Sepetuko

Sepetuko

By Standard MediaNewsPolitics
Download on the App Store

Sepetuko episodes

  • Je, Nairobi Iko Tayari Kukabiliana na Mvua Kubwa?
    Mvua iliyonyesha usiku wa Jumapili imesababisha mauti na uharibifu mkubwa jijini Nairobi. Mvua hiyo imeonesha wazi jinsi miundomsingi iliyopo haina uwezo wa kustahimili mvua kubwa, hivyo kuna haja ya uekezaji wa kumaanisha katika miundomsingi ya ukusanyaji maji taka (drainage) ili kuwaepushia wakazi madhara.
    5 min
  • Mgomo wa Madaktari: Wananchi Waathirika, Suluhisho Lahitajika Haraka
    Vitisho vinavyotolewa na Waziri wa Afya Susan Nakhumicha na Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja dhidi ya madaktari wanaogoma si sahihi. Havitoi suluhisho kwa mgomo huu ambao umelemaza shughuli katika hospitali za umma nchini. Wanaoumia ni wananchi wanaotegemea huduma hizi na hawana pesa za kutafuta huduma katika hospitali binafsi. Serikali itafute suluhisho la kusitisha mgomo huu mara moja.
    5 min
  • Mgomo wa Madaktari, Ukosefu wa Ajira, Ufisadi Vyaongezea Huzuni kwa Wakenya: SEPETUKO
    Umoja wa Mataifa juzi umetoa orodha ya mataifa yenye furaha zaidi duniani. Finland kwa mara nyingine tena imeibuka nafasi ya kwanza, kutokana na huduma bora wananchi wa taifa hilo wanapata kutoka kwa serikali. Kenya iko katika nafasi ya 114 duniani. Sepetuko inakiri kuwa Wakenya wengi hawana furaha kutokana na ugumu wanaopitia, huku serikali ya siku ikionekana kutojali. Wakenya watafurahi vipi wakati madaktari wanaendelea na mgomo, nafasi za ajira hazipo nchini, ufisadi umesheni serikalini, fedha za kufadhili elimu zinacheleweshwa miongoni mwa masaibu mengine.
    5 min
  • Ni Nani Anayewajibika kwa Mbolea Ghushi?- Sepetuko
    Taarifa za wakulima nchini kuuziwa mbolea ghushi zinaibua swali la Je, Kenya ni nchi ya ughushi? Tulifikaje kiwango hiki cha kuanza kuchezea uti wa mgongo wa uchumi wa nchi hii -Kilimo? Sepetuko inasisitiza kuwa kamwe haiwezekani tuendelee kufanya michezo hii na uzalishaji wa chakula nchini.
    5 min
  • Wito kwa Rais Ruto Kuzuia Maziko ya Vyombo vya Habari: Sepetuko
    Vyombo vya habari vilivyo dhabiti na huru ni msingi mojawapo wa demokrasia. Kwa demokrasia kuendelea kudumu nchini Kenya, ni muhimu kwa serikali kutolemaza vyombo vya habari vya kibinafsi vilivyopo. Sepetuko inamrai Rais William Ruto kutoruhusu maziko ya vyombo vya habari kufanyika wakati wa hatamu yake.
    5 min
  • Mgomo wa Madaktari: Serikali Yalaumiwa Kwa Kupuuza Afya ya Wananchi
    Mgomo wa madaktari unaoendelea nchini unaionesha serikali kuwa isiyomjali raia. Afya ni kiungo muhimu katika uhai wa binadamu, hivyo serikali lazima ifanye kipaumbele suala la kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma bora za matibabu. Ni muhimu kwa serikali kufanya mazungumzo na vyama vya madaktari ili kuhakikisha mwananchi hataabiki kupata huduma za matibabu.
    5 min
  • Siasa za Urithi ODM: Nani Afaa Kuvaa Kiatu cha Odinga?- SEPETUKO
    Hatua ya Kiongozi wa ODM kutangaza kuwania uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika AUC imeibua mjadala mkubwa kuhusu nani anafaa kuvaa kiatu chake kuongoza chama hicho? Sepetuko inakariri kauli ya muigizaji wa Marekani William Powell kuwa ''power must be taken. It is not given."
    Yeyote asiketi hapo na kusubiri kukabidhiwa usukani wa ODM.
    5 min
  • Kenya Kusaidia Haiti- Je, Ni Kafara au Ushujaa?: Sepetuko
    Marekani imeanza kuwaondoa nchini Haiti raia wake wanaofanya kazi kwenye Ubalozi wake nchini humo. Wakati uo huo, serikali ya nchi inaiomba Kenya kuharakisha mchakato wa kuwatuma maafisa wake wa polisi kuenda kudumisha usalama katika taifa hilo la eneo la Karibea.
    Hayo yanajiri huku magenge ya uhalifu yakiendeleza uhalifu katika nchi hiyo ya jumla ya watu milioni 11. Sepetuko inakariri kuwa kuwatuma maafisa wa polisi katika taifa hilo ni kuwatoa kafara wana wetu. Mbona serikali isifanye kipaumbele usalama wa raia wake kuliko kuwatuma walindausalama zaidi ya kilomita elfu 12 kutoka Kenya?
    5 min
  • Miaka 30 ya Kusubiri-Mwanajeshi Mstaafu Ahangaika Kupata Pensheni
    Isaiah Ochanda, Afisa wa Jeshi aliyestaafu alifika mbele ya Kamati ya Ulinzi ya Seneti akiwa kwenye kitanda cha hospitalini. Ochanda alistaafu kutoka Jeshini miaka ya 1990s na kwa miaka hiyo yote juhudi zake za kupata pesa zake za baada ya kustaafu zimegonga mwamba. Kulikoni? Mbona wafanyakazi wa serikali waliostaafu hutaabishwa mno kupata malipo ya uzeeni? Iko wapi serikali kuangazia suala hili?
    5 min

About Sepetuko

From the publisher's feed

Kurunzi ya falsafa inayoangazia bila woga masuala mazito yanayoiathiri jamii.