Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 14 MEI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia haki za wanawake na wasichana nchini Sudan na hali ya kina mama na wanawake wajawazitio katika ukanda wa Gaza. Makala tukwenda nchini Burundi na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Wataalamu huru wa haki za binadamu, leo Mei 14 wamekemea vikali ukiukwaji mkubwa na wa kimfumo dhidi ya wanawake na wasichana nchini Sudan ukiwemo ukatili wa kingono unaohusiana na vita, utekaji nyara, na mauaji, ambayo mengi yameripotiwa kufanywa na kundi la kijeshi la Rapid Support Forces (RSF).Huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli, wanawake na wasichana wakiwemo wanawake wajawazito na wale waliojifungua, wamelazimika kukimbia makazi yao na wanaishi katika mazingira hatarishi bila huduma za msingi za kiafya. Sharon Jebichii anaangazia simulizi ya mama mmoja, mkazi wa kambi ya wakimbizi ya Jabalia, Kaskazini mwa Gaza, ambaye alijifungua akiwa amekimbia vita,na sasa anahangaika kumtunza binti yake mchanga.Katika makala Assumpta Massoi kwa makala hiyo na zaidi ya yote shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi nchini Burundi kwa kuiandaa na kuhakikisha wakimbizi wanapata usaidizi.Na mashinani, fursa ni yake Juliana Sanga, mama kutoka Mkoa wa Njombe nchini Tanzania ambaye ni mnufaika wa mafunzo ya lishe bora kwa ajili ya kupunguza udumavu kwa watoto inayofanikishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF Tanzania. Yeye anaeleza kile anachoondoka nacho.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
    11 min
  • Akina mama wakimbizi katika ukanda wa Gaza wanataabika bila huduma za afya
    Huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli, wanawake na wasichana wakiwemo wanawake wajawazito na wale waliojifungua, wamelazimika kukimbia makazi yao na wanaishi katika mazingira hatarishi bila huduma za msingi za kiafya. Sharon Jebichii anaangazia simulizi ya mama mmoja, mkazi wa kambi ya wakimbizi ya Jabalia, Kaskazini mwa Gaza, ambaye alijifungua akiwa amekimbia vita,na sasa anahangaika kumtunza binti yake mchanga.
    3 min
  • 13 MEI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika lengo namba moja la Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDG1 la kutokomeza umaskini na inatupeleka nchini Tanzania ambako Umoja wa Mataifa umeona bora kusaidia wafugaji kuku kuondokana na umaskini.Katika mkutano wa ngazi ya mawaziri kuhusu mustakabali wa ulinzi wa amani unaofanyika leo mjini  Berlin Ujerumani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameeleza vipaumbele vitatu vya msingi katika mageuzi ya ulinzi wa amani kwa muktadha wa dunia inayobadilika kwa kasi.Mashariki ya Kati leo shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limeonya kuhusu vifo vya watoto kutokana na utapiamlo Gaza, sababu kubwa ikiwa ni kuendelea kukosekana kwa msaada wa kibinadamu unaojumuisha lishe maalum kwa watoto.Wakati mahitaji ya kibinadamu yakizidi kuongezeka duniani watu milioni 308 katika nchi 73 wakihitaji msaada wa dharura , Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women limeonya kuwa wanawake na wasichana ndio wanaoathirika zaidi wa migogoro, wakikumbwa na utapiamlo, vifo vinavyoweza kuzuilika vinavyohusiana na ujauzito, na ukatili wa kingono kwa kiwango cha juu, huku mfumo wa misaada ya kibinadamu ukikumbwa na ukata wa fedha.Na katika mashinani, fursa ni yake Jean Todt, Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu usalama barabarani akieleza ni jambo gani lifanyike kuhakikisha usalama barabarani wakati huu dunia inaadhimisha Wiki ya Usalama Barabarani maudhui yakijikita kwenye kuhakikisha barabara ni salama kwa ajili ya waenda kwa miguu na waendesha baiskeli.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    12 min
  • Bi. Joy :Teknolojia inatatua changamoto za kijamii - Wasichana katika TEHAMA
    Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano TEHAMA, au ICT inaendelea kutawala na kuunda fursa mpya, lakini wanawake bado wanakumbana na changamoto kubwa ya upungufu wa uwakilishi. Hata hivyo, wanawake wanavuka mipaka na sasa Bi. Joy, msichana kutoka Nairobi Kenya, ambaye ni mtaalamu katika teknolojia ya kidijitali, amekalia nafasi muhimu katika kubadili mtindo wa maisha kupitia elimu ya ICT. Katika mahojiano na washirika wetu Radio Domus, alizungumzia umuhimu wa kuhamasisha wasichana kujiunga na masomo ya teknolojia ili kutengeneza mustakabali mpya wa kidijitali, na kubadili dunia kwa njia ya kidigitali na usawa. Sharon Jebichii na Makala zaidi
    4 min
  • 12 MEI 2025
    Hali mbaya ya hewa na mabadiliko ya tabianchi vyaliacha hoi bara la Afrika yaonya WMO.WHO yahaha kukabiliana na kipindupindu Angola.Makala Sharon Jebichii anatupeleka nchini Kenya, kumulika masuala ya wasichana katika ICT.Mashinani leo inaangazia ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa wiki ya usalama barababarni.
    12 min
  • WHO na vita dhidi ya kipundupindu Angola.
    Tangu Januari mwaka huu 2025 nchini Angola, ugonjwa wa kipindupindu umesambaa katika majimbo 17 kati ya 21 ya nchi hiyo. Mlipuko huu tayari umesababisha karibu vifo 600 linaeleza Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO. António Catunda, ni Msimamizi wa Uhamasishaji wa Afya katika kituo cha afya cha Sambizanga jimboni Luanda unakopatikana mji Mkuu wa Angola. Kupitia video iliyoandaliwa na WHO, anaielezea hali ilivyo.
    3 min
  • Chokoleti itengenezwayo Uganda yavuka mpaka na mabara -UNCTAD
    Kutoka kakao ghafi huko Bundibugyo, magharibi mwa Uganda hadi Kampala mji mkuu wa kibiashara wa taifa hilo la Afrika Mashariki ndiko kunapatikana kiwanda cha kutengeneza chokoleti cha Equator kinachomilikiwa na Barbara Gonget na mume wake Gustav. Awali wazo la biashara hii lilionekana kutokuwa na mashiko. Ingawa hivyo baada ya ITC, ambacho ni Kituo cha Kimataifa ha Biashara kilicho chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo, UNCTAD pamoja na wadau wao kuweka usaidizi wao, hali imebadilika na sasa biashara inavuka sio tu mipaka bali mabara. Wawili hao Kwa kuchanganya mbinu za hali ya juu, zinazojali jamii, na ufundi wa kitaalamu, wanabadili taswira ya uzalishaji wa chokoleti nchini humo.Je wamefanya nini? Assumpta Massoi anafafanua zaidi kwenye makala hii iliyofanikishwa na ITC.
    4 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners