Karibu sana kusikiliza mafundisho ya Biblia katika Wagalatia. Tunafanya mfululizo kwa waraka mzima, na hiyo ni namba 6, katika kifungu Gal 3:15–22. Hapa Paulo anaonyesha tofauti baina ya sheria na ya ahadi za Mungu ambazo ni wokovu wetu tukimpokea Yesu kwa imani.
karibu.
Mwalimu Maiki. Mchungaji Mmasa.
Soma Biblia
Wagalatia 3:15–22
15 Ndugu zangu, nanena kwa jinsi ya kibinadamu. Lijapokuwa ni agano la mwanadamu, hata hivyo likiisha kuthibitika, hakuna mtu alibatilishaye, wala kuliongeza neno. 16 Basi ahadi zilinenwa kwa Abrahamu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa wazawa, kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani, Kristo. 17 Nisemalo ni hili; agano lililothibitishwa kwanza na Mungu, torati iliyotokea miaka mia nne na thelathini baadaye hailitangui, hata kuibatilisha ile ahadi. 18 Kwa maana urithi ukiwa kwa sheria, hauwi tena kwa ahadi; lakini Mungu alimkirimia Abrahamu kwa njia ya ahadi.
19 Torati ni nini basi? Iliingizwa kwa sababu ya makosa, hadi aje huyo mzao aliyepewa ile ahadi; iliamriwa kwa utumishi wa malaika kwa mkono wa mjumbe. 20 Basi aliye mjumbe si mjumbe wa mmoja; bali Mungu ni mmoja. 21 Basi je! Torati haipatani na ahadi za Mungu? La hasha! Kwa kuwa, kama ingalitolewa sheria iwezayo kuhuisha, hakika haki ingalipatikana kwa sheria. 22 Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi hao waaminio wapewe ile ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.
This is a public episode. If you would like to discuss this with other subscribers or get access to bonus episodes, visit mwalimumike.substack.com