Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 10 JUNI 2023
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika ukanda wa Gaza, huko mashariki ya Kati kwenye eneo la Palestina lialokaliwa kimabavu na Israeli ambapo vinazidi kuibua changamoto mpya kila uchao.Changamoto ya uzazi duniani si kuhusu watu kukataa kuwa wazazi ni kuhusu kunyimwa fursa ya kuchagua kuwa mzazi imesema ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA iliyotolewa leo na kuonesha kuwa kuwa matatizo ya kiuchumi, ukosefu wa usawa wa kijinsia, na hofu kuhusu maisha ya baadaye vinawazuia mamilioni ya watu kupata familia wanazotamani.Tishio la baa la njaa linaendelea kuiandama Sudan iliyoharibiwa vibaya na vita, limeonya leo Shirika laUmoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP, likitoa wito wa dharura kwa jamii ya kimataifa kusaidia kukidhi mahitaji yanayoongezeka na kuzuia maafa zaidi ya kibinadamu.Kwa mara ya kwanza dunia inaadhimisha siku ya kimataifa ya Mazungumzo baina ya Ustaarabu tofauti yenye lengo la kuchagiza amani, maelewano na mshikamano katika ulimwengu wa sasa uliogubikwa na chuki na mizozo.Na katika mashinani fursa ni yake Maria “Mãezinha” Sábado de Horta Fidalgo, Rais wa Ushirika wa wavuvi wadogo wa samaki katika kijiji cha Rincão kilichoko kisiwa cha Santiano nchini Cabo Verde barani Afrika anaelezea jinsi wanakabiliana na uhaba wa samaki kwenye eneo lao, na hii ni kutokana na mradi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs unaotekelezwa na mashirka ya Umoja wa Mataifa.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    11 min
  • UNEP inashirikiana na taifa la Tanzania kupambana na taka za plastiki - Clara Makenya
    Mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataiifa kuhusu Bahari UNOC3 ukiendelea mjini Nice, Ufaranzsa, tunakuletea mahojiano kati ya Nafisa Didi afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania UNIC Dar es salaam na Clara Makenya, Mkuu wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP nchini Tanzania na Afisa Mawasiliano wa shirika hilo kwa Namibia, wakimulika mchango wa UNEP katika kuzisaidia nchi kupambana na taka za plastiki ambayo ni mada kuu ya mkutano wa UNOC3.
    7 min
  • Mustakabali wa bahari u mikononi mwetu sisi tunaoiharibu - UN
    Mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari umeanza leo huko Nice nchini Ufaransa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo António Guterres bila kumung’unya maneno ameelezea bayana jinsi binadamu anavyozidi kuhatarisha ustawi wa bahari lakini akionesha matumaini ya hali bora ya bahari iwapo hatua zitachukuliwa kwa maslahi ya binadamu na viumbe vya baharini. Assumpta Massoi amefuatilia na kuandaa taarifa hii.
    3 min
  • 09 JUNI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia Mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari umeanza leo huko Nice nchini Ufaransa, na masuala ya baharini ikiwa ni pamoja na uvuvi nchini Sao Tome, umuhimu wa kutunza mazingira nchini Kenya na uondoaji wa taka za plastiki Tanzania.Mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari umeanza leo huko Nice nchini Ufaransa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo António Guterres bila kumung’unya maneno ameelezea bayana jinsi binadamu anavyozidi kuhatarisha ustawi wa bahari lakini akionesha matumaini ya hali bora ya bahari iwapo hatua zitachukuliwa kwa maslahi ya binadamu na viumbe vya baharini.Nchini São Tomé na Príncipe, nchi ya visiwa viwili vidogo huko Afrika ya Kati, mpango wa FISH4ACP unaoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO unalenga kusaidia wavuvi na wauzaji samaki hasa wanawake na vijana kuongeza kipato na manufaa ya kijamii kwa njia endelevu huku wakipunguza athari mbaya kwa makazi ya asili na viumbe wa baharini. Paola Afè Do Espiritu Afonso ni miongoni mwa wanawake wanaonufaika.Makala, tunasalia na mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataiifa kuhusu Bahari UNOC3, tunakuletea sehemu ya mwisho ya mahojiano kati ya Nafisa Didi afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania UNIC Dar es salaam na Clara Makenya, Mkuu wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP nchini Tanzania na Afisa Mawasiliano wa shirika hilo kwa Namibia, wakimulika mchango wa UNEP katika kuzisaidia nchi kupambana na taka za plastiki ambayo ni mada kuu ya mkutano wa UNOC3.Na katika mashinani fursa ni yake Kaara Waithaka, Mwanamazingira kutoka kaunti ya Kajiado nchini Kenya ambaye kupitia mahojiano yaliyofanikishwa na washirika wetu Radio Domus anatoa wito kwa vijana kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    12 min
  • São Tomé na Príncipe: Viumbe wa bahari, samaki, ni chanzo cha mapato, kuinua jamii na kuondoa umaskini
    Nchini São Tomé na Príncipe, nchi ya visiwa viwili vidogo huko Afrika ya Kati, mpango wa FISH4ACP unaoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO unalenga kusaidia wavuvi na wauzaji samaki hasa wanawake na vijana kuongeza kipato na manufaa ya kijamii kwa njia endelevu huku wakipunguza athari mbaya kwa makazi ya asili na viumbe wa baharini. Paola Afè Do Espiritu Afonso ni miongoni mwa wanawake wanaonufaika, Sharon Jebichi na maelezo zaidi.
    2 min
  • 05 JUNI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo leo ikiwa ni siku ya mazingira duniani mwaka ikibeba maudhui “Tokomeza taka za Plastiki,” tunakwenda Tanzania kumsikia Clara Makenya, Mkua wa UNEP nchini humo na afisa mawasiliano wa shirika hilo kwa ajili ya Namibia akizungumza kuhusu changamoto ya taka za plastiki Tanzania na nini kifanyike kuzitokomeza.Naanzia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani ambapo leo kumefanyika tukio maalum la kukumbuka na kuenzi watumishi 168 wa Umoja wa Mataifa waliopoteza maisha wakitekeleza majukumu yao ya ulinzi wa amani, haki, na usaidizi, Mishumaa iliwashwa na kisha walitajwa majina yao mmoja baada ya mwingine akiwemo Nats.. mlinda amani wa UN kutoka Tanzania. Wanafamilia walipokea tuzo maalum za kutambua mchango wao.Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya mazingira, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametaka hatua za dharura kutokomeza janga la uchafuzi utokanao na taka za plastiki, akilitaja kama “janga” linaloikaba dunia na kutishia afya ya binadamu, mifumo ya ikolojia, na hali ya hewa. Guterres amesema, kadri plastiki zinavyovunjika na kuwa vipande vidogo vidogo zinaingia kila mahali: kuanziaubongo wa binadamu hadi maziwa ya mama.Huko nchini Tanzania hii leo kwenye Chuo Kikuu Mzumbe mjini Morogoro, kumefanyika kongamano kumulika uhaba wa maji na sera bora zinazoweza kufanikisha upatikanaji wa huduma hiyo, kongamano lililoandaliwa kwa pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP na Muungano wa Ulaya. Dkt. Saida Fundi Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe anasema.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "KIHEREHERE!.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
    12 min
  • 04 JUNI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia haki za jamii za Ogiek nchini Kenya, na masuala ya baharí na tabianchi. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulikoni?Mtaalamu wa UN ataka kusitishwa mara moja kwa uwekaji  mipaka unaotishia haki za Waogiek Kenya. Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa ameitaka Serikali ya Kenya kusitisha mara moja shughuli za uwekaji mipaka katika Msitu wa Mau Mashariki nchini humo, akisema kuwa unakiuka haki za jamii ya asili ya Waogiek na kupuuza maamuzi ya lazima ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR).Mkutano wa siku mbili kuhusu Ubia wa Kimataifa kwa ajili ya dunia endelevu umekunja jamvi huko Hamburg nchini Ujerumani ambako Balozi wa Mabadiliok ya Tabianchi wa Vijana wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Tanzania, Madina Jubilate Kimaro ameshiriki. Akiwa huko Hamburg nimemuuliza Madina ni kipi amejulisha washiriki wenzake kuwa kinapaswa kufanyika ili dunia iwe endelevu?.Makala, katika kuelekea mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari (UNOC3) utakaofanyika  mjini Nice, Ufaransa, kuanzia tarehe 9 hadi 13 Juni 2025 ukijikita na maudhui "Kuharakisha hatua na kuhamasisha wadau wote kuhifadhi na kutumia bahari kwa njia endelevu", tunaelekea nchini Tanzania kwa Clara Makenya Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP nchini humo na afisa mawasiliano wa shirika hilo kwa ajili ya Namibia, akizungumza na kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania UNIC Dar es salaam anaeeleza nini kinapaswa kufanywa na jamii ya kitaifa na kimataifa ili kutekeleza azma ya mkutano huo.Na katika mashinani Debora, mkazi wa Sake jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC, aliyekimbilia mji wa Goma jimboni humo humo kutokana na machafuko sasa amerejea tena Sake ambako wanapatiwa msaada wa chakula kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP. Akisema PAM anamaanisha WFP.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners