Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Wakimbizi wanaokimbia machafuko nchini DRC wanapokea huduma za matibabu - WHO

    Nchini Jamhuri ya kidemokrasia kongo DRC Jimboni kivu kaskazini zaidi ya wakimbizi milioni 2.5 wanaishi katika kambi za wakimbizi ambazo zina hali mbaya ambayo ni tishio kwa afya zao. Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO linatoa usaidizi kwa wakimbizi hao.

    Kambi ya wakimbizi ya Bulengo iliyoko jimboni kivu kaskazini, Video ya WHO inaonesha maelfu ya mahema meupe chini udongo mweusi wa mfinyazi, mamia ya watu wanaenda huku na kule ndani ya kambi hiyo.

    WHO inahofia mlundikano huu wa wakimbizi kuleta mlipuko wa magonjwa kama Malaria, magonjwa ya kupumua, ya kuhara na mengine ya kuambukiza. WHO ikishirikiana na wadau wengine wameanzisha vituo vya afya na wagonjwa wanafika kupata huduma, mmoja wao ni Desange Ndamwenge na mwanae. 

    “Nimemleta mtoto wangu hapa asubuhi kwa ajili ya matibabu na ili tupate dawa. Mtoto ana mwaka mmoja na nimgonjwa sana ndio maana nimemleta hapa. Na mimi pia ni mgonjwa. Tumepata dawa wameshatupatia dawa za maji.”

    Aubedi Dunia Sebirayi ni nesi mkuu katika kambi ya Bulengo na anasema, “Hapa tunatoa huduma ya afya ya msingi, wakimbizi hawa wanapokuja na ninwagonjwa hawana hela ya kwenda hospitali kupata matibabu. Tunatoa huduma bure, kwa siku tunaona wagonjwa kati ya 80 mpaka 120 na kati yao unakuta wagonjwa wawili au watatu tunawapeleka katika hospitali.”

    Kwa mujibu wa Meneja wa Matukio wa WHO nchini DRC Dkt. Guy Kalambayi wakimbizi hao wa ndani wanakabiliwa na changamoto nyingi za kiafya lakini kwa kuwapatia dawa, kutoa huduma za kujifungua, kutoa chanjo, na kutibu kipindupindu wanazuia vifo vingi sana na kuokoa maisha.

    Takwimu za WHO zinaonesha kwa wastani tangu mwezi Februari 2023 kwa mwezi wanawake 100 wanajifungua na hakuna kifo cha mjamzito hata mmoja tangu wameanza kutoa huduma. Kavira Mwaliweka ni mkunga katika kituo cha afya ya Bulengo.

    “Kama tusingekuwa na wodi hii ya kujifungulia hapa Bulengo tungekuwa na vifo vingi sana vya wajawazito kwasababu kambi hii iko mbali sana na kituo cha afya. Tunajisika kuwa na bahati sana kwa kutokuwa na kifo hata kimoja cha mjamzito.”

    Elise ni mmoja ya wajawazito waliojifungua salama na sasa anarejea nyumbani kambini na mwanaye kwa furaha. 

    3 min
  • UNICEF Rwanda: Je wajua  kwamba watoto Rwanda wanaanza kupokea chanjo zao za kawaida karibu na nyumbani?

    Katika makala tunaangazia chanjo kwa watoto nchini Rwanda ambako Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaifadhili Rwanda Biomedical Centre (RBC) ambalo ni shirika kuu la kitaifa la utekelezaji wa afya lenye jukumu la kufanya utafiti wa kisayansi, kutoa huduma za uchunguzi, na kutekeleza afua za kiafya ili kulinda taifa la Rwanda dhidi ya magonjwa na matishio mengine ya kiafya. Anold Kayanda anasimulia.

    4 min
  • UNMISS: Uongozi wa jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini waomba usaidizi zaidi wa ulinzi

    Huku mzozo wa Sudan ukiendelea, wakimbizi na wanaorejea wanamiminika katika mipaka ya nchi jirani ya Sudan Kusini, wengi wamekuwa wakitafuta hifadhi katika jimbo la Upper Nile nchini humo na wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu.  Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umefanya mazungumzo na uongozi wa jimbo hilo kuona namna ya kuwasaidia. 

    Kama ulivyoeleza kutokana na hali hiyo ya ongezeko la wakimbizi katika jimbo la Upper Nile, Anita Kiki Gbeho, Naibu Mwakilishi Maalum mpya wa Katibu Mkuu kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini Sudan Kusini UNMISS, na ambaye pia ni Mratibu Mkazi wa Misaada ya Kibinadamu nchini humo amefanya ziara yake ya kwanza huko Malakal kujionea hali iliyo. 

    Bi. Anita alijionea wakimbizi wakiandikishwa, aliketi chini na kusikiliza baadhi ya wakimbizi na kuwapongeza wafanyakazi wa mashirika ya kimataifa kwa kazi kubwa wanayofanya na kisha kuwa na kikao na viongozi wa jimbo la Upper Nile

    “Itakuwa vyema kusikia kutoka kwako, Kaimu Gavana, na baraza lako jinsi unavyoona mustakabali ulivyo na tena jinsi gani tunaweza kuwaunga mkono kwa sababu hatimaye, tunataka kuona watu wa Sudan Kusini wanaoamua kurejea wanapata usaidizi, na tunachojaribu kufanya ni kukuunga mkono katika safari ya kusonga mbele”.

    Jeremiah Deng ambaye ni Kaimu Gavana wa jimbo la Upper Nile alimueleza kiongozi huyo wa UNMISS kuwa kazi ya kusimamia watu wanaorejea makwao na wakimbizi katika maeneo yenye watu wengi kama hapo ni kubwa kupita kiasi na imekuwa si rahisi kwa mamlaka za serikali.

    “Tuna mpaka mrefu ambao uko wazi sana kwamba watu wanaweza kuvuka kutoka upande wowote na kufurika kwa watu kutoka Sudan kuja Sudan Kusini. Watu wengine wanatumia barabara ya mpakani na nyinginezo tofauti, vivukio haramu. Vikosi vyetu vya usalama havina uwezo wa kufunika safu nzima ya mpaka”.

    UNMISS inatoa usaidizi wa kufanya doria za mara kwa mara ili kufuatilia kituo cha usalama huku mashirika ya kibinadamu yakifanya kazi ya ziada kutoa misaada inayohitajika.

    3 min
  • 28 FEBRUARI 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa chakula nchini Sudan, na ulinzi wa amani katika jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini amabapo idadi ya wakimbizi imeongezeka. Makala tunakupeleka nchini Rwanda na mashinani nchini Kenya, kulikoni?  

    1. Msaada wa chakula cha dharura uliotolewa na Ukraine kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kwa ajili ya operesheni zake nchini Sudan, leo umewasili katika bandari ya Port Sudan na kuapakiwa Kwenye malori tayari kwa kuwasambazia mamilioni ya watu wenye uhitaji wa haraka.
    2. Huku mzozo wa Sudan ukiendelea, wakimbizi na wanaorejea wanamiminika katika mipaka ya nchi jirani ya Sudan Kusini, wengi wamekuwa wakitafuta hifadhi katika jimbo la Upper Nile nchini humo na wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu.  Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umefanya mazungumzo na uongozi wa jimbo hilo kuona namna ya kuwasaidia. 
    3. Makala tunaangazia chanjo kwa watoto nchini Rwanda ambako Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaifadhili Rwanda Biomedical Centre (RBC) ambalo ni shirika kuu la kitaifa la utekelezaji wa afya lenye jukumu la kufanya utafiti wa kisayansi, kutoa huduma za uchunguzi, na kutekeleza afua za kiafya ili kulinda taifa la Rwanda dhidi ya magonjwa na matishio mengine ya kiafya.
    4. Na mashinani tutaelekea nchini Kenya kusikia ujumbe wa mfugaji kuhusu uwekezaji katika sekta ya uzalishaji wa mifugo unaowezeshwa na Benki ya Dunia.

