Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 23 OKTOBA 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia siku ya Umoja wa Mataifa na tutasikia kutoka mashinani wananchi na asasi za kiraia zina yapi ya kusema kuhusu shirika hili kubwa na la kipekee linalounganisha nchi wanachama 193 duniani.Mashirika manne ya Umoja wa Mataifa lile la uhamiaji IOM, la kuhudumia wakimbizi UNHCR, la Kuhudumia watoto UNICEF na la mpango wa chakula duniani WFP leo yametoa wito wa dharura kwa dunia kuchukua hatua mara moja kukabiliana na janga la kibinadamu linaloongezeka nchini Sudan. Zaidi ya watu milioni 30 wanahitaji msaada, nchini humo wakiwemo watoto milioni 15 na wakimbizi karibu milioni moja.Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) jana Oktoba 22 ilisema Israeli lazima itimize majukumu yake kama “anayekalia kimabavu” kwa kuhakikisha kuwa msaada unaweza kupita bila vizuizi na kwa kuheshimu haki za Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kibinadamu yanayofanya kazi katika Ardhi ya Palestina Iliyokaliwa kwa Mabavu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameelezea maoni hayo ya ICJ kuwa “muhimu sana,” akiongeza kuwa yametolewa wakati ambapo Umoja wa Mataifa unafanya kila juhudi kuongeza kasi ya misaada kuingia Gaza baada ya kusitishwa kwa mapigano.Nchini Kenya, wahudumu wa afya waliokuwa wakisubiri hadi siku 15 kupata malipo sasa wanapokea pesa ndani ya saa 72 pekee, shukrani kwa mfumo mpya wa malipo ya kidijitali uliotolewa na Shirika la Sfya la Umoja wa Mataifa WHO na Wizara ya Afya ya nchi hiyo. Mfumo huu unapeleka fedha moja kwa moja kwenye pochi za simu za wafanyakazi, ukipunguza ucheleweshaji, gharama na kuongeza motisha. Wafanyakazi zaidi ya 120,000 sasa wanafaidika, kuboresha ufanisi wa kampeni za chanjo na juhudi za kudhibiti polio.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    16 min
  • UNMISS yasaidia katika utoaji wa elimu ya uraia nchini Sudan Kusini
    Kuanzia furaha ya uhuru hadi maumivu ya kurejea kwa mzozo, safari ya amani ya kudumu Sudan Kusini imekuwa ndefu na bado inaendelea. Licha ya changamoto hizo, matumaini bado ni makubwa miongoni mwa jamii nchini kote kwamba uchaguzi wa amani, huru na wa haki utaleta usalama uliotafutwa kwa muda mrefu pamoja na fursa za maendeleo na ukuaji wa uchumi. Leah Mushi anatuletea taarifa ikiangazia namna Sudan Kusini inavyojiandaa na uchaguzi wake mkuu mwakani 2026. 
    4 min
  • 22 OKTOBA 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia mifumo ya tahadhari za mapema dhidi ya majanga, elimu kuhusu uraia nchini Sudan kusini, na kilimo endelevu na vijana nchini Rwanda.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema mifumo ya tahadhari za mapema dhidi ya majanga si chaguo tena, bali ni lazima kwa kila mtu duniani, akisisitiza kuwa hatua hizo zinaokoa maisha na mali.Kuanzia furaha ya uhuru hadi maumivu ya kurejea kwa mzozo, safari ya amani ya kudumu Sudan Kusini imekuwa ndefu na bado inaendelea. Licha ya changamoto hizo, matumaini bado ni makubwa miongoni mwa jamii nchini kote kwamba uchaguzi wa amani, huru na wa haki utaleta usalama uliotafutwa kwa muda mrefu pamoja na fursa za maendeleo na ukuaji wa uchumi.Wanawake ni nguzo muhimu katika maendeleo ya kilimo na jamii za vijijini. Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo( IFAD) inahakikisha zaidi ya asilimia 50 ya washiriki wa miradi yake ni wanawake, kwa lengo la kuimarisha usawa wa kijinsia na kupunguza umaskini. Kupitia mafunzo, huduma za kifedha, na upatikanaji wa masoko, wanawake wanawezeshwa kiuchumi na kijamii. Tafiti zinaonesha kuwa kufuta pengo la kijinsia katika kilimo kunaweza kuongeza pato la dunia kwa asilimia 1. Nchini Rwanda, miradi kama R-YES imewezesha wanawake vijana kuanzisha biashara za kilimo na kutoa ajira.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    12 min
  • IFAD imewasaidia wanawake wakulima Rwanda kupata ajira na kuimarisha maisha
    Wanawake ni nguzo muhimu katika maendeleo ya kilimo na jamii za vijijini. Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo( IFAD) inahakikisha zaidi ya asilimia 50 ya washiriki wa miradi yake ni wanawake, kwa lengo la kuimarisha usawa wa kijinsia na kupunguza umaskini. Kupitia mafunzo, huduma za kifedha, na upatikanaji wa masoko, wanawake wanawezeshwa kiuchumi na kijamii. Tafiti zinaonesha kuwa kufuta pengo la kijinsia katika kilimo kunaweza kuongeza pato la dunia kwa asilimia 1. Nchini Rwanda, miradi kama R-YES imewezesha wanawake vijana kuanzisha biashara za kilimo na kutoa ajira. Sheilah Jepngetich na taarifa zaidi.
    4 min
  • “NG'OMBE WA MNYONGE HAZAI"
    Leo mchambuzi ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "NG'OMBE WA MNYONGE HAZAI"
    1 min
  • 21 OKTOBA 2025
    Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Leah Mushi anakuletea-Gaza Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula Duniani WFP lasema usitishaji wa mapigano umeleta afueni kwa wakaazi kwani sasa misaada inaendelea kuwafikia wenye uhitaji-Naibu Mratibu wa Misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Joyce Msuya amekuwa ziarani Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR na kujionea hali halisi ya wakimbizi, wakimbizi wa ndani na msaada wa kibinadamu-Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa leo limesema katika tathimini yake kuwa ukataji wa misitu umepungua duniani kote ingawa bado kuna shinikizo na hatua zaidi zahitajika-Katika mada kwa kina tunakupeleka nchini Tanzania ambako Vyuo Vikuu vinachukua hatua ya kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs hususan lile namba 17 la ubia kupitia umataifishaji. -Na kwenye jifunze Kiswahili unapata ufafanuzi wa methali " “NG'OMBE WA MNYONGE HAZAI" 
    14 min
  • Askari watoto waachiliwa Sudan Kusini
    Sudan Kusini yaahidi kutotumikisha tena watoto jeshiniHuko nchini Sudan Kusini barani Afrika, matumaini mapya yamechipua baada ya watoto waliokuwa wametumikishwa kwenye jeshi la nchi hiyo, SSPDF kuachiliwa rasmi katika hafla iliyoungwa mkono na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, UNMISS. Tukio hilo limeelezwa kuwa ishara muhimu ya kumaliza utumikishaji wa watoto katika jeshi na kuwapa nafasi ya kujenga maisha mapya. Sabrina Saidi ana taarifa zaidi...(TAARIFA YA SABRINA SAIDI)Nats..Video ya UNMISS inaanzia kwenye tukio la viongozi wakikabidhi vifaa vya shule kwa watoto walioachiliwa kutoka jeshi la serikali.Nats..Ni siku ya matumaini hapa mjini Yambio, jimbo la Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini — siku ambayo watoto waliopoteza utoto wao vitani, sasa wanaupokea tena, wakiwa na ndoto mpya za elimu na maisha bora zaidi.Hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwa ushirikiano kati ya Jeshi la serikali na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo (UNMISS), imeashiria azma ya serikali ya kuondokana na utumikishaji wa watoto jeshini.Brigedia Akech Maker, Kamanda wa Kikosi cha 16 cha SSPDF, anasema ….Clip- Sauti ya Brigedia Akech Maker“Hatutaruhusu watoto kujiunga na jeshi. Watoto wanaoonesha nia, tutawaelekeza kwenye elimu, na taasisi ziwaunge mkono ili wasirudi kambini.”Afisa wa Ulinzi wa Watoto UNMISS,, Rita Bampo, akatoa ahadi akisema watoto lazima warejee kwenye jamii, na kwamba…Clip- Sauti ya Rita Bampo“Tutahakikisha mchakato huu unafanikiwa na hakuna atakayewarudisha kwenye makundi ya kijeshi. Viongozi wote wahakikishe watoto wanapelekwa kwa mashirika yanayohusika."UNICEF pia imetoa huduma za kisaikolojia na vifaa vya kujifunzia kwa watoto hao, kuwasaidia kuanza upya safari yao ya elimu na matumaini.
    2 min
  • Warsha za UNDP Tanzania zaleta matokeo chanya
    Matunda ya warsha zilizokuwa zinaendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la  Mpango wa Maendeleo, (UNDP) nchini Tanzania katika mikoa ya Tanga na Mtwara iliyoko kando mwa baharí ya Hindi kuhusu uchumi rejeshi yameanza kuonekana na mipango zaidi inafanyika ili matunda hayo yasambae mikoa mingine.Afisa wa UNDP Peter Nyanda ameiambia Idhaa ya Umoja wa Mataifa hivi karibuni kuwa warsha hizo mbili zilizofanyika mwaka huu na kujumuisha vikundi vya kijamii na mamlaka za serikali za mitaa katika mikoa husika zililenga pamoja na mambo mengine kuhakikisha taka hasa taka ngumu hazitupwi bali zinarejeshwa katika mzunguko wa thamani kwa njia za ubunifu na endelevu.Nyanda anataja baadhi ya matokeo;(Sauti ya Peter Nyanda 1)“Ni kuwa na mpango wa utekelezaji katika kila mkoa ambao wadau hawa wanajiwekea ili kubainisha hatua za haraka, fursa na namna gani wanaweza kupata uwekezaji. Lakini pia tumeweza kuwatambua wadau katika uchumi rejeshi na pia tumeangalia wabunifu walioko kwenye maeneo ya viwanda. Kwa mfano tu kwa Mtwara tumefahamishwa hapa kwamba kiwanda cha Dangote tayari kinatumia taka katika kuwasha mitambo yake hasa . Lakini pia tunatarajia majadiliano pamoja na wafadhili na wadau wengine wa kimaendeleo hasa sekta binafsi katika kupata rasilimali za kufanya uwekezaji.”Akazungumzia pia matarajio ya baadaye ya UNDP  kupitia warsha hizo akisema,(Sauti ya Peter Nyanda 2)“Ni kuanzisha vituo vya ubunifu na ubora katika ujenzi wa miundombinu, sio UNDP peke yake bali kwa ujumla, kama matarajio ya wadau. Lakini pia kuna wabunifu kama kuanzisha vituo vya kutenganisha taka. Lakini kufanikisha ushirikiano kati ya serikali, sekta binafsi na taasisi za kifedha, ambao ni muundo wa utatu tunaojaribu kufanikisha kwa serikali, wadau na UNDP ikiwemo kuweza kuhakikisha mitaji inapatikana ili kuweza kusaidia kukuza biashara hizo. Kingine ni kupanua juhudi katika mikoa mingine sio tu ile ambayo mikoa mingine ya pwani ya sasa tunajua taka hizi za plastiki zinaathiri zaidi maeneo ya baharini.”Na hatimaye,(Sauti ya Peter Nyanda 3)“Ujumbe wangu wa mwisho ni kwamba uchumi rejeshi ni fursa ya kiuchumi, kiteknolojia na kimazingira. Kwa kuwekeza katika kurejesha thamani ya taka, tunalinda mazingira na wakati huo huo tunafungua ajira za ubunifu mpya kwa vijana na jamii yetu.”
    4 min
  • WMO na wadau wajadili kuhusu tahadhari za mapema
    Shirika la Umoja wa Mataifa ka Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani WMO linaongeza kasi ya jitihada za kulinda maisha ya watu dhidi ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Mkutano wake Maalum uliofunguliwa leo mjini Geneva Uswisi, unalenga kuharakisha mpango wa kimataifa wa Tahadhari za Mapema kwa Wote, sambamba na maadhimisho ya miaka 75 ya WMO. Flora Nducha amefuatilia na anafafanua zaidi (TAAFIFA YA FLORA NDUCHA)Asante Leah, kwa mujibu wa WMO idadi ya nchi zenye mifumo ya tahadhari za mapema kwa ajili ya majanga ya tabianchi imeongezeka maradufu katika kipindi cha miaka kumi iliyopita lakini bado mamilioni ya watu hawana ulinzi dhidi yah atua hiyo muhimu.Ndiyo maana shirika hilo limewakutanisha mawaziri na wataalamu kutoka nchi wanachama 193 kuharakisha mpango wa Tahadhari za Mapema kwa Wote, uliozinduliwa mwaka 2022 na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres unatekelezwa kwa vitendo.Katika mkutano huo Celeste Saulo Katibu Mkuu wa WMO amesema “Miaka 75 iliyopita, Shirika la WMO lilianzishwa kutokana na ukweli kwamba hali ya hewa, maji na tabianchi havina mipaka ya kitaifa. Ushirikiano wa kimataifa katika uchunguzi na utabiri ni wa lazima, kwa sababu hakuna nchi inayoweza kufanya hivyo peke yake.”Ripoti mpya ya WMO, iliyopewa jina Tahadhari za Mapema kwa Wote Mtazamo wa Dunia, inaonesha kuwa licha ya maendeleo makubwa katika ubadilishanaji wa takwimu na utabiri wa kidijitali, bado kuna mapengo makubwa, hasa katika nchi maskini na visiwa vidogo vinavyoendelea.Celeste amesisitiza kuwa“Tahadhari za Mapema kwa Wote sasa siyo mpango tena, bali ni nembo ya mshikamano wa dunia. Pamoja, tunaokoa maisha, tunaunda sera, na kuimarisha mnepo.”Takwimu za shirika hilo zinaonesha uzito wa changamoto. Katika miaka 50 iliyopita, WMO inasema majanga yanayohusiana na hali ya hewa na maji yamesababisha vifo vya zaidi ya watu milioni mbili huku asilimia 90 kati yao ni katika nchi zinazoendelea.Na ingawa mataifa 108 sasa yana mifumo ya tahadhari za majanga mchanganyiko, shirika hilo linasema viwango vya vifo bado ni mara sita zaidi katika maeneo yasiyo na mifumo hiyo.WMO inasema teknolojia mpya ikiwemo akili mnemba na matumizi ya takwimu za setilaiti kwa wakati halisi zinabadilisha uwezo wa utabiri, lakini pengo la kidijitali bado linawaacha wengi wakiwa hatarini.“Mafanikio ya Tahadhari za Mapema kwa Wote hayapimwi kwa ripoti au maazimio, anasema Celesto bali kwa maisha yanayookolewa na riziki zinazolindwa. Tunapoelekea mwaka 2027, hebu tuongeze juhudi kuhakikisha hakuna mtu anayeachwa bila ulinzi.”Mkutano huo Maalum wa WMO utaendelea wiki nzima mjini Geneva, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akitarajiwa kuhutubia siku ya Jumatano.Shirika la WMO wakati likiadhimisha miaka 75 ya kile linachoita Sayansi kwa Vitendo  linataka kuhakikisha sayansi hiyo inawafikia wote, kabla ya majanga kutokea.
    4 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners