
Sign up to save your podcasts
Or


Hii leo jaridani tunaangazia kumbukizi wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, na wakimbizi wa Sudan wanaovuka mpaka kuelekea nchini Sudan Kusini. Makala na mashinani tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulikoni?
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Tarehe 15 April wiki ijayo siku ya jumatatu nchi ya Sudan itatimiza mwaka mmoja rasmi tangu kuanza kwa mzozo kati ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na Vikosi vya jeshi la Sudan (SAF). Vita hiyo imesababisha maelfu ya watu kuwa wakimbizi wa ndani na wengine kusaka hifadhi nchi Jirani. Mashirika ya misaada ya kibinadamu nayo yamekuwa mstari wa mbele kusaidia wananchi wenye uhitaji japo yanakabiliwa na ufinyu wa bajeti.
Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP inaanza kwa kuonesha wananchi wakiwa na vifurushi mikononi, wengine wakiwa wamepanda usafiri unaosukumwa na ngombe na wengine mabasi wakiingia katika mpaka wa Joda nchini Sudan kusini wakitokea nchini Sudan.
“Tumesafiri kwakutumia basi na imetuchukua siku mbili kufika hapa”, ndivyo anavyosema Hamida Ibrahim mkimbizi kutoka Sudan. Anaendelea kwa kueleza kile wanachohitaji kwa sasa.
“Tunahitaji chakula. Huo ndio msaada wa haraka tunaohitaji ili tuweze kuishi. Kwa sababu tupo na watoto na hawana uwoga wanachojua wanakuja hapa kufata usalama”
Kiongozi wa WFP katika eneo hili Leonidace Rugemalila anasema mzozo huu wa Sudan umemuathiri kila mtu.
“Katika kipindi cha miezi mitatu idadi ya watu wanaovuka mpaka huu kila siku imeongezeka kutoka watu 1,500 mpaka takriban watu 2,500.”
Naye Mkuu wa lishe Aachal Chand anasema wengi wa waaathirika wa mzozo nchini Sudan ni wanawake na watoto, na walioathirika zaidi ni wajawazito, wanawake wanaonyonyesha na watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
“Wanapovuka mpaka, mtu yeyote mwenye umri zaidi ya miaka mitano anapatiwa biskuti za lishe kama chakula cha haraka chakumpa lishe. Kwa watoto chini ya miaka mitano tunawapa chakula maalum cha lishe. Kuanzia saa mbili asubuhi mpaka wakati huu saa 10 jioni wameshatoa lishe kwa takriban watoto 400 ambao wamepokea matibabu ya utapiamlo au huduma za matibabu.”
Chand ameeleza kuwa WFP na wadau wake wanaendelea kutoa msaada hata hivyo wanakabiliwa na ufinyu wa bajeti.
“Watu wanahitaji msaada wa afya na lishe, watu wanahitaji usaidizi katika kupata uhakika wa chakula, watu wanahitaji msaada wa kuweza kuwasaidia kufika katika maeneo wanayotaka kuelekea.Sudan na athari zake kwa nchini ya Sudan Kusini zinasahaulika na tunatakiwa kuhakikisha hatusahau mzozo huu kwasababu hawa ni watu na wanapata athari halisi katika maisha yao.”
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Alice Nderitu, Mshauri Maalum wa Umoja wa Mataifa katika kuzuia mauaji ya kimbari akiwa Kigali hivi majuzi kwenye kumbukizi anamulika nini kifanyike kuhakikisha kitendo kama hicho kinasalia historia. Pia tunakuletea muhtasari wa habari za Gaza, Sudan, Uganda na uchambuzi wa neno “PAMBAJIO”.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania , BAKITA anafafanua maana ya neno “PAMBAJIO”.
Miaka 30 iliyopita mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda yaliyoishangaza, dunia yalitokea kuanzia Aprili 7 mwaka 1994 na kudumu kwa siku 100 zilioghubikwa na ukatili wa hali ya juu na mamilioni ya watu kufurushwa makwao. Tangu wakati huo Umoja wa Mataifa umekuwa mstari wa mbele kuchukua hatua kuhakikisha asilani jinamizi hilo halitokei tena popote pale duniani. Manusura wa mauaji hayo wanasemaje kuhusu kumbukumbu hii? Na je dunia imejifunza nini kutokana na mauaji hayo ya Rwanda taifa ambalo limeshafungua ukurasa mpya na kuyapa kisogo? Twende mjini Kigali ambako kumbukumbu kubwa imefanyika mwishoni mwa wiki na itaendelea kwa siku 100, shuhuda wetu ni Eugene Uwimana afisa mawasiliano wa ofisi ya mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Rwanda.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka mjini Kigali ambako kumbukumbu ya mauaji ya kimbari imefanyika mwishoni mwa wiki na itaendelea kwa siku 100. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani tunakupeleka nchini Sudan Kusini.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Mwanamke akiwezeshwa anaweza, huo ndio umekuwa usemi wa Umoja wa Mataifa ukipigia chepuo wanawake kujumishwa katika kila Nyanja ya Maisha ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuchangia katika maendeleo ya jamii. Usemi huo unaungwa mkono na mwanamke mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambaye sasa anaishi Kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya.
Kutana na Mariam Suleiman ambaye kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR anasema vita ilimfungisha virago Congo DRC hadi hapa kambini Kakuma, ingawa ilimvurugia amani yake haikumkatishia ndoto zake za kuendelea na ufundi wa kuchomelea vyuma na pia kuwa mkufunzi wa kazi hiyo.
