
Sign up to save your podcasts
Or


Kila kijana wa ki Tanzania ambae anaupenda na kuuthamini mpira wa miguu na ambaye angependa ndo iwe kazi ya maisha yake basi Mbwana Ally Samatta ndiye role model wake, hakuna doubt kwamba watakua na mapenzi na Cristiano Ronaldo au Leo Messi au Kylian Mbappe au Marcus Rashford ila yule ambaye amewaaminisha kwamba INAWEZEKANA ukacheza POPOTE hapa duniani na hasa kwenye ligi yetu pendwa ya Uingereza ni Samatta. Rafiki tu kutoka Mbagala rangi tatu ambaye kashacheza saaana ndondo na makombe ya mbuzi wakati anakua na mwisho wa siku akaenda kucheza kwa wazungu na bado anaendelea kutafuta rizki yake huko, hata kama sio ligi ile ambayo hata yeye mwenyewe angependa awepo ila BADO ni MWAMBA wetu. Samatta huyu huyu ndo ambaye alijitwika mpira kichwani na kuitika nyavuni mbele ya beki ambae anaaminika kuwa BORA kwa misimu hii miwili mitatu ndani ya Virgil van Dijk. Hata wakati naandika hii bado mwili unanisisimka kwa wazo tu kwamba nililishuhudia lile, pata picha kwa mtoto ambaye ana ndoto hizo. Lile goli lilimfanyia NINI kwenye ndoto zake. KRC Genk walipoteza mchezo ule wa ugenini wa kombe la mabingwa wa Ulaya kwa magoli 2-1 ila kwenye mitaa yote ya mikoa ya Tanzania ile mechi ilikua ya USHINDI.
Mbwana ametokea kwenye familia ya kawaida sana sana, wazazi wake wote kama kumbukumbu yangu itakua 100 basi walikua polisi, najua kwa hakika Baba yake alikua Polisi kwa asilimia 100. Kwa marehemu Bi Mkubwa wake ndo sina hakika sana ila kwa hakika jibu limo kwenye haya maongezi yetu. Anakumbuka jinsi ambavyo Mzee wake alikua anasisitiza kwenye suala la elimu na heshima, kama mtoto wa mwisho kwenye familia hiyo, Mbwana aliupenda sana mpira, zile za kujiiba na kwenda kucheza mechi za mbali alishafanya sana na matunda ndo haya ya leo. Nadhani ilifika kipindi Mzee mwenyewe aliona basi sawa, twende huko utakako. Familia yao yote ni wapenzi wa mpira na Kaka yake Mouhamed bado anacheza hapa hapa Tanzania. Sasa akiwa kama kioo kikubwa sana kwenye jamii hii Samatta anazungumzia presha ambayo hupewa hasa pale anapoitwa kwenye timu ya Taifa, jinsi maneno mengi ya kashfa yanaporushwa kwake kutoka kwa wananchi na anakumbuka pia wakati bado anacheza T.P Mazembe kuna kipindi kocha aliacha kumuita yeye na Rafiki yake Thomas Ulimwenguna ilisemekana kama pengine hakuna na interest na team au hakua anatoa 100. Pengine kipindi hicho aliumia zaidi maana hiyo haikua jambo zuri kwake.
Mbwana anazungumza na mimi kuhusu urafiki wake na Ulimwengu na maisha ambayo walikua wanaishi pamoja wakati wako DRC, anakumbuka jinsi walivyokua wanapanga kufanikiwa pamoja na mipango yao endelevu kwenye career yao. Ulimwengu nae ana siku yake kwenye kiti chetu In Shaa Allah maana nae ana mengi ya kutuelezea. Majeraha ya mara kwa mara bila ya shaka yalisababisha kwa kiasi kikubwa ndoto zake za kucheza Ulaya kutochukua hatua ya juu kama ambavyo angependa, ila mimi naamini hayo yote maisha tu, kila kitu kilikua tayari kimesha andikwa.
Samatta ni Baba ambaye watoto wake wanasoma hapa hapa nyumbani, nilimuuliza kama watoto wake wanajua yeye ni nani na akanipa story ndogo ya yeye kung’amua kama wanafahamu fika Baba yao ni nani.
Mwenzangu humu kuna mengi sana ambayo yatakufaa na kwa nafasi ya kipekee ningependa kumshukuru Captain wa Taifa kwa kuchukua time kwenye ratiba yake ambayo ilikua imebana kweli kweli ili tu aje kutubarikia meza yetu kwa uwepo wake.
Yangu matumaini uta enjoy sana.
Love,
Salama.
Dr Kumbuka ni influencer mkubwa kwenye masuala ya mahusiano na maelewano inapokuja kwenye suala zima la ushauri na mashauri kwa watu wengi ambao wamekua wakimsikiliza na ambao wanamsikiliza kila siku za wiki anapokua kwenye kipindi cha Uhondo pale EFM. Na yeye kuwa pale hakufika kwa bahati mbaya. Ila pengine alipo anzia kazi yake pale Times FM ndo ilikua kama bahati kufika. Anakumbuka jinsi ambavyo alikua zake tu mtaani wakati mtangazaji wa Times FM wakati huo Bi Dida Shaibu alipokua mtaani akitafuta watu wenye kipaji cha ‘kuchamba’ watu wengine. Anasema wanawake ndo walikua wametawala jukwaa huku wakishusha maneno mengi ya karaha kwa wanaume, na hapo ndo yeye alipoona nafasi ya kupanda jukwaani na kuwawakilisha wanaume wenzie kuhusu ila na karaha ambazo na wao pia wamekua wakizipata kutoka kwa wanawake.
Huo ndo ulikua mwanzo wa safari yake hii ya kuwa mmoja wa watangazaji hodari wa radio kwa muda huo anapokua hewani, EFM walivutiwa na kipaji chake na wao wakaona bora wamvute kwenye radio yao ili awatumikie wao na kipaji chake. Akiwa Baba wa watoto 5 sasa Dr anazungumzia kashfa na maneno mengi ambayo yamekua yakisemwa juu yake na muonekano wake na uzungumzaji wake. Anasema pia akiwa kama Baba na mtoto wake wa kwanza na wa pili nao wameshaanza kutumia mitandao ya kijamii na kuona comments ambazo watu wanaacha chini ya post zake huwa zinamtia unyonge wakati mwengine, hasa ile ambayo inahusu zaidi jinsia yake, mengine ya kwamba anajichubua huwa hayamsumbui asilani maana hiyo ndo rangi yake!
Alilelewa zaidi na Mama yake mzazi ambaye katika umri mdogo kabisa Dr ilibidi naye amlee Marehemu Mama yake maana hakukua na mtu mwengine kwenye familia ambaye angeweza kufanya hivyo, kwa mtoto wa kiume kumuogesha, kumvalisha na kumfanyia mengine ya faragha Mama yake mzazi ilikua mtihani, ila kwa sehemu ambayo alikua wakati huo, hakukua na njia nyengine ya kufanya. Alikua akimaliza kumtaarisha Mama yake anamuacha kwa majirani na hapo ndo yeye anapata nafasi ya kwenda shuleni.
Ni wengi wamepita na kushuhudia mengi wakiwa wanakua na mitihani na majukumu bila ya shaka hutofautiana, kwake yeye anaamini ni Baraka mara dufu kwa yeye kuweza kupata nafasi ya kufanya hayo yote kwa Mama yake kipenzi mpaka Mwenyezi Mungu alipo mchukua.
Na Baba yake je alikua wapi wakati haya yote yanatokea? Na je alikua Mzee wa aina gani?
Majibu ya hayo maswali yote Dr Kumbuka anatupatia katika episode hii ilojaa story nyingi za kukutaka utake kusikia zaidi.
Kama Baba ambaye hakupata nafasi ya kuwa na Mzee wake wakati anakua, Dr Kumbuka anahakikisha watoto wake sasa anawalea mwenyewe na kuwapa asilimia 100 ya uangalizi wake, na hiyo haijalishi kama Mama wa mtoto bado yuko nae au la, kwa yeye kuwa pale ndo kitu ambacho kinamfanya yeye ajiskia vizuri zaidi.
Yangu matumaini kutakua na mengi ya kujifunza kutoka kwenye episode yetu hii ya SABA ya msimu wetu huu mpya ambao tunahakikisha unapata kuwaskiliza watu wa aina mbalimbali ambao story zao zitakuvusha sehemu flani.
Love,
Salama.
Ushawahi kukutana na wale watu ambao wao ni wa pole tu sana na wanajipenda tu sana ila hawana tu muda wa kuringa au kuji mwabafy kwasababu wao wako talented au wana kipawa kutoka kwa Allah na wanajua? Well mi nishawahi kukutana na watu kama hao na mmoja wao ni mgeni wetu RASMI wa wiki hii ya episode ya sita ya SalamaNa msimu huu. Anaongea kwa utaratibu na kujua kile atakacho, anakipataje na akisha kipata atafanya nacho nini. Huyo sasa ndo mwanangu Mtani Nyamakababi, aka Mtani Beskope.
Kijana wa ki Tanzania mwenye kuelewa somo la leo na ukiachana na mitihani ambayo anakua anaipatia na mara nyingi huwa anafaulu kwa masksi za juu sana, kama daraja basi lake huwa ni la kwanza kabisa! Ufahamu wake na kujiongeza kwake kwenye knowledge na udambwi dambwi kwenye yale ayafanyayo kwa hakika ndo kunamfanya awe trend setter na wengine ambao wanafanya kazi kama ambayo yeye anafanya wabakie kumuona kama Role Model, naamini kwa kiasi kikubwa haata yeye bado hajioni kama Role Model maana safari yake ya kufika kule anapo pataka na kupaota ndo kwanza imeanza kustawi.
Miaka 30 ya umri mwaka huu wa 2022 bila ya shaka ni mwaka mkubwa kwake, ukiwa mtoto wa kiume na tegemeo la familia kufikisha miaka 30 ni jambo kubwa, hasa ukiwa hujaoa na una ramani ya maisha kama alo nayo yeye bila ya shaka utakua na mipango mingi, mengine yanawezekana na mengine ni kwa Rehema za Mwenyezi Mungu zaidi. Najua yeye anajua kama Mzee na Mama wanataka kumuona kijana wao akiwaletea wajukuu na I hope wazazi wake hawato subiri kwa kipindi kirefu kama ambacho Mama yangu mimi ameendelea kungoja . Yeye tayari yuko kwenye mahusiano ya kueleweka tu na ambayo yanaonekana yanaelekea mahali pazuri kwa mujibu wa maongezi yetu haya.
Kama binadamu wa kawaida of course alishawahi kuumizwa kwa uongo na kutokua na uaminifu kwenye mahusiano ila hilo halikuwahi kumrudisha nyuma kwa kuamini huyo alonaye sasa ni wake na anamfaa sana, anamsaidia sana na anamuongoza sana, vitu kama hivi mmoja huhitaji kuskia, hasa yule ambaye tochi yake imefifia mwanga, mwangaza wa mapenzi. Anamkubali sana yule anaye share nae siri zake na struggle zake na ushindi wake mwingi na hata frustrations zake. Na anajua pia kama kuna kupanda na ku shuka kwenye mahusiano na maisha kwa ujumla.
Kwenye meza yetu kulikua na maongezi kuhusu wazazi wake na principle zao za maisha, mdogo wake… Biashara zake na ushindani, mapenzi na uaminifu. Urafiki, ku shinda na kushindwa na pia maoni yake zaidi kwenye vitu mbali mbali ambavyo vinahusu ambayo anafanya na vile ambavyo amekua akitamani kuvifanya. Wapi anajiona baada ya miaka 5 mengine? Well… Hatukuongelea masuala ya hela maana najua hiyo ingemfanya asiwe huru mbele yetu maana mambo kama hayo yanahitaji mtu ambaye hana noma za hivyo ila kwa Ndugu yangu huyu yeye noma anazo, tena nyingi kwahiyo kistaarabu kabisa nikaona NIMUACHE.
Yangu matumaini utaokota kadhaa humu ambayo yatakupa mafuta ya ZIADA ya kutaka kesho uamke salama na kwenda kuwa BORA zaidi ya JANA kwa lolote ambalo utaamua kufanya na lenye kheri na wewe. Mimi nakutakia BARAK ZOTE kwenye hilo maana mifano hai ya wanao jituma na kufanikiwa ipo. Maana yake ni kwamba, inawezekana. Wewe tu!
Love,
Salama.
Mwaka 2018 ndo nilimfahamu Oscar baada ya kukutana nae kwenye kituo changu cha kazi ya kutangaza mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika jijini Johannesburg nchini Afrika ya Kusini. Alikua mmoja ya watu ambao walinikaribisha vizuri sana kwenye team na kwa wakati huo yeye ndo alikua anaishikilia rekodi ya kuwa ndo mtangazaji mdogo zaidi kwenye team ya watangazaji nami nikaja kama Binti PEKEE ambaye ambaye alikua anatangaza mpira wa miguu kwa lugha ya Kiswahili. Combination yetu ilikua nzuri sana na kwa kipindi hiko ambacho kilikua cha mwezi mmoja tulielewana na ku bond vizuri sana.
Oscar anapenda raha, anapenda kucheka na kuishi vizuri, anapenda ukweli na kubwa zaidi ni Rafiki mzuri sana. Pengine la zaidi ambalo nna uhakika Mama yake mzazi kule Kaliuwa anajuvunia sana ni la usomi, ni mwanafunzi mzuri ambaye anapenda kujiendeleza, sasa anamalizia Masters yake kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alishawahi kuwa Mwalimu kipindi cha nyumba kwenye maisha yake na kwa mawazo yangu ya haraka hii ndo ambayo inamfanya awe ni mmoja kati ya wachambuzi makini kabisa ambao nchi hii inayo, nguvu yake ni kuhakikisha pale kwenye ukweli unasemwa hata kama itakua kwa njia ya mas’hara, ila atausema!
Aliamua kuwa Baba na hili ni kwa mujibu wake baada ya kunikatalia katakata kwamba mtoto wake wa kwanza alikua ni wa ‘bahati mbaya’ kama ambavyo baadhi ya wazazi husema, Oscar anasem alikua anajua nini anafanya na Mama wa mtoto yule so kusema alikuja kwa bahati mbaya ni kama kumkosea mtoto yule ambaye alikuja kipindi ambacho Oscar alikua bado hajajiweka vizuri kwenye maisha yake na zaidi kwenye masuala ya kazi, na pia ananikumbusha jinsi alivyokua anajiona anajua saana na kama vile watu waliokua wanampa nafasi kipindi kile kama vile walikua hawanuelewi kabisa.
Anaamini kwenye kujifunza kila kukicha ili kupanua wigo wa uerevu na kwake yeye Elimu ndo ufunguo wa maisha toka siku ya kwanza.
Kama Baba wa watoto wawili ambao kwa kiasi kikubwa amekua hapo kwaajili ya vijana wake, Oscar anaamini kwenye kuwa pale kwaajili yao, kuwapa kile ambacho yeye hakukipata kutoka kwa Mzee wake wakati anakua, kuwa pale kwaajili ya watu wa familia yake na zaidi Mama yake ambaye kwa mujibu wa Oscar Mama ndo nguzo yake. Binafsi nayajua mengi ambayo amayafanya Kijijini kwao Kaliuwa kwaajili ya familia yake na hata ambao hawamhusu.