    Mwenyeji wako ni Evarist Mapesa, karibu!

    12 min
  • WFP: Msaada wa chakula wa dharura kutoka Ukraine wawasili Sudan

    Msaada wa chakula cha dharura uliotolewa na Ukraine kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kwa ajili ya operesheni zake nchini Sudan, leo umewasili katika bandari ya Port Sudan na kuapakiwa Kwenye malori tayari kwa kuwasambazia watu wenye uhitaji wa haraka.

    Ama kwa hakika wahenga hawakukosea kusema kutoa ni moyo , kwani kwa mujibu wa WFP Ukraine ambayo yenyewe iko katikati ya vita bado imeona umuhimu wa kuwasaidia wenye uhitaji zaidi kwa kuipa WFP ngano ambayo shirika hilo linasema itatosheleza kutoa mgao wa chakula wa mwezi mmoja kwa waathirika wa vita ndani ya Sudan.

    Kuwasili kwa shehena hiyo ambayo ni sehemu ya mradi wa kibinadamu wa nafaka uliozinduliwa na Rais Zelensky wa Ukraine kumefanikishwa na serikali ya Ujerumani iliyolipia gharama zote ambazo ni Euro milioni 15 sawa na takriban dola milioni 16.2.

    Vita ikishika kasi Sudan WFP inasema mahitaji ya kibinadamu na hasa chkula yanaongezeka kwa kasi pia. 

    Kwa mujibu wa Eddie Rowe mkurugenzi wa WFP nchini Sudan "Hali ya kibinadamu nchini Sudan ni janga lakini tunahitaji kuchukua hatua sasa ili kuizuia kuendelea kuwa mbaya zaidi. WFP inafanya kazi kwa kasi kuweza kufikisha msaada wa chakula mikononi mwa familia zinazohitaji msaada huo haraka iwezekanavyo.”

    WFP inasema msaada wa ngano hiyo ambao ni tani 7,600 utagawanywa kwa familia ambazo nyingi zimefurushwa makwao kutokana na mapigano yanayoendelea na zinahaha kila uchao kuweka mlo mezani.

    Rowe amesema msaada huu umewasili wakati muafaka kwani mapigano yakiendelea mgogoro wa njaa nchini Sudan unajongea hasa kabla ya msimu wa muambo mwezi Mei, wakati chakula kinakuwa haba, na njaa inaongezeka.

    Amemalizia kwa kusema kuwa "Msaada huu utaiwezesha WFP kusaidia watu ambao maisha yao yamepinduliwa kabisa na vita. Tunaishukuru sana Ukraine na Ujerumani kwa kuwasaidia watu wa Sudan katika wakati ambao uhitaji ni mkubwa.” 

    3 min
  • Umoja wa Mataifa sio tatizo – Rais wa Baraza Kuu

    Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Dennis Francis Pamoja na mambo mengine amesema Umoja wa Mataifa "sio tatizo" bali tatizo linatokana na kwamba baadhi ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wanahisi wanaweza kukiuka mkataba wa Umoja wa Mataifa watakavyo na kukiuka sheria za kimataifa bila kuadhibiwa. Anold Kayanda anaeleza zaidi.

    5 min
  • WHO/UNHCR: Asilimia 75 ya vifo vyote duniani vinatokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza

    Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani WHO  na la kuhudumia wakimbizi duniani UNHCR leo yameonya kwamba athari zinazoletwa na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile saratani, magonjywa na mfumo wa hewa na kisukari kwa maisha ya watu duniani ni kubwa huku yakiwa ni chanzo cha asilimia 75 ya vifo vyote. 

    Katika tarifa yao ya pamoja iliyotolewa mjini Geneva Uswis kwa mashirika hayo yamesema Watu walioathiriwa na dharura za kibinadamu wako katika hatari zaidi ya kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza NCDs huku ikikadiriwa kuwa magonjwa ya kiharusi na shinikizo la damu  yana uwezekano wa kuongezeka mara tatu zaidi kunapokuwa na majanga ya kibinadamu.

    Hata hivyo, yameongeza kuwa huduma na matibabu ya NCDs mara nyingi havijumuishwi kama sehemu ya kawaida ya maandalizi ya hatua za dharura ya kibinadamu, ambayo huzingatia mahitaji ya haraka zaidi.

    Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema. "Watu wanaoishi na NCDs katika majanga ya kibinadamu wana uwezekano mkubwa wa kuona hali zao zikiwa mbaya zaidi kutokana na kiwewe, msongo wa mawazo, au kutoweza kupata dawa au huduma. Mahitaji ni makubwa, lakini rasilimali hazitoshi. Lazima tutafute njia za kuunganisha vyema huduma za NCD katika kukabiliana na dharura, ili kulinda maisha zaidi kutokana na majanga haya yanayoweza kuepukika na kuboresha usalama wa afya."

    Wakimbizi wametajwa kwamba mara nyingi wanakabiliwa na ukosefu wa huduma za afya, kutokana na hali mbaya ya maisha, matatizo ya kifedha, na hali mbaya ya kisheria.

    Filippo Grandi,ambaye ni  Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi amesema "Kadiri watu wanaofurushwa makwao wanavyoongezeka, lazima tufanye kazi ili kuhakikisha haki ya afya ya wakimbizi, watu wengine waliolazimika kukimbia na jamii zinazowapokea. Ni muhimu kwamba sera, na rasilimali ziwepo ili kusaidia kujumuishwa kwa wakimbizi katika mifumo ya afya ya kitaifa, ikiwa ni pamoja na kupata huduma za magonjwa yasiyoambukiza. Lazima tuwe wabunifu, na kufanya kazi na serikali na washirika kutatua changamoto kama hizi."

    NCDs zilichangia asilimia kubwa ya vifo vyote katika nchi zinazotoa wakimbizi wengi wanaosaidiwa na UNHCRambapoasilimia 75 Syria, asilimia 92 nchini Ukraine, asilimia 50 nchini Afghanistan na asilimia 28 Sudan Kusini.

    3 min
  • 27 FEBRUARI 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia hatari ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza na wakimbizi wa Sudan wanaovuka mpaka kuelekea Sudan Kusini. Makala tunakuletea majibu ya Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Dennis Francis alipohojiwa na UNTV kandoni mwa Kikao cha 55 cha Baraza la Haki za Binadamu kinachoendelea jijini Geneva Uswisi na mashinani tunakupeleka nchini Afghanistan, kulikoni?  

    1. Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani WHO na la kuhudumia wakimbizi duniani UNHCR leo yameonya kwamba athari zinazoletwa na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile saratani, magonjywa na mfumo wa hewa na kisukari kwa maisha ya watu duniani ni kubwa huku yakiwa ni chanzo cha asilimia 75 ya vifo vyote.
    2. Wananchi waliokimbia makazi yao kutokana na vita inayoendelea nchini Sudan wanasaidiwa nchini Sudan Kusini na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM ambalo limeeleza zaidi ya watu nusu milioni wamevuka mpaka na kuingia eneo la Renk na sasa wanawapatia usaidizi wa usafiri ili kufika kwenye maeneo watakayopata usaidizi. 
    3. Katika makala Anold Kayanda anaangazia majibu ya Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Dennis Francis alipohojiwa na UNTV kandoni mwa Kikao cha 55 cha Baraza la Haki za Binadamu kinachoendelea jijini Geneva Uswisi. Pamoja na mambo mengine Balozi Francis amesema Umoja wa Mataifa "sio tatizo" bali tatizo linatokana na kwamba baadhi ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wanahisi wanaweza kukiuka mkataba wa Umoja wa Mataifa na  sheria za kimataifa watakavyo.
    4. Na mashinani tutaelekea nchini Afghanistan kusikia jinsi UNICEF ilivyorejesha huduma za afya, matibabu na mafunzo kwa wataalam ili kuwafikia watoto na wanawake popote walipo.

    Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

    12 min
  • Wakimbizi wanaofika mpakani mwa Sudan na Sudan Kusini wanasaidiwa na IOM kusafiri

    Wananchi waliokimbia makazi yao kutokana na vita inayoendelea nchini Sudan wanasaidiwa nchini Sudan Kusini na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM ambalo limeeleza zaidi ya watu nusu milioni wamevuka mpaka na kuingia eneo la Renk na sasa wanawapatia usaidizi wa usafiri ili kufika kwenye maeneo watakayopata usaidizi. 

    Maelfu ya watu wanavuka mpaka katika eneo la Renk nchini Sudan Kusini ambako IOM imesema lina hali ngumu kwani hakuna maji, chakula, usafiri wala usalama wa aina yeyote na ni eneo lililo mbali. Maelfu ya watu wameovuka mpaka wanaonekana kuwa ni dhaifu. Wengi wao wana kiwewe. 

    Msemaji wa IOM Afrika Mashariki Yvonne Ndege anasema wamezungumza na wanawake, watoto na wazee ambao wamekimbia ghasia na wametumia wiki na miezi, kujaribu kufikia mpaka huo.

    “Hali waliyoielezea, waliyo yashuhudia ni ya kutisha kabisa. Wengine wanasema walikimbia vurugu. Wengine wanasema walikimbia risasi. Wengine wanasema walifanyiwa ukatili wa kijinsia wakiwa safarini. Wengine wanasema walitumia siku nyingi sana msituni wakijaribu kufikia mpaka huu. Tulizungumza na familia moja, mama akiwa na binti zake wawili na mama yake mwenyewe, ambaye alisafiri kutoka mji mkuu wa Sudan, Khartoum, mpaka kufika mpaka huu na kuvuka salama. Aliumia sana, alifadhaika sana. Lakini anamshukuru Mungu kwamba alikuwa ametoroka na uhai wake.”

    Msemaji huyo wa IOM imeeleza wameandaa zaidi ya safari za ndege 1,200 vile vile kuna usafiri wa maji ambapo wakimbizi wengine watasafirishwa kwa siku tatu kutoka Renk kupitia mto Nile mpaka kufika Malakal mji mkuu wa jimbo la Upper Nile. 

    “Usaidizi huu ni muhimu kabisa kwa sababu kile IOM na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa hawataki, ni kambi za wakimbizi kuibuka katika eneo hili kwa sababu liko mbali sana. Hakuna miundombinu. Hakuna hospitali, hakuna vifaa vya matibabu. Hakuna rasilimali za aina yoyote kwa watu.”

    Pamoja na usaidizi huo unaotolewa na IOM pamoja na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa bado Kuna wasiwasi mkubwa juu ya hatari ya kuibuka kwa magonjwa, njaa na vurugu zaidi.

    IOM imekuwa ikifanya ukaguzi wa kimatibabu na kutoa chanjo kabla ya kuwasafirishwa.

    3 min
  • Namna ngamia walivyobadili maisha ya wanajamii wa Samburu Kenya

    Kwa wafugaji hususan walio katika maeneo ya ukame kwa miongo kadhaa wamekuwa wakiathirika na athari za mabadiliko ya tabianchi kutokana na mifugo yao kutozalisha kiwango kinachohitajika cha maziwa na nyama cha kuwatosheleza wao wenyewe kula na kingine kuuza na kujipatia fedha. 

    Ni kutokana na changamoto hiyo ndio maana mradi wa Pear Innovation ukaanzishwa huko kaunti ya Samburu nchini Kenya ambao ulilenga kutoa ngamia kwa wanawake ili wawaze kutumia maziwa ya ngamia hao kama lishe kwa familia zao na kisha kuuza mazao mengine na kujipatia fedha. Tuungane na Leah Mushi katika Makala hii. 

    6 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

17 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners