Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Kuelekea Mkutano wa Bahari UNOC3, UNEP yatoa wito wa hatua za kukabili taka za plastiki
    Katika kuelekea Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari UNOC3, utakaofanyika mjini Nice, Ufaransa kuanzia tarehe 9 hadi 13 Juni 2025, Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP nchini Tanzania imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka na madhubuti kukabiliana na changamoto ya uchafuzi wa bahari, hasa wa taka za plastiki. Akizungumza na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini humo UNIC jijini Dar es Salaam, Clara Makenya, Mkuu wa Ofisi ya UNEP nchini Tanzania na Afisa Mawasiliano wa shirika hilo kwa Namibia, alisisitiza umuhimu wa kushughulikia kwa haraka tatizo la taka za plastiki ambazo nyingi hutokea nchi kavu na kuishia baharini.
    4 min
  • 03 JUNI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kinainayomulika kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi katika kaunti kama Kajiado, Kenya, ambayo jamii hukumbwa na hali ya ukame na mazingira magumu, mabadiliko chanya yanaonekana.Mustakabali wa mzingiro wa Israeli kwenye eneo la Palestina la Gaza inalokalia kimabavu ukiendelea kukumbwa na sintofahamu, wanawake na wasichana wamesimulia adha ya ukosefu taulo za kike wakati wanapokuwa kwenye hedhi huku upatikanaji wa maji ukiwa ni wa taabu.Idadi ya wakazi wa nchi zenye maendeleo duni, LDCs na zile za visiwa vidogo, SIDS  wanaopata huduma zilizoboreshwa au za kisasa za maonyo ya mapema kabla ya majanga imefikia takribani milioni 400 na hii ni kutokana na programu ya CREWS iliyoanzishwa mwaka 2015 na shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, WMO.Rebecca Kalonji, al maaruf Sista Becky, mwimbaji chipukizi wa mtindo wa kufokafoka kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hii leo ametangazwa kuwa Muungano Mkono wa Ngazi ya Juu wa masuala ya lishe na ulaji wenye afya wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP katika taifa hilo la Maziwa Makuu. Watu milioni 28 wakikabiliwa na njaa kali nchini mwake, Sista Becky amesema atatumia sauti na kazi yake kupatia vijana changamoto ya sio tu kupaza sauti zao bali pia kuchukua hatua kwenye masuala nyeti yanayogusa mustakabali wao ikiwemo kupata lishe bora na fursa bora kwa wanawake na Watoto wa kike.Na katika mashinani fursa ni yake Christiana, mama wa watoto sita ambaye ni mwathirika wa mashambulizi ya hivi majuzi ya waasi wenye silaha katika wilaya za Mirebalais na Saut-d'Eau yaliyosababisha watu wengi kuyahama makazi yao. Anasema ana matumaini kwani Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto, UNICEF limewapelekea huduma za afya kupitia kniki tembezi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    11 min
  • Shirika la kiraia lawezesha vijana wa kike kujiajiri badala ya kutumbukia kwenye umaskini
    Nchini Tanzania ugumu wa maisha na kukabiliwa na vishawishi, umewapa fikra mpya vijana wa kike mkoani Morogoro, mashariki mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ambao sasa wanajimudu kiuchumi,  kwa kuanzisha biashara na shughuli za ujasiriamali. Wanasongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs hususan namba 8 la ajira zenye staha, nan amba 1 la kutokomeza umaskini. Hamad Rashid wa Redio washirika Tanzania Kids Time FM amewatembelea vijana hao na kuandaa makala hii.
    4 min
  • 02 JUNI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia haki za kibidamu katika ukanda wa Gaza, na hali ya misaada ya kibinadamu huko huko Gaza. Makala yunakwenda nchini Tanzania kusikia harakati za kusaidia vijana wa kike, na mashinani tunakupeleka nchini Uganda kusikia kuhusu mradi wa mlo shuleni.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameeleza kughadhabishwa kufuatia kusambuliwa, kujeruhiwa na kuuawa kwa Wapalestina walipokuwa wakijaribu kupata msaada wa kibinadamu huko Gaza jana Jumapili, Juni Mosi.Maisha ya raia wa Gaza ambao karibu wote ni wakimbizi wa ndani yanazidi kuwa mtihani usio na majawabu kila uchao kwa mujibu wa mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa. Mateso wanayopitia nis awa na kuishi jrehanamu, wengi wamekata tamaa na wanaona bora kufa kuliko kuishi katika hali hiyo. Flora Nducha akusimulia madhila ya mmoja wa wakimbizi hao wa ndani Moamen Abu Asr na mkewe Zeinat..  Makala inakupeleka nchini Tanzania kusikia harakati za kunasua vijana wa kike kutoka vishawishi vinavyoweza kuwatumbukiza kwenye lindi la umaskini. Msimulizi wako ni Hamad Rashid wa Radio washirika Tanzania Kids Time FM.Na katika Moses Okiror, Naibu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Rainbow iliyoko Karamoja kaskazini-masharikimwa Uganda anaeleza jinsi Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula (WFP) limeboresha mpango wa mlo shuleni kwa kuwakabidhi mashine ya kusagisha nafaka aina mbalimbali yenye vinu vinavyotumia nishati ya jua.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    12 min
  • Tumefika mwisho, ni bora kufa kuliko mateso haya: Wakimbizi Gaza
    Maisha ya raia wa Gaza ambao karibu wote ni wakimbizi wa ndani yanazidi kuwa mtihani usio na majawabu kila uchao kwa mujibu wa mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa. Mateso wanayopitia nis awa na kuishi jrehanamu, wengi wamekata tamaa na wanaona bora kufa kuliko kuishi katika hali hiyo. Flora Nducha akusimulia madhila ya mmoja wa wakimbizi hao wa ndani Moamen Abu Asr na mkewe Zeinat. 
    3 min
  • Walinda amani kutoka Tanzania TANZBATT 11 wajivunia kazi zao za kuwaunga mkono raia DRC
    Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC jimboni Kivu Kaskazini katika kitongoji cha Mavivi tunakutana na walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, kikosi cha 11, TANZBATT11, wanaohudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO wakielezea sio tu majukumu yao, bali pia wanajivunia kile wanachofanya kwa kuzingatia Mei 29 imeadhimishwa siku ya kimataifa ya walinda amani. Afisa Habari wa TANZBATT 11 Meja Fadhila Nayopa amefuatilia hadithi zao. 
    3 min
  • Licha ya ukata UNICEF yajitahidi watoto nchini DRC warejee shuleni
    Wakati ghasia zinazoendelea huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC zinaripotiwa kusababisha zaidi ya watoto milioni 1.8 kutokuweko shuleni, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF nchini humo linajitahidi kwa udi na uvumba kuhakikisha watoto wanapata elimu kwani ni haki yao ya msingi. Je ni kwa vipi? Anold Kayanda anasimulia zaidi.
    3 min
  • 30 MEI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya elimu kwa watoto mashariki mwa DRC na Mkutano wa pili wa Baraza Kuu la Makazi la shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani UNHABITAT unaofunga pazia leo jijini Nairobi Kenya. Makala inaturejesha nchini DRC na mashinani inatupeleka katika bonde la Ziwa Victoria, kulikoni?Wakati ghasia zinazoendelea huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC zinaripotiwa kusababisha zaidi ya watoto milioni 1.8 kutokuweko shuleni, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF nchini humo linajitahidi kwa udi na uvumba kuhakikisha watoto wanapata elimu kwani ni haki yao ya msingi.Mkutano wa pili wa siku mbili wa Baraza Kuu la Makazi la shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani UNHABITAT leo unafunga pazia jijini Nairobi Kenya. Baraza hilo linalofanyika kila baada ya miaka minne ni chombo cha juu kabisa duniani cha kufanya maamuzi kuhusu maendeleo ya miji endelevu na limewaleta pamoja wawakilishi kutoka nchi zote 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa pamoja na wadau mbalimbali wa amendeleo ya miji.Makala inakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hususan jimboni Kivu Kaskazini katika kitongoji cha Mavivi kuwasikia walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania,kikosi cha 11, TANZBATT11, wanaohudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO wakielezea sio tu majukumu yao, bali pia wanajivunia kile wanachofanya kwa kuzingatia Mei 29 imeadhimishwa siku ya kimataifa ya walinda amani.Na katika fursa ni yake Mhandisi Coletha Ruhamya, Naibu Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria, Mradi unaofanikishwa na Benki ya Dunia ambao unakabiliana na masuala ya usafi wa mazingira katika ziwa hilo. Anaeleza umuhimu wa usimamizi endelevu wa bonde hilo kote nchini Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners