Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 03 JULAI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayokupeleka nchini Uganda katika Mbuga ya Wanyama inayofahamika kwa jina Murchison Falls National Park kuangazia namna washiriki wa Kongamano la kimataifa la lugha ya Kiswahili lililofanyika mapema mwaka huu jijini Kampala walivyofurahia mazigira asili nchini Uganda na namna yanavyounufaisha ulimwengu.Mkutano wa 4 wa ufadhili kwa maendeleo umemalizika leo huko Sevilla, Hispania ambapo mashirika ya kiraia yametaka utekelezaji kwa vitendo kwa yale yaliyomo katika nyaraka iliyopitishwa iliyopatiwa jina Makubaliano ya Sevilla.Mmoja wa wawakilishi wa mashirika ya kiraia, Paula Sevilla amesema kinachohitajika ni uongozi kutoka nchi tajiri ambako ndiko zilizko kampuni kubwa zinazokwepa kodi.Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO kuhusu vijana na mifumo ya uzalishaij chakula na kilimo inaonesha kuwa karibu asilimia 85 ya vijana duniani wanaishi katika nchi za kipato cha chini na cha kati, ambako mifumo hiyo ni muhimu kwa ajira na maisha yao. Ripoti inasema kuwajumuisha vyema vijana katika mifumo hiyo kunaweza kuleta mchango wa hadi trilioni moja ya dola kwa uchumi wa dunia..Na mwezi uliopita wa Juni umeshuhudia ongezeko kubwa la familia za raia wa Afghanistan zikirejeshwa nyumbani kutoka Iran, tofauti na awali ambapo waliokuwa wakirejeshwa walikuwa ni wanaume peke yao.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchabuzi wetu Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA nchini Tanzania, anachambua neno KUTOHOA.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    10 min
  • UNDP Tanzania yahimiza ubunifu wa vyanzo vya mapato ili kuvutia wawekezaji
    Mkutano wa 4 wa Ufadhili wa Maendeleo (FFD4) ukiendelea huko Sevilla Hispania, juhudi za kuhakikisha nchi zinajitegemea kifedha kupitia vyanzo jumuishi na vya ubunifu zimezidi kupewa kipaumbele. Katika hafla ya kufungua mafunzo ya Muongozo wa Upatikanaji wa Fedha kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa, au Intergrated Local Financing Framework (ILFF) yaliyofanyika katika Manispaa ya Morogoro kaskazini-mashariki mwa Tanzania  hivi majuzi , Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Mpango wa Maendeleo nchini humo, UNDP umetoa mafunzo ya  namna halmashauri zinaweza kuandaa mikakati madhubuti ya kuhimiza maendeleo ya ndani kupitia ushirikiano kati ya sekta binafsi, mashirika ya kiraia, benki na jamii. Lengo ni kuendelea kuunga mkono serikali na wadau mbalimbali barani Afrika  katika kutafuta mbinu mbadala za kufadhili maendeleo.Sharon Jebichii na maelezon zaidi.
    4 min
  • IOM yasema uwekezaji wa kibunifu katika uhamiaji ni muhimu
    Katika Mkutano wa nne wa kimataifa wa Ufadhili wa Maendeleo (FFD4) unaoendelea jijini Seville, Hispania, Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limetoa wito wa kuimarisha uwekezaji wa kibunifu katika uhamiaji wa watu ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kusaidia kuziba pengo la kila mwaka la dola trilioni 4 za ufadhili wa maendeleo. Anold Kayanda anaeleza zaidi.
    2 min
  • 02 JULAI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia wahamiaji na njia bunifu ya kuwawezesha kujikimu kimaisha, na malezi bora ya watoto nchini Tanzania. Makala tunasalia huko huko Tanzania kumulika uwekezaji na ufadhili wa miradi ya maendeleo, na mashinani tunakwenda nchini Kenya.Katika Mkutano wa 4 wa Kimataifa wa Ufadhili wa Maendeleo (FFD4) unaoendelea jijini Seville, Hispania, Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limetoa wito wa kuimarisha uwekezaji wa kibunifu katika uhamiaji wa watu ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kusaidia kuziba pengo la kila mwaka la dola trilioni 4 za ufadhili wa maendeleo.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limekuwa likihimiza umuhimu wa malezi na makuzi chanya kwa watoto kama njia mojawapo ya kulinda haki kuu nne za msingi za mtoto ambazo ni kuishi, kuendelezwa, kushirikishwa na kulindwa..Katika makala mkutano wa 4 wa Ufadhili wa Maendeleo (FFD4) ukikunja jamvi leo huko Sevilla Hispania, juhudi za kuhakikisha nchi zinajitegemea kifedha kupitia vyanzo jumuishi na vya ubunifu zimezidi kupewa kipaumbele. Katika hafla ya kufungua mafunzo ya Muongozo wa Upatikanaji wa Fedha kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa, au Intergrated Local Financing Framework (ILFF) yaliyofanyika katika Manispaa ya Morogoro kaskazini-mashariki mwa Tanzania  hivi majuzi , Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Mpango wa Maendeleo nchini humo, UNDP umetoa mafunzo ya  namna halmashauri zinaweza kuandaa mikakati madhubuti ya kuhimiza maendeleo ya ndani kupitia ushirikiano kati ya sekta binafsi, mashirika ya kiraia, benki na jamii.Na mashinani, vijana na wahudumu wa afya katika kaunti ya Kajiado nchini Kenya, wameshikamana kuhamasisha umma kuhusu hedhi salama. Kupitia video iliyoandaliwa na washirika wetu Radio Domua, mmoja wa vijana anaelezea umuhimmu wa hedhi salama kama njia ya kutokomeza unyanyapaa dhidi ya wanawake na wasichana.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    10 min
  • 01 JULAI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulika ukame na uhakika wa upatikanaji wa maji na kusikia jinsi taifa la Chile, linatumia sera kushawishi mabadiliko yanayoweza kukabiliana na tatizo hilo. Pia tunakuletea muhtasari na mashinani.Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Iran, Stefan Priesner amesema wanachofanya hivi sasa ni kupanga upya programu za Umoja wa Mataifa nchini humo wakimulika vipaumbele vipya kufuatia mashambulizi yaliyoanza tarehe 13 mwezi Juni mwaka huu na kubadili mwelekeo wa kazi zao. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kutokea Tehran mji mkuu wa Iran, Bwana Priesner amesema sasa tuko kwenye mazugumzo ya serikali kuona ni vipi tutapanga upya programu zetu kukidhi mahitaji mapya yanayoanza kuwa dhahiri, ikiwa ni siku chache tu tangu mashambulizi yakome baada ya sitisho la mapigano kuridhiwa.Huko huko Geneva, Uswisi lakini akizungumza kutoka Nairobi Kenya, Shaun Hughes, ambaye ni Mratibu wa Dharura kwa mzozo wa Sudan katika shirika la Umoja wa MAtaifa la Mpango wa Chakula, WFP amewaambia waandishi wa habari kuwa hali ni tete kwa mamilioni ya raia wa Sudan waliokimbilia nchi jirani kuepuka mapigano nchini mwao.Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women linapotimiza miaka 15 tangu kuanzishwa kwake, limesema dunia imeshuhudia maendeleo muhimu katika usawa wa kijinsia ambayo yamebadilisha maisha ya wanawake na wasichana kote duniani. Licha ya ya kusherehekea, juhudi za kusukuma usawa wa kijinsia zinaonekana kurudi nyuma.Na mashinani, Mkutano wa 4 wa Ufadhili wa Maendeleo (FFD4) ukiendelea huko Sevilla Hispania, Natalia Toschi, Mkuu wa kitengo cha uwekezaji wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD annasema ni wakati wa kufikiria upya jinsi maendeleo yanavyofadhiliwa kwa kuzingatia mifumo ya kilimo cha mazao ya chakula ili kukuza ukuaji wa kiuchumi vijijini.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • Guterres awaambia viongozi wa dunia huko Sevilla Ni wakati wa kufadhili mustakabali wetu na kubadilisha mwelekeo
    Mkutano  wa 4 wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo FFD4 umeng’oa nanga rasmi leo huko Selilla Hispania kwa wito wa kuziba pengo la ufadhili wa maendeleo ili kutimiza ahadi ya kimataifa ya kutomwacha yeyote nyumba. Mkutano huo uliowaleta pamoja washiriki 2,500 kutoka nchi 150 wakiwemo wakuu wa nhi 50 na wadau wengine unasema kuna pengo la dola trilioni 4 katika ufadhili wa maendeleo linalohitaji kuzibwa. Anold Kayanda amefuatilia na anatupasha zaidi
    3 min
  • 30 JUNI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa 4 wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo FFD4 huko Sevilla Hispania, na siku ya Mabunge tukizungumza na mmoja wao kutoka Tanzania. Makala inatupeleka nchi Kenya na mashinani tunarejea huko huko Tanzania, kulikoni?Mkutano wa 4 wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo FFD4 umeng’oa nanga rasmi leo huko Selilla Hispania kwa wito wa kuziba pengo la ufadhili wa maendeleo ili kutimiza ahadi ya kimataifa ya kutomwacha yeyote nyumba. Mkutano huo uliowaleta pamoja washiriki 2,500 kutoka nchi 150 wakiwemo wakuu wa nhi 50 na wadau wengine unasema kuna pengo la dola trilioni 4 katika ufadhili wa maendeleo linalohitaji kuzibwa.Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya mabunge ikijikita katika harakati za kuwezesha mabunge kufanikisha usawa wa kijinsia wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa unaeleza ni kwa vipi Wanawake bado hawawakilishwi kwa kiwango cha kutosha katika mabunge ya kitaifa na ya mitaa duniani kote, jambo ambalo linapunguza haki zao za kisiasa na ushawishi wao juu ya sheria na bajeti..Katika makala tanatupeleka kaunti ya Kajiado, Kenya, katika eneo la EMbulbul, kukutana na vijana wanaotumia maarifa ya kilimo cha kisasa kubadilisha maisha yao na ya jamii, wakisema teknolojia imefungua njia mpya ya kuinua maisha ya wakulima wadogo, hasa kwa kutumia ukulima wa kisasa unaotumia maarifa na Teknolojia.Na mashinani, fursa ni yake Sandra Aloyce, Msichana mwenye umri wa miaka 12 kutoka Tanzania ambaye kupitia Mpango wa Vijana unaofadhiliwa na shirika la UNICEF uitwao “Furaha” unaotoa mafunzo kwa wazazi kuhusu umuhimu wa uwepo wa wazazi wote katika ukuaji wa mtoto ana ujumbe.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
    12 min
  • Siku ya mabunge duniani - Harakati za Usawa wa kijinsia Tanzania
    Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya mabunge ikijikita katika harakati za kuwezesha mabunge kufanikisha usawa wa kijinsia wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa unaeleza ni kwa vipi Wanawake bado hawawakilishwi kwa kiwango cha kutosha katika mabunge ya kitaifa na ya mitaa duniani kote, jambo ambalo linapunguza haki zao za kisiasa na ushawishi wao juu ya sheria na bajeti.
    3 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners