
Sign up to save your podcasts
Or


Jeffrey Jessey Mmbungu ni kijana wa ki Tanzania ambaye aliangaliaaa wapi pa kupata rizki ili mambo yake yamuendee kama anavyopenda na akafanikiwa kwa asilimia nyingi sana huku akipata pointi nyingi za kujiamini na kuthubutu kutoka kwangu. Ni rafiki yangu kwa miaka zaidi ya minne sasa, tunagombana tunapatana, kisha tunagombana tena alafu tunapatana, kisha tunagombana kwasababu ya Manchester United alafu tunapatana tena kabla hatujagombana tena kwasababu ya suit yangu kutotobolewa mashimo ya vifungo vya pembeni ya suruali yangu, au pengine kwasababu nlikua nataka kumpiga kirungu akachomoa, au pengine simu yake haipatikani kiiiila wakati wakati yeye ni mtu ambaye hatakiwi simu yake iwe na mizinguo hiyo, ilimradi ni vita tu kati yetu. Najua hili lakini, kwamba wagombanao ndo wapendanao, kiasi cha heshima na kumuamini na kumu admire ni cha hali ya juu sana.
Kuna habari zilienea kipindi flani kuhusu maamuzi yake ya kuacha kazi benki ya dunia na kuamua kujiajiri, na kwamba ni mtoto wa kishua ila anajitia umaskini ili apate huruma kutoka kwa watu na yake yamuendee. Shutuma nzito haswa kwa upande wake. Kwenye kipindi hiki nadhani hatukuacha kitu, yote yalipewa ufafanuzi na pia tukapewa elimu ya yale tusoyajua ambayo ki ukweli tulikua tunajifanya tunayajua sana. Kuanzia hilo suala la kazi mpaka alivyokutana na Cecilia Mosha aka Ceci kama ambayo Jeff humuita. Wana watoto wawili wa kiume ambao wote wamepewa majina ya wachezaji wa zamani wa Manchester United, na ndoto yake ni kuwa vijana wake hao waje kuwa wachezaji wa mpira, niko hapa kuzidisha maombi hayo ili dua za Baba zitimie nami kama shangazi niweze kwenda kukaa kwenye ‘private box’ za Wembley au OT kuangalia vijana wetu wakilisakata gozi
So biashara wake aliingiaje huko? Na kweli alijiona akitoa ajira kwa watu zaidi ya hamsini ambao wako chini yake? Mitihani gani haswa hupata? Yeye kama yeye ana thamani ya kiasi gani? Pesa ngapi huwa anatengeneza kwenye kazi yake hii? Kuna changamoto? Nani mteja wake mkuu? Mahusiano yake na Diamond Platnumz? Walikutana wapi? Huwa Platnumz analipia nguo zake zinazotoka kwa Jeff? Ana biashara nyengine anazofanya? Na elimu yake je? Wapi alienda skuli? Alisomea nini? Kusema za ukweli maswali ni mengi ila tuli pata wa kumuuliza maana alinyoosha vizuri na nilicheka sana na ku enjoy haswa. Yangu matumaini nawe pia utafanya hivyo. Kuna ya kujifunza mengi hapa, ya kukupa muangazo pia yanapatikana humu kwa wingi.
Tafadhali enjoy.
Love,
Salama.
Sifa za Bwana inabidi zisemwe kwa zawadi hii alotupa sisi wanadamu, tunamshkuru sana kwa kipaji cha Goodluck Gosbert na tunamshkuru pia kwa kumfanya ni wa kwetu, kutoka nchini kwetu, kwamba ni mwenzetu. Kwa kweli binafsi nimependa sana na najivunia yeye.
Utamu wa sauti yake nadhani cha kwanza wengi tulikipenda sana, baada ya kumsikia tu, kama ilivyokua mara ya kwanza anataka kujifunza kupiga gitaa akaenda kanisani, na akaskika akiimba na wana kwaya wa kanisa hilo na wakampenda toka siku hiyo mpaka leo, ndo ilivyokua kwetu pia naamini. Kipaji chake cha pili ni utajiri wa mashairi, kipaji kikubwa cha kuandika na wakati naongea nae alitaja baadhi ya nyimbo kubwa alizowahi kuandika ambazo ni za ‘kidunia’ na pia kama zilimtia matatani kiasi maana imekua ikileta tafsiri nyengine kwa baadhi ya watu ambao wao wanamuona kwenye njia nyengine. Lakini hutunga nyimbo zake mwenyewe na pia anawaandikia wengine na katika hizo zinajumuisha kazi zake za nzuri tu alizowahi kufanya ambazo zilitufanya mimi na wewe tumkubali.
Kutoka kuwa mtoto pekee wa kiume nyumbani, na pia kukuzwa na Mama tu ambaye kwa mujibu wa Goodluck alikua muhangaikaji haswa, alifanya kila aliloweza kwa kujituma kuhakikisha watoto wake wanapata elimu ili ije kuwasaidia baadae lakini pia kukua kwenye maadili yaliyo bora kwa kumpenda na kumtanguliza Mungu. Mama yake hakuamini siku ya kwanza alipojua mtoto wake ni amejiunga na kwaya ya kanisani kwake. Na yaliyofuata baada ya hapo ni historia tu. Ungana nami kumskiliza Goodluck hapa na kama ilivyo kawaida, natumai utapata mawili matatu ya kukusogeza katika maisha yako. Tafadhali enjoy.
Love,
Salama.
Follow:
Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown
Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown
Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown
Mtaani huwa wanasema ‘hizo kazi za wanaume’, maana mambo ya kukesha na watoto wa kiume na kuhangaika nao usiku na mchana kwa mwanamke inakua ngumu, na pengine inaweza ikaleta mambo yasiyohusu au ikasababisha vitu nyengine visiende kwasababu tu anayefanya hiyo kazi ni MWANAMKE. Ila kwa Christine ‘Seven’ Mosha nadhani hayo maneno yalikua ndo mafuta kwenye utambi wake na aliyatumia hayo kuweza kutoa mwanga maridhawa ulioset standard ya kuvutia. Kuna kipindi na mpaka sasa, ukiwataja ma meneja wa wasanii walio hodari hapa kwetu basi la Seven litakua la kwanza kwa mujibu wangu Mimi, maana kwa kuwa mfano kwenye tasnia aliweza haswa!
So swali ni alifikaje huko? Kabla hatujafika huko niseme ambavyo mimi namfahamu yeye rafiki yangu huyu. Kwanza hatupishani umri kabisa na pili nimekua fan wake wa muda mrefu. Napenda jinsi anavyojibeba. Napenda anavyojiweka, anavyofanya mambo yake, anavyokua bora kila miaka inavyozidi kwenda lakini kikubwa zaidi ni jinsi anavyojua mziki wetu na anavyopambana kuweka kipaji chake na cha wale anaowasisamia vizuri sana, na haswa ukimuacha akuongoze kwa mfano. Nayasema haya kwasababu nna idea ya jinsi anavyowaona watu na vipaji vyao na anavyotaka kuwanyooshea yao kwa moyo mmoja ili yao na yake yaende vizuri sana. Kwenye tasnia ambayo imejaa wanaume yeye ameweza kukaa miaka yote hiyo na huku akihakikisha heshima na maendeleo yake na anayewaongoza yakiongea yenyewe.
Kwenye kikao hiki nilitaka kumfahamu kwa undani haswa kwa faida yetu sote lakini kama kawaida, alikua mgumu kuongelea maisha yake binafsi, na unaweza kumuelewa maana si kila mtu anapenda kuyaanika maisha yake na ya awapemdao hadharani, so tuligusia tu kwa uchache lakini tuliongelea sana mambo ya biashara, muziki, Ali, Lady JD, Ommy Dimpoz, Rockstar yake na jinsi alivyoanza na mpaka hapa alipo. Pia tuliongelea mahusiano yake na Marehemu Ruge Mutahaba na enzi hizo alivyoanza kama mtangazaji wa radio na kufikia level ya kusimamia talanta za watu wengine. Seven alianza na TID wakati huo hata usimamizi wa vipaji halikua jambo muhimu.
Pia Seven si mtu wa kutopenda kuwa mbele mbele kama mfuko wa shati, na kwa uelewa wangu anapenda mnoo kuona watu wanakua na wanafaidika na vipaji vyao walivyopewa na Mwenyezi Mungu. Je game imekua kiasi gani? Muelekeo wetu je, tunaelekea kuzuri? Tunakua? Nini tufanye ili watu wafaidike zaidi? Kuna hayo na mwengine ya kumwaga katika maongezi yetu haya, na yangu matumaini utamfahamu zaidi Christine na kumpa heshima yake anayostahili. Tafadhali enjoy.
Love,
Salama.
Follow:
Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown
Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown
Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown
Wakati Parklane iko juu sana wengi wetu tulikua tunamfahamu zaidi Sumalee na ilikua haswa Sumalee na yule mwengine mwenye sauti nzito ambaye alikua anatupia tu vichombezo vya hapa na pale, hata kwenye posters za show na mambo mengine Ismail Sadiq aka Sumalee ndo alikua kila kitu mpaka pale kundi lilipovunjika na kila mmoja akaenda upande wake, hapo ndio tulipoanza kufaidi kipaji cha huyu mwanachama mwengine wa hiyo duo, jina la serikali ni Ilunga Khalifa aka Cpwaa alianza kung’ara zaidi na kupata mpaka show za kimataifa.
Yuko na swagg, anaweza kuongea kiswahili na kizungu kwa ufasaha na vile vile yeye ndo mfalme wa crank music hapa nyumbani Tanzania. Nani ambaye hakuzimia style ile ambayo Cpwaa alikuja nayo? Nani ambaye hakushangaa alipoona kipaji chake kama solo artist kipindi kile? Maana ki ukweli yeye alikua wa juu kwa juu tu kwenye kundi na zaidi mwenzake ndo alikua anafahamika zaidi? Alitushangaza sote na pia tulimpoke kwa mikono miwili.
Kama mwanafunzi Ilunga alikua ni mtu wa kupasi kwa maksi za juu haswa na nna uhakika kama insengekua mziki kipindi kile (sijaribu kusema kwamba mziki ni kitu kibaya) ila anagezingatia masomo kwa asilimia mia moja basi naamini anagekua mbaaali kuliko alipo sasa (na si kwamba alipo sasa ni pabaya). Akiwa anazunguka kwenye tour yeye na mwanaye Ismail kipindi hicho, Ilunga alikua anakosa sana masomo mpaka kuna kipindi ilikua inabidi atungiwe mtihani mwengine na aufanye peke yake maana wenzake wanakua washafanya mitihani yao wakati yeye alikua nje ya Dar es Salaam kuendeleza kipaji chake na kutoa burudani.
Sasa, nini haswa kilotokea kati yake yeye na Ismail? Kwanza haswa walikutana lini? Wapi? Ilikuaje siku ya kwanza? Na kama kundi walikua wanaishi vipi? Waliwezaje ku handle umaarufu kipindi hicho? Walikua wanatengeneza pesa? Je wazazi wake walikua wanamruhusu kukosa shule na kufanya mziki? Nani alimfanya yeye avutiwe na mziki? Ana majuto yoyote katika maisha yake? Na je Baba na Mama yake ni watu wa aina gani? Ameoa? Mtoto? Kazi gani anafanya? Pia alikua rafiki mzuri wa Marehemu Mangwair, kifo chake kimemuathiri vipi? Na industry ya sasa je anaweza kutoboa? Wallahi kulikua na maswali mengi Ila na majibu nayo hayakua nyuma, yangu matumaini na hii pia itakufunza jambo, tafadhali enjoy.
Love,
Salama.
Follow:
Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown
Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown
Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown
Fatma Abeid Amani Karume ni mtoto wa kwanza wa rais wa sita wa Zanzibar na pia ni mjukuu wa rais wa kwanza wa Zanzibar na kiongozi wa mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 na pia ni mwanasheria hodari, na siku za hivi karibuni amekua mstari wa mbeeele kupaza sauti kwenye masuala ya kisiasa hapa nyumbani Tanzania na ni kitu ambacho kimempa umaarufu mwingi kwa wananchi na kupachikwa jina la Shangazi, yeye ndo SHANGAZI wa Taifa.
Kuzungumza naye imekua kama mtihani kiasi maana yeye ni wakili na sote tunafahamu jinsi ambavyo mawakili wanavyojua kuongea kwahiyo ilibidi nitulize nywele kweli kweli ili tuweze kwenda sawa, mwanzo ulikua mgumu lakini tuliweza kutuwamisha maji baada ya muda kiasi na natumai utapata majibu ya maswali ulokua unajiuliza. Pia ilikua emotional kwa kiasi flani maana habari ya ofisi yake kupigwa bomu mwaka 2017 na kupigwa risasi kwa aliyekua rais wa chama cha wanasheria Tanganyika na mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu siku kumi tu baada ya tukio la ofisi kutokea Dar es Salaam lilimfanya awe emotional. Na kama utakua unakumbuka vizuri Shangazi ndo aliyefuata kuwa rais wa TLS baada ya hapo.
Zaidi mi nilitaka kufahamu haswa nia na madhumuni ya kupambana kwake na kutonyamaza kwake kwenye masuala yote ya uongozi na serikali. Na kama pengine na yeye ana ndoto za siku moja kuwa kiongozi, au pengine leo simu ikiita akapewa cheo, je atakichukua? Na nini anataka, nini angependa kibadilike? Huwa anapokea simu toka nyumbani na kuambiwa pengine apunguze kelele kidogo? Au yuko huru tu kuongea? Na mambo ya familia? Na je kuhusu Babu yake na enzi za ASP? Anazikumbuka hizo enzi? Na kuhusu shule je? Alisoma wapi? Alikua smart alipokua mtoto? Anamkumbuka Babu yake? Lini mara ya kwanza alijua kama yeye ni “special”? Na kuhusu mapenzi je? Mara yake ya kwanza kumpenda mtu? Alikua nani? Alikutana na mumewe akiwa na miaka mpingapi? Na kwao je wako wa ngapi? Na yeye ni wa ngapi? Shule ipi alienda?
Kuna suala la yeye kuzuiliwa kufanya kazi pia, licence yake imezuiliwa hapa, pia nilitaka kujua sasa anashije? Na kama ana watoto? Yeye ni mama wa aina gani? Akiacha kuwa Twitter huwa anafanya nini? Kuna mambo anayopenda kuyafanya ambayo sisi hatuyajui? Na kama kuna uwezekano wa yeye kujikita kwenye siasa? Maongezi yalikua marefu na machachari rafiki, na matumaini yangu utapata majibu ya maswali ulokua unajiuliza juu yake… Tafadhali enjoy.
Love,
Salama.
Follow:
Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown
Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown
Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown
Sebastian Bigacho Ndege, jina kubwa nchini kwetu na anajulikana na watu wa aina tofauti tofauti, hiyo ndo tofauti yake yeye na ‘celebrities’ wengine. Ukiachana na kwamba ni Daktari hodari tu na mtangazaji wa radio mahiri kabisa ambale alijenga historia miaka ya nyuma kwa kuwafanya watu wawe huru kuongelea juu ya suala la maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi, Seba (hivyo ndo anavyofahamika zaidi au Dr Seba au hata Jembe ni Jembe) aliweza kuwafanya watu wawe huru kuongelea pia masuala ya magonjwa ya zinaa na unyanyasaji wa kijinsia kwenye kipindi chake cha NJIA PANDA. Kutumia kipindi hiki, aliweza pia kubadilisha maisha ya yatu wengi ambao walikua wanaishi maisha ya ukimya kwenye suala la ugonjwa na unyanyasaji wa kijinsia, kupitia kipindi hake alitoa elimu ya waziwazi kwenye suala la gonjwa la Ukimwi na kuwafanya watu kuuelewa ugonjwa na jinsi ya kupambana nao na kujikinga pia.
Toka alivyokua mwanafunzi Dr Seba alikua mjanja na muerevu, alijifunza mambo mengi kwenye muda wake wa ziada, na ndo yalimfanya awe mbele ya wenzake wengi. Nafasi za kuelimisha na uongozi zilipokua zinajitokeza Seba alikua wa kwanza kuzipata maana tayari alikua na ufahamu kuliko wenzake wengi. Alikua mwanafunzi wa kupasi daraja la juu na hilo lilitokana na kutokea kwenye familia ya kisomi ambayo iliweka elimu mbele kabla ya mambo mengine.
Dr Seba anafanya kazi zaidi ya nne hata alipokuja kwenye maogezi haya ilibidi tumsubiri kwa muda ili amalizie ku edit CV yake ambayo alikua akiituma sehemu ili aweze kupata kazi aliyokua akiifukuzia. Yeye ni Mkurugenzi wa Jembe ni Jembe FM pia ni Mkurugenzi wa Ndege Insurance lakini pia miaka ya nyuma alikua na Band ambayo kusema za ukweli ilitoa ajira kwa vijana wengi na pia kutoa ushindani kwa band nyengine ambazo pia zilikua zinafanya vyema kipindi hicho.
So,anawezaji kufanya yote hayo? Kumbuka pia kuna wakati huwa anafanya yale makongamano ya kuhamasisha vijana kwenye mambo mbali mbali na pia ni moja ya vitu anavyoviweza sana ukichukulia kuongea pia ni moja ya vipaji vyake. Anawezaje? Anajipangaje? Bila ya shaka unafahamu pia kama mwaka huu alitangwazwa kuwa ni mmoja kati ya watu ambao wanamsisamia Harmonize kwenye mziki wake, kitu ambacho kilinyanyua nyusi za baadhi ya watu. Je ana uzoefu huo? Ataweza? Ni mtu sahihi kwa nafasi hiyo? Na kuhusu familia yake je? Ulikua unafahamu kwamba ametokea katika familia ambayo Mungu aliibariki kwa kipato? Pengine mafanikio yalianza kutokea huko?
Majibu ya maswali yetu yalipatikana baada ya kuongea nae pale tu alipomaliza kutuma CV yake. Tuliongea kuhusu udaktari, njia panda, familia, biashara, challenges za maisha, ubunifu na of course Harmonize. Yangu matumaini utapata jambo la kujifunza humu na ku enjoy pia.
Love,
Salama.
Follow:
Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown
Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown
Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown
Kusema ukweli kabisa mimi na mgeni wetu wa wiki hii hatuna urafiki wala mazoea kabisa, ila tunafamiana kwa mbali na pengine (naamini) kila mmoja anamheshimu mwenzake kutokana na kazi ambazo kila mmoja wetu ameshafanya, na hiyo ndo ambayo imeleta heshima kati yetu. Pia tukumbuke heshima hainunuliwi wala haihongwi, huja yenyewe na kutuwama pale inapoona inafaa.
Kwa kipaji na jina lake kuwa kule na huku nami ndo nilimfahamu Baba Levo. Utani wake kwa wasanii wengine (hasa siku za hivi karibuni) watanzania wamekua wakiuona sana. Ila kwa mujibu wa historia chache juu yake ambayo nilikua naifahamu Baba Levo siku zote amekua mtu wa utani mwingi, na kwa uelewa wangu pia amekua akitumia utani huo pia kufikisha ujumbe wake kwa alomdhamiria, na kwa aliyetumiwa ujumbe pia ataupata pengine huku akiwa anacheka. Nani atasahau matani yake kwa Peter Msechu juu ya uzito wake uliopitiliza ambao pengine unahatarisha maisha yake. Baba Levo amekua mstari wa mbele kumbukusha Peter hilo.
Pia kuna ishu za yeye kuwa ‘Chawa’ wa baadhi ya wasanii na viongozi. Lakini pia yeye ni KIONGOZI ambaye wananchi wamemchagua, na chama cha ACT kiliridhia yeye kuwakilisha Chama, hilo si jambo ya mzaha na bila ya shaka anahitaji heshima kuliko ile ambayo tunamuonyesha ingawa pengine jinsi yeye binafsi navyojijeba ndo kunatufanya tumchukulie hivyo, lakini haiondoi heshima na uaminifu ambao Chama chake kilimpa pamoja na uaminifu kwa kuwatumikia wananchi wa Kigoma kule, kama diwani wao walompa dhamana. Baba Levo pia ashawahi kuingia matatani kwa ugomvi wake na dola baada ya kuvunja sheria za barabarani, kisa ambacho kilimfanya akae jela kwa takriban miezi mitano.
Mengi sana yalikua yanahitaji uchambuzi na ufafanuzi, na kujuana pia kati yangu na yeye. Maongezi yetu yalikua kati ya muuliza maswali na mtoa majibu ambae alikua ana maelezo yake mengi sana na kwa hilo namkubali sana. Tumeongea kuhusu Siasa, muziki, familia, uongozi na marafiki. Yangu matumaini una enjoy kama ambavyo nami nili enjoy na kujifunza kutokana na maongezi haya. Nakutakia kheri na tafadhali enjoy.
Love,
Salama.
Follow:
Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown
Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown
Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown
Jina halisi ni Salim Ahmed Issa, na kwa mujibu wa niloyasoma ni mjukuu wa moja ya watu maarufu mkoani Iringa ambaye alikua anatambulika kama Mtogapaafwe Kiyeyeu. Huyo alikua ni BABU wa Gabo Zigamba kabisaa ambaye binti yake Rafia Issa Kiyeyeu ndo Mama mzazi wa Gabo huyu tunayemfahamu mimi na wewe. Unaambiwa kaburi la Marehemu Mzee Mtogapaafwe lilikua na maajabu sana, ila hiyo ni khadithi ya siku nyengine. Hapa ilikua juu ya utambulisho wetu kwake na sifa zake actor hodari toka kwetu Tanzania.
Gabo si moja ya marafiki zangu ila baada ya kuonana hapa ndo urafiki wetu ulipoanzia baada ya kujua pia tunafanana kwa mambo mengi kwa kweli. Gabo ni MTENDAJI, kuongea anaongea pale anapokua huru na mazingira ila mara nyingi huwa hasemi sana bali anatenda zaidi. Toka nimemsikia mara ya kwanza mwaka 2016, kijana huyu amekua akishinda tuzo mbali mbali na kutengeneza base yake vizuri kabisa. Na ukimuuliza mtu yoyote anayefuatilia mambo ya filamu kuhusu yeye basi hakika utaskia kipaji chake kikizungumziwa pia. Tuzo mbali mbali Gabo ameziokota sana na mpaka kuna kipindi ilikua inasemekana kwamba yeye ndo ‘mrithi’ wa Marehemu Steven Kanumba kitu ambacho kinaweza ikawa motivation au viatu vikubwa sana kwa miguu yake. Swali ni je, anajua watu wanamuona huko?
Kwenye kikao chetu zaidi mimi nilitaka kumfahamu haswa, kumfahamu yeye binafsi na familia yake, nilitaka kufahamu kinachompa raha na karaha. Nilitaka kujua alianzia wapi, nilitaka kujua starehe yake, mipango yake, mitihani yake. Nilitaka kujua kuhusu jina lake, kuhusu kipaji chake, kuhusu dini na mahusiano. Kuhusu industry na ushindani wa ndani na nje na Sanaa kwa ujumla. Na nashkuru alinipa time yake na yangu matumaini humu utapata chochote kitu cha kukufunza jambo. Tafadhali enjoy.
Love,
Salama.
Follow:
Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown
Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown
Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown
Kwa Judith Wambura Mbibo kuongea anayoyawaza bila ya kupepesa au kutafuta sapoti kabla hajafanya hivyo ndo hulka yake haswa, si wa kukwepeshakwepesha au kung’ata maneno ili yawe malaini zaidi kwa anayeambiwa asijikie vibaya labda. Kwake yeye lilivyo ndo lilivyo, kazi ya kupaka mawingu rangi huwaachia wahusika, yeye yake ni kuhakikisha mawingu yapo, na kwa hilo? Mimi namheshimu sana.
Mwanangu mwengine ambaye hii ni mara yetu ya kwanza kukaa chini na kutia story ili wananchi waweze kupata majibu ya baadhi ya maswali waliyokua nayo muda mrefu sana pengine. Na round hii nilihakikisha sichezi mbali naye kama Chama na Mogella, na kwa bahati nzuri muda wake na wangu ukaenda vizuri kabisa kwa sote kuweza kuifanya kazi hii. Ijumaa ya kuamkia Jumamosi ili kuweza kuifanya kazi hii ulikua usiku mfupi sana kwangu. Mawazo yalikua huko tu kwa Jide na kwa kwa watu wengine watatu ambao nlikua na kikao nao. Na Nashkuru Mungu mambo yalienda kama yalivyopangwa.
Kuanzia kulelewa na Kaka zake alipokuja Dar es Salaam na kuhakikisha anakua katika maadili mema kwahiyo haikua rahisi kwake kuhakikisha agenda yake ya kutaka kuwa msanii na mara nyengine alikua akichezea kichapo kwasababu tu alikua harudi nyumbani kwa wakati au nyendo zake zilipokua hazieleweki. Baba yake alifariki zamani na Mama yake alifariki 2017 kama nitakua sawasawa. Sikutaka kwenda kwenye details sana juu ya kifo cha Mama yake ila zaidi nilikua nataka tuongelee ubora wake ambao umekua ni kivutio kikubwa kwa wale wanaoanza na ambao tayari washaanza. Kujifunza kwake juu ya ukomavu, uvumilivu, jinsi ya kujibeba. Kutafuta nafasi, kutokata tamaa na kuandika historia. Na kwa hilo alituambia mengi.
Kuna issue ya wivu, ndoa, kazi, mahusiano, kipaji na kuwa mwanamke ndani ya kiwanda kichanga ambacho kimezungukwa na wanaume na jinsi ya kupasua milango ya kuziba matabaka ili mambo yaende na historia iandikwe. Vipi aliwezaje ku push hivyo? Na lini haswa alijua ana kipaji chake kikubwa ambacho kinatakiwa kuonekana? Kuna support yoyote aliipata toka nyumbani? Na je baada ya mlango kufunguka, aliwezaje ku maintain hiyo nafasi? Mwaka huu wa 2020 Lady Jay Dee anatimiza miaka ISHIRINI toka ameanza kufanya mziki RASMI. Je hii ndo definition ya MAFANIKIO kwake?
Yangu matumaini maongezi yetu yatasaidia sehemu flani na kuongeza jambo kwenye mbio zako za kutaka kuzifuata ndoto zako. Tafadhali enjoy.
Love,
Salama.
Follow:
Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown
Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown
Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown
From the publisher's feed