Sign up to save your podcastsEmail addressPasswordRegisterOrContinue with GoogleAlready have an account? Log in here.
FAQs about Sepetuko:How many episodes does Sepetuko have?The podcast currently has 153 episodes available.
June 26, 2024Ulinzi wa Amani au Uvunjaji wa Haki za Binadamu?Tukio la vijana waliokuwa wakiandamana kuingia katika majengo ya Bunge kamwe sio la kushabikiwa. Hata hivyo, tukio hilo na mengine ya waandamanaji kuharibu mali ya umma na kibinafsi hayatoi sababu tosha kwa maafisa wa usalama kuwafyatulia risasi na kuwaua waandamanaji. Hayatoi sababu kwa Rais kuwaita Wakenya kuwa wahalifu na wahaini....more5minPlay
June 25, 2024Sauti ya Vijana Haipuuzwi TenaMaandamano yanayoendelezwa dhidi ya Mswada wa Fedha wa mwaka wa 2024 ni ukumbusho kwa serikali kuhusu jinsi sauti ya vijana imekuwa ikipuuzwa. Vijana wanakumbwa na changamoto mbalimbali, kuu miongoni mwazo, ikiwa ni ukosefu wa ajira nchini. Serikali haina budi kutafakari mbinu mahsusi ya kutatua hili na changamoto nyingine zinazowakumba vijana....more5minPlay
June 24, 2024Serikali Yalazimika Kukubali Ukweli wa Maandamano ya VijanaSerikali sasa imegundua kuwa haiwezekani kupuuza maandamano yanayoendelezwa na kizazi cha vijana dhidi ya Mswada wa Fedha wa mwaka wa 2024. Rais mwenyewe amekiri kuwa ipo haja ya kufanyika mazungumzo kati yake na vijana hawa. Kiukweli, hakuwa na budi. Kuanzia mwanzo haingewezekana tu kuwapuuza vijana hawa kutokana na sababu kadhaa....more5minPlay
June 21, 2024Maandamano ya Amani: Kulinda Haki za Wananchi wa Kenya na KatibaKuandamana ni haki ya wananchi wa Kenya, na inalinda na Katiba ya sasa ya nchi. Bora tu maandamano haya yafanywe kwa amani bila kuvuruga usalama. Hatua ya maafisa wa usalama kuwakabili waandamanaji wanaoandamana kwa amani ni uvunjaji wa sheria....more5minPlay
June 20, 2024Maandamano ya Wakenya dhidi ya Mswada wa Fedha wa 2024Maandamano yanayoendelezwa na Wakenya dhidi ya Mswada wa Fedha wa mwaka wa 2024 ni zaidi ya Mswada wa Fedha. Ni dhihirisho la kutaabika kwa muda mrefu ambako Mkenya amekuwa akipitia mikononi mwa serikali isiyojali na inayowadharau, kwa miaka. Hii ni sababu tosha ya serikali kuwa na wasiwasi....more5minPlay
June 19, 2024Maandamano ya Wakenya Dhidi ya Mswada wa FedhaMaandamano ya Wakenya dhidi ya Mswada wa Fedha yahweh onyo kwa serikali. Onyo kuwa wananchi wamejifundisha kujitetea na kutetea haki yao wanapohisi kuhujumiwa. Kinyume na maandamano ya miaka ya nyuma, haya yanaongozwa na Wakenya wenyewe, na sio wanasiasa....more5minPlay
June 18, 2024Udhaifu wa Maamuzi ya BungeMwenendo wa Wabunge wetu wakati wa kufanya maamuzi muhimu yanayomhusu Mkenya wa kawaida ni dhihirisho tosha la maamuzi duni ambayo huwa tunafanya Bungeni. Haimhitaji mpigakura kumtumia arafa Mbunge ama kuandamana ili wafanye maamuzi bora ya kutuwakilisha. Tujifundishe kitu, inatupasa kufanya maamuzi bora debeni siku za usoni....more4minPlay
June 18, 2024Junior Starlets Wafuzu kwa Kombe la Dunia la Wanawake Chini ya Miaka 17Heko kwa Junior Starlets kwa kufuzu kushiriki Kombe la Dunia kwa wanawake chipukizi chini ya miaka 17. Historia iliyoje! Junior Starlets inakuwa timu ya kwanza kabisa ya Kenya ya kandanda kufuzu kwa Kombe la Dunia. Maandalizi ya kushiriki kombe hilo yaanze sasa....more4minPlay
June 14, 2024Pengo Kubwa katika Bajeti ya 2024/2025Makadirio ya Bajeti ya Mwaka wa Kifedha wa 2024/2025 yalisomwa Bungeni na Waziri wa Fedha Njuguna Ndungu. Katika makadirio hayo ya jumla ya shilingi trilioni 3.99 lipo pengo la shilingi bilioni 600. Pengo hili lazima likutie wasiwasi. Unajua kwa nini?...more5minPlay
June 13, 2024Kuwajibika kwa Mafao ya Rais Mstaafu: Je, Jopo ni Lazima?Suala la mafao ya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta halistahili jopo, ni suala ambalo sheria za nchi zinatosha katika kulitatua. Kenyatta anauliza kipi kilifanyika kwa mgao wake wa bajeti kwa miaka miwili, kwa mfano, haihitaji jopo kujibu swali hilo....more5minPlay
FAQs about Sepetuko:How many episodes does Sepetuko have?The podcast currently has 153 episodes available.