Sepetuko

Sepetuko

By Standard MediaNewsPolitics
Download on the App Store

Sepetuko episodes

  • Kupunguzwa kwa Washauri Serikalini
    Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei amewaandikia Mawaziri wote kuwataka kupunguza idadi ya washauri kutoka wawili hadi mmoja kwa kila Waziri ili kupunguza matumizi ya pesa za serikali. Hatua hii imeibua swali la hivi hawa washauri wamekuwa wakifanya kazi gani ikiwa kwa kipindi cha miaka miwili serikali hii imekuwa ikifanya baadhi ya maamuzi mabovu mno, kiasi cha kugeuka na kuwa shubiri kiasi hiki? Je, washauri hawa wamefeli katika majukumu yao au ushauri wao umekuwa ukipuuzwa na viongozi wanaoshauriwa?
    5 min
  • Kenya Baada ya Miaka Sitini: Mabadiliko Makubwa Yaja!
    Miaka sitini tangu kupata uhuru uongozi wa nchi ya Kenya umekuwa ukiendeshwa na wanasiasa wabinafsi wasiomjali yeyote ila maslahi yao tu.
    Hali inaonekana inabadilika na sasa wananchi wataanza kujiamulia wanavyotaka kuongozwa. Hilo lifanyikapo, basi ole wao hawa wanasiasa. Interesting times ahead!
    5 min
  • Mgomo wa Maafisa wa Kliniki Wamalizika Baada ya Siku 99
    Maafisa wa Kliniki wametamatisha mgomo wao ambao umedumu siku 99 baada ya mapatano kati yao na Baraza la Magavana COG. Hii ni nafuu kubwa kwa Wakenya ambao hutegemea huduma katika hospitali za umma, japo inatoa changamoto kwa serikali kutafuta ufumbuzi wa kudumu kwa migomo hii ya mara kwa mara katika sekta ya afya.
    5 min
  • Unyenyekevu wa Wanasiasa Baada ya Maandamano ya Vijana
    Viwango vya unyenyekevu miongoni mwa wanasiasa wetu, ambavyo vinashuhudiwa baada ya maandamano na harakati za vijana wa kizazi cha Gen Zs na wengine ni mfano hai wa uwezo wa watu. Yaani hadi wanasiasa wetu wenyewe wanakataa nyongeza ya mishahara waliyokuwa wameongezewa na Tume ya Utathmini wa Mishahara na Marupurupu SRC! Huu unafaa kusalia kuwa mkondo. Wanasiasa kujua kuwa kuipuuza sauti ya mwananchi ni kujiweka taabani.
    5 min
  • Maandamano Yafanyike Kwa Amani
    Maandamano yanayoendelezwa nchini dhidi ya serikali yanalindwa na Katiba ya Kenya, bora tu yafanywe kwa amani. Inasikitisha kuwaona wahuni wakihitilafiana na maandamano haya, kuwapora Wakenya mali yao waliyoitafuta kwa jasho lao. Wacha watuhumiwa hawa wasakwe na kukabiliwa na mkono wa sheria kutokana na shughuli zao za kihalifu. Hawa sio sehemu ya waandamanaji na kamwe hawafai kuchukuliwa hivyo.
    5 min
  • Tishio kwa Amani na Utawala wa Sheria
    Visa vinavyoendelezwa na serikali vya kuwateka nyara vijana na wanasiasa wanaohusishwa na maandamano dhidi ya serikali yanatia shubiri uwezekano wa kufumbua fumbo hili. Zaidi ni uhuni ambao ni kinyume kabisa na sheria za nchi. Amani haipatikana kwa kiganja kilichofumbatwa.
    5 min
  • Matatizo ya serikali yanatokana na Rais asiyeaminika
    Sehemu kubwa ya matatizo yanayokumba serikali hii ni Wakenya kukosa imani kwake kutokana na kuwapo Rais asiyependa ukweli. Rais ambaye hadi leo amekwama katika uongo wa kuwatetea maafisa wa usalama waliohusika katika ukatili dhidi ya waandamanaji. Rais anayesema hili, kisha naye anafanya jingine. Ni hadi Rais Ruto amaanishe ayasemayo, afanye anayosema na ajifundishe kusema ukweli ndipo hali hii ya sasa itaimarika.
    5 min
  • Uwezo wa Vijana Katika Maandamano ya Demokrasia
    Vijana wa Gen Zs na vijana wengine ambao wamekuwa wakiendeleza maandamano dhidi ya Mswada wa Fedha wa mwaka wa 2024 wametukumbusha uwezo tulio nao kama wananchi wapigakura. Uwezo wa kupiga kura kuwachagua viongozi wetu, lakini zaidi kuwawajibisha wanapokuwa ofisini. Harakati hii haifai kukoma. Huu unafaa kuwa mwanzo tu wa kutetea Katiba yetu na kudai uongozi bora ambao tunastahili.
    5 min
  • Aibu Kwa Bunge la Kitaifa!
    Hatua ya serikali kuwatuma wanajeshi kusaidia polisi kuwakabili waandamanaji ni ukiukaji mkubwa wa sheria za nchi. Inasikitisha kuwa Bunge la Kitaifa limetumiwa kutia muhuri uhayani huu! So unfortunate!
    5 min

About Sepetuko

From the publisher's feed

Kurunzi ya falsafa inayoangazia bila woga masuala mazito yanayoiathiri jamii.