
Sign up to save your podcasts
Or


Hii leo jaridani tunaangazia mizozo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, na mabomu ya kutegwa ardhini nchini Ukraine. Makala tukupeleka katika ukanda wa Gaza na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Umoja wa Mataifa umesema Ukraine sasa ni moja ya nchi zilizoathiriwa zaidi na mabomu ya kutegwa ardhini duniani huku ikadiriwa kwamba karibu thuluthi moja ya nchi hiyo imeghubikwa na vita eneo ambalo ukubwa wake ni mara nne na nusu ya nchi ya Uswisi. Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanya kazi na serikali ya Ukraine kwa miaka 30 na umekuwa ukiongoza mpango wa utekelezaji wa uteguaji wa mabomu ya kutegwa ardhini tangu 2016.
Paul Heslop Mshauri Mkuu wa Kiufundi wa utekelezaji wa program ya hatua ya uteguaji mabomu ya kutegwa ardhini ya shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP nchini Ukraine akisema amekuwa akifanya kazi ya uteguzi wa mabomu ya kutegwa ardhini kwa miaka thelathini katika maeneo hatari yenye vita, kuanzia Msumbiji hadi Afghanistan. Lakini aliyoyashuhudia ilikuwa maandalizi tu mtihani kamili ambao sasa uko Ukraine
“Ni mazingira magumu sana iwe ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiufundi, kwanza kabisa kwa maana ya kieneo, ni nchi kubwa. Kuna mstari wa mbele wa vita ambao sasa ni zaidi ya kilomita elfu moja, kuna uwezekano wa kazi kubwa ya kufanya. theluthi moja ya nchi inashukiwa kuathirika na mabomu ya ardhini. Hiyo ni ukubwa wa kama nchi mbili za Ufaransa.”
Mathalani Paul anasema,
“Endapo makombora 30,000 yanarushwa kwa siku, hayo ni mabomu 3,000 yasiyolipuka kwa siku. Na, wakati mzozo unafikia siku elfu moja basi, hayo ni mabomu milioni 3 na vilipuzi vingine ambayo hviajalipuka.”
Licha a hali kuonekana ni ya kutisha lakini haimkatishi tamaa Paul wala kumfanya ajutie kufanyakazi ya ya Umoja wa Mataifa ya uteguzi mabomu
“Nimebaini kwamba kufanya kazi kya kutegua mabomu kuwa ni kazi bora zaidi ambayo ningeweza kuwa nayo. Nimeona ushujaa ambao siwezi hata kuamini na nimeshuhudia matukio ambayo yananitia hofu kubwa.”
Kwa mujibu wa UNDP ambayo ni mratibu wa hatua za kutegua mabomu ya ardhini Ukraine hadi kufikia Juni mwaka huu mabomu na vilipuzi 540,000 ambavyo havikulipuka vimeteguliwa, lakini kuifanya Ukraine kuwa salama kabisa ni kibarua kigumu na cha gharama kubwa, huku Benk ya dunia ikikadiria kuwa kutegua vilipuzi na mabomu yote nchini humo kutagharimu dola zaidi ya bilioni 37.
Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Bintou Keita, ameliambia Baraza la Usalama kwamba ana wasiwasi mkubwa kutokana na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na sheria za kimataifa unaofanywa katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa M23, ambapo vuguvugu hilo linalenga watendaji wa mashirika ya kiraia, hasa watetezi wa haki za binadamu na waandishi wa habari.
Akihutubia Baraza la Usalama lililokaa jana kuanzia saa tisa alasiri saa za New York Marekani ili kuijadili hali ya DRC, kwa njia ya video akiwa nchini DRC, Bintou Keita ambaye pia ni Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, ameeleza kinagaubaga hali ya usalama inavyozidi kudorora mashariki mwa nchi hiyo ya pili kwa ukubwa wa eneo barani Afrika.
“Idadi ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na M23 inaendelea kuongezeka, huku takriban raia 150 wakiuawa tangu kuanza tena kwa mapigano Novemba 2023, wakiwemo watu 77 Januari 2024.”
Aidha Bi. Keita akasisitiza kuhusu changamoto wanazokutana nazo MONUSCO kutokana na kuendelea kukabiliwa na wimbi la taarifa potofu na za uongo kuhusu uhusika wa MONUSCO kwenye mapigano yanayoendelea hivi sasa.
“Kampeni za mtandaoni zinazoilenga MONUSCO zimekuwa zikifanywa na vyanzo ambavyo hasa viko nje ya DRC. Hii imesababisha vitendo vya uhasama dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa na vikwazo vya kutembea vinavyowekwa na makundi yenye silaha na askari wa serikali.”
Kwa mujibu wa Mwakilishi huyo maalumu wa Katibu Mkuu nchini, zaidi ya watu 400,000 waliokimbia makazi yao karibu na mji wa Goma sasa wametafuta hifadhi katika mji huo, wakiwemo watu 65,000 katika wiki mbili zilizopita, na hivyo kusababisha ongezeko kubwa la wagonjwa wa kipindupindu kutokana na ukosefu wa maji safi ya kunywa na usafi wa jumla wa mazingira.
Karibu kusikiliza jarida la habari za Umoja wa Mataifa hii leo ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya Haki ya Kijamii Duniani.
Jarida linaletwa kwako na LEAH MUSHI na kubwa hii leo ni mada kwa kina kutoka nchini Kenya ambako serikali na wadau wa wanyamapori wamechukua hatua kulinda moja ya Wanyama walio hatarini kutoweka , Faru.
Pia utapata fursa ya kusikiliza muhtasari wa habari na ujumbe kutoka mashinani.
Karibu.
Mgogoro wa Sudan ni tishio kwa ukanda mzima huku njaa ya utapiamlo vikiongezeka WFP imeonya.
Maelfu ya watu wayakimbia machafuko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Makala: UNICEF na UNFPA waungana kutokomeza ndoa za utotoni nchini Nepal.
Mashinani : Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Sudan Kusini Jean-Pierre Lacroix afanya ziara kutatathimini hali.
Ikiwa wiki hii ulimwengu umeadhimisha Siku ya redio Duniani, Mwanahabari gwiji wa siku nyingi nchini Tanzania Rose Haji anakubaliana na mtazamo wa Umoja wa Mataifa kuwa redio bado ni chombo muhimu sana katika mawasiliano ya ulimwengu lakini anaona kwamba kwa upande wa taaluma ya utangazaji wa redio kuna tatizo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo katika mkutano wa usalama unaofanyika mjini Munich Ujerumani ametoa wito wa kuwepo utaratibu wa kimataifa ambao unafanya kazi kwa kila mtu.
Asante Evarist Guterres katika hotuba yake amesisitiza wito huo wa amani na utaratibu wa kisasa wa kimataifa akisema utaratibu wa leo wa kimataifa haufanyi kazi kwa kila mtu, "Kwa kweli, ningeenda mbali zaidi na kusema kwamba haufanyi kazi kwa mtu yeyote."
Akielezea hali ya kimataifa, Katibu Mkuu amesema hivi sasa dunia inakabiliwa na changamoto lukuki, lakini jumuiya ya kimataifa imegawanyika zaidi kuliko wakati mwingine wowote katika miaka 75 iliyopita.
Amesisitiza kwamba "Leo hii tunashuhudia nchi zikifanya chochote wapendacho, bila uwajibikaji."
Ameonya kwamba “Kama Ripoti ya Usalama ya Munich inavyoweka bayana mafanikio ya jamii kupitia ushindani kati ya nchi yanapewa kipaumbele badala ya kuangalia faida kwa wote, kupitia ushirikiano”.
Ripoti ya Usalama ya Munich huchapishwa kila mwaka kabla ya mkutano na kuchambua masuala muhimu ya sera ya usalama.
Guterres ameongeza kuwa migogoro inaongezeka, inayohusishwa na ushindani na kutokujali.
Hivyo amesisitiza kuwa utaratibu wa kimataifa ambalo linafanya kazi kwa kila mtu lazima lishughulikie mapungufu haya na kutoa suluhisho.
"Ikiwa nchi zingetimiza wajibu wao chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa, kila mtu duniani angeishi kwa amani na utu".
Katibu Mkuu amegusia pia migogoro inayoendelea duniani mathalan amesema hali ya Gaza ni janga la kutisha la mkwamo katika uhusiano wa kimataifa.
Hakuna kinachoweza kuhalalisha mashambulizi ya kiholela yaliyoanzishwa na Hamas tarehe 7 Oktoba, Guterres amesisitiza kwa wakuu wa nchi na serikali kutoka duniani kote mjini Munich na kuongeza kuwa “Na hakuna kinachoweza kuhalalisha adhabu ya pamoja ya watu wa Palestina katika hatua za kijeshi za Israeli.
Mashambulizi ya kila upande dhidi ya mji wa Gaza yatakuwa mabaya kwa raia wa Palestina ambao tayari wako kwenye zahma kubwa, ameonya Guterres katika hotuba yake kwa washiriki wa ngazi za juu wa mkutano huo.
Masuala mengine aliyozungumzia ni mkutano wa siku zijazo ambao utafanyika Septemba kmwa huu ambapo amesema “tunahitaji kuimarisha usanifu wa amani na usalama wa kimataifa ili kukabiliana na vitisho na changamoto za leo, kama vile mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi, akili bandia au akili mnemba, au kutumia mtandao kama silaha.”
Na Jana Alhamisi, siku moja kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Usalama wa Munich, Guterres alitembelea sinagogi la "Ohel Jakob"
ambako kuna majina ya Wayahudi zaidi ya 4,500 wa Munich ambao waliuawa wakati wa enzi ya Manazi na kusistiza kuwa chuki dhidi ya Wayahudi inapaswa kukomeshwa kote duniani.
Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa usalama unaofanyika mjini Munich Ujerumani, na elimu kwa watoto katika mzozo nchini Afghanistan. Makala tunasikia ujumbe kuhusu matatizo kwa upande wa taaluma ya utangazaji wa redio. Mashinani tunasikia ujumbe wa mkulima nchini Kenya.
Mwenyeji wako ni Evarist Mapesa, karibu!
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF linafanya kila juhudi kuhakikisha watoto wanapata mahitaji yao ikiwemo elimu. Huko nchini Afghanistan shirika hilo limehakikisha zaidi ya wanafunzi 683,000 wanapata elimu wangali katika mazingira wanayoishi.
Mtoto Khadija ni mmoja wa wanufaika wa madarasa ya elimu ya kijamii huko nchini Afghanistan. Kabla ya kuanza kwa programu hii inayofadhiliwa na UNICEF mtoto huyu na wenzake walikuwa hawaendi shule.
Hapo awali, tulikuwa tunagombana na marafiki zangu sababu hatukujua kile kilicho bora. Mimi na marafiki zangu tulikuwa tunacheza sehemu yoyote ile hata kwenye uchafu, sababu hatukujua kuwa ni tatizo.
Lakini baada ya kuandikishwa na kuanza kushiriki katika madarasa ya elimu ya kijamii, Khadija anasema anafurahia mambo anayojifunza shuleni na kushirikiana na wanafunzi wenzake darasani.
Nina jisikia furaha na fahari. Napenda kujifunza hisabati, Dari, ujuzi wa kijamii na kuandika. Ninapokuja shuleni najifunza vitu vingi sana.
Asilimia 60 ya wanufaika wa programu hii ya madarasa ya elimu ya kijamii inayotolewa kwa wanafunzi 683,000 nchini Afghanistani ni watoto wa kike.
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “MBEJAA”.
From the publisher's feed

14 Listeners

43 Listeners

5 Listeners

95 Listeners

25 Listeners

9 Listeners

17 Listeners

4 Listeners

6 Listeners

15 Listeners

8 Listeners

9 Listeners

4 Listeners

4 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners