Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Chaguo Langu Haki Yangu: Kuwezesha wanawake na wasichana nchini Tanzania - UNFPA
    Mpango wa “Chaguo Langu, Haki Yangu” nchini Tanzania ni jitihada thabiti zinazolenga kuwawezesha wanawake na wasichana kuishi maisha huru dhidi ya ukatili na vitendo hatarishi. Kwa ufadhili wa Serikali ya Finland, Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la IPS, linafanya mabadiliko halisi katika jamii. Sheilah Jepngetich anafafanua zaidi.
    3 min
  • 31 OKTOBA 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya Kimataifa ya Majiji, vifo na majeruhi vilivyotokea katika maandamano yanayohusiana na uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Tanzania na uwezeshaji wa wanawake nchini huko huko Tanzania.Dunia leo ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Majiji, majiji ya kisasa pamoja na kukumbatia teknolojia yametakiwa kuhakikisha yanazingatia zaidi watu ili wengine wasiachwe nyuma au kutengwa na maendeleo hayo.Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu imeeleza wasiwasi mkubwa kufuatia vifo na majeruhi vilivyotokea katika maandamano yanayohusiana na uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Tanzania tarehe 29 mwezi huu wa Oktoba.Mpango wa “Chaguo Langu, Haki Yangu” nchini Tanzania ni jitihada thabiti zinazolenga kuwawezesha wanawake na wasichana kuishi maisha huru dhidi ya ukatili na vitendo hatarishi. Kwa ufadhili wa Serikali ya Finland, Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la IPS, linafanya mabadiliko halisi katika jamii.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    10 min
  • 30 OKTOBA 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo Bi. Lucy Githinji, mkazi wa jimbo la New Jersey nchini Marekani amezungumza na idhaa hii baada ya matembezi ya hiari kwa ajili ya kuhamasisha jamii kuhusu saratani ya titi, akisema hakika dawa zinafanya kazi.Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Kibinadamu nchini Sudan, Denise Brown amesema ni kweli wamepokea ripoti za mauaji ya baadhi ya wahudumu wa kujitolea huko El Fasher jimboni Darfur wakati huu ambapo mji huo umetwaliwa na wapiganaji wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka, (RSF).Kimbunga Melissa kimepungua nguvu baada ya kutua nchini Jamaica kama kimbunga cha kiwango cha 5, na kuvunja rekodi ya kimbunga chenye nguvu zaidi, kabla ya kuelekea kaskazini mashariki kupita Cuba hadi Bahamas, na kusababisha mafuriko makubwa, uharibifu na kukatika kwa umeme katika maeneo mbalimbali ya Karibea na Amerika ya Kati.Nchini Cameroon, kufuatia mauaji ya raia wakati wa maandamano ya kupinga kutangazwa kwa Paul Biya kuwa mshindi wa kiti cha Urais kwenye uchaguzi uliofanyika Oktoba 12, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu imeeleza wasiwasi wake juu ya ripoti za vifo hivyo.Na katika Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo,  mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "SUMIA."Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    12 min
  • Hali si hali huko El Fasher nchini Sudan, watoto 'walipa gharama' zaidi
    Ghasia zinazoendelea kwa kasi zinawakwamisha zaidi watoto katikati ya mashambulizi ya mabomu yasiyokoma, mapigano makali, na uhaba mkubwa wa chakula, maji salama na dawa kwa zaidi ya siku 500 sasa.“Hakuna mtoto aliye salama,” anasema Catherine Russell, Mkurugenzi Mtendaji wa Shrika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF kupitia taarifa iliyotolewa na makao makuu ya shirika hilo jijini New York, Marekani leo.Taarifa hiyo pia inamnukuu Catherine Russell akisema, “ingawa athari kamili bado haijulikani kutokana na kukatika kwa mawasiliano kote nchini Sudan, inakadiriwa kuwa watoto wapatao 130,000 huko Al Fasher wako katika hatari kubwa ya kukiukwa haki zao, huku kukiripotiwa visa vya utekaji nyara, mauaji na ukataji viungo vya mwili, pamoja na ukatili wa kingono.”Pia kuna taarifa za wafanyakazi wa mashirika ya kibinadamu kukamatwa au kuuawa.UNICEF inatoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano, kuhakikisha upatikanaji salama na usiokatizwa wa misaada ya kibinadamu, ulinzi wa raia hasa watoto, na kupatiwa uhakika wa njia salama kwa familia zinazotafuta hifadhi, kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kibinadamu. Wale wanaohusika na ukiukaji lazima wawajibishwe.Wakati huohuo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limethibitisha kwamba Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imewataarifu kuwa viongozi  wawili wa juu wa WFP nchini  wametangazwa kuwa watu wasiotakiwa nchini Sudan na hivyo wameamriwa kuondoka nchini humo ndani ya saa 72, bila maelezo yoyote.WFP inaeleza kwamba uamuzi huu wa kuwafukuza Mkurugenzi wa WFP nchini Sudan na Mratibu wa Dharura wa WFP nchini humo unakuja katika kipindi muhimu kwani mahitaji ya kibinadamu nchini Sudan hayajawahi kuwa makubwa zaidi kama kipindi hiki, huku zaidi ya watu milioni 24 wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na jamii zikikumbwa na baa la njaa.Wakati ambapo WFP na washirika wake wanapaswa kupanua wigo wa msaada, uamuzi huu unalazimisha shirika kubadilisha uongozi bila mpango, jambo linalohatarisha shughuli zinazowaunga mkono mamilioni ya Wasudani walio hatarini kukumbwa na njaa kali, utapiamlo, na hata kifo kutokana na njaa.WFP na maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa wanaendelea kuzungumza na mamlaka za Sudan kupinga hatua hii na kutaka ufafanuzi wa uamuzi huo.Tags: Sudan, El Fasher, WFP, UNICEF
    3 min
  • Wagonjwa wanaohitaji tiba zaidi Gaza wasafirishwa kupata tiba zaidi Afrika Kusini na kwingineko
    Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO, limeongoza uhamishwaji wa wagonjwa kutoka Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, ikiwa ni  mara ya kwanza tangu kuanza kwa awamu mpya ya kusitishwa kwa mapigano kwenye  ukanda huo.Katika muda wa siku mbili, wagonjwa 41 waliokuwa katika hali mbaya pamoja na familia zao 145 wamehamishwa kutoka eneo la mgogoro, kuelekea Afrika Kusini, Uswisi na kwingineko, huku maelfu zaidi wakiendelea kusubiri matibabu ya dharura.Katika hospital iliyojengwa kwa mahema  katika eneo la AL-MAWASI, RAFAH kwenye Ukanda wa Gaza wagonjwa wakihudumiwa kila kona watoto kwa wakubwa Miongoni mwao ni Ibrahim Abu Ashiba, mkurugenzi wa filamu ambaye maisha yake yamebadilika ghafla. Anakumbuka wakati alipojeruhiwa. Anasema, "Nilipigwa risasi mara kadhaa, mara moja kwenye kifua, mara moja kwenye bega, mara mbili mkononi. Risasi hizo mbili zilikata mishipa ya neva ya mkono wangu. Sasa siwezi kushika kamera wala kunyoosha mkono wangu kawaida. Ghafla, maisha yangu yote yalisimama."Safari ya kupona kwa Ibrahim inaanzia Afrika Kusini, ambapo amekubaliwa kwenda kupokea matibabu maalum ambapo anasema "Maisha yangu yote yalikuwa yamesimama baada ya kujeruhiwa hadi waliponipigia simu na kunijulishakwamba nitasafiri kwenda Afrika Kusini kwa matibabu. Ilionekana kama nimezaliwa upya."Mgonjwa mwingine katika hospitali hii ni, Maria Al-Shaer, alijeruhiwa vibaya katika mashambulizi yaliyokuwa yakiendelea Gaza, huku akipoteza ndugu zake. Mama yake, Raghda Ahmed Al Shaer, anaelezea mateso hayo. "Maria amepoteza baba yake na ndugu zake wote. Alijeruhiwa na kuvunjika mguu, mifupa na kupoteza nyama. Anahitaji upasuaji wa kuwekewa viungo bandia. Maisha yake yamegeuka, hawezi kutembea, na hali yake ya kisaikolojia imeathirika sana."Uhamishwaji huu umeratibiwa na Shirikisho la Chama cha Msalaba Mwekundu Palestina, kwa msaada wa WHO. Dkt. Luca Pigozzi, Mratibu wa Timu ya Dharura ya WHO, anafafanua umuhimu wake."Huu ni uhamishaji wa kwanza wa matibabu tangu kusitishwa kwa mapigano Oktoba 10. Tumejizatiti kuongeza uwezo wetu kusaidia na kuratibu uhamishaji kwa ajili ya matibabu, kwa ushirikiano wa karibu na Shirikisho la chama cha Msalaba Mwekundu la Palestina."Raghda anaeleza matumaini kwa ajili ya binti yake wanapohama kwenda Uswisi. "Wametupigia kutuarifu kwamba Maria amekubaliwa kusafiri kwenda Uswisi kwa matibabu. Tumefurahi sana kwamba atatembea tena, na hali yake ya kisaikolojia itaboreka. Atarudi kuwa Maria wa kawaida kama tuliyemjua."WHO inasisitiza kuwa wagonjwa takriban 15,000 bado wanangojea idhini ya kupata matibabu nje ya Gaza na inatoa wito kwa nchi zote kufungua milango yote za dharura kwa ajili ya uokoaji wa wagonjwa.
    4 min
  • Kimbunga Jamaica, Katibu Mkuu wa UN azungumza
    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonesha wasiwasi mkubwa wakati huu Kimbunga Melissa kikiwa miongoni mwa vimbunga vyenye nguvu zaidi kuwahi kurekodiwa katika Bahari ya Atlantiki kinaendelea kusababisha uharibifu mkubwa katika eneo la Karibea.Kupitia taarifa yake iliyotolewa leo mjini New York Marekani na msemaji wake, Katibu Mkuu amesema kimbunga hicho kimeacha madhara makubwa nchini Jamaica, Cuba na Bahamas  huku mafuriko makubwa yakiripotiwa pia nchini Haiti na Jamhuri ya Dominika.Taarifa hiyo imemnukuu Katibu  Mkuu wa Umoja wa Mataifa  kwamba “ana wasiwasi mkubwa” na anashikamana na serikali pamoja na wananchi walioathiriwa vibaya na Kimbunga Melissa.”Katibu Mkuu pia “Amewapa pole familia zote za waliopoteza wapendwa wao katika kimbunga hicho na anawatakia majeruhi wote ahueni ya haraka.”Umoja wa Mataifa umeanza kutoa msaada wa dharura, huku timu zake zikiwa tayari mashinani kusaidia kutathmini madhara na kusaidia juhudi za kitaifa. Pia, umetoa dola milioni nne kwa Haiti na vile vile dola milione nne kwa Cuba kutoka Mfuko wake wa Dharura (CERF) ili kusaidia jamii kujiandaa na kupunguza madhara ya kimbunga hicho.Taarifa hiyo imesema Umoja wa Mataifa uko tayari “kutuma wahudumu wa ziada kwa muda mfupi na kuzindua maombi ya misaada ya dharura kukabiliana na mahitaji ya kibinadamu yatakayosababishwa na kimbunga hicho.”Kimbunga Melissa ni miongoni mwa vimbunga vyenye nguvu zaidi kuwahi kuikumba Karibea, na kinatishia maisha ya mamilioni ya watu kutokana na mafuriko, uharibifu na watu kufurushwa katika makazi yao.
    2 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners