Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 19 JUNI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, ikiwa kesho tarehe 20 mwezi Juni ni siku ya kimataifa ya wakimbizi maudhui yakiwa Mshikamano na Wakimbizi, tunakupeleka kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko kaunti ya Turkana, kaskazini-magharibi mwa Kenya.Uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje FDI umeshuka kwa mwaka wa pili mfululizo, ukihatarisha mustakabali wa maendeleo katika nchi zinazoendelea, kwa mujibu wa wa ripoti iliyotolewa leo na kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD. ikionya kuwa pengo la mitaji linaongezeka huku sekta muhimu kama nishati safi na miundombinu zikikosa ufadhili wa muda mrefu.Katika siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili wa kingono kwenye mizozo, Umoja wa Mataifa umetoa onyo kuwa ukatili wa kingono unazidi kutumika kama silaha ya vita huku wanawake na wasichana wakiathirika zaidi. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA "Huu si uharibifu wa bahati mbaya  ni uhalifu wa kivita. Na waathirika lazima wawe kiini cha amani, haki, na urejeshwaji wa maisha."Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa  Duniani (WHO) leo limezindua mwongozo wake wa kwanza wa kimataifa wa kudhibiti ugonjwa wa seli mundu (sickle cell) wakati wa ujauzito, ukilenga kupunguza hatari za maisha kwa mama na mtoto. WHO inasema wanawake wenye ugonjwa huu wana hatari hadi mara 11 zaidi ya kufariki dunia wakati wa ujauzito. Hivyo huduma bora za afya zinaweza kuokoa maisha, lakini visa vya seli mundu vinaongezeka duniani, huku Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ikichangia asilimia 80.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "KIHORO!.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    11 min
  • Guterres: Tuepushe kauli za chuki kwenye ujumbe chanya
    Leo Juni 18 ni siku ya kimataifa ya kupambana na kauli za chuki ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametumia ujumbe wake kwa siku hii kutoa onyo kuhusu hatari zinazoongezeka za chuki mtandaoni, hasa zikichochewa na akili mnemba au (AI) na  na majukwaa ya kidijitali. Flora Nducha na taarifa zaidi.
    2 min
  • Ujumuishaji wazazi wa kiume kwenye malezi ya watoto waleta manufaa kwa jamii
    Katika Kaunti ya Kilifi, iliyoko pwani ya Kenya barani Afrika,  Mpango wa Kuboresha Lishe kwa kupatia jamii Fedha na Elimu ya Afya (NICHE) unasaidia kuwaelimisha wazazi kuhusu umuhimu wa baba na mama kulea watoto wao kwa pamoja, mradi unaotekelezwa na shirika la Umoja wa MAtaifa la kuhudumia watoto, UNICEF. Assumpta Massoi anamulika moja ya familia zilizonufaika.
    3 min
  • 18 JUNI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu Guterres, wa siku ya kimataifa ya kupambana na kauli za chuki na mradi wa lishe bora kwa watoto huko Kilifi Kenya. Makala tunakwenda nchini Rwanda na mashinani nchini Ghana, kulikoni?Leo Juni 18 ni siku ya kimataifa ya kupambana na kauli za chuki ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametumia ujumbe wake kwa siku hii kutoa onyo kuhusu hatari zinazoongezeka za chuki mtandaoni, hasa zikichochewa na akili mnemba au (AI) na  na majukwaa ya kidijitali.Katika Kaunti ya Kilifi, iliyoko pwani ya Kenya barani Afrika, Mpango wa Kuboresha Lishe kwa kupatia jamii Fedha na Elimu ya Afya (NICHE) unasaidia kuwaelimisha wazazi kuhusu umuhimu wa baba na mama kulea watoto wao kwa pamoja, mradi unaotekelezwa na shirika la Umoja wa MAtaifa la kuhudumia watoto, UNICEF.Katika makala shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, kwa kushirikiana na Serikali ya Rwanda, linaendelea kujenga uwezo wa kitaifa katika kuhimiza matumizi ya mbinu rafiki kwa mazingira katika kilimo pamoja na usimamizi salama wa viuatilifu. Hili linafanyika kupitia utekelezaji wa awamu ya tatu ya mradi wa ACP MEAs 3 unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya EU. Mpango huu unalenga kuwawezesha wakulima wadogo kuhamia kwenye mifumo ya kilimo endelevu kimazingira na kuwajengea uwezo wa utekelezaji wa mikataba ya kimataifa ya mazingira.Na katika mashinani leo ikiwa ni siku ya kimataifa Sayansi ya Mapishi au Gastronomia,  fursa ni yake Mpishi Mkuu mashuhuri Fatmata Binta kutoka Sierra Leone, ambaye kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, ya kipindi kiitwacho Mazungumzo ya Jikoni , anapazia sauti matumizi ya vyakula vya kiasili kama njia ya kuepuka kusahaulika kwa vyakula vya kiasili ili hatimaye kuweko na lishe endelevu.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    11 min
  • Mafanikio ya Mradi wa ACP MEAs 3 Rwanda katika kuboresha kilimo endelevu
    Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, kwa kushirikiana na Serikali ya Rwanda, linaendelea kujenga uwezo wa kitaifa katika kuhimiza matumizi ya mbinu rafiki kwa mazingira katika kilimo pamoja na usimamizi salama wa viuatilifu. Hili linafanyika kupitia utekelezaji wa awamu ya tatu ya mradi wa ACP MEAs 3 unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya EU. Mpango huu unalenga kuwawezesha wakulima wadogo kuhamia kwenye mifumo ya kilimo endelevu kimazingira na kuwajengea uwezo wa utekelezaji wa mikataba ya kimataifa ya mazingira. Sharon Jebichii anatupeleka nchini humo kumulika mradi huo..
    4 min
  • Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetunga sera jumuishi zinazotetea haki za watu wenye ulemavu - Abeida Rashid Abdallah
    Mahojiano hayo leo inamulika juhuddi za Serikali ya Mapinzudi ya Zanzibar katika kuwajumuisha watu wenye ulemavu kwenye masuala mbalimbali katika jamii, Abeida Rashid Abdallah Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto ya kisiwani humo hivi karibununi akiwa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kushiriki mkutano wa 69 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW69 alizungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ungana nao
    7 min
  • 17 JUNI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika juhuddi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuwajumuisha watu wenye ulemavu kwenye masuala mbalimbali katika jamii, tukipata ujumbe wa Abeida Rashid Abdallah Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto ya kisiwani humo amabye hivi karibuni alihudhuria mkutano wa CSW69.Watu wa Ukraine hawapaswi kulazimika kujificha kusaka hifadhi kila jua lizamapo, amesema Matthias Schmale, Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Misaada ya Kibinadamu nchini humo, kufuatia mashambulizi ya usiku wa kuamkia leo yaliyofanywa na jeshi la Urusi huko Kyiv, Odesa na miji mingine na kuua raia 12 na kujeruhi wengine zaidi ya 50.Mfumo wa afya wa huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli unazidi kudarimika, ukizidiwa uwezo kutokana na idadi kubwa ya watu waliouawa au kujeruhiwa karibu na maeneo ya usambazaji wa misaada, amesema Afisa wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya, WHO Dkt. Thanon Gargavanis. Akizungumza na waandishi wa habari Geneva, Uswisi kutokea Gaza, Dkt Gargavanis amesema “tuko katika hali mbaya kila siku ya uwezo wetu wa kutoa huduma kikamilifu au kukumbwa na janga kamili.Leo ni Siku ya Kimataifa ya Kupambana na kuenea kwa Jangwa na ukame na mwaka huu 2025 inasisitiza hatua za dharura kurejesha ubora wa ardhi na kusongesha maendeleo endelevu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres katika ujumbe wake ametaka hatua zichukuliwe huku akionya kuwa uharibifu wa ardhi unazidi kuongezeka duniani kote na kugharimu uchumi wa dunia kwa takriban dola bilioni 880 kila mwaka, kiasi kikubwa kuliko uwekezaji unaohitajika kurekebisha hali hiyo.Na katika mashinani leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kupambana na jangwa na ukame inayobeba maudhui Rejesha ardhi, fungua fursa Meja Katja Dorner kutoka Boni kupitia video iyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa Jangwa UNCCD anatoa ujumbe kuhusu matumizi endelevu ya ardhi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • Akili mnemba na watu wenye ulemavu ni moja ya ajenda za COSP18 tutakazozingatia Tazania: Mpanju
    Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa 18 COSP18 wa mkataba wa watu wenye ulemavu CRPD, uliokunja jamvi mwishoni mwa wiki kwenye Makao Mkuu ya Umoja wa Mataifa ulijadili ajenda mbalimbali za kuhakikisha watu wenye ulemavu wanajumuisha, kushirikishwa na kutoachwa nyumba. Amon Anastaz Mpanju Naibu Katibu Mkuu wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum nchini Tanzania alikuwa miongoni mwa washiriki wa mkutano huo na aliketi chini na kuzungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ambaye alitaka kufahamu  ni nini kikubwa anachoondoka nacho kwenye mkutano huo kitakachofanyiwa kazi Tanzania na kuleta tija kwa watu wenye ulemavu.
    3 min
  • 16 JUNI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia baa la njaa katika nchi 13 duniania amabzo hakuna uhakika wa chakula, na hali ya kibinadamu kwa wakimbizi wa DRC. Makala tunasalia hapa makao makuu na mashinani tunakwenda nchini Nepal, kulikoni?Ripoti mpya ya pamoja ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo jijini Roma, Italia inatahadharisha kuwa watu katika nchi 5 kati ya nchi 13 zenye njaa duniani wako kwenye hatari kubwa ya kukumbwa na njaa kali, vifo na maafa ikiwa msaada wa kibinadamu hautatolewa haraka na juhudi za kimataifa hazitaelekezwa kukomesha migogoro, kupunguza ufurushwaji na kuongeza msaada wa haraka kwa kiwango kikubwa.Huko jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, juhudi za kidiplomasia zinaendelea kumaliza mapigano, huko nalo shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP likitoa wito wa msaada kwa watu waliofurushwa makwao kutokana na mashambulizi ya waasi wa M23, msaada ambao utawasaidia kujenga upya maisha yao na njia zao za kujipatia riziki.  Katika makala leo Flora Nducha wa Idhaa hii amemuuliza Amon Anastaz Mpanju, Naibu Katibu Mkuu wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum nchini Tanzania aliyeshiriki mkutano wa 18 wa mkataba wa watu wenye ulemavu COSP18 uliokunja jamvi mwishoni mwa wiki nini kikubwa alichotoka nacho kwenye mkutano huo.Na katika mashinani leo ikiwa ni siku ya Kimataifa ya utumaji fedha kwa familia kutoka ughaibuni, fursa ni yake Bibha kutoka Chinnamastrial nchini Nepal, mnufaika wa utumaji fedha kutoka wanafamilia walioko ughaibuni akielezea jinsi ambavyo fedha hizo zinavyosaidia jamii zake kuondokana na umaskini.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners