Uchumi na Biashara

Uchumi na Biashara

By Standard MediaArtsFood
Download on the App Store

Uchumi na Biashara episodes

  • Uchumi na Biashara Podcast: Korona yaathiri biashara ya magari
    Patrick Wachira, mfanyabiashara wa kuyauza magari anasema amefanya biashara hiyo kwa zaidi ya miaka sita ila korona ilimsababishia hasara ya mamilioni ya fedha. Kwa mujibu wa Wachira, biashara ya magari ni bahati nasibu kwani huwezi kujua idadi ya magari utakayouza kwa mwezi au wiki. Aidha, Wachiri amesema Wakenya hawajakumbatia magari ya umeme kikamilifu. Robert Menza amezungumza naye.
    18 min
  • Uchumi na Biashara Podcast; Biashara ufuoni, mapato tosha kwa vijana
    Biashara za ufuoni katika Kaunti ya Kilifi zimesadia vijana wengi kujimudu kimaisha na kuacha uraibu wa mihadarati. Gibson Kombe ni baharia na mwanzilishi wa fuo moja maarufu[vidazini beach, Kilifi ambaye amefungua biashara mbalimbali katika fuo hiyo na pia kuwaajiri vijana wengi na kuwawezesha kuanza kujimudu kimaisha kwa zaidi ya miaka kumi sasa. Mwanahabari wetu Marion Kithi anatupambia sehemu hii.
    13 min
  • Uchumi na Biashara Podcast: Wauza-bidhaa katika hafla za kisiasa
    Wanasiasa wakiendeleza mikutano katika kaunti mbalimbali nchini, ni afueni kwa wafanyabiashara ambao biashara zao zilikuwa zimeathirika kutokana na Covid-19. Wengi wa wafanyabiashara hunufaika pakubwa na mikutano ya kisiasa kwa kuuza bidhaa zao katika majukwaa hayo. Katika Kaunti ya Pokot Magharibi, wanasiasa wameendelea kuziinua biashara kwa kuwanunulia wafuasi wao bidhaa mbalimbali. Moses Kiraese amefanya mazungumzo na wafanyabiashara mjini Kapenguria
    15 min
  • Uchumi na Biashara Podcast; Mapato ya ushonaji nguo yashinda mshahara wa Dubai
    Mama Esther anavyotambulika na wateja wake ,ni mama wa watoto watano na amekuwa akifanya kazi ya cherehani kwa miaka minane. Kazi hii inampa mapato tosha kwani amewasomesha nduguze na kumjengea mamaye nyumba. Hata hivyo, janga la korona limetikisa biashara yake kwani wateja wamepungua. Mwanahabari wetu Marion Kithi amemtembelea na kuzungumza naye kuhusu biashara yake.
    11 min
  • Uchumi na Biashara Podcast; Korona ilinipokonya ajira, sasa nauza mboga Nyamira
    Chris Agata, ana shahada katika Taaluma ya Uhasibu. Licha ya kukamilisha masomo na kuhitimu, Agata ni mfanyabiashara wa mboga, anazotoa shambani mwake. Alifutwa kazi kutokana na janga la korona, hivyo kumlazimu kuzamia biashara ili kujikimu maishani. Anasema biashara yake inaendelea kukua, hivyo amekumbatia mfumo wa kujiajiri. Agata amezungumza na mwanahabari wetu, William Omasire.
    15 min
  • Uchumi na Biashara Podcast; Usidharau Mutura, inanipa mapato tosha
    Mutura ni mojawapo ya kitoweo kinachopendwa na wengi, mutura huuzwa nyakati za jioni jioni, wateja wakisema utamu wake ni giza, vumbi na kutojua unakula nyama ya nini hasa. Mutura ni mchanganyiko wa vipande vipande vya nyama, wenyewe huita sausage ya watu wa kawaida. Caleb Kimtai, mfanyabiashara mjini Makutano Kaunti ya Pokot Magharibi amezungumza na mwanahabari wetu Moses Kiraese na anakiri kuwa japo baadhi hudharau mutura, anajua siri ni nini kwani kupitia mutura, anakimu familia yake na pia ametekeleza miradi mbalimbali nyumbani kwao
    8 min
  • Uchumi na Biashara Podcast: Utalii Pwani wanoga Krisimasi na Mwaka Mpya
    Licha ya athari za janga la korona, sekta ya utalii inazidi kunawiri msimu huu wa Krisimasi na Mwaka Mpya kulinganishwa na mwaka jana. Ilivyo sasa hoteli nyingi zimeandikisha takriban asimilia tisini ya wageni. Asilimia kubwa ni watalii wa humu nchini. Maeneo mengine pia ya kitalii yamenakili idadi ya juu ya wageni ambao wameyazuru na wengine ambao pia wananuia kuyazuru. Mwanahabari wetu, Robert Menza amezungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Kitaifa cha Sekta ya Watalii wa humu nchini, Dkt. Tuqa Jirmo.
    18 min
  • Uchumi na Biashara Podcast; Biashara ya maji imeninunulia ploti na nyumba
    Maji ni uhai, ni hitaji la kila mtu. Hapa jijini Nairobi, kuna wakati watu hawana maji katika nyumba zao, na ndipo Justus Ambani sawa na wengine wengi, hujihusisha na kazi ya kuuza maji kutumia mkokoteni. Ambani anayeendesha shughuli hii katika mitaa ya Fedha na Tassia Embakasi Mashariki, anasema kupitia biashara hii amenunua kipande cha ardhi vilevile nyumba. Esther Kirong' amemhoji katika makala ya leo ambapo anasema aliacha kazi ya kuajiriwa kisha kujiajiri. Ameweza kuwaajiri wengine wakiwamo vijana.
    15 min
  • Uchumi na Biashara Podcast: Krismasi ya taabu; bidhaa ghali, maisha magumu
    Msimu wa Krismasi na mwaka mpya kwa kawaida huwa wenye shamrashamra. Watu wengi hununua vyakula, wengine nao husafiri kwenda kusherehekea pamoja na jamaa, ndugu na marafiki. Lakini msimu huu, huenda mambo yakawa tofauti kulinganishwa na miaka ya awali kutokana na kupanda kwa bei za bidhaa za msingi. Mwanahabari wetu, Martin Ndiema amezungumza na baadhi ya Wakenya kuhusu kupanda kwa bei za bidhaa na jinsi wanavyopanga kusherehekea msimu huu.
    8 min
  • Uchumi na Biashara Podcast; Biashara ya ndizi mbichi
    Ndizi ni zao la biashara. Katika Kaunti za Kisii na Nyamira, karibu kila familia ina ndizi kwa ajili ya chakula na biashara. Kijijini Konate Nyamira, William Mose Gesora anajihusisha na biashara ya ndizi mbichi. Gesora anasema biashara hii imemsaidia si kupata mahitaji ya kimsingi tu bali hata kuwalipia wanawe karo. Gesora ambaye ana shamba ekari mbili la ndizi amezungumza na mwanahabari wetu William Omasire na anasema biashara yakupasa uwe wa kwanza kuwajibika ili kutojilaumu.
    13 min

About Uchumi na Biashara

From the publisher's feed

Inahusu masuala ya ujasiriamali, biashara ndogo ndogo, ushauri kuhusu uwekezaji na shughuli nyinginezo za kiuchumi.