Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 27 MACHI 2025
    Karibu kusikiliza jarida la Umoja wa Mataifa ambapo hii leo tunaendelea na kuwasikia wadau waliohudhuria mkutano uliomalizika wiki iliyopita wa Kamisheni ya hali ya wanawake CSW69 unaotathmini Azimio la Beijing na Mpango wa Utekelezaji vilivyopitishwa mwaka 1995 katika mkutano wa 4 wa kimataifa wa wanawake huko Beijing China. Pia utapata fursa ya kusikiliza muhtasari wa habari na kujifunza kiswahili ambapo leo utapata ufafanuzi wa methali "NDOTO NJEMA HAIHADITHIWI"
    12 min
  • Chad: Wanakikundi watumia faida ya biashara yao kuanzisha shule
    Nchini Chad, wanawake wanakikundi cha kutengeneza sabuni na mafuta ya kupata mwilini wameamua kuchukua hatua ili umamuma wa kutokujua kusoma na kuandika ambao umewakumba wao, usiwakumbe pia watoto wao wa kike. Wanakikundi hao wa APROFiCA wanaopata ufadhili kutoka Benki ya Dunia wameona ni vema kuchukua hatua hiyo ili kufanikisha lengo namba 4 la Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs la Umoja wa Mataifa kuhusu elimu, kwani elimu ni mkombozi kwa binadamu. Je wamefanya nini? Assumpta Massoi anafafanua kupitia video ya Benki ya Dunia.
    4 min
  • Baada ya kukimbilia Burundi, wakimbizi wa DRC wakubwa na uhaba wa mahitaji muhimu
    Hali ya kibinadamu ya wakimbizi zaidi ya 100,000 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, waliokimbilia nchini Burundi kusaka usalama kutokana na mapigano mashariki mwa nchi yao katika katika kipindi cha chini ya miezi mitatu, iliyopita ni ya mashaka, wakati huu ambapo ufadhili unazidi kukumbwa na mkwamo, wakikabiliwa na uhaba wa huduma kama chakula, huku kukiwa na pengo la ufadhili. Je ni madhila yapi?  Sharon Jebichii anafafanua zaidi kupitia video iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR.
    3 min
  • 25 MACHI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo tunasalia hapa makao makuu katika mkutano wa CSW69 uliokunja chamvi Ijumaa wiki jana, tunamsikia aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa 4 wa Umoja wa Mataifa wa Wanawake, Mkutano wa Beijing Bi. Gertrude Mongella.Hapa New York, Umoja wa Mataifa leo umetoa wito wa kuachiliwa kwa wafanyakazi wake wanaoshikiliwa kote ulimwenguni ambao wamejikuta matatani wakati wakiwahudumia watu walio katika hatari, huku wakihatarisha usalama wao binafsi kwa kukabiliwa na vitisho vya kutekwa nyara, vurugu, unyanyasaji, na kifungo katika maeneo yenye migogoro na majanga.Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kuhusu vifo vya watoto imeonya kwamba miongo ya maendeleo katika kupunguza vifo vya watoto na watoto wachanga wakati wa kuzaliwa yako hatarini kutokana na kupunguzwa kwa ufadhili. Idadi ya vifo vya watoto wa chini ya umri wa miaka mitano ilipungua hadi watoto milioni 4.8 mwaka 2023, huku vifo vya wakati wa kuzaliwa vikiendelea kubaki takriban milioni 1.9.Leo ni Siku ya Kimataifa ya Kumbukumbu ya Waathirika wa Utumwa na Biashara ya Watumwa ya Bahari ya Atlantiki, ikiwakumbuka mamilioni ya Waafrika walioteswa, kunyanyaswa, na kunyimwa utu wao. Katika ujumbe wake wa siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema “Kwa zaidi ya karne nne, mamilioni ya Waafrika walitekwa kwa nguvu, kusafirishwa kwa meli hadi mataifa ya kigeni, na kufanyishwa kazi katika hali mbaya za kikatili.”Na katika mashinani kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP, Lea mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye sasa amekimbilia Burundi na familia anasilimua hali ilivyokuwa wakati wa kukimbia.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!  
