Sign up to save your podcastsEmail addressPasswordRegisterOrContinue with GoogleAlready have an account? Log in here.
FAQs about Sepetuko:How many episodes does Sepetuko have?The podcast currently has 153 episodes available.
December 03, 2021Sepetuko Podcast; Uchumi wa Fuliza sio utajiri!Rais katangaza kwamba Kenya sasa ni namba 6 kwa utajiri barani Afrika, Je utajiri huo uko wapi? Je upo miongoni mwa wakenya wanaotegemea mikopo ya Fuliza? Mbona magazeti yamejaa matangazo ya madalali kuuza mali ya watu wanaoshindwa kulipa mikopo ya benki?...more6minPlay
December 02, 2021Sepetuko Podcast; Iwapo uchumi umekua mbona vijana hawapati kazi?Rais amedai uchumi umekua ajabu hivi kwamba sasa Kenya ni namba 6 kwa utajiri barani Afrika, lakini mbona uchumi huo umeshindwa kubuni nafasi za kazi. Mojawapo ya dalili za ukuaji wa uchumi ni biashara za watu kupata faida huku watu wa umri wa kufanya kazi wakipata hizo kazi!...more6minPlay
November 30, 2021Sepetuko Podcast; George Kinoti ajipeleke jela ahudumie kifungo kwanza!Ni vigumu kwa afisa wa serikali ambaye mahakama imemtaja kuwa mfungwa kuendelea kuhudumu katika idara muhimu kwenye utaratibu wa kulinda sheria nchini -DCI. Itakuwa vigumu kwa mahakama kukubali saini zake kwenye rekodi za kesi zinazowasilishwa na idara ya upelelezi wa jinai....more6minPlay
November 29, 2021Sepetuko Podcast; Ubaguzi dhidi ya Afrika kufuatia ugunduzi wa virusi vya OmicronWazungu wamekuwa wepesi katika kutoa marufuku kwa ndege za mataifa ya kusini mwa Afrika na hali kile Afrika kusini ilifanya ni kugundua aina mpya ya virusi vya Korona-haikumaanisha kwamba Omicron imeanzia Afrika Kusini au Botswana....more6minPlay
November 24, 2021Sepetuko Podcast; Mike Sonko aomboleza ‘mkasa’ wa kupoteza ugavana!Kinachomchochea aliyekuwa gavana wa Nairobi kuandaa kanda za video zilizonasa kwa siri watu anaoamini wamemdhulumu kwa namna, ikiwemo kumwondoa mamlakani Nairobi, ni kupoteza kiti cha ugavana. Hata sio suala la kuwakabili wafisadi....more6minPlay
November 23, 2021Sepetuko Podcast; JE bodaboda watakataa pesa za abiria ambao hawajachanjwa?Hoteli zinatazamia kukusanya faida msimu wa likizo ya krisimasi, magari ya matatu pia yanajiandaa kufaidika zaidi msimu wa likizo hasa kwa kuwa msimu wa Korona uliathiri vibaya shughuli zao. Je serikali itatekeleza vipi maagizo kwamba wakenya ambao hawajachanjwa wanyimwe huduma?...more6minPlay
November 22, 2021Sepetuko Podcast; Wafanyakazi wadogo kubebeshwa mzigo wa makosa ya wakubwa!Kamati inayoongoza shughuli za kufufua Kenya Power yakiuka haki za wafanyakazi kwa kuwaitisha habari za akaunti zao za benki na mpesa. Ni mara nyingine tena ambapo wafanyakazi wadogo wanabebeshwa mzigo wa makosa ya mameneja!...more6minPlay
November 19, 2021Sepetuko Podcast; Wepesi katika kukabili suala la Kamiti- lakini imekuwapo walakin!Kuondolewa kwa mkuu wa magereza Whycliffe Ogallo kulifanywa kana kwamba alikuwa ndiye mfungwa wa Kamiti aliyekuwa ametoroka jela. Kuwaondoa wakubwa afisini kwafaa kuandamana na heshima zinazoendana na daraja la afisi zao....more7minPlay
November 18, 2021Sepetuko Podcast; Kumzuia Miguna Miguna kunaipa serikali sifa mbayaSuala la raia wa Kenya kila mara kukwama katika viwanja vya ndege barani ulaya, huku ikidaiwa kwamba serikali ya Kenya imemzuia asirejee nchi aliyozaliwa, linaifanya Kenya kuchekwa na mataifa ya wazungu; ni hali inayochangia katika utani dhidi ya waafrika!...more6minPlay
November 16, 2021Sepetuko Podcast; FKF imekuwa kaburi la kuzika vipawa vya sokaVijana wakiwa shuleni ni mashujaa katika kucheza soka. Lakini punde wakishajiunga na sekta ya soka nchini vipawa hufa; sababu ni FKF kutowapa nafasi watu wanaoweza kuongoza soka kwa roho safi ili kuboresha viwango vya mchezo huo nchini....more6minPlay
FAQs about Sepetuko:How many episodes does Sepetuko have?The podcast currently has 153 episodes available.