa mtaa wajipange na kuandamana kwenda kwa Baba yake Nizar kumuombea ruhusa midfielder maestro aachiwe na kwenda kutoa burudani. Kama ilivyokua kwa mzazi yoyote, uzito kwenye maisha ya Nizar ulikua ni elimu zaidi na hapo ndipo Baba yake alipotaka mwanaye apakazie sana.
    Haikuchukua muda Nizar kuonekana na team nyengine na pia kuitwa kwenye team ya Taifa ya vijana ambako kipaji chake kiling’ara kama mwezi ulotimia. Akatoka team moja kwenda nyengine mpaka safari ya Canada ilipoiva! Haikua rahisi pia kama unavyodhani maana masuala ya visa zaidi ndo yalionekana kuchukua muda mpaka kama Nizar alikata tamaa hivi ila Mungu ni mwema, mzigo ukatoka na safari ya Vancouver ikaanza.
    Maongezi haya zaidi ni kuhusu huko Canada, mpaka akarudi na kuanzia Yanga ingawa chaguo la kwanza lilikua Simba ila watu walizidiana kete na ujanja na mwisho wa siku kiungo huyo wa kimataifa wa Tanzania aliishia Jangwani kwa miaka kadhaa kabla hajahamia Singida.
    Mimi nilitaka kujua zaidi hiyo safari na kipi haswa kilimfanya achague Yanga (hii ni personal kidogo ) na challenges alizowahi kupata akiwa ugenini. Maisha baada kurudi nyumbani, mustakabali wa watu kuitwa ‘wazee’ wakati bado umri wao unaruhusu kukipiga daraja la juu na maisha yake kama yeye. Mwaka huu Nizar alimpoteza mke wake (Mwenyezi Mungu Amlaze
    Mahali Pema Peponi) baada ya kuugua si kwa muda mrefu. Nizar atatuelezea kilichotokea, na vile vile kuna challenges kama binadamu wa kawaida alizipitia. Haikua rahisi sana kuongelea kila kitu ila ilikua vyema sana kuongea nae na kujua pia plans zake za mbeleni. Yangu matumaini utaelewa na kujifunza jambo!
    Love,
    Salama.
    Follow:
    Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown
    Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown
    Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown
    1 hr 26 min
  • Ep. 22 - Salama Na Isaya | KOMAA NAO

    Mimi na Isaya mara ya kwanza tumekutana kwenye set wakati tunatengeneza episode hii ya 22 lakini kabla ya hapo ilikua ni kufahamiana tu kule kwa social media na respect kwa kila mmoja wetu kwa kile ambacho mwenzake anakifanya. Kwahiyo mkutano wetu wa kwanza ulikua ndo wa kwanza kabisa na haikua ngumu kuanzisha maongezi kati yetu.

    Wakati nishamseti ili aje kwenye meza pia niliwauliza wenzangu tunaofanya hii kazi pamoja, kila mmoja apendekeze jina au majina ya watu ambao wangependa waje kwenye kipindi na kila jina liwe na sababu ya kwanini tumpe nafasi huyo mtu. Basi jina lake pia lilikua ni muongoni mwa majina yaliyotajwa. Unaweza ukaelewa mpaka hapo juu ya impact ya shughuli anazozifanya.

    Kama Isaya asingeelezea khadithi ya maisha yake toka utotoni basi hata kwa miaka 100 nisingeweza kudhania alipita kwenye mitihani na mazingira magumu toka akiwa mtoto. Wengi wetu tuna historia za makuaji yetu ila ya mwenzetu huyu ina ujasiri na masikitiko mengi yatakayokutaka uhakikishe mwanao hatokaa akue kwenye mazingira hayo. Elimu kuipata ilikua kwa mbinde, kuwaona Baba na Mama yake ilikua mtihani, kuishi kwenye ahadi zilikokua hazitimizwi na mpaka kufikia kuwa machinga akiwa mtoto kwenye mitaa ya katikati ya Jiji la Mwanza. Ila ukimuona leo hii alivyopendeza na suti yake pengine ya Mtani Nyamakababi utamjua? Kiatu chake kinanga’aa na tabasamu na kujiamini kunamfanya afunge madili ya mamilioni ya dola kwenye project zake mbali mbali. Huwezi ukaamini ndo yeye aliyekua anaenda kuchota maji mtoni kwa baiskeli siku nzima wakati nduguze wanaenda shuleni!

    Isaya alipambana, jarida la Forbes Africa lilimtaja kama ni moja kati ya vijana 30 walio chini ya umri wa miaka 30 ambao watakuja kuleta mabadiliko makubwa kwenye upande wa teknolojia na mpaka sasa yuko njia sahihi ya kulitimiza hilo kwa mujibu wa maongezi yetu haya. Isaya ametimiza miaka 30 mwezi wa kumi mwaka jana.

    Ukiachana na kigugumizi kikubwa ambacho naamini pia kilichangiwa na hasira nyingi alizokua nazo wakati mdogo na kukua nazo, Isaya ni muongeaji na natumai kwenye hilo utapata jambo la kujifunza na ku enjoy pia.

    Love,

    Salama.


    Follow:

    Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown

    Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown

    Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown

    55 min
  • Ep. 21 - Salama Na Baraka | FAHARI TOKA ITETE

    Mimi ni kama wewe tu juu ya ufahamu wa huyu mtu ambaye ameibeba Itete iliyopo kata ya Isuto tarafa ya Isangati, wilaya ya Mbeya vijijini mkoani Mbeya na Tanzania kwa ujumla, jina ni Baraka Adson Mpenja.

    Wengi humuita sauti ya radi, utamshi wake wa maneno na majina ya wachezaji na viongozi ni wa namna ya kipekee haswa, na bila ya shaka hiyo ndo tofauti kuuubwa kabisa kati yake yeye na watangazaji wengine wa kabumbu ikiwa pamoja na mimi hapa Tanzania. Ni kijana na ni maridadi na pia hajasahau wapi ametoka na ndoto zake ndo hizi ananoziishi sasa kwa mujibu wa maongezi yetu haya.

    Umaarufu wake si wa kulazimisha wala si wa skendo, kazi yake maridadi aifanyayo kwa ustadi wa hali ya juu ndo imemtambulisha kwetu hapa nyumbani na kanda nyengine za Afrika ambapo king’amuzi cha Azam kinafika. Burudani ambayo anaitoa huku akipeperusha umaarufu wa ligi kuu ya Tanzania bara na mashindano ya kimataifa ni ya mfano wa kuufuata hasa. Yangu hakika katika sajili bora ambazo AzamTV walishawahi kufanya basi ya Baraka Adson Mpenja inaweza ikawa ya kuokota dodo chini ya Mvinje.

    Basi umaridadi wake huo ndo ulotusukuma haswa sisi kumuita kwenye meza yetu, na akaja bila ya kusita. Tuliongea kuhusu chimbuko lake, ndoto zake jinsi anavyojifunza kila siku kutoka kwa wazoefu walomzunguka, masomo, ndoa, maisha kwa ujumla na mapenzi yake kwa mpira wa miguu. Ilikua matani na ung’amuzi mwingi wakati naongea naye na yangu matumaini uta enjoy.

    Love,

    Salama.


    Follow:

    Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown

    Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown

    Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown

    1 hr 30 min
  • Ep. 20 - Salama Na Lord Eyes | HAWATUWEZI

    Isaac ndo jinsi jina lake linavyoandikwa, kipaji adhimu kabisa kutoka Kaskazini mwa Tanzania, Allah kamjaalia kila ambalo msanii anaomba abarikiwe nalo wakati anapewa kipaji. Mrefu, muonekano mzuri, mashairi ya kibabe na kujiamini kulikokaa sehemu yake haswa.

    Walipoanza kama kundi hapo ndo attention yangu waliipata wana Nako 2 Nako Soldiers kutoka Ara, kila kitu kilikua tofauti juu yao, mavazi, style, matamshi na hata muonekano. Hii ilikua chachu ya kuwafikisha popote ambapo walikua wamepalenga. Mashabiki kila kona ya Tanzania na Afrika na dunia kwa ujumla, hakuna radio utakayoskilizia ambayo walikua hawapati nafasi. Walikua marafiki wa kila kituo na kazi yao waliifanya vizuri haswa.

    Nia ya mazungumzo haya ilikua ni ku catch up na rafiki yangu Isaac aka Lord Eyes aka Lodii. Kiasi cha heshima nilichokua nacho juu yake ni cha hali ya juu, uwezo wake wa kufanya kazi aliyopewa kipaji na Jalali ni wa kipekee. So nini kilienda kombo haswa kwa baadhi ya wanachama katika kundi lake na kwake yeye binafsi? Niamini haikua kazi rahisi kuweza kupata ujasiri wa kutaka kuyajua yote. Ni ngumu wakati mwingi kumuuliza mtu kuhusu struggle zake ambazo bado anapigana nazo na hii haijalishi hata kama mmezoeana kiasi gani.

