Uchumi na Biashara

Uchumi na Biashara

By Standard MediaArtsFood
Download on the App Store

Uchumi na Biashara episodes

  • Uchumi na Biashara Podcast; Kipato cha pombe ya mnazi, ila polisi wanasumbua
    Pombe ya mnazi ni kinywaji cha kiasili kinachopendwa sana na ni maarufu zaidi kwenye maeneo ya Pwani na baadhi ya wenyeji wamekuwa wakitegemea pombe hiyo kibiashara. Jackline Kenga, mmoja wa wafanyabiashara wa pombe ya mnazi anasema licha ya kwamba biashara hiyo inamsaidia, anahangaishwa na polisi wanaoendesha oparesheni kila uchao. Hata hivyo, anasema kamwe hataasi biashara yenyewe kwani anapata mapato ya kutosha. Marioni Kithi amezungumza naye.
    10 min
  • Uchumi na Biashara Podcast; Nguo za Kimijikenda
    Edna Dhababu mwenye umri wa miaka 27, mkazi wa Rabai katika Kaunti ya Kilifi ni mfanyabiashara anyejihusisha na uuzaji wa mavazi ya utamaduni wa Jamii ya Mijikenda. Si hilo tu, Dhahabu pia hukodisha mavazi hayo kwa wateja ambao huwa na hafla mbalimbali zikiwamo za ukumbusho wa kuzaliwa na harusi. Mwanahabari wetu Robert Menza ametangamana naye na kufanya mahojiano ya moja kwa moja.
    21 min
  • Uchumi na Biashara Podcast; Uuzaji wa Samaki, kipato tosha
    Nelson Babu ana taaluma ya uhasibu. Alifutwa kazi wakati korona iliporipotiwa nchini. Hata hivyo hakukata tamaa; amezamia biashara ya samaki mtaani Pipeline, Nairobi. Biashara yake licha ya kuanza ikiwa ndogo, amefanikiwa kufungua tawi jingine mtaani Umoja na anatazamia kufungua matawi zaidi, mbali na kuwapa vijana ajira. Esther Kirong' amezungumza naye
    29 min
  • Uchumi na Biashara Podcast: Mitumba imeniwezesha kununua mashamba
    Peter Mureithi maarufu Boiyoo anauza long'i za mitumba mjini Kapenguria, Pokot Magharibi. Boiyoo ameuza nguo hizi kwa zaidi ya miaka thelathini. Anasema kazi hii imemsaidia kununua vipande kadhaa vya ardhi. Katika mazungumzo na mwanahabari wetu Moses Kiraese, anaelezea matumaini ya kufurahia matunda ya biashara yake hata atakapostaafu.
    8 min
  • Uchumi na Biashara Podcast; Biashara ya mitumba
    Katika podcast hii tunaangazia panda-shuka za wafanyabiashara wa nguo za mitumba wakati huu wa janga la korona.
    Mmoja wa wafanyabiashara hao mjini Kitale kwa jina Andrew Chongo anayeuza suti za mitumba anasema kupigwa marufuku kwa uagizaji wa baadhi hizo kulisambaratisha biashara zao na hata wengine kulazimika kubadili biashara ili kuzikimu familia zao.
    Chogo anasema amri ya Rais Kenyatta ya kuondoa kafyu itastawisha uchumi wa taifa hili ikizingatiwa kwamba sasa wanaweza kusafiri ama kuagiza nguo kutoka mataifa mengine.
    Hata hivyo Chogo analipendekezea serikali kufufua na kuanzisha viwanda vya pamba na kuwawezesha wakulima kupanda mmea huo na kuwafuga kondoo aina ya merino ili kutoa ajira kwa vijana na kuwapiga jeki wakulima kiuchumi.
    Mwanahabari wetu wa Trans Nzoia, Martin Ndiema amemhoji mfanyabiasha huyo.
    10 min
  • Uchumi na Biashara Podcast; Biashara ya ngozi yaathirika Turkana
    Wafanyabiashara wa ngozi katika Kaunti ya Turkana wanakadiria hasara kutokana na ukosefu wa karo baada ya soko na bei ya ngozi kusambaratika. Wakizungumza na mwanahabari wetu wa Turkana, Mike Ekutan wafanyabiashara hao wanalazimika kutupa ngozi za ng'ombe, kondoo na mbuzi kwa kukosa thamani. Hata hivyo, wanaowachinja punda wanapata faida kwani ngozi yake hununuliwa na kupelekwa Uchina.
    23 min
  • Uchumi na Biashara Podcast; COVI-19, pigo kwa sekta ya hoteli
    Athari za virusi vya korona zinazidi kushuhudiwa katika sekta mbalimbali hasa zinazotegemewa na Wakenya, huku baadhi ya sekta hizo zikikadiria hasara kubwa au mapato ya chini ikilinganishwa na hapo awali.
    Mwanahabari wetu wa Kunti ya Taita Taveta, Rajab Kafuta amezuru baadhi ya hoteli za kitalii katika Mbuga ya Wanyamapori ya Tsavo, na kufanya mahojiano na Willie Mwadilo ambaye ni Meneja wa Hoteli za Taita Hills. Mwadilo ameweka wazi jinsi hali ilivyokuwa kabla ya taifa hili kukumbwa na korona na hali ilivyo kwa sasa ikizingatiwa maagizo yaliyowekwa na Wizara ya Afya kudhibiti virusi hivyo. Kuu linalojitokeza katika mahojiano haya ni kwamba sekta hiyo ingali inakadiria hasara ya mamilioni ya fedha na kuna haja ya masharti kulegezwa ili kuikwamua.
    9 min
  • Uchumi na Biashara Podcast; Bei za mafuta, pigo kwa sekta ya matatu
    Anthony Ndirangu, Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha Uchukuzi wa Umma la NYENA SACCO anaeleza masaibu wanayopitia kufuatia kupanda kwa bei za mafuta. Ndirangu anasema shirika hilo limekuwa likiandikisha hasara kubwa hasa baada ya mafuta kuongezwa bei licha ya kuwa limekuwa likipata hasara kutokana na athari za korona. Kwa mujibu wa Ndirangu, serikali inazidi kuikandamiza sekta ya uchukuzi.
    Mwanahabari wetu, John Mbuthia amezungumza naye ambapo anasimulia yanayowasibu kutokana na kupanda kwa bei za mafuta.
    20 min
  • Uchumi na Biashara Podcast: Mtumba Man; sarakasi za kuwavutia wateja
    Steve Opondo, maarufu Mtumba Man kutoka Kaunti ya Kisumu ni mfanyabiashara aliyejipatia umaarufu kutokana na sarakasi zake wakati wa kuuza nguo za mitumba. Anasema aliamua kubuni njia ya kuwavutia wateja wake ambao wengi ni akina dada. Mtumba Man sasa ni jina kubwa; amepewa kandarasi ya miaka mitano katika duka la nguo la Devine Collections hapa jijini Nairobi. Maishani, anatazamia kuwa mfanyabiashara mkubwa. Mtumba Man amezungumza na mwanahabari wetu, Esther Kirong' katika podcast hii.
    12 min

About Uchumi na Biashara

From the publisher's feed

Inahusu masuala ya ujasiriamali, biashara ndogo ndogo, ushauri kuhusu uwekezaji na shughuli nyinginezo za kiuchumi.