Sepetuko

Sepetuko

By Standard MediaNewsPolitics
Download on the App Store

Sepetuko episodes

  • Kilio cha Mfanyakazi Mkenya
    Kenya inaungana na dunia kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi. Sepetuko inakariri kuwa mfanyakazi Mkenya hana lolote la kusherehekea. Mishahara ni duni, ushuru anaotozwa ni maradufu, mazingira anamofanyia kazi ni duni na masaibu mengine mengi anayokumbana nayo.
    5 min
  • Janga la Mafuriko: Msaada wa Dharura Unahitajika!
    Janga linaloendelea nchini la mafuriko ambayo yamesababisha vifo vya takriban watu 150 linahitaji juhudi za pamoja na dharura kutoka kwa serikali na washikadau wengine. Sepetuko inairai serikali kuweka kando mipango mwingine yoyote isiyokuwa ya dharura na ya lazima, na kulifanya janga hili kuwa kipaumbele.
    5 min
  • Nini cha Kufanya Wakati wa Mafuriko
    Mafuriko yanayoendelea nchini yameendelea kusababisha mauti na uharibifu mkubwa. Ndiyo, tuilaumu serikali kwa kukosa kujiandalia majanga kama haya, lakini ni muhimu pia uchukue tahadhari. Usalama wako wakati huu unaanza na mimi na wewe.
    5 min
  • Mafuriko Yanabainisha Udhaifu wa Serikali na Miundombinu Duni
    Mafuriko yanayoshuhudiwa jijini Nairobi na kote nchini yanaonesha wazi uwezo duni wa serikali kujiandaa kwa ajili ya majanga, na pia kuwepo kwa miundomsingi duni kustahimili majanga yanapotokea. Sepetuko inazirai Serikali za Kaunti na ya Kitaifa kuweka mikakati kabambe ya kujiandalia majanga kama mafuriko ili kuepusha mauti yanayoshuhudiwa.
    5 min
  • Huduma za Afya Zimepooza kwa Siku 40: Serikali Inawajali Wakenya Kweli?
    Kwa zaidi ya siku 40, Wakenya wameendelea kukosa huduma za matibabu katika hospitali za umma kufuatia mgomo wa madaktari. Madai ya serikali eti kunao mwafaka unaoelekea kutiwa saini kati yake na madaktari inaonekana ilikuwa njama tu ya kuwashinikiza madaktari kusalimu amri. Hii ni serikali aina gani inayowachezea watu wake kiasi hiki? Mbona idai kuna mwafaka ilhali huo sio ukweli? Nani anamjali Mkenya wa kawaida?
    5 min
  • Kifo cha CDF Ogolla Kimezua Maswali Mengi; Wakenya Wadai Majibu
    Kweli ajali haina kinga. Hata hivyo tukio la Jenerali wa Jeshi la Nchi kufariki kwenye ajali ya ndege, akiwa ndani mwa nchi yake, ni jambo ambalo lazima lichunguzwe. Je, kunao waliolala kazini kiasi cha kuruhusu tukio hili kutokea au ni ajali tu kama ajali nyingine? Lazima pafanyike uchunguzi wa kina kubaini kilichojiri.
    5 min
  • Serikali Inajitahidi Kweli Kupunguza Matumizi?
    Juma hili kumefanyika Kongamano la Kutathmini Viwango vya Mishahara na Marupurupu wanayopata wafanyakazi wa serikali. Rais amekariri kuwa serikali yake inajizatiti kupunguza mianya ya ufujaji serikalini. Sepetuko inasema kuwa kongamano hili na juhudi hizi ni kazi bure ikiwa serikali bado inaendelea kupanua viwango vya mishahara kwa kuwaajiri Mawaziri Wasaidizi CAS.
    5 min

About Sepetuko

From the publisher's feed

Kurunzi ya falsafa inayoangazia bila woga masuala mazito yanayoiathiri jamii.