Uchumi na Biashara

Uchumi na Biashara

By Standard MediaArtsFood
Download on the App Store

Uchumi na Biashara episodes

  • Uchumi na Biashara Podcast; Wabunge ni wasaliti-deni kila siku
    Wakenya wameendelea kulalamikia kupanda kwa gharama ya maisha, serikali nayo ikizidisha deni hadi trilioni 10 sasa. Aidha, wabunge na maseneta wamelaumiwa kwa kupitisha pendekezo la kuongeza deni la taifa kutoka shilingi trilioni 9, hadi 10 hali inayochangia kupanda kwa bei za bidhaa.
    Mike Ekutan ametangamana na Wakenya mjini Lodwar, Kaunti ya Turkana.
    15 min
  • Uchumi na Biashara Podcast; Bidhaa ghali, pigo kwa uuzaji chakula
    Bi. Mwansa, mwanamke mwenye umri wa miaka 70 amekuwa akijihusisha na upishi wa vyakula mbalimbali ambavyo huviuza kwa wateja kila siku, biashara ambayo ameifanya kwa zaidi ya miaka arubaini sasa. Biashara hii aliitegemea sana kuyakidhi mahitaji yake pamoja na wanawe kukiwamo kugharimia karo ya ya wanawe. Mwanamke huyu ambaye ni mkazi wa Majengo, Mvita katika Kaunti ya Mombasa anajihuisha na upishi wa chapati na maharagwe ya nazi.
    Vyakula vingine ambavyo pia Bi. Mwansa hupika ni mikate ya sinia na mitai. Kupanda kwa gharama ya bidhaa za upishi ukiwamo ya unga wa ngano, mafuta ya kupikia miongoni mwa bidhaa nyingine ambapo huzitumia kwa upishi kumemwathiri sana. Mwanahabari wetu wa Mombasa Robert Menza amezungumza naye katika Uchumi na Biashara Podcast
    22 min
  • Madharau kazini yanavunja moyo
    Vincent Oduor akumbuka jinsi alivyoathiriwa na ghasia za baada ya uchaguzi, kazi yake ya ushonaji kutumia cherahani ikiathirika pakubwa. Anakumbukwa jinsi mashine za ushonaji zilivyoibwa wakati wa ghasia hizo. Kwa sasa kazi yake inanawiri na anapata faida
    10 min
  • Uchumi umeimarika kwa asilimia 7.5, nani amefaidika?
    Uchumi wa Kenya uliimarika mwaka wa 2021 baada ya kuathirika kufuatia Janga la Korona mwaka wa 2020. Kwa mujibu wa ripoti ya Taasisi ya Takwimu, KNBS uchumi ulikua kwa asilimia 7.5, kiwango hiki kikitajwa kuwa cha juu zaidi baada ya kipindi cha miaka kumi na mmoja. Aidha, nafasi 923,100 za kazi zilibuniwa katika mwaka huo wa 2021, wageni waliokuja nchini wakiongezeka hadi 871,300. Esther Kirong ametupambia makala haya.
    4 min
  • Kiwango cha chini cha nyongeza ya mshahara: Uhuru
    Je, tangazo la Rais Kenyatta kuhusu asimilia 12 ya nyongeza ya mshahara wa chini kwa wafanyakazi, linamaanisha nini?
    Na je, ni wafanyakazi gani hasa watakanufaika kutokana na agizo hili ambalo limetakiwa kutekelezwa kuanzi mwezi huu?
    Jinsi anavyoarifu Victor Mulama, ni wafanyakazi wa viwango vya chini pekee ndio watakaoathirika, na licha ya hayo nyongeza ya mshahara itatozwa kodi.
    8 min
  • Uchumi na Biashara Podcast: Makazi bora; ushirikiano mwema na serikali
    Serikali ikijizatiti kufanikisha mpango wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa Wakenya, Kampuni ya ABC Homes vilevile imeweka mikakati kuhakikisha mpango huo unafaulu. Mhandisi Eveline Muringa ambaye ni Meneja wa Mradi wa ujenzi wa nyumba hizo anasema kwamba lengo lao hasa ni kuhakikisha Wakenya wengi wanamiliki nyumba kwa gharama ya chini. Robert Menza amezungumza naye.
    15 min
  • Wanabodaboda wakerwa na polisi wanaoitisha hongo
    Leo katika kitengo hiki tunaandazia mahangaiko ya waendeshaji pikipiki kufuatia msako katika harakati za kuinadhifisha sekta ya bodaboda. Msako huo ambao hata hivyo ulisitishwa kuruhusu mazungumzo, umesababisha madhara wahudumu hao wanaokiri ndoa zao zinayumba, wake zao wakiwatoroka kwa kutokuwa na fedha. Mwanahabari wetu wa Kaunti ya Trans Nzoia , Martin Ndiema ametangamana na baadhi yao na kufanya mahojiano nao.
    8 min
  • Uchumi na Biashara Podcast; Bei ghali ya mbolea na pembejeo nyinginezo
    Wakenya kwenye maeneo yanayoendeshwa kilimo msimu huu wanalalamikia kupanda kwa bei ya mbolea kwa zaidi ya asilimia hamsini, huku mbolea gunia moja ya kilo hamsini ikiuzwa kwa shilingi elfu sita na hata elfu saba mia saba katika baadhi ya maduka.
    Wakulima wanadai kuwa bei ya mbolea ni ya juu sana ikilinganishwa na bei ya mahindi gunia moja la kilo tisini hivyo kupandisha maradufu gharama ya uzalishaji. Aidha, kuna wale ambao tayari wanasema kuwa hawataweza kupanda mahindi msimu huu kutokana na kupanda kwa gharama ya uzalishaji. Tumezungumza na mkulima Samuel Lelei Karuma.
    12 min
  • Uchumi na Biashara Podcast; Kilio cha wanabodaboda kwa Rais Kenyatta
    Wahudumu wa bodaboda wamewalaumu polisi kwa kuwahangaisha wakitekeleza agizo la Rais kunadhifisha sekta hiyo. Kulingana Wycliffe Nyanamba, Mwenyekiti wa Wanabodaboda hapa jijini Nairobi, polisi wanawahangaisha hadi kwenye makazi yao wakiendesha msako huo wengine wakiwapunja pesa. Hata hivyo, Nyanamba amewalaumu baadhi ya wahudumu hao kwa kukiuka sheria za trafiki. Msako huu unafuatia kisa ambapo wanabodaboda wa Forest Road walimvamia na kumdhulumu kimapenzi mwanamke mmoja. Kauli yake inajiri wakati ambapo oparesheni hiyo imesitishwa kwa muda kupisha mazungumzo.
    11 min

About Uchumi na Biashara

From the publisher's feed

Inahusu masuala ya ujasiriamali, biashara ndogo ndogo, ushauri kuhusu uwekezaji na shughuli nyinginezo za kiuchumi.