Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • DRC: WFP waomba msaada wa $Mil 425 kusaidia wakimbizi wa ndani
    Wakati Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemorkasia Kongo DRC ikiripoti kuwa na zaidi ya wakimbizi wa ndani 738,000 kwa kipindi cha mwaka huu wa 2024 pekee kutokana na kuongezeka kwa machafuko, Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limeeleza kuwa na uhitaji wa haraka wa dola milioni 425 ili waweze kuwasaidia wakimbizi hao wanaoongezeka kila uchao. Mratibu wa masuala ya dharura wa WFP huko mashariki mwa DRC Bi. Cynthia Jones amesema  hapo awali walipata bahati ya kuanzisha mpango ambapo walikuwa wanaweza ama kuwapatia wakimbizi wa ndani chakula au kuwapatia fedha taslimu na hiyo iliwaruhusu kutoa aina thabiti zaidi ya usaidizi lakini kwa sasa hali ilivyo watalazimika kufanya maamuzi magumu. “Sasa hivi tulikuwa katika hali ambayo tunajitahidi kufikia watu milioni 1.2 na sasa tuna wakimbizi wengine milioni 1.2 wameongezeka. Na kwa hivyo itamaanisha tunapaswa kufanya maamuzi magumu juu ya jinsi tunavyotanguliza nani atakula na nani asile. Tunajaribu kuchukua rasilimali tulizo nazo na kuzitumia vyema na kuzisambaza, lakini sio jambo la maana kwani kitendo hicho ni kusema tuna sawazisha hali mbaya zaidi ya Kivu Kaskazini ni kwamba tunapaswa kupungua, inaweza kuwa ituri au Kivu Kusini. Hayo pia ni maamuzi magumu kwa sababu kuna watu wengi ambao hawana uhakika wa chakula katika maeneo hayo pia.”Bi.Jones amesema pamoja na kuwa na fahari na kazi kubwa waliyoifanya ya kusaidia wakimbizi wengi hapo awali, mtiririko mkubwa wa wakimbizi wanaowasili kusaka hifadhi katika makambi katika miezi ya hivi karibuni umefanya kazi yao kuwa ngumu zaidi.
    2 min
  • 22 APRILI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya hali ya joto dunianina madhara yake kwa afya na wafanyakazi, Naomi la ufadhili kwa ajili ya wakimbizi wa ndani DR Congo. Makala tunakupeleka nchini Sudan na mashinani nchini Sudan Kusini, kulikoni? Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa duniani ILO, inasema zaidi ya asilimia 70 ya wafanyakazi wote duniani wanakabiliwa na uwezekano wa hatari za kiafya kutokana na mabadiliko ya tabianchi.Wakati Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemorkasia Kongo DRC ikiripoti kuwa na zaidi ya wakimbizi wa ndani 738,000 kwa kipindi cha mwaka huu wa 2024 pekee kutokana na kuongezeka kwa machafuko, Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limeeleza kuwa na uhitaji wa haraka wa dola milioni 425 ili waweze kuwasaidia wakimbizi hao wanaoongezeka kila uchao.  Katika mahojiano na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, afisa mwandamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) anayehusika na masuala ya dharura na mnepo, Rein Paulsen ametahadharisha kuwa hatari ya kutokea baa la njaa nchini Sudan ni halisi na kwa hivyo wakati wa kuchukua hatua ni sasa.Na mashinani tutapeleka Tambunra nchini Sudan Kusini kumsikia mkimbizi wa ndani akisihi kurejea kwa amani illi aweze kurudia nyumbani.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    12 min
  • ILO: Joto la kupindukia linaathiri asilimia 70 yawafanyakazi kote duniani

    Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa duniani ILO, inasema zaidi ya asilimia 70 ya wafanyakazi wote duniani wanakabiliwa na uwezekano wa hatari za kiafya kutokana na mabadiliko ya tabianchi. 

    Asante Anold, akizungumza na waandishi wa habari hii leo mjini Geneva Uswis wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo Manal Azzi, afisa wa masuala ya usalama kazini na afya wa shirika la ILO amesema takwimu hizi za kustaajabisha zinasisitiza haja kubwa ya kurekebisha hatua zilizopo za usalama na afya kazini ili kushughulikia ipasavyo vitisho vinayojitokeza kutokana na hatari zinazohusiana na changamoto za hali ya hewa.

    Ameongeza kuwa “Zaidi ya asilimia 70 ya wafanyakazi wetu wanakabiliwa na joto jingi, angalau joto la kupindukia, katika wakati mmoja wa maisha yao ya kazi. Hiyo ni jumla ya wafanyakazi bilioni 2.4 duniani kote, kati ya wafanyakazi wa kimataifa wa bilioni 3.4.”

    Ripoti hiyo iliyopewa jina “Kuhakikisha usalama na afya kazini katika mazingira yanayobadilika” inaeleza kwamba mabadiliko ya tabianchi tayari yameleta athari kubwa kwa usalama na afya ya wafanyakazi katika kanda zote duniani.

    Kwa mujibu wa ILO waafanyakazi, hasa wale walio katika maeneo yenye umaskini zaidi duniani, wanakabiliwa na uwezekano mkubwa wa kukabiliwa na hatari za mabadiliko ya tabianchi kama vile joto kali, ukame wa muda mrefu, moto mkubwa wa nyika, na vimbunga vikali.

    Bi. Azzi amesema "Wafanyakazi zaidi ya milioni 22 wanaugua magonjwa na majeraha yanayohusiana na joto kali na haya yanaweza kutoka na sababu mbalimbali ikiwemo ajali katika usafiri, katika ajali za barabarani kutokana na usingizi kwa kutolala vizuri usiku kwa sababu kulikuwa na joto kupita kiasi, hadi ajali za ujenzi, majeraha, kuteleza na kuanguka. kunkohusiana na ongezeko la joto  kali."

