Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 23 MEI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia haki za kibinadamu za raia nchini Uganda, na simulizi ya mkimbizi nchini Mexico ambaye alikimbia machafuko nchini mwake Haiti. Makala tunakwenda nchini Kenya na mashinani nchini Ethiopia, kulikoni?Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa , Volker Türk, leo Ijumaa mjini Geneva, Uswisi kupitia msemaji wake ameelezea wasiwasi wake kuhusu kupitishwa kwa muswada uliopendekezwa na Bunge la Uganda unaoruhusu raia kuhukumiwa katika mahakama za kijeshi.Wakati raia wa Haiti Giovanni Rotschild alipowasili Mexico mwaka 2022 baada ya safari ndefu isiyo na uhakika kutoka nchi mwake kulikosheheni ghasia, hakufahamu mtu yeyote wala hakuzungumza kabisa lugha ya kispanyola. Lakinialipata msaada kumwezesha kujenga upya maisha na kupata jamii mpya.Makala tukielekea siku ya kandanda, kabumbu au mpira wa miguu duniani itakayoadhimishwa Jumapili wiki hii Mei 25 ikibeba maudhui nguvu ya kdandanda katika kuleta mabadiliko tuabisha hodi Nairobi Kenya ambapo leo Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Global Youth Forum linalounganisha vijana Kenya kwa lengo la kutokomeza umasikini na kuishi maisha bora kupitia michezo mbalimbali ikiwemo kandanda akizungumza na Idhaa hii ya Kiswahili anaeleza umuhimu wa kandanda katika ajenda ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu.Na katika mashinani, fursa ni yake Hola msichana mwenye umri wa miaka 15 kutoka wilaya ya Sire nchini  Ethiopia ambaye  kutokana na mafunzo ya stadi za maisha ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF yanayoungwa mkono na asasi ya kupinga ndoa za utotoni ya GPChild Marriage ameweza kuepuka ndoa za utotoni na sasa anatumia mafunzo hayo kutahadharisha na kulinda wenzake.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    10 min
  • Mkimbizi wa Haiti aliyepata faraja na matumaini nchini Mexico
    Wakati raia wa Haiti Giovanni Rotschild alipowasili Mexico mwaka 2022 baada ya safari ndefu isiyo na uhakika kutoka nchi mwake kulikosheheni ghasia, hakufahamu mtu yeyote wala hakuzungumza kabisa lugha ya kispanyola. Lakini msaada alipata msaada kumwezesha kujenga upya maisha na kupata jamii mpya. Flora Nducha na maelezo zaidi.
    3 min
  • 22 MEI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini kumsikia mgeni wetu Prof. Wallah Bin Wallah, mwandishi mashuhuri wa vitabu vya Kiswahili kutoka Kenya ambaye anamulika umuhimu wa vitabu katika kukuza lugha ya Kiswahili. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno.Kwa mara ya kwanza tangu mwezi Februari, msaada wa kuokoa maisha umefika Gaza. Baada ya wiki 11 za kizuizi kutoka kwa mamlaka za Israeli, malori 198 yaliyobeba chakula, dawa na unga wa ngano yameingia leo kupitia mpaka wa Kerem Shalom kwa mujibu wa mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa.Mratibu mkuu wa misaada wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, ameiitaja hatua hiyo kuwa ya muhimu sana, huku malori 90 yakipakuliwa usiku kwa ajili ya kusambazwa haraka.Mwaka 2024, vita havikuishia kwenye uwanja wa mapambano pekee      vilivunja nyumba, masoko na shule. Kuanzia Gaza hadi Ukraine, Sudan hadi Myanmar na zaidi ya raia 36,000 walipoteza maisha yao katika mizozo 14 ya kivita kulimgana na ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwa Baraza la Usalama hii leo linalojadili ulinzi wa raia katika mizozo ya silaha.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "DAHARI”Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • Mapambano dhidi ya ndoa za kulazimishwa - Fatou Cissé
    Wakati ulimwengu ukiendelea kupaza sauti dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia, tunaelekea nchini Mali, ambako Fatou Cissé, mkurugenzi wa filamu na mwanzilishi wa filamu iitwayo FURU, anatumia sanaa kuangazia suala zito la ndoa za kulazimishwa. Kupitia video maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa, tunapata simulizi hiyo inayohusu wasichana wawili waliokumbwa na changamoto hizi. Fatou anawapa wasichana wa Kiafrika sauti na jukwaa la kuzungumza hadharani kuhusu dhuluma wanazokumbana nazo. Sharon Jebichii anasimulia.
    4 min
  • 21 MEI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na mradi wa kutengeneza barabara katika kaunti ya Meru nchini Kenya. Makala tunaangazia simulizi ya mkurugenzi na mwanzilishi wa filamu iitwayo FURU, na mashinani tunakwenda Tanzania.Wafanyakazi wa misaada wa Umoja wa Mataifa leo wamesema kwamba bado wanangoja kibali kutoka kwa Israel ili kusambaza msaada wa kuokoa maisha ulioruhusiwa kuingia Gaza mwanzoni mwa wiki ambapo  malori matano yalifanikiwa kuingia baada ya vikwazo kwa wiki 11.Nchini Kenya, katika kaunti ya Meru hatua rahisi iliyochukuliwa inaleta mabadiliko makubwa na dhahiri kwani maeneo ambako awali barabara zilikuwa hazipitiki na hakuna mawasiliano, ubunifu wa kijapani umerejesha matumaini.Katika makala wakati ulimwengu ukiendelea kupaza sauti dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia, tunaelekea nchini Mali, ambako Fatou Cissé, mkurugenzi wa filamu na mwanzilishi wa filamu iitwayo FURU, anatumia sanaa kuangazia suala zito la ndoa za kulazimishwa.Na mashinani, fursa ni yake Ruth Nkurlu, Mtaalamu wa lishe kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF Tanzania, ambaye anatoa mafunzo ya lishe bora kwa watoto Mkoani Njombe kwa ajili ya kupunguza udumavu wakati wa ukuaji wa mtoto.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • 20 MEI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika wafugaji wa nyuki nchini Tanzania leo ikiwa ni siku ya nyuki duniani iliyopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 20 Desemba mwaka 2017 kupitia azimio namba A/72/211.Baada ya miaka mitatu ya majadiliano, leo katika Mkutano wa Kimataifa wa Afya unaoendelea Geneva, Uswisi, nchi zimepitisha rasmi makubaliano ya kihistoria ya kuzuia, kujiandaa, na kukabiliana vyema na majanga ya magonjwa kwa siku zijazo. Taratibu zote zitakapopitishwa na angalau nchi 60, mkataba utaanza kutumika rasmi mwakani.Kutokana na mamlaka za Israeli kulegeza kwa muda mzingiro uliodumu kwa wiki 11, angalau sasa matumaini kidogo yamerejea Gaza, yameeleza leo mashirika ya Umoja wa Mataifa. Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya dharura, OCHA, Jens Laerke amesema tayari wamepata ruhusa ya kuyavusha malori matano yaliyokuwa yamezuiliwa jana.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP limetahadharisha  leo kwamba bila ufadhili zaidi, huenda katika muda wa wiki chache zijazo likalazimika kusitisha msaada wa chakula kwa takribani nusu ya watu linaowahudumia kwa sasa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.Na katika mashinani, fursa ni yake Hanan Al-Dayya, Mkimbizi wa ndani katika ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli, akisimulia  madhara ya mashambulizi yanayoendelea kutoka Israeli.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
    13 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners