
Sign up to save your podcasts
Or


Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Flora Nducha anamulika siku ya wanawake duniani kuanzia habari ya kwanza hadi ya mwisho maudhui yakiwa Wekeza kwa wanawake - songesha maendeleo.
Nchini Afrika Kusini katika jimbo la Western Cape kufuatia mafunzo kuhusu unyanyasaji wa kijinsia yaliyotolewa na kikundi cha wanawake cha Ilitha Labantu kwa vituo kadhaa vya polisi, sasa kuna ushahidi wa wazi kwamba vituo vya polisi vimeweka mazingira rafiki ya kuwasikiliza wanawake walionyanyaswa kuliko ilivyokuwa hapo awali. Anold Kayanda ameufuatilia mradi huo. Karibu Anold utueleze zaidi.
(Taarifa ya Anold Kayanda)
Asante sana Flora Nducha. Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake (UN Women) linasema kiwango cha unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana nchini Afrika Kusini ni miongoni mwa viwango vya juu zaidi duniani na wanafafanua wakisema kwamba mwanamke mmoja kati ya watano walio katika uhusiano amepitia ukatili wa kimwili uliofanywa na mpenzi wake.
Wengi zaidi wameteseka na aina nyingine za vurugu kutoka kwa wanaume wanaowajua na wasiowajua lakini changamoto zaidi ni namna ya kuyashughulikia masuala haya kwani matukio mengi ya unyanyasaji hayaripotiwi kwa mamlaka kutokana na imani ndogo kwa vyombo vya sheria.
Ella Mangisa, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo la Ilitha Labantu anasema ulikuwa unakuta mwanamke anayekimbia hali ya vurugu, akifika polisi ataambiwa arudi nyumbani akaelewane na mnyanyasaji wake au kuambiwa haya ni masuala ya kibinafsi wanayohitaji kutatua wao wenyewe."
Kupitia ushirikiano na UN Women na wadau wengine ndipo Ilitha Labantu mwaka 2021 ilizindua mpango wa kufanya kazi na Huduma ya Polisi ya Afrika Kusini (SAPS) kuwaelimisha maafisa kufanya kazi na waathirika wa ukatili wa kijinsia. Mpango umetekelezwa katika vituo 75 vya polisi huko Cape Metro na Cape Winelands katika Mkoa wa Western Cape.
Ilitha Labantu inapanga kupanua zaidi mpango huo na kushirikisha mashirika mengine yenye utaalamu tofauti. Shirika hilo pia linatarajia kujumuisha maudhui ya mafunzo yao katika mtaala wa vyuo vya polisi kote nchini Afrika Kusini.
Katika kusherehekea siku ya wanawake duniani kote Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewapongeza wanawake na wasichana kwa kupata mafanikio makubwa na kuondoa vikwazo, kuvunja fikra potofu na kuchochea maendeleo kuelekea dunia yenye haki na usawa zaidi. Leah Mushi na maelezo zaidi.
Katika ujumbe wake kwa siku hii Katibu Mkuu Guterres amesema “Pamoja na juhudi wanazozifanya kila siku bado wanakabiliwa na vikwazo vikubwa. Mabilioni ya wanawake na wasichana wanakabiliwa na kuenguliwa, ukosefu wa haki na ubaguzi, ilhali janga lililojikita la ukatili dhidi ya wanawake lilikimomonyoa ubinamu.”
Amesema ni vyema kuongeza juhudi ikiwemo za kisheria katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili wanawake kwani kwa kasi ya sasa itachukua miaka miatatu kupata usawa.
Akieleza nini kifanyike amesema “ tunapaswa kuwekeza kwenye miradi ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na kuchochea ujumuishaji wanawake na uongozi wa wanawake kwenye uchumi, teknolojia za kidijitali, ujenzi wa amani na hatua kwa tabianchi.Yote hii inategemea kupatikana kwa fedha kwa ajili ya maendeleo endelevu ili nchi ziwe na fedha za kuwekeza kwa wanawake na wasichana.”
Kauli mbiu ya siku ya wanawake kwa mwaka huu ni wekeza kwa wanawake ili kuharakisha maendeleo na Mkuu huyo wa umoja wa Mataifa amesema inatukumbusha kuwa kutokomeza mfumo dume kunahitaji kuweko kwa fedha mezani.
“Tunahitaji pia kuongeza idadi ya wanawake viongozi kwenye sekta ya biashara, Benki Kuu na Wizara za Fedha. Hii inaweza kusaidia kuchochea uwekezaji kwenye sera na miradi inayokidhi mahitaji ya wanawake na wasichana.
Haki za wanawake zimedhihirisha kuwa njia ya haki ya jamii zenye haki, amani na ustawi. Hii ni vema kwetu sote.
“Kwa Pamoja, hebu na tuchukue hatua za haraka kufanya kuwa halisia.”
Usawa kwa woteNalo shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women linaadhimisha siku hii kwa kufanya mkutano mkubwa katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani utakao wakutanisha pamoja viongozi wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa masuala ya wanawake.
UN Women wamesema katika mwaka huu ambapo karibu nusu ya watu duniani wanaishi katika nchi zinazoshiriki katika uchaguzi, Siku hii ya Kimataifa ya Wanawake ni fursa muhimu ya kufafanua siku zijazo tunazotaka.
Wakati mizozo, mabadiliko ya tabianchi na jamii zenye mgawanyiko zikididimiza miongo kadhaa ya maendeleo katika usawa wa kijinsia, UN Women inatoa wito waku "Wekeza kwa wanawake ili Kuharakisha Maendeleo" ili hatimae dunia iweze kufikia faida ya usawa wa kijinsia kwa wote.
Hii leo jaridani tunaangazia miradi inayotekelezwa na Umoja wa Mataifa huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo -DRC kusaidia wanawake ikiwa ni kuelekea siku ya wanawake duniani hapo kesho Machi 8.
Pia utapata fursa ya kusikiliza muhtasari wa habari na kujifunza lugha ya kiswahili ambapo leo ni ufafanuzi wa methali 'AFUNGAYE KIBWEBWE SI BURE ANA MCHEZO'
Wiki hii Ijumaa tarehe 8 Machi 2024, ulimwengu utaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambapo mwaka huu ina maudhui “Wekeza kwa wanawake: Harakisha maendeleo,” lakini Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women linasema ni dhahiri kwamba ulimwengu bado unakabiliwa na migogoro mingi, kuanzia mizozo ya kijiografia hadi viwango vya umaskini vinavyoongezeka, ukosefu wa usawa na kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabianchi.
Kwa kuwekeza kwa wanawake, tunaweza kuibua mabadiliko na kuharakisha mpito kuelekea dunia yenye afya, usalama na usawa zaidi kwa wote. Nchini Kenya tunakutana na mama mjasiriamali ambaye alianza kwa kufanya kazi na shirika lisilo la kiserikali liitwalo Sime Food, ambalo linahusika na kilimo endelevu, lishe bora, na stadi za biashara ndogo ndogo ili wawe na maarifa na ujuzi unaohitajika ili kupatia familia zao lishe bora mwaka mzima na kuuza masalio ili kusaidia kulipia mahitaji mengine ya kaya. Baada ya kupata mafunzo hayo na fedha za kuanzisha biashara zake, Lucy anachochea kinamama na vijana wa kike wajiunge naye katika sekta ya biashara ili waweze kujikwamua kiuchumi. Selina Jerobon wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amefuatilia na kutuandalia makala hii.
Hii leo jaridani tunaangazia mizozo na janga la kibinadamu nchini Sudan, na kuondoka kwa MONUSCO nchini DRC. Makala inatupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Uganda, kulikoni?
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Harakati za ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, za kuondoka nchini humo zikiendelea, tunamulika hatua chanya zilizochukuliwa na ujumbe huo katika kunusuru vijana waliokuwa wanatumikishwa na waasi mashariki mwa nchi hiyo.
Miongoni mwao ni Charles, mwenye umri wa miaka 16 ambaye si jina lake halisi. Yeye alitumikishwa msituni na waasi kwa kipindi cha miaka miwili.
Akizungumza huku sura yake ikiwa imefichwa kwenye video ya MONUSCO, Charles anakumbuka kuwa walikuwa shambani wanalima wakati waasi wa Mai Mai walipofika na kuwakamata.
“Walitueleza kuwa hawana watu wa kuwasaidia mapigano hivyo wakatuchukua. Tulipofika walituona kuwa tuna mawazo ya kutoroka hivyo walitufungia ndani kwa wiki tatu,” anasema Charles.
Anasema walipotoka fikra za kutoroka zikatoweka, wakafundishwa kupigana msituni na walipigana mara sita. Lakini haikuwa rahisi kwani wenzake 12 waliuawa huku porini wakati wa mapigano huku yeye mwenyewe akishuhudia.
“Niliumia sana. Chakula nacho kilikuwa shida kupata, maisha yalikuwa magumu mno. Nikafikiria nikaona bora nirejee kwa familia yangu.’
Walichofanya yeye na wenzake, usiku wa saa saba walitoroka hadi mji wa jirani ambako huko walijisalimisha kwa kiongozi mmoja na kumweleza kuwa wamechoka kuishi na kupigana porini.
Kiongozi huyo aliwachukua na kuwapeleka Beni, mji ulioko jimboni Kivu Kaskazini.
Charles anasema kiongozi huyo aliwasaidia kuwakutanisha na shirika la kiraia la ACOPE, mdau wa MONUSCO. Hapo walipata mafunzo kwa wiki tatu ikiwemo utengenezaji majiko banifu yasiyochafua mazingira.
“Sasa maisha ni mazuri hapa na wito wangu kwa wale watoto na vijana walioko msituni wakipigana ni kwamba waondoke huko waache kupigana, waje wajisalimishe kwa serikali ili waweze kujiendeleza.”
Takriban miezi 11 tangu majenerali wapinzani watangaze vita nchini Sudan, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa leo walionya kwamba mzozo huo unaweza kusababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani.
Sudan, nchi iliyo kaskazini mashariki mwa Afrika tayari iko katika mzozo mkubwa zaidi wa watu waliofuriushwa makwao duniani kwa mujibu, Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa, WFP.
Na mapigano yanayoendelea kati ya Jeshi la Sudan SAF na kundi hasimu la msaada wa haraka RSF yamesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine milioni nane kuyahama makazi yao ndani ya nchi na wengine kukimbilia nchi jirani.
Hivi sasa watoto milioni 14 wanahitaji haraka msaada wa kuokoa maisha, limesema Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF katika tahadhari yale ya hivi karibuni, huku kukiwa na wasiwasi kwamba mzozo huo unaweza kuenea kwenye mipaka ya Sudan, na kutishia maisha na amani katika eneo hilo, endapo mapigano hayo hayatokoma.
Cindy McCain, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa WFP amesema "Miaka ishirini iliyopita, Darfur ilikuwa janga kubwa zaidi la njaa duniani na ulimwengu ulijitolea kuchukua hatua. Lakini leo hii watu wa Sudan wamesahaulika. Mamilioni ya maisha ya watu, amani na utulivu wa eneo zima viko hatarini,”
Bi. McCain ameyasema hayo akiwa Sudan Kusini, ambako amekutana na familia zilizokimbia ghasia na hali mbaya ya njaa Sudan na kuingia hiyo jirani zao.
Amesema hivi sasa WFP inahaha kutimiza mahitaji ya chakula na kuongeza kuwa "Nimekutana na kina mama na watoto ambao wamekimbia Sudan ili kuokoa maisha yao sio mara moja, lakini mara nyingi, na sasa njaa inawanyemelea. Madhara ya kutochukua hatua yanakwenda mbali zaidi ya mama kushindwa kulisha mtoto wake na yataathili eneo hilo kwa miaka mingi ijayo”.
WFP inasema leo hii chini ya mtu mmoja kati ya 20 Sudan ndiye anayeweza kumudu kupata chakula, watu 9 kati ya 10 wanakabiliwa na njaa na mgogoro wa chakula umesambaa hadi nchi jirani zinazohifadhi wakimbizi wa Sudan na kuathiri watu zaidi ya milioni 25 Sudan, Sudan Kusini, na Chad.
Hii leo jaridani tunakuletea mada ambayo inaangazia jitihada za taasisi ya ProjeKt Inspire ya nchini Tanzania katika kuhamasisha masomo ya STEM yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za Gaza, haki za binadamu, ukulima na usawa wa kijinsia. Mashinani tukielekea siku ya wanawake duniani tutakupeleka katika kaunti ya Kajiado nchini Kenya.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Katika kuelekea siku ya wanawake duniani ambayo itaadhimishwa Ijumaa wiki hii Machi 8 mchango wa wanawake katika kulinda na kuhifadhi mazingira umeelezwa kuwa ni mkubwa na wa thamani sana. Kandoni mwa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Baraza la mazingira duniani UNEA6 uliofanyika Nairobi Kenya na kukunja jamvi mwishoni mwa wiki, nada mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo mchango wa wanawake. Stella Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa Nairobi UNIS alizungumza na Balozi na mtafiti katika Mradi wa Green Transition nchini Kenya Dkt. Josephine Ojiambo kuzungumzia mchango huo wa wanawake katika kulinda mazingira.
From the publisher's feed

14 Listeners

43 Listeners

5 Listeners

95 Listeners

25 Listeners

9 Listeners

17 Listeners

4 Listeners

6 Listeners

15 Listeners

8 Listeners

9 Listeners

4 Listeners

4 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners