Mchungaji Mmasa na Mwalimu Mike tunafundisha Biblia katika masomo ya siku kwa Jumapili ijayo ili kuwasaidia watu wote na hasa watumishi katika maandilizi yao.
Wiki hii ya Jumapili tarehe 24/3 ni Jumapili ya Mitende, ukurasa 93 katika kitabu cha sala.
Kwenye hiyo sehemu ya pili tunafundisha juu ya wazo kuu la Njia ya Msalaba, 1 Wakorintho 1:18–25, Isaya 50:4–9, Zaburi 22. Kuna tofauti gani kati ya kuheshimu msalaba na ujumbe wa msalaba? Kuna nini katika Zaburi na Isaya inayoonekana katika mateso ya Yesu? Nini maana ya Yesu kusema Mungu wangu mbona uniacha? Karibu kusikiliza mafundisho yetu.
Katika sehemu ya kwanza, podi iliyotangulia, tulifundisha juu ya tukio la Yesu kuingia Yerusalemu kwa shangwe katika Marko 11:1–10 na tukafafanua baadhi ya mambo makuu katika somo la Injili, Marko14:32–15:41. Hiyo unaweza kusikia hapa
Karibu!
This is a public episode. If you would like to discuss this with other subscribers or get access to bonus episodes, visit mwalimumike.substack.com