    Lodii alikua hana cha kujificha, hana kinyongo wala hana kisasi na mtu yoyote, kubwa analolifanya ni kuwa bora one day at a time na kuelekea kwenye sehemu salama anayotaka kufika. So nini haswa kilitokea kwa Wanako? Na yeye alijikutaje kazama kwenye dimwi na madawa na maisha ambayo alikua hayataki? Siku ya kwanza kuonja ilikua lini? Na je ni lini alikua ana tatizo na akaanza kulifanyia kazi? Wazazi wake? Ana mtoto au watoto? Ni mapenzi yakimfikisha huko? Au marafiki? Au maisha? Na pia aliwezaje kutoka huko? Lini aliona haswa kama imetosha na basi aanze kujikomboa?

    Kusema za ukweli story ni ndefu ila tulipata wa kutusimulia na yangu matumaini kuna mambo mawili matatu utajifunza juu ya maisha, umaarufu, marafiki na maamuzi ambayo unaweza ukafanya. Tafadhali enjoy.

    Love,

    Salama


    Follow: 

    Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown

    Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown

    Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown

    54 min
  • Ep. 19 - Salama Na Monalisa | MASHHURA

    Kabla sijasema jinsi ambavyo nampenda na kumheshimu mgeni wetu wa wiki hii napenda kusema cha kwanza ambacho nilikipenda kwake kwanza ilikua jina lake, Ms Yvonne Cherrie kisha Monalisa. Rafiki mzuri, mstaarabu na mtu mwema sana.

    Mona pia ana bahati sana, bahati ya kuwa na Mama ambaye ni hodari na mcheshi ambaye nae alifanya kazi yake ya kuhakikisha bintiye kwanza anafanya yote anayostahili kufanya kama mtoto kabla haja mshika mwanaye mkono na kumtambulisha kwenye dunia ya sanaa ambayo ilitufanya tumtambue na kumpenda pia na pia kuwakubali zaidi kama Mama na mtoto ambao ni mahodari sana.

    Kwenye kikao chetu hiki ambacho kilifanyika wakati Corona imependa moto na ndani ya mwezi Mtukufu wa Ramadhan Mona hakutusumbua kabisa, alitaka tu kupata uhakika wa usalama eneo la tukio na alikua pale on time kabisa, na pengine sisi inawezekana tulimsumbua kwa kutopokea simu kwa wakati.

    Mimi na Monalisa tunajuana kitambo kiasi so mazungumzo yetu yalianzia siku zile tulipokua tunaonana karibia kila siku, enzi za utoto wetu. Yeye alikua msanii hodari lakini pia alikua mmoja ya watangazaji mahiri kabisa wa Radio One na hata ITV. Enzi za kuwa ukurasa wa mbele wa magazeti ya udaku karibia kila Ijumaa na Jumatatu. Tulianzia hapo. Sote tunajua alipitia mambo meeeengi sana maskini ya Mungu, kuanzia maisha hayo ya umaarufu wa kuuza gazeti, mahusiano yake na Marehemu Meddy Mpakanjia na Amina Chifupa. Sanaa yake ya awali, ndoa yake na Marehemu George Tyson. Watoto wake, mahusiano yake na Mama yake, elimu, kazi na Sanaa kwa ujumla.

    Nilikua na wakati mzuri sana wakati tunarekodi hii na yangu matumaini pia uta enjoy.

    Love,

    Salama.

    Follow:

    Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown

    Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown

    Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown

    1 hr 1 min
  • Ep. 18 - Salama Na Madee | MPAKA MISHALE

    Mara zote ukiwaza Manzese kama wewe ni mpenzi wa Bongo Flava basi utawaza Madee tu. Waliosema au alipojiita Rais wa kule sidhani kama kulikua na upinzani wowote, najua kulikua na mtu mwengine ambae alikua anataka hiyo title ila tayari ilikua na mwenyewe ambaye inamkaa haswa.

    Busara zake za miaka ya karibuni na haswa niseme zaidi mwaka huu ni moja ya vitu vilinivutia kutaka kuongea nae. Maana si mara nyingi kwa kijana ambaye amekulia maisha ya ‘ki gangster’ kuwaza watu wengine au hata kuonyesha kuguswa na kitu flani. Ili mtu afikie kufikiria suala la umri kwenda na kuanza kujijengea kwenye maisha ya baadae siku Muumba atakapotuita ni jambo ambalo tunatakiwa kujifunza kutoka kwake. Na pia ni moja ya idea maridhawa nimeskia mwaka huu. Na kubwa kabisa ni kuwa mimi na yeye hatukuwahi kuwa na maongezi ya aina hii, wakati muafaka kabisa...

    Seneda yeye haswa alizaliwa wapi? Ametokea kwenye familia ya mziki? Wazazi wake ni watu wa aina gani haswa? Kule Manzese ndo kwao? Au ilikua maskani tu? Na kama si hivyo aliwezaje kujikita mpaka akawa rais? Suala la elimu je? Wakati anakua kuna makashkashi yoyote alipitia? Na muziki? Na Babu Tale? Na Abdu Bonge aliwatoa wapi? Na TipTop Connection nayo chimbuko lake ni wapi?

    Niliongea naye kuhusu hayo na kuwa ‘chawa’ ili yake yamuendee kwenye suala zima la kujijengea empire yake... Muziki umemfanyia nini? Kama Baba ni kitu gani ambacho watoto wake wanapenda kuhusu yeye? Yuko na hao Mama za watoto wake? Ki ukweli kuna mengi tumezungumza naye lejendari huyu wa Bongo Flava ikiwa pia pamoja na wimbo wa ‘Pombe Yangu’ ambao nao pia una story yake ya kipekee.

    Yangu matumaini uta enjoy kama nilivyo enjoy mimi na wenzangu wakati tuna film hii.

    Love,

    Salama.../

    Follow:

    Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown

    Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown

    Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown

    1 hr 9 min
  • Ep. 17 - Salama Na Shikana | DYNAMITE

    Mi na rafiki yanyu huyu tumepishana zaidi ya miaka kumi na nne, wakati anazaliwa mimi nilikua nagombana na makondakta kupata nafasi kwenye chai maharagwe ya kutoka Buguruni kuelekea Posta. Ila kupishana kwetu kwa umri naamini ndo kunaufanya ushoga wetu uwe special zaidi, maana yeye akiwa ananikhadithia kinachokiki kwenye umri wake, nami nakua namuelezea challenges za unapozidi kukua na naamini hii inatufanya tuwe bora zaidi. Na ki ukweli mara nyingi yeye amekua shujaa wangu, maana kuna mengine mazito kwake yanakua mepesi tu na hunisaidia kuona mambo kwa picha tofauti. Kwa hilo namshukuru sana. Wakati mwengine wanasema umri sio kipimo cha busara, rafiki yangu huyu kupitia mengi, kwahiyo moyo wake wa ‘chuma’ unatusaidia wengi kwenye kuweza kupambana na dhurba mbali mbali.

    Hapa sina haja hata ya kukuambia alipitia mitihani kiasi gani maana dunia nzima inajua, ila naweza tu kukuambia kwamba hakuna binti mwenye moyo wa utayari na ambae hana uwoga pale anapokua anasimamia lake kama Elizabeth Michael Kimemeta. Kwanza akiweka nia kwenye jambo lake lazima liwe... Atafunga, atakesha asali, ataweka akili na mawazo yake yote humo mpaka Mwenyezi Mungu amtimizie, nishashuhudia hilo sio mara moja wala mbili na naweza nikasema binafsi ameni inspire sana kwenye suala zima la funga na sala. Nani kamfundisha hayo? Kwa umri wake aliokua nao wakati matatizo mazito yalipomfika pengine usingedhani angekua binti wa dizaini hiyo. Miaka minne au mitano ambayo Alikutwa na yale matatizo ya kesi na mpaka akatumikia kifungo ni miaka ambayo ilimfaya akue sana. Ki imani na kiakili.

    Kwenye kipindi hiki hakua bado tayari kuzungumzia usiku ule ulobadilisha maisha yake ila kaniahidi akiwa tayari basi atafiria kutushirikisha kwenye hayo maongezi ila inawezekana pia hiyo siku isifike, nna hisia hiyo ni kurasa ya kwenye kitabu ambayo amechagua kuiruka kwa sasa au pengine milele, na maamuzi hayo mimi na wenzangu tuliyaheshimu.

    Sote tunakumbuka wakati anakua, kila kukicha yuko kwenye gazeti ila kwa sasa huyo si yule, amekua ki mwili, ki akili na hata ki sanaa pia. Mambo yake si ‘hadharani’ tena kama ilivyokua miaka ya nyuma. Sasa amekua influencer ambaye kampuni kubwa kadhaa zinamuamini yeye kuwatangazia biashara yao. Amekua Mama kwa mdogo wake Eric ambaye naye tumemuona akikua kwenye macho yetu. Mama kwa watoto wawili ambao amewakuta wakiwa wanaishi na mchumba wake nyumba moja.

    Kwenye haya maongezi yetu tuligusia hilo la hao watoto, na watoto wengine, kazi, yeye kama binti ambae amekua akikutana na mawe mengi. Muonekano wake. Familia kwa upande wa Mama na Baba na mambo mengine kadhaa. Niko hapa kukutakia uangaliaji mwema wa kipindi hiki na yangu matumaini utavutiwa na jambo ambalo litakufanya ubadili maisha yako kwa uzuri zaidi. Tafadhali enjoy.

    Love,

    Salama.


    Follow:

    Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown

    Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown

    Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown

    46 min
  • Ep. 16 - Salama Na Darassa | KAWIA UFIKE

    Thabit Shariff Ramadhan my guy, siku zote mkimya, yupo kama hayupo, anayeona lakini humkuti anaangalia na mwenye kuyabeba yanayobebeka na kuyaacha ambayo hayapaswi kuchukuliwa, huyo ndo yeye na leo ukimuona mpe tu heshima zake, pengina si kwasababu kakuzidi umri, ila kwasababu aliyechelewa lakini KAFIKA.

    Tena, sikumbuki lini ilikua mara ya kwanza mi naye kukutana ila nakumbuka nilipomuona 2016 mwezi wa 12 kwenye mazoezi ya show ya usiku ya Tuzo za Muziki za EATV, alikua wa mootoh, ukiachana na watu waliokua ndani ya game, hakuna aliyejua alitokea wapi, ila boom!! Kwenye sikio na kila mdomo wa wana Afrika ya Mashariki dunia kwa ujumla, kiiila mtu alikua anaimba MUZIKI wa (ya) Darassa.

    Hapa atatuambia kwamba alikua kwenye game muda mbona? Ila muda wake tu ulikua haujafika (pengine ushaisikia hiyo story) ila ni kweli, muda wako kama Mwenyezi Mungu hajasema ndo huu basi inakua hata ufanyeje haufiki mjini. Imagine kuwepo toka enzi za ECT, Dully wakati wamooto, wakati Complex bado yuhai na Q Chief ana nywele zake zote kichwani na rasta juu lakini 2016 ndo akapata break yake kubwa ya kwanza sio mchezo. Kwa hilo pekee tunafaa tumpe salute zake.

    Muziki haikua single yake ya kwanza, haukua wimbo wake wa kwanza kurekodi, haikua video yake ya kwanza aidha, ila kwa baadhi ya watu Darassa alikua ‘msanii mpya’. Hapa, tuliongea juu ya maisha baada ya MUZIKI, na kabla. Baada ni kwasababu lilikua ndo swali la kila mtu, kipi kilikosewa, nini kilitokea? Hakua na uwezo wa kutengeneza hit tena? Ilikua bahati tu ile? Na kabla ya hapo alitokea wapi haswa? Ali struggle kabla ya kupata mwanya? Shuleni ni vipi? Changamoto za kazi? Ana mtoto? Mke? Mwenza? Nani ni rafiki yake kwenye muziki? Subira haswa anayo? Alijifunzia wapi?

    Majibu yako humu, tafadhali enjoy.

    Love,

    Salama,

    Follow:

    Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown

    Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown

    Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown


    46 min
  • Ep. 15 - Salama Na Rosa Ree | OSHUN

    Ukiwa zako nyumbani umejikalia kwenye sofa unamuangalia Rosaree kwenye TV kwa mara ya kwanza sidhani kama utaweza kugandua macho, pengine ukiwa na watu walokuzidi umri style yake inaweza ikawashtua kiasi na haswa wakiskia anachoimba ni kwa lugha ya Kiswahili ndo kabisa. Ki ufupi binti huyu toka kwenye familia yenye story ambayo kwa ki binadamu si tu yeye pekee amepitia, lakini ni yeye ambaye anafahamika na wengi kati yetu na hii ni nafasi yako na yangu pengine ya kutufanya tuamini kwamba ulichopitia au unachopitia, huko peke yako na pia hayo mambo yana mwisho wake.

