Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 23 AGOSTI 2024
    Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Leah Mushi akimulika ripoti ya kuthibitishwa kwa mgonjwa wa polio huko Gaza; Tukio la uzinduzi wa mpango wa utoaji taarifa mapema kuhusu majanga; Makala ikimulika kazi za Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC na mashinani ikienda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa mhudumu wa afya anayefanikisha kazi za uteguaji wa mabomu yaliyotegwa ardhini.Vuta nikuvute ikiendelea Gaza kuhusu ufikishaji, usambazaji na utoaji wa chanjo dhidi ya polio wakati huu ambapo makombora yanaendelea kurindima kutoka jeshi la Israeli, hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO, limethibitisha kubainika kwa mgonjwa mmoja wa polio, ikiwa ni miaka 25 tangu ugonjwa huo utokomezwe eneo hilo. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi, amezindua mpango wa kitaifa wa kuhakikisha kila mtu anapata Maonyo ya Mapema kuhusu hali ya hewa, EW4All ifikapo mwishoni mwa mwaka 2027 huku akitangaza uwekezaji mpya muhimu ili kuboresha uchunguzi wa kimsingi wa hali ya hewa, uzinduzi uliofanyika katika mji mkuu wa Msumbiji, Maputo.Makala inasalia makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ikiwa leo ni siku ya mwisho ya maonesho ya picha yaliyoandaliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Anold Kayanda anatupitisha katika picha hizo zinazoonesha athari mbalimbali kwa wanadamu kutokana na uhalifu unaotekelezwa katika maeneo mbalimbali duniani. Kwako AnoldMashinani: Fursa ni ya Chantal Zingapako, muuguzi anayejitolea kusaidia timu ya  ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani  nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, ya kutegua mabomu ya ardhini.
    11 min
  • Chiriku hana hisani
    Wiki hii katika kujifunza Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka nchini Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Chiriku hana hisani.” 
    2 min
  • 22 AGOSTI 2024
    Karibu kusikiliza jarida ambapo hii leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kuwakumbuka waathiriwa wa vitendo vya ghasia kwa misingi ya dini na imani, msomaji wako wa jarida ni ANOLD KAYANDA na jaridani anakuletea mada kwa kina ambayo inamulika wanawake wa kimasai na biashara ya bidhaa zitokanazo na shubiri nchini Kenya. Pia utapata fursa ya kusikiliza muhtasari wa habari na kujifunza kiswahili hii leo mtaalamu wetu Dkt.Josephat Gitonga atafafanua maana ya methali “Chiriku hana hisani.”
    12 min
  • Madhila ya ugaidi mpaka lini?
    Tarehe 21 ya mwezi Agosti kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka na Kuwaenzi Wathirika wa Ugaidi, Anold Kayanda anatupitisha katika moja ya shoroba za ndani ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ambako zimewekwa picha za baadhi ya manusura na waathirika wa ugaidi zikiwa na maelezo ya kile kinachowafanya kusonga mbele.
    4 min
  • Haiti: UNICEF imeanzisha kituo cha watoto kujifunza na kufurahi
    Idadi ya watoto wanaoshindwa kupata huduma za msingi ikiwemo maeneo rafiki ya kucheza ikizidi kuongeza nchini Haiti kutokana na magenge ya uhalifu kuendesha ghasia, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaendelea kufungua vituo rafiki kwa watoto ili waweze kujifunza na kucheza badala ya kukumbwa na msongo kama anavyosimulia Bosco Cosmas. (Taarifa ya Bosco Cosmas)Nats..Tuko mkoa wa Artibonite, ulioko kaskazini mwa mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince. Video ya UNICEF imeanzia ndani ya nyumba ya banda la bati,  makazi ya Roseline mama mzazi wa Alicha, mtoto mwenye umri wa miaka 7, wanaonekana wakichambua mboga. Roseline anasema,(Sauti ya Roseline – Mama yake Alicha) Asha “Ni mimi ninampatia chakula Alicha, kila kitu anachokitaka, mimi ndiye ninayewajibika. Baba yake alimuacha tangu alipoanza kujifunza kuketi.” Familia nyingi Haiti, ikiwemo ya Alicha zinahaha kukimu mahitaji ya watoto huku zikitakiwa kuwapatia malezi ili wakue. Shule zimefungwa kutokana na ghasia za magenge. Na ndio maana UNICEF ikaanzisha maeneo rafiki kwa watoto. (Sauti ya Roseline – Mama yake Alicha) Asha “Nimefahamu kuhusu klabu hiki cha watoto kutoka kwa kiongozi wa kuchaguliwa wa eneo hili. Alinieleza kuna sehemu rafiki kwa watoto, na Alicha alipoiona na kuona watoto wanacheza alikuja kuniambia mama sitaki kukaa tena kwa bibi, kwa sababu nimeipenda ile klabu ya watoto na ninataka kwenda”. Alicha akiwa kwenye kituo hicho akiwa anacheza na wenzake na mwalimu akiwaelekeza anasema, “ninaipenda hii sehemu kwa sababu wananifundisha vizuri, wananionesha michezo, wananionesha jinsi ya kuruka Kamba. Ninawapenda mwalimu na ninapenda kila kitu katika sehemu hii.” Video inatamatika kwa Roseline kueleza kuwa anapenda kituo hicho kwani kinawasaidia watoto, na yeye kama mzazi anaipenda kwa ajili yao.
    2 min
  • Guterres: Tujifunze kutoka kwa waathirika wa ugaidi
    Wakati dunia hii leo inawakumbuka na kutoa heshima kwa waathirika na manusura wote wa ugaidi duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema huu ni wakati muhimu wa kuwasilikiza waathirika hao na kujifunza kutoka kwao.Katika ujumbe wake wa siku hii alioutoa kwa njia ya video Guterres amesema vitendo vya ugaidi vinaleta huzuni isiyoelezeka, na familia na jamii zinazokumbwa na vitendo hivyo husambaratishwa milele huku makovu yanayoonekana na yasiyo onekana hayawezi kupona kikamilifu.Cue Guterres – Evarist“Tunatoa heshima zetu kwa waathirika na manusura wote, ikiwemo wale waliochagua kutushirikisha simulizi zao kuhusu uvumilivu na msamaha huku tukitafakari juu ya kiwewe walichopitia ili kuelimisha wengine kuhusu vitendo vyao vya ujasiri mkubwa. Siku hii inatuhimiza sote tusikilize na kujifunza na ukumbusho kuwa lazima wote tutafute nuru ya matumaini. Kwa pamoja, tunaweza kupaza sauti za waathiriwa na manusura wote. Kwa pamoja, tunaweza kusaidia kuelimisha vizazi vya sasa na vijavyo na kwa pamoja, tunaweza kujenga jamii zenye amani na uthabiti zaidi kwa wote.”Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya kuwakumbuka waathirika wa ugaidi mwaka huu inasema “Sauti za amani: Wahanga wa ugaidi kama watetezi wa amani na waelimishaji.”Katibu Mkuu Guterres pia amesifu subira za waathirika wa ugaidi kwa kueleza licha ya kupitia mateso na maafa lakini dunia imeshuhudia mifano yao ya ustahimilivu na nguvu ya ubinadamu wetu wa pamoja.
    2 min
  • 21 AGOSTI 2024
    Hii leo ikiwa ni siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka na Kuwaenzi Wathirika wa Ugaidi msomaji wako Leah Mushi anakuletea ujumbe uliotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuhusu haja ya kuwasikiliza na kujifunza kutoka kwa waaathirika wa ugaidi, pia utapata simulizi ya maonesho ya picha za wahanga wa ugaidi zilizowekwa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani na utasikia wito wa mmoja wa watu waliowahi kutekwa na magaidi kwa miaka 8 na kisha kuokolewa. Mbali na masuala ya ugaidi utasikia jinsi watoto walioko Haiti wanavyosaidiwa kutopata msongo wa mawazo kutokana na changamoto za usalama wanazo kabiliana nazo. 
    10 min
  • 20 AGOSTI 2024
    Karibu kusikiliza jarida linalo letwa kwako na Anold Kayanda ambapo hii leo anakuletea mada kwa kina ambayo inamulika wahudumu wa kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hususan kile kinachosababisha waendelee kutekeleza jukumu hilo licha ya changamoto za kiusalama wanazopitia. Pia utasikia muhtasari wa habari ukiletwa kwako na Leah Mushi ambapo ameangazia suala la nishati ya mafuta huko Gaza, ugonjwa wa Mpox huko barani ulaya, na maadhimisho ya siku ya mbu duniani yanayolenga kuelimisha jamii jinsi ya kupambana na mdudu huyo hatari. 
    10 min
  • IOM kupitia mradi wa COMPASS warejesha ndoto ya maisha bora kwa Burte nchini Ethiopia
    Changamoto za maisha ikiwemo sintofahamu ya nini utakula husababisha binadamu kufikiria kuhamia maeneo mengine ili pengine aweze kujipatia riziki. Ingawa hivyo si kila ahamie eneo lingine anapata kile alichotarajia. Hii imemkuta msichana Burte Kase wa nchini Ethiopia ambaye matarajio ya kuboresha maisha yake kwa kukimbilia Saudi Arabia. Machungu yaliremjesha nyumbani na ndoto zake zikatimizwa nyumbani Ethiopia kwa kupitia mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM. Je ni nini walifanya? Evarist Mapesa anakujulisha kupitia makala hii.
    4 min
  • Watoto Sudan wako taabani, vita ikome - UNICEF
    Mgogoro unaoendelea Sudan unazidisha hali mbaya ya maisha na mustakabali wa haki za kibinadamu hasa kwa watoto ambao wanakumbana na mateso makubwa ikiwemo njaa, ukatili na vitisho. UNICEF kupitia msemaji wake James Elder imetembelea katika moja ya kambi za kuhifadhi wakimbizi na kushuhudia kinachoendelea kama anavyosimulia Bosco Cosmas.Amesema "matukio kote Sudan yanashangaza, ninamaanisha miezi 16 ya watoto wanaoshambuliwa. Sijui kama unaweza kusikia sasa nyuma yangu, milio ya risasi. Hakika, watoto ni wengi hapa. Hivi ndivyo tunavyoshuhudia kila siku, watoto wakishambuliwa. Hawa ni mamilioni ya watoto wanaolazimika kukimbia makwao. Tunaiona hali hii kila mahali."Nini sasa kifanyike, ili kuweka hali ya watoto nchini Sudan katika usalama? Elder anasema "endapo pande zinazopigana na jumuiya ya kimataifa wangezingatia watoto wa Sudan, naweza kukuambia kile ambacho tusingekuwa tunakiona hivi sasa. Tusingekuwa baa la njaa. Tusingeona mamilioni ya watu ambao wamelazimika kukimbia nyumba zao, kazi zao, kuungana na familia zao,kila kitu kwa sababu ya mapigano haya makubwa yanayoendelea. Hatungekuwa tunashuhudia vikifo, majeraha, kiwewe, na unyanyasaji wa kijinsia.”Amesisistiza kuwa "kama sheria za kimataifa za kibinadamu na haki za binadamu zitazingatiwa, watoto wa Sudan watanufaika zaidi na kupata haki zao za msingi ikiwemo elimu na maisha bora."
    2 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners