
Sign up to save your podcasts
Or


Mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza yanaendelea nchini Misri kwa siku ya pili leo huku Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa akionya kwamba vita ya Gaza iko katika hatari ya kubadili mweleko na kupanua wigo zaidi utakaoathiri kila nchi Mashariki ya Kati na kwingineko.
Asante Anold. Kamishina Mkuu Volker Türk ameliambia Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswisi kuwa "Nina wasiwasi mkubwa kwamba katika janga hili la vita cheche yoyote zaidi inaweza kusababisha moto mkubwa zaidi,"
Katika taarifa ya hivi karibuni kuhusu migogoro ya kimataifa kwa Nchi 47 Wanachama wa Baraza hilo, Kamishna Mkuu alisisitiza kwamba jumuiya ya kimataifa inapaswa kufanya "kila linalowezekana ili kuepuka kuenea zaidi kwa vita ya Gaza.”
Maoni yake yanakuja huku kukiwa na wito wa "kusitishwa mara moja kwa mapigano kwa angalau wiki sita zijazo ili kuwezesha kuachiliwa huru kwa mateka wa Israeli.’
Wito huo umetoka kwa Makamu wa Rais wa Merika Kamala Harris, wakati wa mazungumzo ya kimataifa ya kusitisha mapigano nchini Misri Jumapili, ambayo yanayoripotiwa kuhusisha Marekani wajumbe wa Qatar na Hamas lakini hadi sasa hakuna wawakilishi wa Israel.
Bwana Türk amesema “Hatari za kuyumbisha usalama wa kikanda tayari zilionekana kusini mwa Lebanon, akisisitiza kwamba wapiganaji wa wanamgambo wanaoiunga mkono Palestina sasa wanahusika katika hali ya kusikitisha sana ya uhasama na majibizano ya risasi na Israeli, katika msitali wa Bluu wa uangalizi wa Umoja wa Mataifa unaotenganisha nchi zote mbili.
Takriban watu 200 wameuawa nchini Lebanon tangu vita ilipozuka Gaza¸ Kamishna Mkuu amesema miongoni mwa waathirika wakubwa ni, watoto, wahudumu wa afya na waandishi wa habari.
Mkuu huyo wa haki za binadamu ameongeza kuwa “takriban watu 90,000 nchini Lebanon wamekimbia makazi yao kutokana na ghasia hizo, huku kukiwa na uharibifu mkubwa wa vituo vya afya, shule na miundombinu muhimu. Jamii za Israeli pia zimeshuhudia watu 80,000 wakiondolewa kutoka maeneo ya mpakani kwa sababu ya kuongezeka kwa vurugu.”
Mashirika ya kibinadamu yameendelea kuripoti kuhusu hali mbayá na ongezeko la vifo vya raia ambapo lile la kuhudumia watoto UNICEF mwishoni mwa wiki likisema hadi sasa watoto 15 wamepoteza Maisha katika hospitali ya Kamal Adwan mjini Gaza kutokana na utapiamlo na ukosefu wa maji mwilini.
UNICEF imeonya kwamba watoto wengi zaidi watapoteza Maisha katika siku zijazo endapo msaada wa haraka unaohitajika hautofikishwa kunusuru Maisha yao.
Nalo shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women linakadiria kuwa wanawake 9,000 wameshauawa tangu vita ilipozuka Gaza miezi mitano iliyopita.
Mamlaka ya afya ya Gaza inasema jumla ya watu waliopoteza Maisha tangu kuanza kwa vita Gaza ni zaidi ya 30,400 na inatarajiwa kuendelea kuongezeka.
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko katika ukanda wa Gaza na uondoaji wa mabomu ya kutegwa ardhini nchini Sudan Kusini. Makala inakupeleka nchini Kenya ambapo hivi karibuni kulifanyika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Baraza la mazingira duniani UNEA6 na mashinani tutaelekea nhcini DR Congo.
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Nchini Sudan Kusini kwa mwaka jana pekee wateguaji wa mabomu ya ardhini wa Umoja wa Mataifa wamefanikiwa kusafisha eneo lenye ukubwa sawa na viwanja 64 vya mpira wa miguu, na hivyo kuondoa hatari nyingi za milipuko, inaeleza UNMISS ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini.
Kupitia Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya misaada ya kutegua mabomu yaliyotegwa ardhini (UNMAS) asilimia 70 ya vilipuzi ambavyo vilikuwa havijalipuka sasa vimeharibiwa au kuondolewa katika maeneo vilimokuwa na hivyo kuwahakikishia watu makazi salama na maeneo ya kilimo.
Mike Fula Rashid, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kitaifa ya Sudan ya Hatua dhidi ya Vilipuzi (NMAA) anapeleka shukrani kwa Umoja wa Mataifa akisema,
"Tunashukuru kwa msaada ambao UNMAS inatupatia kuhusiana na uondoaji wa vilipuzi kwa sababu ukiangalia uwezo wa kuondoa mabomu nchini Sudan Kusini, asilimia 70 inaungwa mkono na UNMAS huku wafadhili wengine wakichangia asilimia 30 iliyobaki.”
Utafiti mpya uliotolewa leo na jarida la kitabibu la Uingereza Lancet na shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO unaonyesha kwamba, mwaka 2022, zaidi ya watu bilioni 1 duniani sasa wanaishi na unene wa kupindukia ama utipwa tipwa. Duniani kote, unene wa kupindukia kwa watu wazima umeongezeka zaidi ya mara mbili tangu mwaka 1990, na umepanda mara nne kwa watoto na vijana wenye umri wa miaka 5 hadi 19.
Utafiti huo pia unaonyesha kwamba ingawa viwango vya utapiamlo vimepungua, bado ni changamoto kubwa ya afya ya umma katika maeneo mengi, hasa Asia Kusini Mashariki na Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Nchi zenye viwango vya juu zaidi vya utipwatipwa na utapiamlo mwaka 2022 zilikuwa ni mataifa ya visiwa katika Pasifiki na Karibea, Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.
Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema utafiti huu mpya unaangazia umuhimu wa kuzuia na kudhibiti unene wa kupindukia tangu utotoni hadi utu uzima kupitia lishe, mazoezi ya mwili, na huduma za kutosha kadri inavyohitajika.
Ghebreyesus ameongeza kuwa ili kupambana na tatizo hilo ni sharti kurejea kwenye mstari ili kufikia malengo ya kimataifa ya kudhibiti unene wa kupindukia itahitaji kazi ya serikali na jamii, ikisaidiwa na sera za WHO na mashirika ya afya ya umma ya kitaifa na sekta binafsi.
Kwa mujibu wa WHO, utapiamlo, katika aina zake zote, ni pamoja na kukonda, kudumaa, uzito mdogo, upungufu wa vitamini au madini, uzito kupita kiasi na unene kupita kiasi, hata hivyo ukosefu wa lishe bora huchangia nusu ya vifo vya watoto chini ya miaka 5 na unene unaweza kusababisha magonjwa yasiyoambukiza kama vile magonjwa ya moyo na mishipa, kisukari na baadhi ya saratani.
Katika Mkutano wa Afya Duniani mwaka 2022, Mataifa Wanachama walikubaliana na Mpango wa WHO wa Kuongeza kasi ya Kusitisha Unene wa Kupindukia, unaounga mkono hatua za ngazi ya nchi hadi 2030. Hadi sasa, serikali 31 zinaongoza njia kudhibiti janga la unene wa kupindukia kwa kutekeleza mpango huo.
Mkurugenzi wa Idara ya Lishe na Usalama wa Chakula wa WHO na mmoja wa waandishi wa utafiti huo Dkt. Francesco Branca amesema kuna changamoto kubwa katika utekelezaji wa sera zinazolenga kuhakikisha upatikanaji wa chakula bora kwa wote na kujenga mazingira ambayo yanakuza shughuli za kimwili na maisha ya afya kwa ujumla kwa kila mtu na kutoa wito kwa nchi kuweka mfumo wa kuzuia na kudhibiti utapwitapwi katika huduma za msingi
Utafiti huo umeweka bayana kwamba ili kukabiliana na utapiamlo kunahitajika hatua za kisekta mbalimbali katika kilimo, ulinzi wa jamii na afya, ili kupunguza uhaba wa chakula, kuboresha upatikanaji wa maji safi na usafi wa mazingira na kuhakikisha upatikanaji wa afua muhimu za lishe kwa wote.
Mkutanowa Umoja wa Mataifa wa Baraza la mazingira duniani UNEA6 leo umekunja jamvi jijini Nairobi Kenya baada ya kukutanisha wadau zaidi ya 7000, kutoka nnyanja mbalimbali kwa lengo la kukabiliana na changamoto kubwa tatu zinazoikabili dunia ambazo ni mabadiliko ya tabianchi, upotevu wa bayoanuai na uchafuzi wa mazingira. Viongozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa wamepata fursa ya kuwasilisha taarifa zao na kushiriki katika mjadiliano. Stella Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa Nairobi UNIS hakuachwa nyuma amekuwa akizungumza na wadau mbalimbali wanaoshiriki mkutano huo wa UNEA6 tangu ulipoanza na leo yuko na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) wa Tanzania Dkt. Selemani Jafo na kwanza amemuuliza anachokibeba kutoka kwenye mkutano huo
Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa 6 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA6 unaokunja chamvi leo, na utafiti mpya uliotolewa leo na jarida la kitabibu la Uingereza Lancet na shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO kuhusu utipwatipwa.
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Mkutano wa 6 WA Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA 6 umefunga pazia leo jijini Nairobi, Kenya baada ya siku 5 za majadiliano na shughuli mbalimbali zilizohusisha zaidi ya waj umbe 7,000 kutoka Nchi 182 Wanachama wa Umoja wa Mataifa. Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Nairobi UNIS, Stella Vuzo amekuwa akizungumza na washiriki mbalimbali kuhusu walivyonufaika na mkutano huo na hapa ni mmoja wao kutoka jamii za wafugaji ambao duniani kote mabadiliko ya tabianchi yanawaathiri moja kwa moja.
Wakati jijini Nairobi Kenya mkutanowa Umoja wa Mataifa wa Baraza la mazingira duniani UNEA6 ukielekea ukingoni leo ikiwa ni siku yake ya 4, vijana wanaoshiriki mkutano huo wamepaza sauti zai na kusistiza kuwa wakipewa nafasi basi wana mchango mkubwa katika vita dhidi ya uharibifu wa mazingira na kusongesha mbele ajenda ya maendeleo endelevu SDGs. Leo mkutanoni huko Stella Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Nairobi UNIS amezungumza na vijana wawili wanaoshiriki mkutano huo ambao ni wanaharakati wa mazingira wanaotumia sayansi na sanaa kuleta mabadiliko katika jamii na pia ndio waliobuni sanaa ya jukwaa la mbao ambalo limewekwa kwenye lango la UNEA6 likipewa jina “Get your Seat at the Table”
Ikiwa leo ndio siku ya mwisho ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia kipindi cha mpito nchini Sudan (UNITAMS), Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema pamoja na kwamba UNITAMS inaondoka Sudan lakini Umoja wa Mataifa hauondoki nchini humo na unaendelea kujitolea kwa dhati kutoa usaidizi wa kibinadamu wa kuokoa maisha na kusaidia watu wa Sudan katika matarajio yao ya mustakabali wenye amani na usalama.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Msemaji wake usiku wa jana Februari 28 saa za New York, Marekani, Katibu Mkuu Guterres ameanza kwa kurudia shukrani zake za dhati kwa wafanyakazi wote wa kimataifa na kitaifa wa UNITAMS kwa kujitolea kwao na huduma kwa watu wa Sudan katika muda wote wa majukumu ya Ujumbe huo.
Stéphane Dujarric ambaye ni Msemaji wa Katibu Mkuu anaeleza kwamba timu ndogo itasalia mjini Port Sudan ili kusimamia mchakato mzima wa makabidhiano kuanzia tarehe 1 Machi na kwamba Katibu Mkuu anategemea ushirikiano kamili wa mamlaka ya Sudan ili kuhakikisha mchakato huu unakamilika kwa urahisi na haraka iwezekanavyo.
Mzozo unaoendelea kupamba moto nchini Sudan unazidi kudidimiza utawala wa sheria na ulinzi wa raia na kuhatarisha nchi nzima na eneo zima. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anatoa wito kwa pande zinazozozana kuweka chini silaha zao na kujitolea kwa mazungumzo mapana ya amani yatakayosababisha kuanzishwa tena kwa mpito wa kidemokrasia unaoongozwa na raia.
Wazo la kutaka UNITAMS ifungwe lilitoka kwa mamlaka za Sudan na baadaye mwishoni mwa mwaka jana, Baraza la Usalama liliridhia ombi hilo na kupitisha azimio.
Mjumbe Binafsi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Sudan, Ramtane Lamamra, ameanza kazi yake ya kuunga mkono juhudi za upatanishi, kwa uratibu na ushirikiano wa karibu na wadau wa Afrika na wengine wa kimataifa. Juhudi hizi za upatanishi zitakamilisha kazi muhimu inayoendelea ya Timu ya Nchi ya Umoja wa Mataifa mashinani, ambayo ni pamoja na kutoa usaidizi wa kibinadamu wa kuokoa maisha. Katibu Mkuu anatoa wito kwa mamlaka za Sudan kuendeleza ushirikiano wao, ikiwa ni pamoja na kuwezesha utoaji wa visa ya kuingia kwa wakati na kutowawekea vikwazo wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wadau nchini humo kutoa msaada unaohitajika.
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya mwisho ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia kipindi cha mpito nchini Sudan (UNITAMS), na afya kwa wakimbizi wa DRC jimboni Kivu Kaskazini. Makala na mashinani tunaangazia mkutano huo wa Baraza la mazingira duniani UNEA6 leo ikiwa ni siku yake ya 4.
Mwenyeji wako ni Evarist Mapesa, karibu!
From the publisher's feed

14 Listeners

43 Listeners

5 Listeners

95 Listeners

25 Listeners

9 Listeners

17 Listeners

4 Listeners

6 Listeners

15 Listeners

8 Listeners

9 Listeners

4 Listeners

4 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners