
Sign up to save your podcasts
Or


Moja ya watu walopigana vita zao wenyewe kimya kimya na wengine wakashuhudia tu mtu yuko jukwaa la kimataifa na anazidi kusoga. Maana halisi ya nitafanya kama ilivyo ili tuone mbele itakuaje maana Mungu amekua mwema haswa, so kwake yeye hakuna kinachoshindikana na kiukweli kabisa kama wewe ni wa mbili basi utaendelea kuzivaa maana mwenye hizo mbili kuvaa moja abadan!
Mimi nilikutana naye kwa mara ya kwanza kwenye mahangaiko ya kazi yangu ya kwanza, radio mpya ilikua imeanzishwa hapa mjini, kwa msaada wa Soggy Doggy Anter aka Chief Rumanyika nikapata nafasi ya angalau kuingia mule ndani na nikakutana na watu kadhaa ikiwa pamoja na Zee A aka Zuhura Yunus huyu wa sauti tamu na lafdhi ya kutaka tu umskilze mwenye kuendesha ‘Dira ya Dunia” na siku za hivi karibuni “Focus on Africa” na hapo pia (sehemu tulokutana mara ya kwanza nami nilipata kazi yangu ya kwanza kama mtangazaji wa radio)
Hakuamka tu asubuhi akawa mtangazaji wa BBC, ila allipita kule na huku na kujiongeza ki elimu ndo mpaka leo yuko hapo. Umaarufu wake ukanza kujijenga kidogo kidogo na uwezo wake wa kuongea Kiswahili fasaha pia ukampa nafasi ya kuweza kupata kazi hiyo baada ya kuwa nchini Uingereza ili kujiendeleza na masomo, basi naam… Internship akaanza na baada ya hapo BBC wakawa wanaajiri mengine ndo stori tu kama nnayokupa hapa
Zuhura alikua katika mipango yetu ya kuweza kupata nafasi ya kukaa chini na kuongea nae mambo kadhaa ili wananchi wapate kumfahamu zaidi. Lakini msukumo pia ulikuja baada ya baadhi ya watazamaji na waskilizaji wetu pia kutaka kumfahamu zaidi na likawa ni moja kati ya majina yalokua yakitwajwa zaidi yawe kwenye kipindi chetu na haikua kesi kwetu hata robo maana mipango ilikua kama mitego ya ki Vietnam. Dadaake akajaa.
So yeye ni nani? Kwao wapi? Wazazi wake ni kina nani? Ana ndugu walozaliwa pamoja? Wako wapi? Lini alianza hiii kazi ambayo anaifanya na sisi inatuvutia sana? Shuleni je ni wapi? Khadithi juu ya yeye kujifunika ushungi? Alilazimishwa? Anatokea kwenye familia iloshika dini sana? Kazi yake ya kwanza ilikua ipi? Yuko na mtu anayemsaidia kufungua zipu ya gauni akirudi nyumbani kutoka ofisini huku akiwa kachoka sana? Sisi mwenzangu tuliuliza hayo yooote na zaidi. Ukiachana kwamba yeye ni mtangazaji hodari na mtu poa sana, ambaye anapenda tu kucheka masaa yote basi Zuhura pia ni performer mzuri tu wa mziki, anaweza kuimba, kuchana na kucheza, ila hiyo iwe siri yako mwenzangu.
Pia huyu ni mmoja kati ya yatu wanao ni inspire na kupenda zaidi kazi zao.
Cheers kwa Dadaake
Love,
Salama.
Follow:
Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown
Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown
Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown
Mara nyingi huwa tunahukumu watu ambao hata hatuwafahamu na pengine hatujawahi hata kuongea nao hata mara moja kwasababu tu ya muonekano wao au kwa kitu tumeskia wamefanya au wamesema, au kwasababu fulani kasema jambo fulani kuhusu yeye ndo hapo nasi tunajifanya tunawajua sana na kutoa hukumu zetu juu yao, kama vile tunawafahamu sana au tunajua sababu ya yote ambayo tumeona au kuskia tu wamefanya au kusema. Hayo ndo maisha ambayo mgeni wetu wa wiki hii amekua akiishi kwa miaka kadhaa sasa.
Jina lake ni Zawadi aka Gift, binafsi sikumbuki siku ya kwanza kukutana naye au kumsikia ila nakumbuka siku ya kwanza kusikia wimbo wake na kusema unajua nini, huyu kadadaa akituliza maskio yake basi anaweza kufika sehemu, akaja akatoa single nyengine, pia ilikua moto na mashairi na pengine sababu ya yeye kusema alichokua anakisema mule ndo kilinifanya haswa nijue ndani yake kuna kitu cha kupewa nafasi na uangalifu ili apelekwe panapotakiwa. Najua muziki kwa miaka ya hivi karibuni umekua ‘ukiingiliwa’ na vipaji feki na vya kulazimisha vingi tu na kila mmoja ana sababu yake ya kutaka kufanya hivyo. Mimi na wewe tunatakiwa kuheshimu kila hustle ya mwenzetu tunayoina au kukutana nayo maana mtu anakua anajaribu na kwa hilo tunastahili kuheshimu, haijalishi anafanya nini, kama kinakukera au kukufurahisha, as long as kinamfaidisha yeye na kumpa raha basi sisi tunatakiwa kuheshimu na ndo hiyo heshima tunatakiwa kumpa Zawadi pia.
Kikubwa kwa Gigy ni mdomo wake ambao kwa wengi wetu tunasema na kuamini hauna chujio hata kidogo. Haogopi kuongelea maisha yake ya binafsi na kwa hilo linajumuisha mahusiono ya ki mapenzi, mahusiano na Mama yake, rafiki zake, watu alokua nao na pengine hata kazi... Ila sasa ni kitu gani kinamfanya mpaka leo bado anapata ma deal ya kazi, ana marafiki wazuri, halali nje na anakula vizuri na mtoto wake anaishi vizuri tu?
Hiyo ndo sababu ya mimi haswa kutaka kukutana nae na kuongea nae kwa kiasi changu. Kipi haswa kilutufanya tumfahamu? Anadhani ubora wake uko wapi? Huwa anawaza kabla hajaongea? Kipaji chake anadhani ni nini? Mama yake ni mtu wa aina gani? Bintiye je alitokea wapi? Kuna mambo ya imani za kishirikina pia huwa yanaongelewa sana hayo nayo? Style yake ya maisha haimgharimu na masuala mengine ya maana kweli?
Majibu yako humu ya ile khadithi ulokua unazisikia kila siku mimi na wewe, yangu matumaini tutayapa yote. Tafadhali enjoy.
Love,
Salama.
Soundtrack Yeah by @MarcoChali https://www.youtube.com/watch?v=Cue1HB4fnLQ
Follow:
Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown
Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown
Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown
Katika pita pita zanguangu kwenye mitandao leo asubuhi nilikutana na video ya Ben Pol akiwa anaelekea kupanda zake helicopter na video ikamuonyesha akiwa anazunguka kwenye fukwe za huko alipokua na baadae ikaishia kwa kuonyesha watu wawili wakiwa wanaelea hewani... Mmoja wapo bila ya shaka alikua ni yeye, kuna mtu ambae amekua aki enjoy maisha yake miaka ya hivi karibuni kama yeye? Niko hapa nangoja jibu lako... na bila ya shaka mmoja wa watu hao wawili alikua ni yeye. Kutoogopa na kutimiza malengo aliyojiwekea ndo siri ya kukamilisha hesabu alizokua kapiga, na bila ya shaka baraka za Mwenyezi Mungu zinakamilisha yote. Kuna mtu ambae amekua eki enjoy maisha miaka ya hivi karibuni kama yeye? Niko hapa nangoja jibu lako… 😁
Mpole, mcheshi, mwenye kusikiliza wakati mwengine akiwa anaongea, mwenye akili iliyo makini kwa umri wake na mpenda familia. Ben Pol amekuwa kwenye industry ya muziki wetu kwa miaka zaidi ya tisa sasa. Uhodari wake wa kuimba na kumiliki jukwaa vyema kabisa kitu ambacho ni adimu kwa waimbaji wanaofanya muziki wa aina yake, ila kwake yeye haikuwahi kuwa kazi ngumu toka siku ya kwanza alipokabidhiwa jukwaa, na kama unaniamini mimi, basi si jukwaa la muziki tu ndo amekua akilimudu uzi analoliweza kweli kweli, bali jukwaa la majukumu, la uandishi na hata ya uongozi. Amekua akipewa majukumu wakatia bado mdogo na aliweza kuyamiliki vizuri na matunda yake kuonekana mapema kabisa.
Mzaliwa wa Dar es Salaam, na wakati anazaliwa Mzee wake hakua nyumbani na mazingira ambayo alizaliwa nayo yeye pekee ndo anaweza kutukhadithia na pengine kutokea huko na mazingira aliyokulia, aliyosomea, aliyoyapitia mpaka leo hii tunamfahamu ndo yamemfanya awe aina ya mtu aliye leo. Tushawaona watu wengi wakiwa wanabadilika mara tu baada ya kupata umaarufu. Simu zikawa hazipokelewi tena, pengine hata namba kubadilishwa, marafiki kubadilika, uchelewaji wa kwenye interview na kazi ikawa jambo la kawaida, marafiki wa kike kujaa kwenye phonebook na mambo mengine ya kukera, ila si kwa kwake yeye. Ameweza kutenganisha ukweli kwamba yeye ni mwanamuziki mkubwa na hodari ambae anawafurahisha wengi lakini pia ni mwana tu ambae ni mtoto kwa wazazi wake wapendwa na Kaka kwa mdogo wake, Baba kwa Mali na bila ya shaka mchumba kwa Anerlisa.
Kwahiyo kitu gani haswa kimemfanya awe makini kwenye mambo yake na maamuzi anayofanya? Unadhani yeye ndo mwanamuziki mwenye vokali noma zaidi hapa kwetu? Au pengine ndo muimbaji anajielewa zaidi? Kipi kinampa hiyo nguvu ya kuwa humble kuweza kunyosha mambo yake kama yamepimwa kwa rula? Well… Majibu yako humu kwenye haya maongezi yangu naye. Kutoka kuzaliwa nyumbani kwa msaada ya jirani akiwa na Mama tu, maisha ya ujana ya Baba yake, mtihani walioupata kama familia baada ya kutokea kifo ndani ya nyumba yao, alipokua mdogo alikua mwanafunzi wa aina gani, na khadithi za mtoto wake. Tulikua na uwanja mpana wa mazungumzo na kilichozungumzwa kitakusaidia kukupeleka sehemu flani.
Enjoy.
Love,
Salama
Soundtrack Yeah by @MarcoChali https://www.youtube.com/watch?v=Cue1HB4fnLQ
Follow:
Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown
Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown
Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown
Weekend mbili zilitopita rafiki yangu Mwinyi aka Mpwa aka Cousin aka Hamis alikua akiadhimisha siku ya kuzaliwa kwake na alikua amefiksha umri wa kustahili kusherehekea kwa kweli na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa maisha, mke wake kipenzi alinipigia simu siku nne kabla ya birthday ya mumewe na kutaka tujumuike nae kum suprise, pia akaniambia ana kazi sana ya kuweza kukamilisha hilo tukio maana jamaa (Mwana FA) kashasema yeye hana mango wa kutaka shughuli, angependa maisha yaendelee tu kama kawaida. Pengine alikua akitarajia dinner nyumbani na mkewe na wanawe basi. So kukawa na zoezi hapo la kuhakikisha jamaa hasomi mchongo na kwamba zoezi ni lazima lifanikiwe. Malika binti yeke kwa kwanza ndo alikua amiri jeshi mkuu wa kuhakikisha Baba anarudi nyumbani by saa mbili usiku ili ale na familia chakula cha usiku. Suala hili lilizidi kuwa tamu pale Malika alipofanikiwa kutimiza ombi lake kwa Baba na sisi wengine ikawa rahisi kuibuka nyumbani na kumaliza mchongo mzima. Ulikua usiku mzuri ambao umeandaliwa kwa mapenzi mengi, na kila kitu kilipangwa kwa uangalifu by saa nne unusu tunaimba kata keki tule 😃. Ila kitu unique kabisa kwenye sherehe hiyo ilikua ni vipande vya karatasi ambayo tuligaiwa, vilikua na namba na namba yako ikitajwa basi kuna swali ilikua unatakiwa kulijibu, ili kuonyesha ukaribu wetu, unataka kujua mimi nilipata swali gani? Ok, swali lilikua ni kama nakumbuka siku yangu ya kwanza kukutana na Mwana FA! Hiyo story itaendelea siku nyengine ila kwa sasa nikuambie tu mahusiano yangu na yeye Mwinyi. Tumekua pamoja naweza sema baada ya kukutana hapa mini Dar es Salaam mwanzoni mwa miaka ya 2000, sote tukiwa wembamba na watoto tu, ila bila ya shaka kila maja akiwa na nia na madhumuni ya kufika hapa tulipo na zaidi panapo majaaliwa, kuna smile flani ivi ambalo mpaka leo halijawahi kubadilika ndo ID yake pamoja na mwanya flani unaokamilisha muonekano wake, style za misuko ya nywele tofauti pia ilikua ikimtenganisha yeye na wanamuziki wengine, ila kikubwa zaidi ambacho kinamfanya yeye awe kasimama mbali na wenzake ni jinsi anavyoandika, anavyowasilisha na anavyowakuna pia washabiki wake ambao kila siku zinavyozidi kwenda wamekua wakiongezeka, nadhani ni baada ya kampa sikio la moja kwa moja ambako kumewafanya wamsikilize kwa umakini zaidi. Siku za hivi karibuni rafiki yangu aliibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii zaidi Twitter baada ya kuamua kujiita yeye Shaaban Robert wa enzi zetu, kama ulikua hufahamu Shaaban Bin Robert alikua mi mshairi, muandishi wa vitabu na essay na pia inaaminika alikua moja kati ya wafikiri wazuri wa lugha ya Kiswahili kutoka Afrika ya Mashariki. Mwana FA ni mmoja kati wa washairi wazuri na mwenye style tamu pia ya kuwakilisha uandishi wake kwa miaka mingi sasa ya muziki huu wa kizazi kipya. Kama unadhani anastahili kujiweka ligi moja au hata nyumba moja na Shaaban Robert au pengine hana nafasi hiyo mimi sina cha kusema juu ya hilo, ila ninaloweza kusema ni kwamba rafiki yangu huyu ameonekana kukua mbele ya macho yangu kwa zaidi ya miaka kumi na tano sana, alianza kufanya kazi zake mapema tu kama solo artist na ngoma sake ya kwana tu ilikua HIT, Unaikumbuka INGEKUA VIPI? Kisha ikaja ECT, baadae kama Duo yeye na AY huku akiwa anaendelea kufanya solo projects na baada ya hapo ameendelea kusimama mwenyewe na kujiimarisha kila mara anapotupa nyimbo mpya, na kwa hilo basi niko hapa kwaajili ya kutoa heshima zangu kwake na kumtakia kila lenye kheri naye. P.S Mwana FA pia ni rafiki mzuri na Baba kipenzi kwa mabinti zake. Enjoy. Love, Salama. Soundtrack Yeah by @MarcoChali https://www.youtube.com/watch?v=Cue1HB4fnLQ Follow: Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown
Khadija Omar Kopa.
