Sign up to save your podcastsEmail addressPasswordRegisterOrContinue with GoogleAlready have an account? Log in here.
FAQs about Sepetuko:How many episodes does Sepetuko have?The podcast currently has 153 episodes available.
April 16, 2024Nairobi Yazamishwa na Mafuriko: Serikali Iko Wapi?Mvua inayonyesha nchini inaanika wazi upungufu wa serikali katika kujiandaa kwa ajili ya msimu wa mvua ambao hutabiriwa mapema. Sepetuko inatoa changamoto kwa serikali kutafuta mbinu ya kuimarisha mfumo wa uzoaji majitaka, na kuvuna maji ya mvua kusaidia siku za usoni....more5minPlay
April 12, 2024Mbolea Ghushi: Serikali YajichanganyaSerikali imeendelea kujikanganya kuhusu taarifa za kuwapo mbolea ghushi nchini. Waziri wa Kilimo sasa anadai kuwa iliyokuwapo sio mbolea ghushi ila mbolea isiyokuwa na madini hitajika. Who's fooling who?...more5minPlay
April 11, 2024Mgomo wa Madaktari: Uhai wa Wakenya Uko HatariniMgomo wa madaktari unaoendelea sasa unatishia haki ya binadamu kwa uhai. Sepetuko inatoa wito kwa serikali na vyama vya madaktari kulegeza misimamo na kufumbua fumbo hili kwa faida ya raia....more5minPlay
April 09, 2024Iweje Serikali Ikose Pesa Kulipa Madaktari, Lakini Iwe na za MaCAS na Ziara za Viongozi?Mgomo wa madaktari unapoendelea, Rais William Ruto amewarai madaktari kurejea kazini, akisema serikali haina pesa na kuwa hali ni ngumu. Sepetuko inashangaa ni vipi serikali haina pesa za kuwaajiri madaktari wanagenzi lakini ina hela za kuwaajiri maCAS na kufadhili ziara za hapa na pale za Rais na Mawaziri serikalini....more5minPlay
April 08, 2024Usalama Barabarani: Kila Mtu Akiwajibika Kupunguza AjaliDescription - Maelfu ya Wakenya wanaendelea kuaga dunia nchini kutokana na ajali barabarani. Familia zinaendelea kupoteza wapendwa wao kwa mnyama huyu anayeweza kuepukika. Ni wakati sasa sote tuwajibikie usalama barabarani -madereva, watumiaji wa miguu, wahudumu wa bodaboda na raia wengine. Jukumu la usalama barabarani sasa lazima liwe letu sote....more5minPlay
April 04, 2024Uchaguzi wa UDA: Uingiliaji wa Serikali Kupitia Wenyeviti wa KRA na KPLC?Uteuzi wa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Ushuru Nchini KRA na mwenzake wa Kampuni ya Nguvu za Umeme KPLC kusimamia uchaguzi wa viongozi wa chama cha UDA haufai kabisa. Sepetuko inasema wacha uongozi wa chama utenganishwe na uongozi wa nchi na mashirika yake. Mambo haya mawili kamwe yasichanganywe....more5minPlay
April 03, 2024Masomo kwa Kenya Kutoka kwa Ufanisi wa Diomaye Faye, Rais Mpya Wa SenegalRais mpya wa Senegal Bassirou Diomaye Faye ameapishwa rasmi kuiongoza nchi hiyo. Faye, mwenye umri wa miaka 44 anakuwa Rais wa tano wa taifa hilo na Rais mchanga zaidi kuongoza taifa hilo la Afrika Magharibi. Ushindi wake katika uchaguzi mkuu uliopita ni wa kihistoria kutokana na kuwa yeye si mtu maarufu mno katika siasa nchini humo, na aliondoka jela siku tisa tu kuelekea Uchaguzi Mkuu. Tunajifunza nini kutokana na hadithi ya ufanisi wa Faye? Kenya inaweza kujifundisha nini?...more5minPlay
April 02, 2024Mgogoro wa Afya: Maisha ya Wakenya Yapo Hatarini!Baada ya wiki kadhaa za mgomo wa madaktari, hali katika hospitali na vituo vya afya vya umma nchini Kenya imechukuwa sura mbaya zaidi kufuatia kujiunga kwa matabibu katika mgomo huo. Mgogoro huu umepelekea athari kubwa kwa mfumo wa afya nchini, na kusababisha ugumu mkubwa kwa wananchi wanaotegemea huduma za matibabu kutoka hospitali za umma. Sharti seriklai ifanye jambo kwa upesi mno kuokoa hali. Wakenya wanaumia!...more5minPlay
March 28, 2024Rais Ruto Awe Kiongozi Mwenye Uzalendo, Atatue Mgomo wa Madaktari: SEPETUKOMgomo wa madaktari unaoendelea lazima ufanywe kipaumbele na serikali. Wagonjwa wanaendelea kutaabika kutokana na kushindwa kupatiwa huduma muhimu za matibabu. Sepetuko inasisitiza kuwa ni wakati Rais William Ruto aangazie mbinu za kusitisha mgomo huu ili kuokoa maisha ya Wanjiku....more5minPlay
March 27, 2024Wetangula Dhidi Ya Natembeya: Bora Kwa Demokrasia Ila Sio Kwa VuruguUbabe wa kisiasa kati ya Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetangula na Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya ni dhihirisho la demokrasia ya nchi. Hata hivyo, ubabe huu haufai kuishia kuwa wa vurugu. Sepetuko inakariri kuwa kamwe vurugu hazifai kuwa sehemu ya siasa za taifa hili. Wanaohusika katika kuzua vurugu mazishini, kwenye mikutano ya hadhara au kwingineko kokote kule lazima wawajibishwe kisheria....more5minPlay
FAQs about Sepetuko:How many episodes does Sepetuko have?The podcast currently has 153 episodes available.