Sikiliza historia nzima ya kusisimua ya kumhusu mwanamichezo mkongwe na maarufu wa mpira wa miguu, Diego Armando Maradona. Raia wa Nchini Argentina aliyejipatia umaarufu mkubwa baada ya kufunga bao kwa mkono katika kombe la dunia mwaka 1986 huko Mexico dhidi ya England, goal hilo likipewa jina la "Hand of God" na baadae akifunga tena goli la karne "The Goal of Century". Sikiliza Historia yake, maisha yake ya utukutu, kuhusishwa na madawa ya kulevya, kuwa kocha wa Argentina, vikombe na mataji yake, maisha yake ya kawaida na mengine mengi, mpaka kufariki kwake 25 Nov. 2020. Imeandikwa na Saidi Kawage na kusomwa na Aucland Mudu.