Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 08 APRILI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika shughuli za shirika lisilo la kiserikali la KINNAPA Development Programme la huko nchini Tanzania katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu likijikita zaidi katika usawa wa kijinsia. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani:Uganda, ambayo tayari ni mwenyeji wa wakimbizi wengi zaidi barani Afrika, inakabiliwa na shinikizo kubwa baada ya wakimbizi zaidi ya 41,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kuingia nchini humo tangu Januari mwaka huu, wakikimbia machafuko mapya mashariki mwa nchi yao limesema leo Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. UNHCR imesema watu walioko katika mazingira hatarishi wanatambuliwa kwa msaada maalum, huku familia zilizotengana zikisaidiwa kuunganishwa tena.Siku kumi baada ya matetemeko ya ardhi ya kutisha yaliyoitikisa Myanmar tarehe 28 Machi, idadi ya vifo inaendelea kuongezeka. Titon Mitra, Mwakilishi wa Kikanda wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP nchini humo, akiripoti leo akiwa katika jiji liloharibiwa sana la Mandalay, kwa njia ya video ameripoti kwa waandishi wa habari jijini Geneva, Uswisi akisema, “idadi ya vifo ya hivi karibuni imepita watu 3,500 na “inaweza kuendelea kuongezeka.”Kenya, Uganda na Rwanda zitanufaika na mpango wa mlo shuleni baada ya leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kutangaza kuwa linaendeleza ushirikiano wake na Taasisi ya Novo Nordisk, kupitia ushirikiano wa kihistoria kati ya sekta binafsi na ya umma unaojumuisha Wizara ya Mambo ya Nje ya Denmark na Taasisi ya Grundfos, ili kupanua mpango wa mlo shuleni kutokana na chakula kinachozalishwa ndani ya nchi husika. Ushirikiano huu utajenga mfumo wa msaada unaohakikisha uendelevu wa muda mrefu wa mpango huu.Na mashinani mashinani jana tarehe 7 Aprili hapa Umoja wa Mataifa kumefanyika kumbukizi ya miaka 31 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda ambapo mmoja wa wazungumzaji alikuwa Germaine Tuyisenge Müller, manusura wa mauaji hayo na wakati huo alikuwa na umri wa miaka 9 wakiishi mji mkuu Kigali.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    12 min
  • Dayspring Foundation nchini Tanzania yatekeleza kivitendo dhana ya UN ya michezo kwa maendeleo
    Siku ya kimataifa ya Michezo kwa ajili ya Maendeleo na Amani imeadhimishwa tarehe 6 mwezi huu wa Aprili maudhui yakiwa Ujumuishaji wa kijamii, hususan makundi ya pembezoni. Umoja wa Mataifa kupitia wavuti wake unasema kuwa siku hii inatambuliwa kutokana na nafasi ya michezo katika kuleta mabadiliko chanya, kuondoa vikwazo na kuvuka mipaka. Na usuli wa maudhui ya mwaka huu ni kwamba fikra potofu kwenye jamii zimesababisha baadhi ya watu kutokana na jinsia yao, umri, au rangi wanashindwa kushiriki kwenye michezo ambayo kwa njia moja au nyingine hutokomeza umaskini kwa kuwezesha washiriki kujipatia kipato. Nchini Tanzania shirika la kiraia la Dayspring Foundation limetambua nafasi ya michezo na limeanza kuchukua hatua. Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Rosemary Mwaipopo ambaye anaanza kwa kuelezea ni kwa nini waliamua kujikita katika kusaka vipaji.
    5 min
  • Kwibuka2025: Katibu Mkuu UN ahimiza mshikamano wa kimataifa dhidi ya chuki
    Dunia inapokumbuka miaka 31 tangu mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma ujumbe mzito wa maombolezo na onyo, akitaka mshikamano wa kimataifa kupambana na ongezeko la chuki, mgawanyiko, na misimamo mikali kupitia mifumo ya kidijitali. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
    3 min
  • 07 APRILI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia makumbusho ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, na Siku ya Afya Duniani. Makala inamulika nafasi ya michezo katika kusongesha amani na maendeleo, na mashinani tunakwenda nchini Kenya, kulikoni?Dunia inapokumbuka miaka 31 tangu mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma ujumbe mzito wa maombolezo na onyo, akitaka mshikamano wa kimataifa kupambana na ongezeko la chuki, mgawanyiko, na misimamo mikali kupitia mifumo ya kidijitali.Leo ni Siku ya Afya Duniani ambayo mwaka huu inangazia suala muhimu kwa afya ya dunia, changamoto maalum wanazokumbana nazo wanawake na wasichana lakini pia vifo vya watoto wachanga, na ili kuhakikisha changamoto hizo zinashughulikiwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO limezindua  kampeni ya mwaka mzima ya “Mwanzo wenye afya ni mustakbali wenye matumaini”..Makala inamulika nafasi ya michezo katika kusongesha amani na maendeleo, ambapo Assumpta Massoi amezungumza na Rosemary Mwaipopo, Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kiraia la DaySpring Foundation nchini Tanzania. Yeye alikuwa ni miongoni mwa washiriki wa Mkutano wa 69 wa Hali ya Wanawake duniani, CSW69 uliofanyika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa mwezi uliopita wa Machi.Na mashinanileo ikiwa leo ni siku ya afya duniani, kupitia mahojiano yaliyofanikishwa na washirika wetu Radio Domus, fursa ni yake Padri Thaddeus Mukaya wa kanisa la katoliki la Parokia ya Embulbul ambalo pamoja na wadau wengine waliandaa huduma za bure za matibabu kwa wenyeji wa eneo hilo ili kusaidia jamii ambazo haziwezi kujimudu kimaisha.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    12 min
  • Hatua za haraka zinahitajika sasa kuzuia vifo na kulinda afya ya wanawake na wasichana: UN
    Leo ni Siku ya Afya Duniani ambayo mwaka huu inangazia suala muhimu kwa afya ya dunia, changamoto maalum wanazokumbana nazo wanawake na wasichana lakini pia vifo vya watoto wachanga, na ili kuhakikisha changamoto hizo zinashughulikiwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO limezindua  kampeni ya mwaka mzima ya “Mwanzo wenye afya ni mustakbali wenye matumaini”. Flora Nducha anafafanua zaidi.
    3 min
  • Uongozi bora na matumizi bora ya rasilimali vitaikomboa Afrika kimaendeleo: Vijana Kenya
    Majadiliano ya siku mbili yanayofanyika kila mwaka ya será kuhusu maendeleo endelevu. Majadiliano hayo yanayokunja jamvi leo jijini Nairobi Kenya yameandaliwa na Club De Madrid na mwaka huu yakijikita na ufadhili wa maendeleo na kuwaleta pamoja wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wastaafu w anchi na serikali, wadau wa maendeleo na vijana. Stella Vuzo kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi amepata fursa ya kuzungumza na baadhi ya vijana wanaoshiriki mkutano huo wa club de Madrid je wanasemaje? Ungana nao katika makala hii
    4 min
  • Umoja wa Mataifa kuendelea kuisaidia Somalia kuonda mabomu ya kutegwa ardhini
    Ikiwa leo ni Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini na Msaada wa Hatua Dhidi ya Mabomu hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akisisitiza mataifa duniani kote kuheshimu mikataba ya kimataifa dhidi ya vilipuzi na silaha nyingine, Umoja wa Mataifa leo umethibitisha tena dhamira yake ya kusaidia Somalia katika mapambano dhidi ya hatari za vilipuzi kwa ajili ya mustakabali salama kwa Wasomali wote. Anold Kayanda na taarifa zaidi.
    2 min
  • 04 APRILI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini. Makala inamulika harakati za kusongesha malengo ya maendeleo endelevu ikitupeleka nchini Kenya na mashinani tunasalia huko huko nchini Kenya, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini na Msaada wa Hatua Dhidi ya Mabomu hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akisisitiza nchi kuheshimu mikataba ya kimataifa dhidi ya vilipuzi na silaha nyingine, Umoja wa Mataifa leo umethibitisha tena dhamira yake ya kusaidia Somalia katika mapambano dhidi ya hatari za vilipuzi kwa ajili ya mustakabali salama kwa Wasomali wote.Mwaka huu wa 2025, Siku ya Kimataifa ya Uhamasishaji Kuhusu Mabomu ya Ardhi na Usaidizi kwa Hatua Dhidi ya Mabomu inaadhimishwa chini ya kaulimbiu “Mustakabali Salama Unaanzia Hapa.” Umoja wa Mataifa inasisitiza umuhimu wa kufadhili miradi midogo yenye athari za haraka kusaidia watu wenye ulemavu wa viungo waliathirika katika mizozo. Juhudi hizi zinaimarisha ulinzi wa raia na kupanua teknolojia na uvumbuzi katika nchi zinazoendelea.Makala ambayo inamulika majadiliano ya siku mbili yanayofanyika kila mwaka ya será kuhusu maendeleo endelevu. Majadiliano hayo yanayokunja jamvi leo jijini Nairobi Kenya yameandaliwa na Club De Madrid na mwaka huu yamejikita na ufadhili wa maendeleo, Stella Vuzo kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi amepata fursa ya kuzungumza na baadhi ya vijana wanaoshiriki mkutano huo wa club de Madrid.Na mashinani leo utamsikia mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Bayero jimboni Kano nchini Nigeria anayeshiriki mkutano wa majadiliano ya ufadhili wa maendeleo endelevu unaofanyika Nairobi Kenya.Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu!
    10 min
  • Uteguaji mabomu ya ardhini ni suala la amani na kiutu - UNMAS
    Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini, kauli mbiu ikiwa Mustakabali salama unaanzia hapa, Umoja wa Mataifa unasisitiza umuhimu wa kufadhili miradi midogo yenye matokeo chanya na ya haraka ili kusaidia sio tu watu wanaopata ulemavu wa viungo kutokana na madhara ya mabomu hayo bali pia kuwezesha watu kurejea kwenye maisha yao ya kawaida Sharon Jebichii anamulika Lebanon na Libya.
    2 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners