Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • UN - Bila usitishaji mapigano hali ya kibinadamu inaendelea kuwa tete Gaza

    Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo kwa mara nyingine yameonya kwamba bila dalili zozote za usitishaji mapigano Gaza hali ya kibinadamu inaendelea kuwa janga huku mashambulizi ya Israel yakiendelea kukatili maisha, kufurusha watu na kusababisha uharibifu usioelezeka na njaa nayo ikiongeza hofu ya hatma ya watu wa eneo hilo. 

    Asante Anold kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA usiku wa kuamkia leo makombora ya Israel yameendelea kuvurumishwa kuelekea Gaza Kaskazini, Khan Younis na Rafah ambako takriban Wapalestina milioni 1.2 sasa wanaishi katika makazi rasmi na yasiyo rasmi na hivyo kuwaongezea hofu ya mustakbali wa maisha yao.

    Pia shirika hilo linasema fursa ya kufikisha misaada ya kibinadamu kwa wenye uhitaji mkubwa bado ni mtihani hasa kutokana na mamlaka ya Israel kuendelea kulinyima vibali shirika la UNRWA kufikisha msaada muhimu wa chakula na mahitaji mengine hasa Gaza Kaskazini.

    Hatua hiyo kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA imezidisha njaa kwa watu ambao tayari wako taaban na mapigano yanayoendelea. 

    Tangu Machi mosi OCHA inasema Israel imekataa kuruhusu asilimia 30 ya operesheni za kibinadamu Gaza Kaskazini na kuathiri kwa kiasi kikubwa operesheni za UNRWA.

    Watoto 27 wameripotiwa kufa njaa kutokana na utapiamlo hadi sasa huku shirika la Kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF likionya kwamba Maisha ya maelfu wengine yako hatarini ukizingatia ukweli kwamba tangu Oktoba 7 mwaka jana watoto zaidi ya 13,000 wameuawa kutokana na vita inayoendelea lakini njaa nayo ni tishio kubwa.

    Kuhusu uharibifu wa miundombinu uliosababishwa na vita inayoendelea ripoti ya pamoja ya tathimini ya Umoja wa Mataifa na Benk ya Dunia iliyotolewa leo inasema uharibifu huo unakadiriwa kuwa takriban dola bilioni 18.5 ambao ni sawa na asilimia 97 ya pato la taifa la Ukingo wa Magharibi na Gaza kwa mwaka 2022.

    Na hapa Makao Makuu leo Umoja wa mataifa umepokea barua rasmi kutoka kwa mamlaka ya Palestina ikiomba kuwa mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa badala ya nafasi ya uangalizi iliyonayo sasa. 

    3 min
  • Bado kazi ipo kupigania haki za mwanamke kote duniani - Paulina Ngurumwa

    Kinara wa elimu nchini Tanzania Paulina Ngurumwa anasema bado kazi ipo kupigania haki za mwanamke kwa hiyo harakati hizo hazitakiwi kupoa. Paulina Ngurumwa ni mwanaharakati wa haki za kijamii kupitia shirika la KINNAPA Development Programme. 

    KINNAPA Development Programme ni shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa na wanajamii ya Wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara, kaskazini mwa Tanzania likiwa ni chombo cha kutatua matatizo yao hasa ya ardhi. Shirika hili lilianzishwa mwaka 1992 na kwa miaka hiyo yote linajivunia kuendelea kufanikisha malengo yake na sasa hata limepanua mawanda ya huduma zake kama anavyoeleza mmoja wa viongozi Paulina Nguruma, katika mahojiano aliyoyafanya na Anold Kayanda wa Idhaa hii hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa. 

    6 min
  • 02 APRILI 2024

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika harakati za kuwainua wanawake na wasichana nchini Tanzania Tanzania, ambapo Paulina Ngurumwa kutoka KINNAPA Development Programme, shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa na wanajamii ya Wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara anazungumza na Anold Kayanda wa idhaa hii. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.

    1. Leo maafisa wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamelaani vikali mauaji ya wafanyakazi wa misaada 7 wa shirika lisilo la kiselikali au NGO la World Central Kitchen yaliyofanywa na jeshi la Israel, maafisa hao wakirejea kueleza hofu yao kwamba hakuna mahali palipo salia kuwa salama Gaza.
    2. Tume ya pamoja ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya UNJHRO imesema kumekuwa na ongezeko la asilimia 14 ya visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini DRC. 
    3. Leo ni siku ya kimataifa ya kuelimishana kuhusu usonji maudhui yakiwa kutoka kuishi kuelekea kwenye ustawi, kwa watu wenye usonji au kwa kiingereza Autism, ambapo kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO, usonji hukumba mtoto mmoja kati ya kila watoto 160 duniani.
    4. Na mashinani tunaelekea Gaza kuona ni kwa jinsi gani mashambulizi ya Israel ya hivi majuzi yameathiri huduma za afya katika hospitali ya Al-Shifa.

    Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

    12 min
  • Mradi wa maji warejesha matumaini kwa familia Wajir

    Maji ni uhai, ni kauli mbiu ya miaka nenda rudi, lakini imesalia ndoto kwa wengi duniani hasa wakati huu mabadiliko ya tabianchi yanachochea ukame unaovuruga maisha ya binadamu, wanyama na mimea. Nchini Kenya katika kaunti ya Wajir, iliyoko kaskazini-mashariki mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, uhaba wa maji ulisababisha familia kupoteza mifugo yao, mazao kukauka na ustawi wa jamii kutoweka. Lakini shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, kwa kushirikiana na serikali ya Kaunti walianzisha mradi wa ujenzi wa kuchimba visima wa Giriftu kwa ili jamii iwe na uhakika wa kupata maji wakati wowote. Mradi umezaa matunda na ndio msingi wa makala yetu ya leo inayoletwa na Assumpta Massoi.

    5 min
  • Griffiths: Jaribio la kuitenga UNRWA lazima likome

    Mratibu Mkuu wa Misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths amesema shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA ni uti wa mgongo wa operesheni za Kibinadamu Gaza hivyo jaribio la kulitenga shirika hilo lazima likome. 

    Bwana Griffiths ametoa kauli hiyo leo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X zamani Twitter akisistiza kuwa juhudi zozote za kusambaza misaada ya kibindamu kwenye Ukanda wa Gaza bila kupitia shirika la UNRWA haziwezi kufanikiwa na watu zaidi ya milioni 2 wanaitegemea UNRWA ili kuendelea kuishi. 

    Ameendelea kusema kwamba hadi sasa hakuna shirika lingine lolote lenye uwezo wa kufika kila kona ya Gaza, uzowefu na imani ya jamii ya kutekeleza majukumu yake kama lilivyo shirika la UNRWA.

    Wakati huohuo shirika la UNRWA limeonya kwamba mashambulizi ya Israel yameendelea tena usiku wa kuamkia leo huko Gaza Kaskazini Khan Younis na Rafah ambako watu milioni 1.2 wanapata hifadhi na kusababisha vifo zaidi.

    Huku lile la afya la Umoja wa Mataifa WHO likisema wakati timu yake ikiwa katika operesheni ya kibinadamu katika hospital ya Al-Aqsa jana Jumapili maeneo ya hospital yalipigwa na shambulio la anga lililokatili maiasha ya watu 4 na kujeruhi wengine 17.

    Nalo shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema linajitahidi kwa kila hali kutoa msaada wa chakula unaohitajika sana kwa watu milioni 1.45 Gaza lakini msaada huo hautoshi na bila usitishaji vita hawawezi kumfikia kila mtu na hivyo kufanya Maisha ya watu wengi kusalia hatarini.

    2 min
  • 01 APRILI 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu Gaza, na jitihada za kukabili habari potofu nchini DR Congo. Makala tunaku[eleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?

    1. Mratibu Mkuu wa Misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths amesema shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA ni uti wa mgongo wa operesheni za Kibinadamu Gaza hivyo jaribio la kulitenga shirika hilo lazima likome.
    2. Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kituo kilichojengwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO kimesaidia vijana kukabiliana na habari potofu na za uongo ambazo huchochea ukosefu wa amani kwenye taifa hilo la Maziwa Makuu barani Afrika. 
    3. Katika makala Assumpta Massoi kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Kenya, anakupeleka kaunti ya Wajir kuona jinsi mradi wa maji ulivyoleta matumaini kwa familia na jamii.
    4. Na mashinani tutaelekea nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu afya kwa watoto.

    Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

    12 min
  • Kituo cha amani DR Congo chakabili habari potofu na za uongo

    Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kituo kilichojengwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO kimesaidia vijana kukabiliana na habari potofu na za uongo ambazo huchochea ukosefu wa amani kwenye taifa hilo la Maziwa Makuu barani Afrika. 

    Jean Claude Batumike, ambaye ni Mkuu wa kituo cha vijana cha Amani, kilichoko eneo la Kamanyola huko jimboni Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akizungumza kupitia video ya MONUSCO iliyochapishwa kwenye mtandao wa Instagram anasema kituo hicho kilipojengwa watu walijihisi wako na amani zaidi.