“Katika kuchomelea vyuma ninafurahia sana kufanyakazi kazi hiyo ninapokwenda kazini na kujikuta ni mwanamke peke yangu uwanjani na hivyo ninajivunia sana kwa sababu sio kazi rahisi kwenda hapo ukiwa mwanamke peke yako katikati ya wanaume 15. Hivyo ninajivunia sana kuwa mchomelea vyuma na mkufunzi wa kuchomelea na kutengeneza vyuma”
Kwa Mariam matunda ya kazi yake yako dhahiri.
“Moja ya kazi zangu zinazovutia ambazo nimefanya ni lango kuu la kliniki 4”
Pamoja na mafanikio hayo Marian anatamani kusoma zaidi kuongeza ujuzi.
“Nilisoma hadi daraja la sita hiyo ni ngazi ya Diploma. Natamani kuchimba ndani zaidi ya hii tasnia ya kuchomelea vyuma lakini hapa Kenya hatuna hiyo kozi. Ipo katika taasisi ya uchomeleaji vyuma ya Afrika Kusini. Ningependa kwenda huko na kusoma uchomeleaji vyuma chini ya maji.”
Na kwa kuwa yeye ameweza anaamini hakuna kinachomshinda mwanamke kwani
“Wanawake tuna uwezo, wanawake tuna ujuzi, wanawake tunaweza kufanyakazi zinazofanywa na wanaume, wanawake tunaweza kufurahia kazi zetu, wanawake hebu tusimame kidete tunaweza”
Kadri siku za MONUSCO kuondoka nchini DRC zinavyokaribia, vivyo hivyo wananchi wanufaika wa miradi iliyofanikishwa na ujumbe huo wanazidi kujitokeza kuelezea hisia zao, kwani ujumbe huo unatakiwa uwe umeondoka nchini humo mwishoni mwa mwaka huu wa 2024.
Miongoni mwa wanufaika ni shule ya msingi Lubumba hapa Kamanyola na Mwalimu Mkuu Texas Chekabiri anaelezea hali ilivyokuwa. Assumpta Massoi amefuatilia na kutuelezea zaidi katika makala hii.
Hii leo jaridani tunaangazia ombi la Palestina kujiunga rasmi kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa, na uwezeshaji wa wanake ambapo tunatembelea mkimbizi katika kambi ya Kakuma nchini Kenya. Makalatunakupeleka nchini DRC na mashinani nchini Tanzania.
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Huko Gaza, watoa misaada ya kibinadamu wakiwa na wasiwasi mkubwa juu ya mipango ya Israel kuvamia eneo la Rafah hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa Palestina imeanza mchakato wa kuwa mwanachama rasmi wa Umoja wa Mataifa kwani hivi sasa ujumbe wake ni uangalizi usioipatia hadhi ya kupiga kura. Mchakato huo unaanzia ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Ratiba ya mikutano hii leo hapa katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa inaonesha kuwa Baraza la Usalama lenye wajumbe 15 kuanzia saa nne kamili asubuhi mpaka saa sita kamili mchana kwa saa za New York Marekani, litakutana kwanza katika kikao cha faragha na kisha kikao kitafunguliwa kwa umma kusikiliza wanapojadili ombi la Palestina kuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa.
Palestina imekuwa ikishiriki katika masuala mbalimbali ndani ya Umoja wa Mataifa lakini kwa ngazi ya muangalizi na sasa uongozi wa Palestina inataka hadhi hiyo kubadilishwa na kuwa mwanachama kama wanachama wengine 193 wa Umoja wa Mataifa.
Wajumbe katika baraza hilo la UN katika mazungumzo yao watazingatia ombi la Wapalestina la mwaka 2011 baada ya ombi lililowasilishwa kwa njia ya maandishi wiki iliyopita na Bwana Riyad Mansour, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mamlaka ya Palestina ambaye pia ni Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa.
Wakati tukisubiri kusikia nini kitajadiliwa na Baraza hilo, huko Ukanda wa Gaza hali bado si hali kwani watoa misada ya kibinadamu wana wasiwasi mkubwa juu ya uvamizi unaopangwa kufanywa na Israel katika eneo la Rafah ambalo limefurika wapalestina waliokimbia kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo kusini, kati na kaskazini mwa Gaza kufuatia mapigano yanayoendelea baina ya wanamgambo wa kipalestina wa Hamas na wanajeshi wa Israel.
Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Misaada ya Kibinadamu katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu, Jamie McGoldrick, akizungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa hapo jana alisema kuwa “Mpango unaendelea wa uvamizi wa Rafah, ambao unaweza kusababisha hadi watu 800,000, kuyakimbia makazi yao…. Tulipata tabu sana kuleta mahitaji muhimu hapa kama vitu ambavyo si vyakula, malazi, nyenzo mbalimbali na maji…. Hatuna tena uwezo na rasilimali kwa sasa. Na tunatatizika sana kujiandaa.”
Ili kuongeza kiwango cha usaidizi wa kibinadamu kufika eneo hilo, Umoja wa Mataifa unaunga mkono wito wa bandari ya Ashdod ya Israel kufunguliwa tena hulo kaskazini mwa Gaza, ili misaada zaidi ipatikane kupitia nchi ya Jordan.
From the publisher's feed

14 Listeners

43 Listeners

5 Listeners

95 Listeners

25 Listeners

9 Listeners

18 Listeners

4 Listeners

6 Listeners

15 Listeners

8 Listeners

9 Listeners

4 Listeners

4 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners