Sign up to save your podcastsEmail addressPasswordRegisterOrContinue with GoogleAlready have an account? Log in here.
FAQs about Sepetuko:How many episodes does Sepetuko have?The podcast currently has 153 episodes available.
May 24, 2024Safari ya Haki: Balozi wa Uingereza Azuru Kenya Kutafuta Ukweli kwa Agnes WanjiruZiara ya Balozi wa Uingereza Nchini Kenya kwa familia ya Mkenya Agnes Wanjiru aliyetuhumiwa kuuliwa na mwanajeshi wa Uingereza kwenye kambi ya Jeshi ya Uingereza iliyoko Nanyuki uwe mwanzo wa kupatikana kwa haki kwa Wanjiru na waathiriwa wengine wa hujuma mikononi mwa wanajeshi wa Uingereza waliomo nchini....more5minPlay
May 23, 2024Serikali Itatue Mgomo wa Walimu wa JSS Kuokoa ElimuJinsi serikali inashughulikia mgomo wa walimu wa JSS kunaonesha serikali isiyojali. Mbona tunachezea elimu ya watoto wetu? Mbona suala hili halifanywi kipaumbele?...more5minPlay
May 21, 2024Mgao wa Fedha za Serikali Kwa Idadi ya Watu Unahatarisha Umoja WetuGumzo la mgao wa fedha za serikali na maendeleo kutolewa kwa msingi wa idadi ya watu, linatishia kurejesha nyuma hatua ambazo zimepigwa kuhakikisha ujenzi wa Kenya moja. Jamii zote zinazoishi Kenya zinastahili kujihisi kuwa nyumbani, bila kujalisha idadi yao....more5minPlay
May 20, 2024Okoa Mpango wa Lishe ShuleniPendekezo la serikali kufutilia mbali mpango wa lishe shuleni sio la hekima. Linatishia kurejesha nyuma hatua zilizopigwa katika kuhakikisha wanafunzi kutoka maeneo kame, mitaa ya mabanda na maeneo mengine yaliyosalia nyuma kimaendeleo wanapata elimu....more5minPlay
May 17, 2024Mswada wa Fedha 2024/2025: Je, Kenya Kwanza Inakujali Wewe?Mapendekezo yaliyomo kwenye Mswada wa Fedha wa mwaka wa kifedha ujao yanaonesha wazi kuwa serikali ya Kenya Kwanza haina ufahamu wa hali halisi ya Mkenya. Haijali kuhusu vipaumbele vya Mkenya. Lakini, nani aliiweka serikali hii mamlakani kama sio Mkenya yuyu huyu. Huwa tunauliza maswali kuhusu nani atafadhili ahadi chungu nzima zinazotolewa na wanasiasa wakati wa kampeini?...more5minPlay
May 16, 2024Ruto na Ushuru: Kutatua Deni au Kutatua Ufisadi?Rais William Ruto amekariri kuwa analenga kupandisha hata zaidi ushuru anaotozwa Mkenya, eti ili kupunguza deni la taifa. Sepetuko inamkumbusha Rais kuwa tatizo la Kenya sio la kimapato, ila ni mianya iliyopo ya uporaji wa mali ya umma....more5minPlay
May 15, 2024Mswada wa Fedha wa Mwaka wa 2024/2025: Je, Ni mzigo Mpya Kwa Wananchi?Mswada wa Fedha wa Mwaka wa 2024/2025 una baadhi ya mapendekezo ambayo kimsingi yatamuongezea Mkenya mzigo wa ushuru ambao tayari ni mzito. Sepetuko inakariri kuwa kamwe haiwezekani kwa nchi kujiendeleza kupitia kuwatoza wananchi wake kodi nyingi! Haiwezekani....more5minPlay
May 13, 2024Fedha za Elimu: Hatari kwa Maendeleo ya Elimu ya JSSShule zinapofunguliwa kwa masomo ya muhula wa pili, Sepetuko inairai serikali kuangazia masuala kadhaa kwenye sekta ya elimu. Miongoni mwa masuala hayo ni kucheleweshwa kwa fedha za serikali za kufadhili elimu, na changamoto zinazokumba elimu ya JSS....more5minPlay
May 10, 2024Mipango ya Kupambana na Ufisadi Kutoka Fiji hadi Kenya: Kesi ya Frank BainimaramaAliyekuwa Waziri Mkuu wa Fiji Frank Bainimarama amefungwa jela kwa kuzuia uchunguzi wa ufisadi. Hapa Kenya, vita dhidi ya ufisadi havijazaa matunda aina hii, na kuibua swali la inawezekanaje kwa mwanasiasa wa haiba hii kufungwa jela. Sepetuko inakariri kuwa vita dhidi ya ufisadi haviwezekani ikiwa yetu ni kuwatetea na hata kuwachagua kwa nyadhfa za juu wanasiasa mafisadi....more5minPlay
May 09, 2024Sakata ya mbolea ghushi: Kesi ya Waziri Mithika LinturiWabunge wana nafasi ya kuwadhihirishia Wakenya kuwa yao ni taasisi huru katika hoja ya kumbandua Waziri wa Kilimo Mithika Linturi iliyoko mbele yake. Hii ni fursa ya kuubaini ukweli na kutoa uamuzi wa haki kwa Linturi, lakini zaidi kwa Wakenya ambao huenda wakadhurika kutokana na wakulima kuuziwa mbolea ghushi....more5minPlay
FAQs about Sepetuko:How many episodes does Sepetuko have?The podcast currently has 153 episodes available.