Malkia wa mipasho na lejendari wa muziki wa Taarab kwenye ukanda huu na duniani kwa ujumla, mwenyewe kaniambia yeye kwenda Arabuni na Ulaya ni jambo la kawaida tu kwake maana hayo kayaanza kuyafanya kitaaambo sana. Kitambo kweli naweza sema, mimi nimeanza kumfahamu Da Khadija toka kigori kabisa, na amekua hapo kwenye standard hiyo hiyo kwa miaka nenda na miaka rudi. Hii bila ya shaka imetokana na kwamba na yeye alianza kufanya hizo kazi akiwa bado msichana mbichi kabisa. Na ameweza kutuliza akili yake na ku maintain standard na status yake kwa miaka nenda miaka rudi kitu ambacho ni kigumu kwa mwanamke, tena kwa mwanamke wa visiwani ambako miongozo ya kidini ina mizizi kama ya mbuyu lakini ameweza kutunza heshima yake na kuonyesha kipaji chake huku akiwa na staha yake. Inabidi uwe na nguvu ya ziada kuweza kuwa na ujasiri wa aina hiyo.
Bila ya shaka alikua pia akipambana na mengi, pengine kukatishwa tamaa au hata vitisho ili aache kufanya alichokua anafanya kwa kutumia kipaji alichopewa na Mwenyezi Mungu lakini wapi, kwa mbwembwe za hali ya juu yeye ndo ameibuka kidedea kwenye vita hiyo na ndo maana heshima ya ulejendari inamhusu moja kwa moja Dada yangu huyu.
Wengine watasema pengine yeye si muimbaji wa taarab mwenye sauti nzuri zaidi ya flani na fulani, pengine kuna ukweli ndani yake, lakini je, hao wenye hizo sauti nzuri zaidi yake wako wapi? Je wana uwezo wa kucheza na kuringa jukwaani kama Khadija Kopa? Je wanajulikana kama yeye? Je wana ushirikiano na wana muziki wa kizazi kipya cha Bongo Flava na kutoa nao nyimbo zilizoshika chati ya juu? Je wana uwezo wa kuingiza Taarab yao kwenye matamasha ya muziki wa kizazi kipya na watu waka bang kama kawa? Mimi na wewe tunajua jibu.
Hii ni kwa ajili ya Dada yangu, fundi wa hizi kazi, tumpe heshima yake maana ‘Mpewa hapokonyeki, aliyepewa kapewa...’
Tafadhali Enjoy.
Love,
Salama.
Follow:
Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown
Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown
Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown
Mimi kama watanzania wengi sikuwa namfahamu Idris, mara yangu ya kwanza kumuona ilikua kwenye TV akiwa mmoja wa wawakilishi wa Taifa hili kwenye kipindi cha Big Brother mwaka 2014. Nilivyouandika hapa huo mwaka ndo imenigusa akilini kwamba ni miaka sita tu imepita toka Idris Sultan amekua kwenye macho na midomo yetu. Na pengine ataendelea kuwepo kwenye midomo na macho yetu kwa miaka mingi zaidi, kuna sehemu nilikua naangalia interview yake moja na alisema yeye umaarufu ndo kitu ambacho anakipenda zaidi, pengine na ndo maana alienda kwenye shindano la Big Brother Africa na toka ametoka mule kama mshindi sidhani kama kuna wa kumsimamisha au cha kumsimamisha yeye kuweza kutimiza ndoto yake hiyo.
Kama kijana mwengine yoyote toka tumfahamu Idris amefanya mambo mengi ya kutuonyesha kipaji chake, kuanzia vipindi vya radio na tv, ku mc shughuli mbali mbali, kufanya comedy na sasa kaamua kujikita kwenye uigizaji na hakuna swali juu ya kipaji chake cha uigizaji kama kimepamba moto ivi na pia inaonekana amenza kijielewa na sidhani kama kuna wa kumsimamisha.
Idris aliweza kushinda zile pesa za Big Brother ambazo zilikua ndo habari ya mjini, inawezekana pia zile pesa zilikua na Tanzania nzima maana nakumbuka hasa mahesabu yalokua anapigiwa baada ya ile hela ‘kuyeyuka’ katika mazingira ya kutatanisha kitu ambacho kilimfanya awe kama kichekesho cha nchi. Inachukua moyo wa ziada kuweza kupambana na mawe ambayo kijana huyu alikua anarushiwa kutoka kila kona ya kuhoji na kudhihaki maisha yake na baadhi ya maamuzi ambayo aliyafanya kwenye maisha yake. Na nadhani mpaka hapa tulipo? Idris 10 sisi 0! Nakumbuka kama miaka mitatu iliyopita nilikua na kikao nae sehemu akaniambia anashkuru sana haya sote yametokea kabla hajafikisha miaka 25, kwa yeye kuweza kufanya mistake kama alofanya nyuma haiwezi kutokea tena. Anaamini amejifunza mengi na kuyaona mengi baada tu ya kupitia mtihani ule.
Kwenye maongezi yetu haya tulikua hatuwezi kuacha kuzizungumzia pesa hizo ‘za taifa’ na kutaka kujua haswa kinaga ubaga juu ya nini haswa kilitokea. Pia kuhusu mahusiano ya kimapenzi yalowahi kutokea maishani mwake, vipi aliweza kupambana na mawe yaliyokua yanarushwa upande wake, humu pia tumezungumzia biashara michongo ya mjini, kipaji chake na mipango yeke endelevu pia. Here’s to our Trooper, tafadhali enjoy!
Love,
Salama.
Follow:
Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown
Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown
Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown
Nakumbuka kipindi ambacho Fidi alikua anaamini kabisa kama kuweka ‘uso wa mbuzi’ ndo kulikua kunakufanya uwe ‘hard core’, sina uhakika lini aliachana na dhana hiyo ila kwa kipindi cha miaka miwili au zaidi tabasamu na bashasha vimekua havibanduki kwenye uso wake, jambo ambalo mimi kama rafiki nalifurahia sana. Nakumbuka baadhi ya marafiki zangu wa kike ambao ni wapenzi haswa wa mziki wake walikua wakiniambia eh, sema rafiki yako mgumu jamani, Kha! Mi hucheka tu na baadae wakishazoeana basi sidhani kama kuna hata mmoja anaweza kusema kitu kibaya kuhusu yeye. Nilikua nacheka kwasababu mimi naamini namfahamu rafiki yangu huyu, yeye hupenda sana matani, na kucheka na marafiki wa karibu wanaweza wakathibitisha hilo maana katika watu ambao unaweza ukawatania weeee mpaka asubuhi, na utani mpaka wa vitu vyengine ambavyo wewe wa karibu unaweza kusema hey, hiyo sasa imepitiliza, yeye waala... Atacheka tu!
Mwenye kipaji chake cha kujifunza mwenyewe, nasema hivyo kwasababu nadhani kufahamiana kwetu na kuelewana kwetu pia kunatokana na kuwa na vitu vinavyofanana ndani yetu. Kajifunza jinsi ya kupenda kusoma vitabu mwenyewe, kujifunza jinsi ya kuandika na kurap mwenyewe, kajiendeleza mwenyewe (bila ya shaka kuna watu walomsaidia kwa tafu za hapa na pale ila walitokea baada ya kuona jitihada zake). Alihakikisha anasafiri kwenda nje ya nchi na Africa kwa jitihada zake mwenyewe na mpaka leo, kukiitwa watu ambao wamesaidia kwa kiasi kikubwa kufikisha Hip Hop ya nyumbani hapa ilipo basi jina lake litakua ni miungoni ya yale yatakayopata heshima ya juu kabisa. Pia anachekesha sana. Uelewa wake wa baadhi ya vitu unaweza ukakuacha mdomo wazi wakati mwengine. Kwenye uwepo wake? Vicheko lazima vitawale.
Hii siku nilitia nae story haikua kama kazi, bali kama mtu na rafikiye tu wakitia story juu ya njia za maisha ambazo tumepitia mpaka sasa. Fidi amekuzwa na Mama yake ambae alikua ni mfanyakazi wa serikalini (ameshastaafu), alikulia mkoani kama wengi wetu, alifika Dar akakaa kwa ndugu kama wengi wetu, alianzia sehemu na kutoka hapo mdogomdogo akajijenga kufikia hapa alipo. Humu tumeongelea hayo, watoto, muziki, ndoa, maisha ya wasanii na maendeleo kwa ujumla. Yangu matumaini uta enjoy na kuelewa baadhi ya vitu zaidi na zaidi.