    Ripoti hiyo inabainisha kuwa baadhi ya athari za kiafya kwa wafanyakazi zilizohusishwa na mabadiliko ya tabianchi, ni pamoja na saratani, ugonjwa wa moyo na mishipa, magonjwa ya kupumua, figo kuharibika na hali ya afya ya akili. 

    Pia kuongezeka kwa joto na unyevu wa hali ya juu, dawa nyingi za wadudu hutumiwa katika sekta ya kilimo na kufanya wafanyikazi milioni 870 katika kilimo kuwa na uwezekano wa kuathiriwa na viuatilifu, huku kukiwa na zaidi ya vifo 300,000 vinavyohusishwa na sumu ya dawa hizo kila mwaka.

    Bi Azzi amesisitiza kuwa mambo haya yote yanaingiliana na kwamba zana zinazofaa zinapaswa kuwepo ili kupima athari na kuwa na uwezo wa kufanyia kazi mapendekezo.

    Mkutano mkuu umepangwa kufanyika 2025 na ILO kwa kushirikisha wawakilishi wa serikali, waajiri na wafanyakazi ili kutoa mwongozo wa sera kuhusu hatari za mabadiliko ya tabianchi katika masuala ya kazi.

    3 min
  • Lugha ya kichina imepanua fursa za ajira kwa wanafunzi wa SAUT

    Lugha ni miongoni mwa njia za kimsingi za kujenga utangamano duniani. Umoja wa Mataifa unatambua kuwa lugha ni chombo cha kusongesha tamaduni na miongoni mwa lugha zilizotengewa siku mahsusi kusherehekewa ni kichina ambacho shamrashamra zake ni tarehe20 mwezi Aprili ya kila mwaka.Lugha hii imesambaa duniani ikiwemo Tanzania ambako hii leo Sabrina Moshi wa redio washirika SAUT FM ya mkoani Mwanza kaskazini magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki amefuatilia mafunzo yake kwenye Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino.

    6 min
  • 19 APRILI 2024

    Ushirikiano wa kimataifa utasaidia kufanikisha kuhamia katika nishati jadidifu - Francesco La Camera.

    Vijana wa Afrika lazima tuchangamkie fursa na kujifunza: Joram Nkumbi na Vivian Joseph.

    Lugha ya kichina imepanua fursa za ajira kwa wanafunzi wa SAUT – Tanzania.

    Mashinani ni nchini Kenya kusikia jinsi ambavyo mafunzo ya ukulima endelevu na mikopo ya fedha katika mzunguko wa kijamii (Merry-go) inavyowasaidia wakulima kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

    15 min
  • 18 APRILI 2024

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina amabyo hivi karibuni tulizungumza na Peter Mmbando kutoka Tanzania akifafanua nini wanafanya ili kuimarisha matumizi endelevu ya teknolojia ya kidijitali. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi na tofauti ya maneno “Adhiri; na  hadhiri."

    1. Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameelezea hofu yao juu mwenendo wa mashambulizi dhidi ya shule, vyuo vikuu, waalimu na wanafunzi kwenye Ukanda wa Gaza hali ambayo wamesema ni ishara ya mpango wa uharibifu mkubwa wa mfumo wa elimu wa Palestina.
    2. Muungano wa chanjo duniani GAVI na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wamekaribisha taarifa kwamba chanjo mpya ya matone ya kipindupindu Euvichol-S, sasa imepokelewa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na inaweza kupatikana katika nchi mbalimbali duniani. Kupitishwa kwa chanjo hiyo mpya kutasaidia kuongeza usambazaji wake kwa takriban dozi milioni 50 mwaka huu ikilinganishwa na dozi milioni 38 zilizosambazwa mwaka 2023.  
    3. Mkutano wa Wiki ya Uendelevu ya Umoja wa Mataifa unaendelea hapa Makao Makuu New York Marekani, leo ukijikita na mada ya miundombinu endelevu na inayoaminika ambayo Umoja wa Mataifa unasema itazisaidia nchi kuelekea kwenye maendeleo yenye miumbombinu bora, isiyo ya hatari na itakayoongeza kasi ya kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs.
    4. Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adhiri; na      hadhiri.”.

    Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

    12 min
  • Vijana wakiwezeshwa wanaweza kuvumbua teknolojia ya kusongesha malengo ya maendeleo endelevu

    Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kunafanyika jukwaa la vijana la Baraza la kiuchumi na kijamii ECCOSOC ambalo linatoa ukumbi wa kimataifa wa mazungumzo kati ya nchi wanachama na viongozi vijana kutoka kote ulimwenguni kujadili suluhu za changamoto zinazoathiri ustawi wa vijana. Hafla hii pia hutumika kama nafasi ya kipekee kwa vijana kushiriki maono na hatua zao ili kuharakisha utekelezaji wa Ajenda ya 2030 na SDGs ikiwemo masuala ya uvumbuzi na teknolojia. Miongoni mwa wanaohuduria jukwaa hilo kutoka Tanzania ni Vivian Joseph Afisa tabibu na mkuu wa wa kitengo cha afya akiwasilisha vijana katika jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC na Joramu Nkumbi mkurugenzi mtendaji wa jukwaa la Afrika la viongozi vijana kwa upande wa Tanzania. Wameketi na Flora Nducha na kumweleza walichoambulia hadi sasa katika jukwaa hilo litakalokunja jamvi kesho..

    9 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners