Sign up to save your podcastsEmail addressPasswordRegisterOrContinue with GoogleAlready have an account? Log in here.
FAQs about Sepetuko:How many episodes does Sepetuko have?The podcast currently has 153 episodes available.
November 10, 2021Sepetuko Podcast; Uteketezaji shule- je walimu wakuu huwasikiza wanafunzi?Shule kadhaa zimeripotiwa kuwatoza wanafunzi wote faini kufuatia visa vya kuteketezwa shule. Mbona kuwabebesha mzigo wanafunzi wote na hali makosa yamefanywa na wachache? Hatua kama hizo zinaashiria kwamba wakuu wa shule bila shaka hawawasikizi wanafunzi!...more6minPlay
November 09, 2021Sepetuko Podcast; Wanafunzi kuteketeza shule kunaashiria tatizo kuu zaidi katika jamii!Kenya imekuwa ikijenga desturi ya haki za kimsingi; haki za watoto, haki za wanawake, haki za wazee lakini imeshindwa kujenga mwenendo wa kuwajibikia makosa! Wanafunzi wanaoteketeza shule wanafikiria kwamba wanapigania haki, hawajui kwamba haki huanza kwa kuwajibikia makosa....more6minPlay
November 08, 2021Sepetuko Podcast; Kuwafuta kazi wafanyakazi KEMSA ni kukosa busara ya kifalmeNchi nzima imefahamu tangu mwaka jana (2020) kwamba wakosaji katika shirika la KEMSA wamekuwa wasimamizi-mameneja. Lakini sasa wanaobebeshwa mzigo ni wafanyakazi wadogo wasio na mamlaka katika taasisi ile; huo unaitwa ukosefu wa ufalme!...more6minPlay
November 04, 2021Sepetuko Podcast; Suala la kisomo cha Oscar Sudi laibua maswali kadhaa!Mbona mbunge wa Kapseret ameshinda uchaguzi wa eneo bunge kwa mihula miwili na hali kiwango chake cha masomo kinatiliwa shaka- amewezaje kuifanya kazi ya ubunge bila elimu ifaayo. Sudi ana kipi bora kinachowafanya wapiga kura wa Kapseret kumpenda?...more6minPlay
November 01, 2021Sepetuko Podcast; Unafiki wa kutaka mawaziri wahusikao siasa wajiuzuluTangu ije serikali ya Jubilee mwaka 2013 baadhi ya mawaziri wametekeleza maagizo ya kisiasa kutoka kwa wakubwa wao wa kisiasa. Mbona wanasiasa wanaolalamika leo hawakulalamika? Tumesema yamekuwapo makosa tangu mwanzo- ni unafiki kuanza kulalamika leo....more6minPlay
October 29, 2021Sepetuko Podcast; Ndoa ya kisiasa ya Anne Waiguru na Mwalimu Ruto PhDMuungano wa Gavana wa Kirinyagah na mwalimu Ruto PhD ni sawa na ushirika wa sungura wawili. Ni watu wawili wanaojua namna ya kujitafutia nafasi ya kujikuza hivi kwamba mioyoni mwao mawazo ya kuihudumia jamii huja baadaye....more6minPlay
October 26, 2021Sepetuko Podcast; Fedheha za Anwar Loitiptip- Seneta wa Lamu.Wakenya wamekuwa wakiskia habari za kufedhehesha kumhusu Seneta wa Lamu; mara amefyatua risasi, mara amefyatuliwa risasi, mara binti amedai kupigwa naye. Visa hivi vingi vinaripotiwa kufanyika usiku wa manane. Tunautaja huo kuwa ukiukaji wa sura ya katiba inayohusu uongozi na maadili....more6minPlay
October 25, 2021Sepetuko Podcast; Sarakasi za Ugavana Nairobi- Jiji yafaa liondolewe miongoni mwa kauntiKwa kuwa jiji la Nairobi huwakilisha Kenya nzima likiwa jiji kuu, yafaa lisimamiwe na idara maalum ya serikali ya taifa wala sio kwa njia za kisiasa. NMS imefanya kazi nzuri kuliko wanasiasa wawili ambao wamekuwa magavana tangu mwaka 2013....more7minPlay
October 21, 2021Sepetuko Podcast; BABA na Mwalimu Ruto wabembeleza kura KirinyagahWanasiasa wawili maarufu zaidi nchini wametumia kilele cha mashujaa dei kule Kirinyagah kubembeleza kura za Mt Kenya. Mwalimu Ruto, PhD, na BABA wametumia ndimi laini kutaka wakubalike Mt Kenya, wala hawakufika Wang’uru Stadium kuhudhuria mashujaa dei!...more6minPlay
October 19, 2021Sepetuko Podcast; Ahadi kwa mjane wa Dedan Kimathi na Mau MauBABA amecheza mchezo wa siasa kwa kupiga magoti mbele ya mjane wa shujaa Dedan Kimathi kupokea baraka. Ametoa ahadi ya kuwafadhili kwa namna wakereketwa wa Mau Mau. Ahadi kwa wakereketwa hao zisiwe ahadi za kawaida za wanasiasa kama ilivyokuwa ahadi za viwanja vya michezo ambazo Jubilee ilizotoa 2013....more6minPlay
FAQs about Sepetuko:How many episodes does Sepetuko have?The podcast currently has 153 episodes available.