Here’s to Ngosha wa Mbasa.
Love,
Salama.
Follow:
Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown
Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown
Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown
LENSMAN Touch yake katika mambo mengi ndo ambayo inamfanya awe tofauti sana na vijana wengine walokuja mjini nae kwa wakati mmoja, uzuri ni kwamba nilikuwepo wakati mabegi (kama yalikuwepo) hata hayajatua uzuri chini ndo hapo nilikutana na Mashala, aka Michael Sylvester ‘Carter’ Mlingwa. Kwanza ilikua kujuana kwa kwenye mitandao tu na hiyo ni khadithi ya siku nyengine. Kwa wanao nifahamu mimi wanajua kama ni ngumu haswa kumuingiza mtu katika maisha yangu, awe karibu yangu, ajue undani wangu ndo maana nina watu wengi ninaofahamiana nao ila wanaonijua ni wachache. Michael ni mmoja ya watu wanaonijua mimi, na naweza kusema nami namjua yeye. Makutano yetu ya kwanza yalikua kwenye kibaraza cha MJ Records pale nje kwa Marco Chali, nakumbuka mpaka alikua kavaa nini, jeans moja kichupa ivi na fulana ya rangi ya udhurungi, mkononi alikua bracelet ya kimasai zile zinazofunika nusu mkono (mawindo ya wazungu yalikua yanahusiana na muonekano 🤣), chini alikua na raba tu simple na begi lake la mgongoni. Wembamba wake ulikua unamfanya aonekane mrefu na rangi wake ulikua utani na mfano kwa kila mtu tutakayemuona ana rangi inayoshabihana na yake. Michael alikua na yake ya kufanikiwa moyoni toka siku ya kwanza ila kikubwa zaidi ni roho yake nzuri na kutaka kila mtu anayetaka msaada kwake afanikiwe na hata wale ambao hawajui alikua akiwatafuta aongee nao ili awaelekeze jinsi ya kufanya baadhi ya vitu ili wajiongezee kipato, haswa wanamuziki. Nakumbuka aliponunua gari yake ya kwanza, alikua ananiachia mimi niendelee nalo na mitkasi yangu kisha yeye anapanda bajaji, si mara moja wala mbili, wala tatu, roho ya aina hii bila ya shaka ndo imemfanya awe anazidi kubarikiwa. Kwa kipindi kisichozidi miaka kumi jamaa yangu huyo amepiga hatua kubwa katika maisha pengine kuliko kijana mwengine yoyote ambae mimi nilimuona toka mwanzo akiwa amefika ‘town’. Kukaa nae kwenye meza halikua jambo la mjadala maana safari yake ya kutoka kushika camera mpaka kuwa kiongozi wa kampuni yake mwenyewe na kuwaajiri vijana wenzake na kuwa partner wangu kwenye biashara hii unayoitizamana nadhani anafaulu kwa alama za juu kabisa. Hapa tunakugusia maisha yeke ya utotoni, shughuli za Marehemu Mzee wake, kukua katika familia yenye watoto wengi, mahusiano yake na watu wa mjini na jinsi ambayo ameweza kuepuka kifo mara mbili kwa ajali ambazo moja alitakiwa kabisa awemo na pengine saa hii tungekua tunasema mengine. Ila kubwa kuliko ni kusoma njia alizopita ili nawe uweze kujifunza jambo. Tafadhali enjoy. Love, Salama.
Follow:
Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown
Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown
Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown
Zuwena Yusuf Mohammed ndo jina alopewa na wazazi wake na siko hapa kuwakosoa kwa chaguo lao hilo ila mi nadhani Shilole ndo limekaa mahala pake zaidi. Anaongea kama Shilole, anacheka kama Shilole, ni shujaa kama Shilole, REAL kama Shilole, anapenda kama Shilole na sisi tunampenda kama Shilole. Ally Rehmtullah alikua anaadhimisha miaka kumi ya kazi yake. So alifanya auditions kwa ajili ya kuchagua models kuelekea kwenye adhimisho lenyewe, Shilole aka Shishi alikua mmoja wa ma judge wa skuihiyo, picha likaanza hakuwepo popote pa kuweza kuonekana, shuguli ambayo ilichelewa kuanza kutokana na mambo mengine ilibidi pia iendelee bila yeye. Akatokea wakati tunakaribia kabisa kumaliza ila alipofika kila mtu alijua kama Shishi KAWASILI. Vicheko na matani vilitawala na kila mtu akasahau kama hata Shishi alichelewa kufika. Shishi ni ‘special’. Kuanzia muonekano mpaka tabia, jinsi anavyoishi maisha yake na jinsi anavyotafuta na kujiongeza kila siku ni mfano tosha kwetu sote ya kwamba ‘mwenda bure si mkaa bure’
Anaweza pia akawa kafanya yote ili kuweza kutumiza ndoto yake au zake. Kaigiza, kaimba, kaishi kwenye mahusiano ambayo hajivunii kama alishawahi kuishi hivyo, kafanya biashara, kapigana na mengine mengi kapitia ambayo yanaweza kumaliza kurasa, yote kwa yote... Ni mfano wa kuigwa kwa watafutaji na wanaoanza wengi.
Kwenye meza yetu pia alikuja kachelewa, huku akiwa kavurugwa na baadhi ya watu lakini tulipokaa tu kwenye viti yote yalisahaulika na tukajikita zaidi kwenye mazunguzo yetu ambayo yalijaa vicheko, masikitiko, simulizi za kuacha midomo wazi na faraja tele.
Tafadhali enjoy, na chukua mawili matatu ambayo yatakufunza jambo katika safari yako na kukufanya uwe bora zaidi.
Love,
Salama.
Barnaba ni mfupi (siko hapa kumtoa kasoro) ila wazungu wana usemi wao ambao nitausema kwa kiswahili, ya kwamba vitu vizuuuri huja kwenye pakeji ndogo. Ukitaka kuelewa maana yake kama hujang’amua basi kamuulize Bibi. Umbo lake na uwezo havifanani , na kama ingekua ubora na kipaji ndo ukubwa wa mwili basi mwenzetu angekua kama HERCULES, pia siko hapa kwaajili ya kumtukuza bali kusema vile nimunavyo katika macho yangu.
Ni kijana ambaye anajifunza kila siku iendayo kwa Mungu, hajawahi kujikweza, mwenye roho ya Imani, mwenye kumuogopa Mungu na pia asiyesahau alipotoka na pia alotoka nao huko alipotoka. Mtanashati pia, na ukiniuliza mimi naamini kabisa hiki ni kitu ambacho kimekua kikistawi kwa siku zinavyokwenda, na huo ndo ukuaji, maana kukua si nywele na kucha tu, hata kujielewa na kufahamu kwamba nyanya pia ni tunda lakini juisi yake mpemba hauzi pia ni ukuaji.
Muziki ndo mpenzi wake wa kwanza, ambao umemuepusha na mengi na kumpa vingi pia na kumkutanisha na watu ambao pengine alikua anawaona kwenye picha tu, kuufahamu kwake mziki kwa kujifunza kupiga gitaa na kuutengeneza kama muandaaji na pia kuweza kuuandika ni kipaji ambacho Jalali kampatia, na jinsi ambavyo si mchoyo wa kuwapa na wenzie wakang’ara (kitu ambacho alijifunza) ndo ambacho pia kinampa utofauti kati yake na wengine wengi.
Kwenye kikao hiki mimi naye tulianzia nyuma kiasi, enzi za kuokota vyuma chakavu ili mambo yaende, kupigiwa kelele ya mwizi na kuponea chupuchupu kuchezea kibiriti, THT, uandishi, heshima, Marehemu Ruge, maisha ya ndoa, social media na mengine ya kutosha. Ilikua siku ya kujifunza mengi kutoka kwake na kwa hilo namshkuru Mungu kwa kunikutanisha nae.
Tafadhali Enjoy.
Love,
Salama
From the publisher's feed