    12 min
  • Wanawake wamefanya mengi lakini hayajarekodiwa - Dkt. Reuben CSW69
    Rekodi ni chache sana ya vitu ambavyo wanawake wamefanya hapa duniani, anasema Dkt. Rose Reuben, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania anapozungumza na Anold Kayanda wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa wakati wa Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake, CSW69, jijini New York, Marekani.Mkutano huu muhimu kuhusu wanawake umefanyika kuanzia tarehe 10 hadi 21Machi 2025 na kuhudhuriwa na maelfu ya wanawake kutoka kote duniani naye Dkt. Rose Reuben akiwa mmoja wao.Kiongozi huyu wa waandishi wa habari nchini Tanzania anaona kwamba kuna hatua nyingi zimepigwa  katika kipindi cha miaka 30 tangu kuwekwa kwa Azimio la Beijing ili kumkomboa mwanamke lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya.“Na hii kazi sipendi kujilaumu sana kwamba je, hakuna kitu ambacho kimefanyika?! Mambo yamefanyika mengi lakini masuala ya kijamii hayamaliziki kwa usiku mmoja kwasababu kila unapoamka jamii inabadilika kwa namna nyingine. Kwa hiyo tukitazama kwa mtazamo huo tunaona kwamba kuna kazi imefanyika.” Anasema Mkrugenzi huyo Mtendaji wa TAMWA.Kwake, mwandishi wa habari nguli, anaona moja ya maeneo ambayo ni muhimu yafanyiwe kazi ni kuzipa nafasi taarifa zinazohusu shughuli kubwa zinazofanywa na wanawake katika jamii kote duniani kwani licha ya wanawake kuwa na michango mikubwa katika mustakabali wa ulimwengu, taarifa zao hazipewi kipaumbele cha kutosha.“Mimi kwa mtazamo wangu naona wanawake wamefanya kazi nyingi lakini hazijarekodiwa. Rekodi ni chache sana.” Anasisitiza na kuongeza, “kwa hiyo tunatakiwa kuanza kurekodi vile vitu ambavyo vilifanywa na wanawake wale wa miaka 30 iliyopita lakini hata na hawa wanaokuja kizazi kipya.”Dkt. Rose Reuben anahamasisha pia vyombo vya habari kuangazia masuala mengine ambayo kwa namna moja amba nyingine yanaigusa jamii moja kwa moja na hiyo ni kusema yanamgusa mwanamke moja kwa moja kama vile mabadiliko ya tabianchi, tekonolojia, “na vitu vingine ambavyo vinaweza kuathiri usawa wa kijinsia na hali ya mwanamke duniani.”Aidha kiongozi huyo wa TAMWA anatoa wito kwa wanawake popote walipo kutumia nyenzo zinazopatikana katika jamii yao kuhakikisha wanapata taarifa, wanasambaza taarifa na kujipatia maarifa.
    4 min
  • 24 MACHI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia hatari za usitishwaji wa misaada kutoka marekani kwa waathirika wa viruzi vya Ukimwi, na ujumbe wa washiriki wa Mkutano wa CSW69 uliokunja chamvi Ijumaa wiki jana. Mashinani tunakupeleka nchini Tanzania, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS leo limeonya kwamba kusitishwa kwa ufadhili wa Marekani sio tu janga kwa vita dhidi ya gonjwa hilo bali ni chachu ya vifo na ongezeko la maambukizi mapya. Flora Nducha amefuatilia onyo hilo lililotolewa leo mjini Geneva Uswisi na Mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS Winnie Byanyima alipozungumza na waandishi wa habari.Wakati Mkutano wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani ulioleta pamoja wawakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya Umoja wa Mataifa  pamoja na mashirka yasiyo ya kiserikali(NGOs) ulikunja jamvi      ijumaa tarehe 21 Machi wiki jana tulipata kuzungumza na wawakilishi wa Shirika lisilo la kiserikali la Forum for Women Democracy Development and Justice, FODAJ ambalo linasaidia wasichana na wanawake waathirika wa ukatili wa kijinsia katika kaunti ya Kajiado nchini Kenya.Makala Anold Kayanda wa Idhaa hii baada ya kukamilika kwa Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake CSW69 uliofikia tamati mwishoni mwa wiki amezungumza na Dkt. Rose Reuben, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanawake wa Vyombo vya Habari Tanzania (TAMWA) kuhusu tathimini yake ya hatua zilizopigwa katika miaka 30 tangu kuwekwa kwa Azimio la Beijing ili kumkomboa mwanamke.Na katika mashinani fursa ni yake Imani Ramadhani kutoka wilaya ya Kilolo, Iringa nchini Tanzania akieleza jinsi ambavyo maisha ya familia yake ilivyobadilika kupitia mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watotot UNICEF, uliofadhiliwa kwa ushirikiano na wadau wake unaolenga kuleta usafi enedelevu wa mazingira, ikiwa ni pamoja na vyoo safi na salama ili kupunguza hatari za kila mara za magonjwa yanayosababishwa na maji machafu.  Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 
    13 min
  • FODAJ CSW69: Vita dhidi ya dhulma kwa wanawake na wasichana
    Wakati Mkutano wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani ulioleta pamoja wawakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya Umoja wa Mataifa  pamoja na mashirka yasiyo ya kiserikali(NGOs) ulikunja jamvi  ijumaa tarehe 21 Machi wiki jana tulipata kuzungumza na wawakilishi wa Shirika lisilo la kiserikali la Forum for Women Democracy Development and Justice, FODAJ ambalo linasaidia wasichana na wanawake waathirika wa ukatili wa kijinsia katika kaunti ya Kajiado nchini Kenya. Sharon Jeichii anaeleza waliochokizungumzia.
    3 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners