
Sign up to save your podcasts
Or


Huyu si moja ya marafiki zangu, as in si Mtu amable nafahamiana naye sana, ambaye nishawahi kukaa naye muda mrefu na kupiga story, au kusafiri naye au kuwa studio wakati anafanya mambo yake au namjua mzazi wake au mtu wake wa karibu kwenye familia yake ila nawajua watu ambao wanamfahamu kwa ukaribu na watu hao ndo ambao walinipa mimi mawazo ya kutaka kumfahamu vizuri binti huyu hodari wa ki Tanzania bila ya hata ya wao kujua.
Baadhi ya Dada zangu walifahamiana naye kwenye kipindi cha msiba wa Marehemu Ruge Mutahaba, kipindi hiko kilikua cha masikitiko kwao na kwake pia. Nandy alikua na ukaribu mwingi na Ruge, alishawahi kumtembelea hospitali mara kadhaa na pia alikua na mawasiliano ya moja kwa moja na watu wa karibu wa familia kipindi kile ambacho Ruge alikua hana tena mawasiliano naye moja kwa moja. Siku ambayo Ruge alitangulia muelle ya haki, muda si mrefu kabla ya hilo halijatokea Nandy ananiambia alizungumza na nesi wa zamu siku hiyo na pia alimuekea simu kwa ukaribu na alimsikia akiwa anapumua. Wapi alikua wakati anapata habari hii iko kwenye maongezi yetu haya, humu pia utaelewa connection ambayo sisi binadamu tunayo na watu ambao tunawapenda na wanao wanatupenda.
Najua siku hazigandi kama ambavyo Lady Jd alishawahi kuimba na ndo nikawaza, hivi ushawahi kuwaza Nandy amekua kiasi gani toka msiba wa Ruge utokee? Unakumbuka baadhi ya maneno yalosemwa juu ya career yake baada ya msiba ule? Tunafahamu kwamba alipoteza rafiki, mentor, baba na kama tochi yake? Mimi huwaza haya sana, na hilo la yeye kujidhatiti na kukaza mwendo ndo ambalo lilifanya mimi binafsi niseme you know what, it’s time.
Nandy ni MPAMBANAJI, anaupenda muziki na kama mtu mwengine yoyote mwenye jitihada basi Mungu humfungulia milango ya Kheri. Kaniambia humu kwenye mangezi yetu kwamba safari yake ya kwanza kwenda nchini Nigeria kwenye mashindano ya kuimba alimuambia Mama yake wakati yumo ndani ya ndege, alipomaliza hutuba yake fupi alizima simu na wheels up, to Lagos ambako alihakikisha anapigana mpaka fainali na kumaliza nafasi ya tatu. Si kitu kidogo kwa binti ambaye aliamua kuweka shule pembeni ili atimize ndoto yake, ndoto ambayo hata Mama yake mzazi hakua na taarifa nayo.
Siku zinakwenda, maisha yanasonga na yeye ameendelea kukimbiza ndoto yake na mpaka tunaenda mitamboni, Nandy ni mmoja wa wasanii wa kike wakubwa sana hapa nyumbani na barani Afrika na hata Ulaya na Marekani na ukitizama vizuri utajua kwamba huu ni mwanzo tu wa mazuri ambayo yatatokea katika maisha yake. Mimi na yeye tulizungumzia mahusiano hayo pamoja na kukimbiza ndoto zetu. Tuliongelea Bill Nas na kiwanda cha muziki wa Bongo Flava. Tuliongelea muziki wake na collabo ambazo amewahi kufanya. Hapo hapo nilitaka kujua pia yeye ni mtu wa aina gani na ni vitu gani vinamsukuma kutaka atake zaidi na sehemu ambayo anajiona huko mbeleni In Shaa Allah.
Yangu matumaini kama kawaida ni kwamba utajifunza mawili matatu ambayo yatakusaidia kupambana na mitihani ya maisha kwasababu tu umejifunza kutokana na sehemu wenzetu hupitia kwenye maisha yao.
Tafadhali Enjoy.
Love,
Salama.
Haji Sunday Manara nlitaka kusema ni rafiki YANGU ila vacati navaza hilo nikakumbuka mmh, Haji Sunday Manara ni rafiki wa WATU WENGI hususan mashabiki wa klabu wangu pendwa na zaidi kwa watu ambao hawapendi hata mpira ila wanampenda tu jinsi anavyoseti mambo yake na anavyoigeuza sehemu yoyote aendayo kama sehemu yake ya kujitamba na kujitutumua na tofauti yake na WACHACHE ambao wanafanya kazi kama yake ni kwamba yeye anaweza KUYATEMBEA yale anayo YAONGEA.
Hamis Tale Tale ni MWAMBA wa maisha yake na ya wale walomzunguka kwa miaka nenda miaka rudi na kutoka upande huu wa muandishi na mtangazaji ni heshima tu kwenda mbele. Kuna msemo mmoja wa Kiswahili kuhusu nyani ambaye unamkuta mjini. Ya kwamba anakua kashakwepa MISHALE ya kutosha kwahiyo unapomkuta town inabidi umpe heshima zake za kutosha.
Turudi nyuma mwaka 1999 wakati nilipomaliza kidato cha nne kwahiyo nilikua sina mitkasi mingi zaidi ya kumkimbia Mama inapofika mchana ili niende kucheza zangu basketball pale Msasani kiwanja cha Pazi. Nlikua natokea zangu Mbagala Charambe nachukua zangu basi mappa Mbagala Rangi tatu then muunganisho unaendelea mpaka nafika zangu mazoezini, nilifanya urafiki na makonda na madereva weeengi kiasi kwamba nilikua ‘staff’ kwenye daladala nyingi, na huwezi kuamini nyingi pia nilikua nikiingia basi radio nlikua namiliki MIMI. Station gani tunaskiliza au tape gani tunaweka ili safari inoge na muziki. Nakumbuka jinsi ambavyo Sugu alikua anaikosha, anakosha nafsi yangu na ya abiria wote ambao walikua wanasafiri nasi basi moja. Chini ya miaka 18 ilikua inaongea na mimi haswam inanifanya nisitake kuwa yule binti ambale Sugu alikua namuongelea ASILAN! Mikononi mwa Polisi… Album kali kama Nje ya Bongo, Millenium, Muziki na Maisha zilifuata na wakati hizi nyengine zinatoka nami tayari nilishaacha kumtia wasiwasi Mama yangu wa kurudi nyumbani usiku na kuwa DJ wa muda ndani ya Daladala za Mbagala Posta au Mbagala Kariakoo na kuweza kupata kazi yangu ya kwanza pale Times FM kabla sijajiunga na EA Radio na TV.
Kwa muda mrefu nimekua nikitaka kuongea na Mavoko ila ratiba zetu zilikua hazijawahi kuwa sawa na hivyo tukawa tunapishana tu. Kama mimi sina program naye basi yeye atakua free, na mimi nikiwa free basi yeye atakua na mipango ya kutoa kazi mpya ambayo itanifanya ningoje ili viende pamoja, au atakua kasafiri, au mimi nitakua nishaset watu wengine, ilikua kama tunacheza kidali po ila katikati ya mwezi wa kumi na mbili hatimaye yakatimia.
Hakuna doubt juu ya uwezo wake popote pale utakapoenda ingawa baada ya yeye kuamua kuondoka kwenye label ya WCB kulikua na mengi yalosemwa na kutendwa na baadhi ya mashabiki yalikua yanaweza kukuaminisha jambo na mpaka kufikia pengine ku doubt huo uwezo wake. Mambo mengi yalisemwa, ya kusikitisha, ndoa haikuvunjika vizuri ila ambacho nilikiona kwake ni ustaarabu wa hali ya juu, wa kuwaacha walimwengu waseme na kufanya watakayo huku yeye akiwa ame focus kwenye kipaji chake na kujipanga upya.
Moto wa Mama Richard anaujua mziki mwingi, ana uwezo mkubwa wa kuimba na kuandika na kucheza pia, ila kabla hajaingia kwenye label alikua anajulikana tu, ila kumfahamu vizuri na kuthamini kipaji chake kulikuja baada ya yeye kushirikiana na mmoja kama si msanii bora zaidi kuwahi kutokea na kuipeperusha zaidi bendera ya Tanzania ndani ya Diamond Platnumz. Ushirikiano wao ulitupa ‘anthem’ kadhaa ambazo mpaka leo ukiziskiliza hazichuji. Ilikua kama team ya wenye vipaji pekee, kama ni mfuatiliaji wa mpira wa kikapu hii tunaweza kuifananisha na ile zile team mbili za Mashariki na Magharibi ambazo zinakusanya wachezaji wenye uwezo wahali ya juu.
Saasa, ikawaje hasa mpaka akaona aachane na all star hiyo na kupeleka team yake uwanjani akiwa solo? Nini hasa kilifanya mpaka afikie maamuzi hayo? Kuna mtu au kitu kilimshinikiza? Je yalikua maamuzi sahihi? Pia kuna masuala binafsi ya kifamilia na suala la yeye kutomfahamu Baba yake takati anakua, elimu yeke, ndugu zake, Mama yake na muziki ulichomfanyia katika maisha yake.
Mavoko huyu ambaye mimi namfahamu nilikutana naye Kampala, Uganda kama maka saba iliyopita na mazungumzo yetu yalikua yanahusu kipaji chake na jinsi ambavyo nilikua naona ‘hapewi’ nafasi maana kama ngoma zake zilikua nzuri tu, video ndo usiseme ila hakuna na spotlight aliyokua anastahili, peleka mbele miaka mpaka 2021 ambapo alipata nafasi kwa miaka takriban miwili na nusu kufanya kazi na lebo bora zaidi ila baada ya muda akaamua kubwaga? Kwanini hasa? Sote tunajua kama nyasi za jirani huonekana zimestawi kweli kweli ila ukifika na kuziona kwa ukaribu utaelewa kwamba si kila kitu kina fanana na kionekanavyo. Ila mpaka kuamua kukusanya na mabegi na kuondoka kwenye ‘jumba kali’?
Majubu yake yalikua ya moja kwa moja tu na nafsi yake ilikua tayari kuhamia nyumba nyengine mwenzangu. Natumai kwa kiasi flani utasoma jambo, ingawa kwangu mimi natamani ningepata zaidi na zaidi ila inaonekana bado hakua tayari kutufungukia mazima. Binafsi namshkuru kwa kuja mezani kwetu na pengine tutaweza kukutana tena mbeleni In Shaa Allah. Yangu matumaini bado utaokota mawili matatu.
Love,
Salama.
Muda si mrefu iliopita nilirudi nyuma kidogo kwenye kumbukumbu ya mawasiliano ya kwanza kabisa kati yangu na moja wa wasaidizi wake Mheshimiwa Jakaya Mrisho wa Kikwete na hiyo ilinirudisha nyuma mpaka mwezi wa tatu mwaka 2020. Kama mtu mwengine yoyote hii ilikua ndoto tu ambayo kwa Rehema na Baraka za Allah ilibidi itimie. Kwa Baraka zake hizo mimi na wenzangu tunashkuru sana sana kwa kuweza kulikamilisha hili.
Lucas Mhaville ni maalum sana, kwa ki vyovyote vile utakakavyotaka wewe, ki maisha, ki muonekano, ki uelewa na jinsi anavyokua mpya kila siku kwenye ulimwengu wake, jinsi anavyo jipa matawi na kujigawa kisanaa. Jinsi anavyotoa character wapya kila mara kwaajili tu ya kuleta ladha mpya kwenye sanaa yake, hili linamfanya aendelee kuwa mchekeshaji pekee kwenye kizazi chetu ambaye huwezi kuona amechuja au hana jipya kwenye kukufurahisha wewe.
Sikuwahi kuujua ufahamu wa Dr Hamisi Kingwangala kwenye suala la dini kwa kiasi ambacho ameniambia wakati tunaongea kwenye kikao chetu hiki, na alinilelezea kwa majina yake ya kizuoni huku akiniambia nini kwa binafsi yake anaweza kukifanya kwa kituo pale anapotaka, lakini pia aliniambia juu ya suala la yeye kutokua anaswali sala tano kama ilivyokua zamani na kwamba si jambo analojivunia asilan!
Hii ilikua mara yangu ya pili kukutana na kuongea nae kwa kituo, kama ilivyokua kwa Taji nae pia niliongea naye miaka ya nyuma wakati nafanya Mkasi, na kwa kuongea naye round hii nimejifunza kwamba hawa ni kama watu wawili tofauti kabisa na si kwa ubaya, yule wa kwanza alikua si muongeaji kama huyo wa sasa kwasababu amekua kwa kiasi flani na kukua ni jambo ambalo sisi wenyewe na wazazi wetu huangalia kwa makini kuanzia pale ulipokua tuseme miaka mitano iliyopita na sasa na mipango na maratajio yako. Kwa hili Sheikh HK kaserebuka nalo vizuri tu. Hakuna mtu asiyemfahamu Hamis Kingwangala ndani ya nchi hii na nje, jinsi ambavyo alifanya kazi nzuri ya kampeni ya kuitangaza Tanzania duniani kwa umaarufu wa vivutio vya utalii wetu na utajiri wa nchi yetu pendwa. Alichukua muda huo pia kutembelea karibu mbuga zote na nchi hii na wakati huo huo kupambana na majangili na waharibifu wa wanyama pori, vita ambayo ilikua ndo stori ya kipindi flani hapo nyuma. Yeye HK alikua anamalizana na maneno ya walimwengu ambao walikua wanaongea mengi kwenye mitandano ni kwa yeye. kuendelea kupiga kazi yake vizuri tu mpaka akamaliza miaka mitano ya kwanza ya Rais aliyempa cheo hicho kwa usalama tu, nasema hivyo kwasababu kuna wengi ambao walikua wanateuliwa lakini siku zao za kukaa ofisini hazikua nyingi sana ila HK aliweza kuendana vizuri na mawimbi kwenye bahari ya uongozi ambayo bila ya shaka ilikua na mitihani yake.
Pia umaarufu wake mwengine Bwana HK ulikuja baada ya kuwa ntumiaji mzuri sana wa Twitter, sehemu ambayo huitumia kwa kufanyia kazi yake ya kuitangaza nchi na pia kumalizana na ‘wabaya’ wake wote ambao wamekua wakila nae sahani moja kila mara panapokua na jambo ambalo yeye amesema au kuwakilisha mooni yake juu ya suala flani. HK hana tabia ya kuona haya kumjibu mtu ambaye kwa namna moja ama nyengine anakua kamgusa pale alipokua hapataki yeye au pengine tofauti tu ya mawazo, muda mwengine utakuta watu wamefika huko.
Kubwa kuliko ilikua hii ya mwaka huu ambayo alihoji juu ya uteuzi wa CEO mpya wa klabu yake pendwa ya Simba na pia suala la mwekezaji kutimiza ahadi yake ya kuipa Simba shilingi bilioni 20 za kuendeleza klabu. Hili suala liliamsha zogo kubwa kati ya HK, muekezaji wa klabu pamoja na mashabiki wa Simba, lilifanya pia tujue siri za ndani za kibiashara kati ya wawili hawa na jinsi ambayo wote wawili walivyokua wanajibizana mitandano ilifanya watu wengi wanyanyue nyusi kwa mshangao na kujuzwa mambo ambayo pengine yalikua hayana faida kwa watu wengine kujua. Hivi karibuni wawili hawa walimaliza tofauti zao huko huko kwenye mitandao hiyo hiyo ya kijamii kama walivyofanya awali.
Niloitaka kujua kama kuna muendelezo wa hayo maongezi yao, kama walishakutana toka majibizano yale yatokee, pia tuliongelea ajali ambayo aliipata akiwa kazini na ambayo pia ilizungumziwa na watu wengi. Pia niliongea nae kuhusu Rais Magufuli, uchaguzi wa mwaka huu ambao chama chake kimeshinda kwa ushindi mnono na jinsi ambavyo hakupata nafasi kwenye baraza la mawaziri na manaibu wake ambalo limeundwa hivi karibuni na ambavyo aliipokea taarifa hiyo.
HK ni mtu poa sana, kijana ambaye ni Kiongozi, Baba, Kaka na mfanyabiasha mzuri tu ndo darasa letu la wiki hii na yangu matumaini kana kawaida atakua na jambo la kukufunza kwahiyo tafadhali enjoy.
Love,
Salama.
Pia anafahamkika kama Master T, mwenye sauti yake tamu ya kumfanya mtu abadilishe mawazo na kufanya anachosema yeye, lafdhi nzuri ya maneno ya Kiswahili na Kiingereza na tabasamu zuri kabisa lililokaa mahala pake na hiyo ndo tofauti ya Taji Liundi na watangazaji pamoja na hata viongozi wa department mbali mbali kwenye vyombo vyetu vya habari vya ‘siku hizi’.
Hassan Mwakinyo kwa Mama yake ni kama ni kama mkate kwa chai tu, lazima ulainike. Sentensi hii imeanzia hapa baada ya kufuatilia kwa makini na kuambiwa hasa ni kitu gani kinachomfanya Champez atake kuwa bora zaidi na zaidi, na kutaka kupata kile anachokipata kwa nguvu zaidi na zaidi kila siku kila asubuhi anapoenda kukimbia, au kila jioni anapokua gym au anapokua ulingoni, na amini kwamba Mama yake ndo anayemfanya atake kuwa bora siku zote ili aweze kumbadilishia maisha yake kwa uzuri.
From the publisher's feed