    Ki kawaida Rosaree sio muongeaji, lakini unapomkuta kwenye ofisi yake ni mtu wa aina nyengine kabisa alojaa ubabe wakati anatema cheche za mashairi yake, swagg za kinyamwezi na kujibeba kwa kipekee haswa, na hiyo ndo tofauti yake na ma rapper wengine hapa Afrika ya mashariki na Afrika kwa ujumla. Ki umbo si mkubwa hata, hata ki umri pia, bado tunaweza kumsamehe kama atakosea wakati anaelekea kwenye safari ya ubora wake. Pia ana haya nyingi, lakini tena, akiwa kwenye zone yake, anakua ‘mnyama’ mwengine kabisa.

    Alipokua chini ya Nahreel na Aika muungano wao ulikua mzuri sana, hits kadhaa zake zilitoka kule, so mimi katika mambo nlotaka kujua ni kwanini kila mtu alienda njia yake? Hapa katikati pia kulikua na picha flani ivi ambazo Baraza la Sanaa na Taifa hazikuzipenda na matokeo yake rapper wetu alifungiwa kufanya kazi zozote zinazohusina na mziki kwa muda wa miezi sita, na kuna masuala ya kufanya kazi nje ya nchi bila ya kibali. Mimi na yeye pia tuligusia masuala ya mahusiono. Mahusiano ya Baba yake na Mama yake, na yeye na nduguze wa tumbo moja na wa kufikia na pia muonekano wake.

    Rosaree ni mwerevu, mwenye mipango, na anayejiamini, hiyo ndo tofauti yake yeye na waliobaki. Na anajua hilo!

    Tafadhali enjoy.

    Love,

    Salama


    Follow:

    Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown

    Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown

    Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown

    43 min
  • Ep. 14 - Salama Na Romy Jones | PLUG

    Romeo boy handsome toka Kinondoni mpaka Tandale na sasa duniani kote. Ni kijana wa town, mcheshi, mtanashati, mwenye madevu na mcha Mungu, Ila pia ni Kaka yake mwanamuziki superstar toka Tanzania ambaye ni Diamond Platnumz.

    Mimi na Romy tunafahamiana miaka mingi, na kama ulivyodhani nilianza kumjua yeye kabla sijafahamiana na Nasib, story yetu inaenda toka enzi za ‘ujana’ wetu, rafiki zake ndo rafiki zangu na tulikua tukikutana karibia kila wiki.

    Toka Platnumz awe al maaruf Romy amekua nyuma yake siku zote, toka video ya kwanza ambayo umemtuambulisha kwetu super star huyu Romy alikuwemo pia kwenye video hiyo kama mume mtarajiwa wa msichana ambaye Platnumz alikua ndo mpenzi wake. Toka siku hiyo tumekua tukiwaona pamoja kila sehemu kama kope kwenye jicho.

    Miaka ya hivi karibuni sikuacha kugundua kwamba rafiki yangu huyu kabadili tabia, siye yule nlokua namfahamu wa miaka mitano iliyopita, kuanzia muonekano, kazi, jinsi anavyojibeba na hata maongezi yake. Pia nimekua nikimuona akifanya kazi ambazo si za bora liende na badala yake ni kazi ambazo zinasimama haswa na kujieleza zenyewe. Kwa mbali nilikua naangalia na nikasema kwanini haswa nisimtafute rafiki yangu huyu ili atuambie mimi na wewe siri haswa ya mafanikio yake? Pia kuhusu maisha yake binafsi maana ameoa miaka ya hivi karibuni, kuhusu Mama yake mzazi, mahusiono yake na Mama yake Naseeb, kazi yake kama actor na Dj, kulea mtoto wa mkewe na fame kwa ujumla. Tulikutana na tukazungumza hayo na zaidi.

    Tafadhali enjoy.

    Love,

    Salama.


    Follow:

    Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown

    Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown

    Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown

    53 min

About Salama Na

From the publisher's feed

‘Salama na’ – meaning ‘Salama and’ is a one hour Podcast chat show hosted by a re known Radio &; TV personality Salama Jabir and available on Both Video and Audio of Various Platforms. In Salama…