Humu mimi na Rafiki YANGU tulijadili mambo mbalimbali ya ki maisha na familia, kazi na muskabali wa biashara ya mpira kwenye NCHI yetu na dunia kwa ujumla, pia tuliongelea umuhimu wa familia na kupata mtoto ukiwa na umri mdogo, suala la ajira na hustle wakati tunakua nalo hatukulicha nyuma. Yangu matumainj nawe uta enjoy pia.
Love,
Salama.
Sheikh Hilali Shaweji Makarani au Sheikh Kipozeo ni mtu wa watu, au niseme kama ambavyo tunasema kwetu Uswazi, Sheikh ni mwana wa wana, anaweza kuwapa wana darsa kwa lugha yao na wakawa huru na wao kusema maoni yao au uelewa wao kwa raha na bashasha nyingi na naamini hii imemfanya yeye awe ni mmoja ya Ma Sheikh wanao tambulika zaidi kwenye mitandao ya kijamii nje na ndani ya Tanzania. Lugha hiyo ya wana ambayo anaitumia inasaidia sana kufikisha ujumbe ambao ameukusudia kwa wakati huo na ikapata mpaka majadilioano, majadiliano hayo ndo huzaa majibu ya maswali mengi ambayo wengi hujiuliza.
Kwetu au kwangu ilikua ni kaji task ambako nilikua najua inabidi nikakamilishe, na jina lake kurejea kutajwa mara kwa mara na watazamaji wa kipindi hiki pia ilichochea dhamira hiyo kwa kiasi kikubwa. Nilikua sijawahi kukutana nae kwahiyo hii nami ilikua ni mara yangu ya kwanza kukutana nae uso kwa macho, shabiki yake? Oh yes, mkubwa tu. Nimekua nikimskiliza na kumuangalia kila nipatapo nafasi ya kukutana na mafunzo yake, kwahiyo hamu ya kutaka kuongea nae ilikua inaongezeka kila siku zinavyozidi kwenda. Wakati ambao Mwenyezi Mungu ameupanga ndo wakati sahihi kabisa. Na naamini huu ndo ulikua muda ambao tulikua tumepangiwa haya mazungumzo kutokea na haikua huko nyuma ambako pengine tulidhani tungemtafuta na kuweza kuongea nae.
Alikua mkarimu kwangu, humchukua muda pia kuongea kama yule wa kwenye video maana kama Mwalimu nadhani huwa anaangalia spidi ambayo uko nayo na kujua anaenda na wewe vipi ili iwe imekaa mahala pake. Na naam, tuliweza kwenda vizuri, alinifanya nami niwe huru na muwazi kwa yale ambayo tulikua tumepanga na wenzangu kumuuliza.
Akiwa Baba na mume mpedwa kwa familia yake, Sheikh Kipozeo amekua akipata mialiko sehemu mbali mbali ili aweze kuwapa watu ‘dawa’. Humu zaidi sisi tulitaka kujua jina lilipo anzia na jitihada zake za kufikisha neno la Mwenyezi Mungu kwa wanaohusika. Alituambia pia kuhusu asili yake na ‘urithi’ wa dini ulipotokea. Lini hasa alijua kwamba ambacho anakifanya sasa ndo ambacho alikua anatakiwa kufanya kwenye maisha yake yote?
Yangu matumaini dawa itaingia na uta enjoy kuangalia au kuskiliza episode hii yetu ya nne.
Love,
Salama.
Abbot Charles ni jina maarufu kwa wanaoijua historia na wana zuoni, pengine umaarufu wa jina ndo sababu ya Baba yake kuamua kumpa mtoto wake wa kiume akitegemea na kijana wake atakua na ukubwa huo kwa lolote ambalo ataamua kufanya kwenye maisha yake, unaujua ule usemi kwa kiswahili kwamba maneno huumba? Mwenzangu, hata majina huumba, tena sana tu kwahiyo wakati mwengine utakapokua unafikiria jina la mwanao ni vyema kujiridhisha kwanza, unafanya kazi flani ya kipolisi ya kuchunguza ili mwanao asije akawa mtu fulani asiye na dira.
Quick Rocka aka Switcher aka Baba aka Kaka Fule ni mdogo wangu, hizo aka alozojipa ni maana halisi ya uwezo wa kuishi kwenye kila character ambayo anayo na ameamua kuiishi. Ni Quick na anaweza kuku rock wakati ana rap, na anaweza ku switch na kuwa singer na mambo yakaenda vizuri tu, au aka switch na kuwa Kaka Fule, aka kufanya utake kuendelea kumuangalia tu kwenye Jua Kali au filamu ambazo amekua akifanya. Switcher pia ni producer mzuri tu wa muziki ambao anaufanya.
Katika vijana wa kuwaangalia jinsi wanavyoelekea kwenye mafanikio yao yeye pia anafaa kuangaliwa na hii naamini inatoka kwenye kampani ambayo amekua nayo tokea siku ya kwanza alipojua anataka kufanya mziki, group aliyokua nayo kwenye Rockers ilikua imesheheni mafundi ambao pengine focus yao haikua kama ambayo Switcher amekua nayo au pengine walikua na vitu vyengine ambavyo ni vizuri pia vya kufanya na kuamua kuachana na muziki, pengine kufanya muziki haikua priority yao ila kwa Quick mambo yalikua tofauti. Ukaribu wake na Master Jay kwa kiasi kikubwa umemsaidia kuweza kuwa focused na mambo yake ya msingi na pia alikiri kwenye maongezi yetu haya kwamba kuna kipindi baada ya msiba wa Marehemu Kaka yake, alikua sehemu mbaya sana kifikra ila Master Jay alimsaidia kwa kiasi kikubwa kurudi kwenye mstari. Na kuanzia hapo sasa focus ya vitu ilianza kuwa 100% na ukiachana na kwamba Master Jay ndiye alimchomoa Quick kutoka kwenye kundi na kutaka asimame mwenyewe kama Solo Artist.
Pia Marco Chali ndiye aliyekua anamtengezea muziki wake wote, na kamsoto flani ambako alikapitia ili kumfanye awe huyu ambaye yuko leo chini ya uangalizi wake kwa kiasi kikubwa pia yalimfanya asogee ki maisha, mambo yote ambayo tunakutana nayo kwenye njia ya kuelekea kwenye mafanikio ni lazima ilikua tuyapitie ili kutufanya tuwe bora kwenye haya maisha tunayoishi sasa. Ambacho hakiku uwi kinakufanya uwe jasiri tu. Na jasiri Quick alikua. Aliweza kufungua studio yake mwenyewe ambayo alimfanya awe huru zaidi na kujijenga zaidi, hapo studio pia alitoa nafasi kwa wenzake ambao nao pia walikua wanatafuta sehemu ya kutokea. Kwenye studio ya Switcher ndiko ambako OMG ya Salmin Swaggz, ConBoy na YoungLunya ilizaliwa, tuseme kwa Quick Rocka kuliwapa tafu ya kufika mjini. Ma producer mbali mbali pia walianzia pale na kupata nafasi ya kufanya mambo makubwa zaidi kwenye sehemu nyengine.
Mimi na enjoy kumuona Abbot anavyokua na kujielewa na kujithamini, anavyo jibeba na kusogeza mambo yake kwa spidi nzuri. Kama kijana nna hakika ana mapungufu yake na kuna makosa alishawahi kufanya huko nyuma na probably hata mbeleni kwenye maisha, ila huwa hatumhukumu mtu kwa makosa aliyowahi kuyafanya bali kwa jinsi ambavyo alitoka kwenye hayo makosa na kuwa mtu bora zaidi.
Yangu matumaini uta enjoy story hizi ambazo zilikua zinapigwa kwa uhuru wa iana yake.
Love,
Salama
Love,
Salama.
Kuna usemi mmoja unaenda kama hivi, kulea mimba si kazi ila kazi ni kulea mtoto, tafsiri yangu naamini mhenga hapo alikua anatuambia kazi pengine inaanza baada ya kupata kazi, tunaelewa jinsi gani ambavyo kupata kazi huwa ni kazi. Tena kazi yoyote, haijalishi kama ni ya upishi au ulinzi au ufundi au hata u daktari, mi nawajua madaktari kadhaa ambao nao pia wanapata shida kupata hizo kazi. Na baada ya kupata shida zote hizo wakati wa kutafuta kazi basi kazi halisi huanza pale unapoipata sasa hiyo kazi yenyewe.
Kazi ya Zuchu ilianza kabla hajaipata hiyo kazi yenyewe na ilikua kazi haswa kuipata na Mama yake Bi Khadija Kopa ndo alikua kinara kwenye hiyo connection ambayo Binti yake alikua anaitaka ili aweze kuwa msanii wa Diamond, na hayo ndo yalikua maneno yake hasa, toka alivyorudi kutoka Nigeria kwenye mashindano ya kusaka vipaji na alikua hajielewi elewi kwa kiasi flani ni kitu gani alikua anataka kufanya na kama basi kutakua na la kufanya inabidi liwe kutoka WCB na sio sehemu nyengine yoyote na agulia nini kilitokea? WCB aliipata na kilichokua kinatakiwa baada ya hapo ni UVUMILIVU wa HALI YA JUU.
Kwenye vitabu vyangu vyote Bi Zuhura Othman Soud ndo muandishi wangu BORA wa KIKE kuwahi kutokea katika kizazi chetu hiki cha Bongo Flava, na naweza sema hivyo wakati wowote iwe usiku au mchana, kipaji hicho ndicho kilichonifanya mimi nistaajabu sana na kutaka kuongea nae na kumuuliza yote yale ambayo nilikua nataka kumuuliza, ingawa humo humo nilikua nishajijibu kutoka kwenye historia ya familia atokayo ingawa hiyo haikutakiwa ndo iwe lazima, lazima mtoto wa Khadija Kopa na Othman Soud awe muandishi mzuri maana wazazi wake wamejaa vipaji tena na Baba yake ndo muandishi mkubwa wa nyimbo nyingi za Mama yake zilizowahi kuvuma.
Kwa umri wake wakati mwengine hujiuliza kajuaje haya maneno yote, anajua maana yake hii? Kasikia wapi hili neno au pengine je huwa anamfikiria Mama yake (ambaye ndo kipenzi chake na ndo amemlea) wakati anaandika hii? Anaona aibu? Je huwa wanaongelea hayo mashairi wanapokua wawili tu? Mazungumzo huendaje?
Sasa turudi kwenye kazi hiyo ya kuanza kuifanya baada ya kuipata sasa WCB, ukiachana na msoto mrefu alopitia, WCB wenyewe walikua waangalifu sana kwenye mipango ambayo ilikua ikiandaliwa kwaajili yake, yeye ndo msanii wa KWANZA wa KIKE kuwahi kutokea kwenye label kwahiyo ukichana na kipaji pia uwekezaji wa hali ya juu ulitakiwa ufanyike and boy they did that. Toka single yake ya kwanza mpaka wakati naandika hii Zuchu hakuwahi kuwa na kazi chafu, album yake ya kwanza alotoka nayo ya I am Zuchu ilikua na nyimbo 7 ambazo zote zilienda kufanya vizuri, na mpaka leo kila wimbo ambao anaachia ni wa moto, tukisema namba moja nadhani namba zake pia zinasema hivyo za kila sehemu, hakuna chumvi yoyote ndani yake.
Vipi sasa anaweza ku maintain hii schedule yake ilojaa mambo kuanzia asubuhi mpaka usiku? Kutoka Jumatatu mpaka Jumapili? Je ana muda kwaajili yake? Ana mpenzi? Mipango yake je? Endelevu? Vipi hizi title ambazo tunampa anazichukuliaje? Kuna pressure yoyote? Na kuhusu familia je? Kuna pressure yoyote kwenye baadhi ya mambo na maamuzi? Na kwenye label nako? Watu na furaha na kazi yake?
Kwa kuanzia msimu wetu wa TANO nadhani introduction ya Ms Zuchu inatufaa sana na yangu matumaini uta enjoy pia.
Asante kwa support ya toka siku ya kwanza ulipoanza kutupa macho na masikio yako.
You’re the best, nakukumbusha tu kwamba mengi yajayo yatakufurahisha In Shaa Allah maana kazi ndo kwaanza imeanza.
Love,
Salama
Kutoka kwao Mbeya mpaka Dar es Salaam kwaajili ya kutafuta maisha bora na maendeleo kama wengi wetu ndo ilikua nia na madhumuni ya Raymond wa enzi hizo. Ingawa kuna kipindi ilifika alikua hataki kabisa kuskia habari za muziki, ila alipoambia kama kuna pesa ndani yake katika huo mchongo wa mashindano ambayo aliitiwa na akiangalia nyumbani moja haikai na mbili haijulikani ilipo akaona basi sawa, kwani nini? Na huo ndo ulikua mwanzo wa safari nzuri ya ki superstar ambayo anaishi nayo sasa.
Najua wengi wenu mlikua mnadhani labda yangezungumziwa madhila alokua nayo sasa ila kwa bahati mbaya (kwako) na nzuri kwetu, sisi tulizungumza naye kabla. So hii ilikua free na natural kama ambayo utaiona au kuiskiliza. Wengi wetu huwa tunapitia madhila na mitihani mingi tu kabla ya kujielewa na kusimama sawa sawa, na kupitia hayo ndo kujifunza na kuwa BORA kunatokea. Kuna msemo mmoja wa Kiswahili unaoenda kama, ‘asipo chafuka, atajifunzaje’, something like that.
Mimi Ray huyu nilianza kumsikia vizuri zaidi kutoka kwa AY ambaye ali spend naye muda mwingi hapa Bongo wakati wanafanya rekodi remix ya Zigo na nchini Afrika ya Kusini wakati Zee ameenda ku shoot video ya wimbo huo ambao Diamond Platnumz ndo ameshirikishwa, ila Vanny Boy alikuwepo all the way na mpaka kwenye video akatokea. AY aliniambia kuhusu ucheshi wake na uhodari wake, na uhodari huo ameuzungumza humu kwenye maongezi yetu mimi na yeye. Aliniambia jinsi ambavyo alikua akitumia kipaji chake enzi hizo kwa kuwaandikia wenzake wimbo mmoja na pengine mpaka album kwa shilingi ELFU THELATHINI TU.
Njia ambazo watu wengi wamepita haiwezi kuwa ndo njia ambayo kila mmoja wetu atapitia pia, ila kunaweza kuwa na mifanano ya hapa na pale, na hii ndo nia na madhumuni ya kipindi hiki. Tunataka wewe usikie na ujifunze ili ujue ‘unatokaje’ au watu walipenya vipi mpaka wakafika!
Sasa ni mmoja ya wasanii wakubwa tu hapa barani Afrika na duniani anafahamika. Bango la album yake linaning’inia kwenye mitaa ya Times Square huko NY City kwenye mji ambao raia wa nchi mbalimbali duniani wanaishi na kupitia. Sidhani kama wakati anahangaikia kufua nguo zake zilizomwagikiwa mafuta ya mawese wakati akiwa safarini kwenye lori kutoka Mbeya kuja Dar aliwahi kuwaza jambo kama hilo.
Mimi na yeye tulizungumzia pia mahusiano yake na wazazi wake, familia ya kufikia ya Baba yake ambaye aliachana na Mama yake na kuhamia na mtu mwengine si mbali na wao walipokua wanakaa. Tumeongelea mapenzi yake na muziki na kipaji chake cha uandishi. Tumeongelea jinsi ambavyo Madee alimpokea na Babu Tale ambavyo alikua na kama kusita hivi kwenye suala la yeye kusajiliwa WCB na mambo mengine mengi ya maisha. Yangu matumaini kama ilivyo ada, hapa utajifunza jambo pia.
Tafadhali enjoy.
Love,
Salama.
From the publisher's feed