    Anasema kituo cha amani kilijengwa kwa ajili ya amani ili kuondoa migogoro kwa vijana na jamii kwa ujumla. Kituo kina kompyuta, mtandao wa intaneti wakati wote na skrini kubwa ambapo katika video hiyo wanaonekana vijana wakipita hapa na pale huku wakipatiwa maelezo na Bwana Batumike.

    Akilinganisha hali kabla na baada ya kujengwa kwa kituo hicho, Bwana Batumike anasema, “mara nyingi wakati tulikuwa na mizozo hapa kwenye eneo letu, hakukuweko na mahali ambapo watu wanaweza kwenda na kutatua mizozo, lakini tangu wamejenga hiki kituo cha Amani, kushikakuweko na mzozo wa vijana au jamii, wanakimbilia kituo cha Amani, wanakaa pamoja na kutatua mizozo na hatimaye mambo yanakuwa mazuri zaidi.”

    Bwana Batumike akaelezea kuwa kituo cha Amani kinasaidia kukabili habari za uongo na potofu kwa kuwa kituo kina mtandao wa uhakika wa intaneti, kompyuta na skrini na wanaweza kupata habar iza ukweli.

    “Mara nyingi vijana wanapokuwa na habari za wasiwasi ambazo hawana uhakika nazo ni rahisi kufika kituo cha Amani, wanajiunganisha kwenye intaneti, wanarambaza na kusogoa na wengine kwa mtandao na kupata habari za ukweli. Na katika sehemu yenye mzozo, unahitaji kupata habari za uhakika,” anasema Bwana Batumike.

    3 min
  • Kituo cha malezi ya watoto nchini Kenya chatekeleza azma ya Umoja wa Mataifa

    Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68 ulifunga pazia hivi majuzi jijini New York Marekani ukipigia chepuo uwekezaji kwa wanawake na wasichana, na leo tunabisha hodi nchini Kenya wasichana waliokumbwa na ujauzito utotoni na kukatishwa ndoto za kuendelea na masomo au kupata ajira wamepata jawabu la changamoto wanazokumbana nazo pindi wakijifungua watoto wao. Changamoto kama vile mahali pa kumwacha mtoto kwa malezi ili aweze kuendelea na shule au kupata ajira. 

    Umoja wa Mataifa unasema kila mtu ana haki ya elimu hata kama amepata changamoto gani maishani. Na  ndipo ushirikiano kati ya mashirika ya kiraia lile la “Work for life”, pamoja na lile la “A Pack a Month”, linalohusika na utoaji wa misaada mbali mbali ikiwemo taulo za kike kwa wazazi wenye mahitaji na wasichana wanaokwenda shule walizindua kituo cha malezi ya watoto wachanga nyakati za mchana katika eneo la Ngong nchini Kenya. Mradi unaungwa mkono na wadau kadhaa ikiwemo serikali  ya Kenya. Selina Jerobon ni msimulizi wetu kupitia mada hii iliyofanikishwa na Redio washirika DOMUS ya huko Kenya. 

    8 min
  • 28 MACHI 2024

    Hii leo jaridani tnakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kufuatilia jitihada za mashirika za kuhahikisha watoto waathrika wa mimba za utotoni wameweza kurejea shule. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za Gaza, Haiti na wakimbizi wakimbizi wa Sudan Kusini. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunapata maana ya neno “UDENDA.” 

    1. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina (UNRWA) leo Machi 28 limetahadharisha kuhusu ujio wa baa la njaa katika Ukanda wa Gaza. UNRWA imesema yenyewe ni uti wa mgongo wa misaada ya kibinadamu Gaza lakini bado misafara yao ya chakula imezuiwa kufika kaskazini, ambako baa la njaa linajongea. Wakati huo huo Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) limesema kati ya hospitali 36 katika Ukanda wa Gaza, ni 10 tu ambazo zimesalia zikifanya kazi japo nazo kwa kiasi kidogo.
    2. Ripoti ya Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa leo inataka hatua za haraka na za ujasiri ili kukabiliana na hali ya "janga" nchini Haiti. Ripoti imeeleza kuwa magenge yanaendelea kutumia unyanyasaji wa kingono kuwatendea unyama, kuwaadhibu na kuwadhibiti watu. Wanawake wamebakwa hata baada ya kushuhudia waume zao wakiuawa mbele yao. 
    3. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), pamoja na wadau wake 123, Alhamis ya leo limetangaza kuwa linatafuta dola bilioni 1.4 mwaka huu ili kukidhi mahitaji ya wakimbizi milioni 2.3 wa Sudan Kusini wanaoishi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Ethiopia, Kenya, Sudan na Uganda. Janga la wakimbizi wa Sudan Kusini linasalia kuwa ndilo kubwa zaidi barani Afrika.
    4. Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “UDENDA”.

    Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

    12 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

17 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners