Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • UNICEF Kenya - Elimu Jumuishi kupitia michezo: Watoto wenye ulemavu wa kuona wapate nafasi sawa
    Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya ulemavu wa uziwi na kutoona, tunamulika hatua kubwa inayochukuliwa nchini Kenya katika kuhakikisha watoto wenye ulemavu wa kuona wanapata elimu bora na jumuishi. Mafunzo maalum yaliyofanyika jijini Nairobi yalileta pamoja wataalamu, walimu na mashirika ya maendeleo, kwa lengo la kuchochea elimu hiyo kwa njia ya michezo, kwa msaada wa Shirika la LEGO kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Kenya. Sharon Jebichii na makala zaidi.
    4 min
  • 27 JUNI 2025
    Hii leo jaridanitunaangazia msaada wa kibinadamu Gaza, na mauaji yaliyofanyika nchini Rwanda kati ya mwaka 1972 hadi 1973. Makala tunamulika inayochukuliwa nchini Kenya za kutekeleza haki za watu wenye ulemavu wa kutoona, na mashinani tunakwenda DRC, kulikoni?Hatimaye shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO limeweza kufikisha huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, shehena ya kwanza ya vifaa vya matibabu ikiwa ni mara ya kwanza tangu tarehe pili mwezi Machi mwaka huu.Serikali ya Burundi inataka mauaji yaliyofanyika nchini mwake kati ya mwaka 1972 hadi 1973 yatambulike kimattaifa kama ni mauaji ya kimbari dhidi ya Wahutu, je kwa nini wito huo umekuja sasa.Katika makala leo ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya viziwi wasioona, tunamulika hatua kubwa inayochukuliwa nchini Kenya katika kuhakikisha watoto wenye ulemavu wa kuona wanapata elimu bora na jumuishi. Mafunzo maalum yaliyofanyika jijini Nairobi yalileta pamoja wataalamu, walimu na mashirika ya maendeleo, kwa lengo la kuchochea elimu hiyo kwa njia ya michezo, kwa msaada wa Shirika la LEGO kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Kenya.Na mashinani, fursa ni yake Tom Fletcher, Mratibu wa Umoja wa mataifa wa Misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura akihitimisha ziara yake Goma Mashariki mwa DRC amezungumza na waandishi wa habari akieleza kuwa raia wameteseka vya kutosha na ukata unawazidishia madhila”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    10 min
  • 26 JUNI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania, ambako mshikamano na wakimbizi unatekelezwa kwa vitendo na mashirika ya Umoja Mataifa likiwemo lile la Chakula na Kilimo (FAO) na la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kupitia Programu wa Pamoja ya Kigoma (KJP).Katika siku ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya na usafirishaji haramu, ripoti mpya ya dunia ya Dawa za Kulevya mwaka 2025 iliyotolewa leo imeonya kuwa kutokuwepo kwa utulivu duniani kunachochea ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu wa kupangwa. Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa na Uhalifu UNODC, watu milioni 316 walitumia mihadarati mwaka 2023. Mkurugenzi Mtendaji wa UNODC, Ghada Waly, amesema "Makundi haramu yanatumia migogoro kama fursa tunahitaji ushirikiano na uwekezaji kulinda jamii zetu.”Leo ni kumbukizi ya uzinduzi wa Chata ya Umoja wa Mataifa miaka 80 iliyopita mjini San Francisco, hatua iliyoweka msingi wa kuundwa kwa Umoja wa Mataifa mnamo Oktoba 24, 1945. Katibu Mkuu António Guterres anasema Umoja wa Mataifa bado unaakisi matumaini yaliyozaliwa kutoka kwenye majivu ya vita naye mwanahistoria Stephen Schlesinger akizungumza na UN News ameakumbusha kuwa “Chata hii ilikuwa kilio cha wanadamu wakitafuta amani, suluhu za mazungumzo, na maisha bora duniani.”Asilimia 93 ya kaya Gaza hazina uhakika wa maji safi kutokana na ukosefu wa mafuta unaopelekea mifumo ya maji kukaribia kusambaratika yameonya mashirika ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yakiongeza kuwa familia zinakumbwa na njaa kali, wakila mlo mmoja kwa siku huku watu wazima wakikosa kula ili kuwasaidia watoto na wazee.Na leo katika kujifunza lugha ya Kiswahili mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya neno "AFRITI KIJITI”Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    11 min
  • UN80: Umoja wa Mataifa wajitathmini kwa ajili ya karne mpya
    Katika dunia inayokumbwa na migogoro inayoendelea kuongezeka, kupanuka kwa pengo la usawa, na kupungua kwa imani katika taasisi za kimataifa, Umoja wa Mataifa umeanzisha juhudi kabambe za kuboresha namna unavyowahudumia watu kote ulimwenguni. Mpango wa UN80, uliotangazwa mwezi Machi na Katibu Mkuu António Guterres, ni juhudi ya mfumo mzima inayolenga kurahisisha utendaji kazi, kuongeza ufanisi, na kuthibitisha tena umuhimu wa Umoja wa Mataifa katika dunia inayobadilika kwa kasi. Je nini nini kinatarajiwa katika mpango huo wa UN80? Ungana na Flora Nducha katika Makala hii
    4 min
  • Upatikanaji wa nishati duniani umeboreka lakini uwezeshaji kifedha bado unahitajika kupunguza tofauti – Ripoti ya UN
    Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inayofuatilia maendeleo kuelekea kutimiza Lengo la Umoja wa Mataifa la Maendeleo Endelevu namba 7 (SDG 7) linaloangazia nafasi muhimu ya nishati mbadala imetoa wito wa ufadhili zaidi kwani ingawa asilimia 92 ya watu duniani sasa wanapata umeme, lakini watu milioni 666 wengi wao wakiwa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara bado hawapati umeme. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
    3 min
  • 25 JUNI 2025
    Hii leo Jarida linamulika ripoti ya nishati jadidifu duniani, Afrika ikiwa bado inasuasua; Harakati za mabaharia wanawake Somalia, Mpango wa Umoja wa Mataifa wa UN80 na baba na malezi ya mtoto nchini Tanzania.Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inayofuatilia maendeleo kuelekea kutimiza Lengo la Umoja wa Mataifa la Maendeleo Endelevu namba 7 (SDG 7) linaloangazia nafasi muhimu ya nishati mbadala imetoa wito wa ufadhili zaidi kwani ingawa asilimia 92 ya watu duniani sasa wanapata umeme, lakini watu milioni 666 wengi wao wakiwa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara bado hawapati umeme. Anold Kayanda na maelezo zaidi.Nchini Somalia, suala la usawa wa kijinsia katika sekta ya baharini limepatiwa kipaumbele kwenye mjadala kuhusu wanawake katika tasnia hiyo, mjadala uliofanyika kwenye mji mkuu Mogadishu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mabaharia inayoadhimishwa tarehe 25 mwezi Juni kila mwaka ikibeba maudhui Meli yangu isiyo na unyanyasaji. Sharon Jebichii anatupasha zaidi.Je wafahamu kuhusu UN80? Flora Nducha anadadavua kwenye makala.Mashinani: Aloyce Siame, baba wa mtoto mwenye umri wa miaka 12 kutoka Tanzania ambaye kupitia Mpango wa Vijana uitwayo “Furaha”, unaoungwa mkono na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na wadau wake sasa ni mmoja wa wanaume wanaojitokeza kwa malezi ya watoto na familia zao.
    11 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners